Invincible,
Mkuu karibu sana hapa kijiweni maanake wewe huonekana tu pale jua linapokuchwa!..
Maneno yako yangekuwa sawa kama sasa hivi sote tungekuwa bado shule ya msingi.
Point yangu kubwa ni kwamba Mwalimu alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi na mengi mabaya/mazuri tulikutana nayo wakati ule ,lakini leo hii tupo shule za secondary na wengine vyuo vikuu wanafanya vibaya basi lawama zinarudi kule walikoanzia masomo yao ya msingi na sii majumbani kwa wazazi wao ama hawa walimu tuliokuwa nao huku secondary na vyuoni.
Nachokataa mimi ni kwamba pamoja na kwamba hawa walimu wetu wa sasa hivi ni kizazi cha Mwalimu haina maana kwamba mwalimu is responsible!...
Mwalimu atalaumiwa kwa wakati wake tulipokula unga wa Yanga, uji wa Bulga na kunywa maziwa ya kutengenezwa na hata vita vya kuikomboa Afrika kama mtapenda kutumia sababu hizo.
Hivyo hivyo Mkoloni atalaumiwa hadi siku ile tulipopata Uhuru wetu baada ya hapo lawama ni zetu wenyewe kwani tulipodai Uhuru tulifahamu fika umasini alotuachia na kwa furaha kubwa tulichagua kuwa Huru na umaskini kuliko kunendelea kutawaliwa..
Mwisho, hivyo hivyo tulipoamua kubadilisha mfumo wa kiuchumi na kuwa Mafisadi sioni sababu ya kumlaumu mwalimu kwani lawama zake zinaishia pale alipoachia kamba..
Matukio ya kutoendelea leo ktk darasa hili la secondary yapo ndani ya darasa hili yaani kama sio walimu wetu hawa kina Mkapa, JK na viongozi wote wanaokutana huko Butiama basi tatizo lipo ktk mfumo wa masomo ama sisi wenyewe wanafunzi!... tumeshindwa kabisa kuelewa somo hili la Ufisadi..Ndivyo Tulivyo ni pale tunapoendelea kutafuta sababu za kushindwa kwetu darasani wakati wanaohudhulia masomoni kila siku ni sisi sio Nyerere.