Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,485
mzee hayo yanayosemwa humo.. binafsi mengine sikujua yamewahi kutokea... how did he do it.. against such odds..?
Mwanakijiji,
Wakati tunashindana nani zaidi wa myopicism in Tanzania, naomba niambatanishe hii habari niliyoikuta mtandaoni kwa bahati!
http://www.raceandhistory.com/cgi-bin/forum/webbbs_config.pl/noframes/read/1560
Ole Ndaskoi said:Mwalimu Julius Nyerere, it is said, told his wife to keep herself out, far away from politics.
Ole Ndaskoi said:In an apparent reference to President Mwinyi himself, Nyerere told the journalists that Tanzanians needed a leader who will defend and promote the national constitution. 'It can't be a person that gets advice from his wife, and tomorrow we see some decision has been made. You can't have such a guy. You won't know what his wife will advise him,' Nyerere said amid applause from more than 100 journalists attending the gathering. His boldness speaks volumes. He made sure that Tanzanians got rid Mwinyi.
I like this thread! Soo deep, ahsanteni wakuu 🙂 !!
SteveD,
Hii ni kwa sababu wale mchafua mada mkuu Mwafrika wa kike na mwenzake KadaMpinzani hawako hapa kuharibu mada. Ustaarabu muda mwingine hupotea wale wakiingia hapa JF
Mambo mengine bwana?
Wewe nimekuambia kila mara hapa kuwa uache kunifuatafuata na wala hutaki kusikia. Kila mara unapenda sana kunifuatilia na kuniita majina mara mtoto mara kuwa naharibu mada.
Mimi nachangia mada chache sana hapa JF, mada nyingi naziacha tu zinapita (kama nilivyokuwa nimeiacha hii). Kwa hakika ninapost wastani wa post 10 tu kwa siku wakati kuna mamia na maelfu ya post zinazowekwa hapa JF kwa siku moja.
Hizo mada zingine zote zinazoharibika ni nani anayeziharibu? Tafadhali sana kwa mara nyingine nakuasa uachane na mimi na ukae mbali kabisa na mimi kwa sababu hauna idea hata kidogo kwa nini niko hapa JF na kwa nini ninaandika the way I do.
Stay away from me na hii ni onyo nimekupa kwa mara ya mwisho.
Asante!
Vitisho vya nini tena mama? Utanifanya nini kwani?
Yaani we hutajwi tu hapa JF? Nilidhani uko off weekend? Wewe huoni kuwa bila wewe hapa hii thread ilikuwa inaenda vizuri?
Acha utoto na ukue na huu ni ushauri tu.
Mimi nimekuambia tu uachane na mimi. Hayo mengine ya ninajua vipi na kuja hapa si business yako.
Asante!
I like this thread! Soo deep, ahsanteni wakuu 🙂 !!
Nyerere ni "Intellectual giant" (siyo 'alikuwa..', bali anaendelea kuwa) Ni mtu aliyeweza kutofautisha miti na msitu. alikuwa si mbinafsi, alikuwa mkweli. Tatizo moja kubwa la Nyerere ni kwamba alikuwa anaona mbali mno, ambapo wengi wetu tunaona karibu tu, hata hatuwezi kufiria mbali. yaani kama ni asubuhi, sana sana tunaweza kufikiria mpaka saa sita tu, jioni hatuoni, kesho ndio kabisaa usiku wa giza.
Mazingira ya utawala wake, nchi ilivyokuwa alivyoanza nayo, na choice ya mambo aliyoamua kuyafanya, inamweka katika class ya aina yake. kiongozi anakuwa na priorities kwa wakati wake. wakati ule priority kubwa ilikuwa kujenga taifa na utaifa.
kuna choice zingine mfano sheria ya ardhi iliyopendekezwa na wakoloni wa kiingereza, na TANU ikaikataa, Kenya wakaipitisha, leo hii ndio moja ya sababu inafanya Kenya wanachinjana.
Mtu asiyekuwa na mtazamo mpana huangalia tu vitu ambavyo hana.
mwenye busara huangalia vyote: alivyo navyo na asivyokuwa navyo. wakati mwingine mtu anahitaji kutafakari zaidi, hata akisafiri huko nchi za nje. katika kuzunguka nchi mbalimbali, nimeshuhudia watu fukara wa kutupa, aina ya fukara ambaye Tanzania haiwezekani kuwa naye, by definition. Mfano India, ukikutana na ombaomba wa India, huna uhakika kama ataweza kutembea hatua 40 baada ya kuachana na wewe. ombaomba wa Tanzania ni uamuzi na pengine dili tu. Fukara wa nchi kama Kenya hana kitu kabisa, hawezi kwenda mahala akasema afungue shamba, kama walivyofanya vijana wa Bongo walipoamua wanakwenda kulima mpunga Ruvu. hilo nchi nyingine haliwezekani!
