Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Mzee Mwanakijiji,
Unajua ukiyasoma yale mahojiano uliyoweka hapo nyuma utaona kuwa Tanzania tumeshapoteza dira ya Taifa!..yaani tunaenda tu hatuna goals zaidi ya kuwaskiliza wazungu!...Kila alilosema MJn na pengine kusema kwa uhakika (kuapa) kimebadilishwa leo hii. Hakuna hata kiongzi mmoja anayeweza kukupa map ya safari yetu zaidi ya kudai kuwa bahari ni chafu tunamwachia Mungu!
Nimesoma jana usiku mzima nikajaribu kuchanganua na hali halisi mjomba ilikuwa kama nimepata msiba!... hakuna kilichobaki!.
Ebu nakuombeni tuyatazame upya mahojiano yale ili tupate ukweli wa mengi ambayo hadi leo hii huwa tunabishana humu.

1. Kuhusu Azimio la Arusha.. ebu tazameni kila alohofia ndio limechukua nafasi leo hii!

MJN: I still travel around with it. I read it over and over to see what I would change. Maybe I would improve on the Kiswahili that was used but the Declaration is still valid: I would not change a thing. Tanzania had been independent for a short time before we began to see a growing gap between the haves and the have-nots in our country. A privileged group was emerging from the political leaders and bureaucrats who had been poor under colonial rule but were now beginning to use their positions in the Party and the Government to enrich themselves. This kind of development would alienate the leadership from the people. So we articulated a new national objective: we stressed that development is about all our people and not just a small and privileged minority.

2. Utawala... Tunayoyaona leo toka CCM. Je, multiparty was a solution?.. or was it too late!
MJN: I never advocated this for everyone. But I did for Tanzania because of our circumstances then. In 1990 the Chama Cha Mapinduzi (CCM) abandoned the one-party state for a multi-party system. But we do not have an opposition. The point I was making when I made the statement was that any party that stays in power too long becomes corrupt. The Communist Party in the Soviet Union, the CCM of Tanzania and the Conservative Party of Britain all stayed in power too long and became corrupt. This is especially so if the opposition is too weak or non-existent.

3. Uchumi wetu... hivi kweli sasa hivi tunapaa?
I was in Washington last year. At the World Bank the first question they asked me was `how did you fail?' I responded that we took over a country with 85 per cent of its adult population illiterate. The British ruled us for 43 years. When they left, there were 2 trained engineers and 12 doctors. This is the country we inherited.
When I stepped down there was 91-per-cent literacy and nearly every child was in school. We trained thousands of engineers and doctors and teachers.
In 1988 Tanzania's per-capita income was $280. Now, in 1998, it is $140. So I asked the World Bank people what went wrong. Because for the last ten years Tanzania has been signing on the dotted line and doing everything the IMF and the World Bank wanted. Enrolment in school has plummeted to 63 per cent and conditions in health and other social services have deteriorated. I asked them again: `what went wrong?' These people just sat there looking at me. Then they asked what could they do? I told them have some humility. Humility - they are so arrogant!

Ikiwa 1988, per-capita income ilikuwa Usd 280, leo hii tumesimama wapi?...Je, ni kweli mlosema Nyerere hakuwa mchumi mzuri maanake hata hao IMF walibaki domo mwaaa!

4. Ili tuendelee tunahitaji nini?...Let us argue the moral case. Let us create a new liberation movement to free us from immoral debt and neo-colonialism - MJN

MJN: It seems that independence of the former colonies has suited the interests of the industrial world for bigger profits at less cost. Independence made it cheaper for them to exploit us. We became neo-colonies. Some African leaders did not realize it. In fact many argued against Kwame (Nkrumah)'s idea of neo-colonialism.
The majority of countries in Africa and the rest of the South are hamstrung by debt, by the IMF. We have too much debt now. It is a heavy burden, a trap. It is debilitating. We must have a new chance. If we doubled our production and debt-servicing capabilities we would still have no money for anything extra like education or development. It is immoral. It is an affront. The conditions and policies of the World Bank and the IMF are to enable countries to pay debt not to develop. That is all! Let us argue the moral case.Let us create a new liberation movement to free us from immoral debt and neo-colonialism. This is one way forward. The other way is through Pan-African unity.
 
Ninashauri kuwa Mwalimu Nyerere Foundation ipewe changamoto ya ku-digitize text, audio na video files zote zenye hotuba, interview na articles zote za Mwalimu waziuze kwenye website yao at reasonable prices kusudi wasambaze busara za Mwalimu kwa generation mpya at the same time wawe wanakusanya pesa kidogo kwa ajili ya kuendeleza Foundation ile.
 
Guys...aliyesema "You Don't Know What You Have, Until It's Gone" alikuwa 101% RIGHT...it's so painful.
 
Yebo Yebo,

Hiyo ni kweli kabisa, kila ninaposema maandiko ya huyu Mzee wetu na kulinganisha na hali ilivyo sasa machozi hunilenga. Mwalimu's words are prophetic he could see very far ahead. Unfortunately today we trampling on his ideals and even painfully it is his trusted "disciples" are fore front, Yuda Iskarioti's. I'm trying to imagine how would he have felt, bora alitangulia kujipumzikia baada ya kutuwekea principles.

Kinachokera zaidi ni jinsi walivyo/wanayotumia jina la Mwalimu kupata kura, its a pity!
 