Falsafa ya Nyerere ililenga maendeleo ya watu, na ndio maana hata mifumo yake ya elimu ililenga kunufaisha wengi zaidi. lakini pia alijua umuhimu wa elimu ya juu ndio maana TANU ilihusika sana na uanzishwaji wa chuo kikuu. kwa hawa wachache aliwakumbusha kwamba ni waliokabidhiwa chakula ili wakatafute chakula cha kijiji chote. Leo hapa sie tunaoongea humu JF, tunafanya nini kuhakikisha tunarejesha chakula kwa wakulima masikini ambao kwa kukatwa kodi lukuki katika mazao yao, tumenufaika kuelimika? Na wengi wetu tunapozungumzia maendeleo, tunazungumzia majengo marefu, huduma bora mijini, matajiri wachache, na wengine walie tu.
Kumkosoa Nyerere inabidi ujiandae hasa. kwanza ujilinganishe naye katika uwezo wa kuona, uone vizuri kama yeye. kama huoni vizuri mbele, utamkosoaje Nyerere?
Wengi wanakosoa Azimio la Arusha, ambalo kimsingi lilidai njia kuu za uchumi zimilikiwe na watanzania. kuna ubaya gani hapo? leo tunashuhudia mali zetu zikiliwa kifirauni. mashirika aliyoyajenga Nyerere, kama NBC, yalivyochukuliwa kirahisi tu. mengine kama TANESCO yanafilisiwa kwanza ili yaonekane hayafai, ili wayauze kirahisi. hata kama ni watanzania binafsi katika makampuni au umoja wao wanamiliki njia hizi, spirit ya Azimio la Arusha itakuwa imetekelezwa. lengo ni milki iwe kwa watanzania. sasa wanamiliki vipi, hilo ni utekelezaji, ambapo tungeweza kumodify kidogo tu. lakini leo utasikia mtu anakandia Azimio la Arusha, wakati hata hajalisoma na kulichambua.
Mwisho, tukumbuke pia kwamba Nyerere alikuwa na maadui wengi tena wenye nguvu. walikuwa na hamu ya "prove him wrong", kwamba siasa zake hazitekelezeki. amehujumiwa sana. lakini hujuma kubwa zaidi ni kutoka ndani ya nchi. wasaidizi wake hasa wenye uroho, alikuwa na kazi kubwa sana ya kupambana nao. hivi mfano ukiangalia wachina wanaokwenda nchi za nje, jinsi wanavyohaha kutafuta tekinolojia ya nje kupeleka kwao. wenzetu japo wanamkosoa Mao, wameendeleza ile spirit yake. sisi watanzania wapi, ndio kwanza hatuna mpango na kwetu kabisa.
Kiswahili ni lulu, wengine wanajua na wanaitukuza. jiulize kwa nini pale chuo kikuu sasa hivi kuna projecti nyingi sana za kiswahili, wageni wanajifunza sana lugha yetu. sisi ndio kwanza tumezubaa katika malumbano yasiyo kichwa wala miguu, kuhusu umuhimu wa Kiswahili. Nyerere alijua yote haya na aliwekeza kweli kweli. Tatizo letu kubwa sio umaskini. tatizo hasa ni ufinyu wa mawazo.
Mindi,
hamna la maana lolote ktk post yako ndeeeeefu kama treni!!! mtoto wa darasa la tano wakati ule wa Nyerere, alikuwa anaweza kuandika uloandika hapo juu.........
Haya mama tuendelee na mada usijekunimeza bure?!
Mimi sina mpango wa kukumeza ila nakukumbusha tu uniache peke yangu (leave me alone) kwenye mijadala yako. Zaidi ya hapo sina tatizo mkuu tuendelee na debate hapa maana taifa limeshauzwa kwa kiwango kikubwa sana na ccm!
Sikujua kama unamezaga watu....kwikwikwiiiii
Kwi kwi kwi kwi, yaani we acha tu! Huyu baba amekuwa ananisakama sana hapa JF na sijui nimemkosea nini. Kama ni hivi nadhani kuna sababu ya kummeza......lol
Dizaini aliwahi kukutokea ukampiga kibuyu na bado haja get over it.....kwikwikwiiiii