Ninashauri kuwa Mwalimu Nyerere Foundation ipewe changamoto ya ku-digitize text, audio na video files zote zenye hotuba, interview na articles zote za Mwalimu waziuze kwenye website yao at reasonable prices kusudi wasambaze busara za Mwalimu kwa generation mpya at the same time wawe wanakusanya pesa kidogo kwa ajili ya kuendeleza Foundation ile.

Jitihada zimefanyika kufanya hili lakini kokosekana kwa utashi miongoni mwa wahusika na ukiritimba usio wa lazima imeshindikana hadi sasa katika upande wa audios and video files. Hali ya sehemu ambako hivi vitu vinanapaswa kuhifadhiwa pale TvT na Radio Tanzania ni mbaya mno kiasi ya kuwa nyingi zitakuwa zimeharibika na kuziserve ni gharama kubwa mno ukichukulia ni wachache wanaoana hilo zoezi kama priority.

Text files zoezi lilikuwa linafanyika. I hope limefanikishwa.

Tatizo lingine ni kuwa nyingi zipo mikononi mwa watu binafsi ambao wanafanya ama walikuwa wakifanya kazi katika asasi zetu mbalimbali. Wapo walioziiba kwa nia ya kuzihifadhi na wapo waliona kuwa zitakuwa dili hapo baadaye.

Ombi langu kwa huyu mheshimiwa mpya TvT ni kulivalia njuga suala hili. Wengi wamejaribu wameshindwa.
 
kama Mwalimu alikuwa mzuri sana mbona nchi iliporomoka? katika masuala ya kuendesha uchumi Mwalimu alifanya vibaya sana.I am sorry guyz, but I am just too RESULTS ORIENTED.

i was there wakati mwalimu anaachia madaraka and trust me i dont want to re-live in that era. hali yetu ilikuwa kama zimbabwe.

vijana walikuwa wanatoroka kwa kukatisha maboda mpaka sudan then egypt. kuna incidence ya vijana wa kitanzania waliotupwa baharini na kuliwa na papa. walikuwa wamekimbia hali ngumu ya maisha iliyosababishwa na utawala wa mwalimu.

azimio la arusha lilipaswa kuwainua na wazawa waafrika waweze kumiliki biashara/uchumi kama wenzao waasia,waarabu na wazungu. badala yake azimio limemkandamiza kila mtu na kuwaacha wananchi ktk dhiki kubwa.

wengi wenu mmekurupuka na kusifia majibu ya mwalimu kwa watendaji wa imf. ukitulia na kulitafakari jibu la mwalimu ni kwamba haoni tatizo for his failures as long as alternative iliyochukuliwa imefeli vilevile.

mwalimu angeulizwa kwanini yeye pamoja na imf wamefeli angesema nini? aliwaita imf ma--arrogant lakini hata yeye alistahili sifa hiyo.

WAKATI ANAONDOKA MADARAKANI KILA MKOA WALIMCHANGIA MWALIMU KUANZIA VYAKULA,MIFUGO,MATREKTA,MASHINE MBALIMBALI,SAMANI,NYUMBA etc etc. Hata mikoa iliyoathirika vibaya kwa sera na maamuzi yake nayo walimchangia!!

miaka ya mwalimu kulikuwa kuna mawaziri wanaacha kazi na kwenda kuishi kwenye nyumba hazina hata milango au madirisha. wengine walikuwa hata jirani zake pale msasani. yeye mwalimu kama alikuwa mwadilifu kwanini hakwenda kuishi maisha ya chini kama mawaziri wake kadhaa[majina naya hifadhi]?
 
Mzee mwanakijiji
pamoja na ukweli kwamba watawala wetu wa sasa wanapenda kuiga wala sio kuwa wabunifu, je ni tatizo gani limeikumba kada ya wasomi wetu ambao wamekimbilia siasa kama mtaji wao kimaisha hali wakizimaliza taaluma zao kisiasa?
 
Jitihada zimefanyika kufanya hili lakini kokosekana kwa utashi miongoni mwa wahusika na ukiritmba usio wa lazima imeshindikana hadi sasa katika upande wa audios and video files. Hali ya sehemu ambako hivi vitu vinanapaswa kuhifadhiwa pale TvT na Radio Tanzania ni mbaya mno kiasi ya kuwa nyingi zitakuwa zimeharibika na kuziserve ni gharama kubwa mno ukichukulia ni wachache wanaoana hilo zoezi kama priority.

Text files zoezi lilikuwa linafanyika. I hope limefanikishwa.

Tatizo lingine ni kuwa nyingi zipo mikononi mwa watu binafsi ambao wanafanya ama walikuwa wakifanya kazi katika asasi zetu mbalimbali. Wapo walioziiba kwa nia ya kuzihifadhi na wapo waliona kuwa zitakuwa dili hapo baadaye.

Ombi langu kwa huyu mheshimiwa mpya TvT ni kulivalia njuga suala hili. Wengi wamejaribu wameshindwa.

I got a good laugh out of that one!!!

Na nyie mabwana tovuti vipi..mbona inaonekana kama mlitaka kuihamisha hii topic?
 
Jokakuu,
Wale vijana waliotupwa baharini ilikuwa wakati wa Mwinyi, sasa lete story nyingine maanake sote tulikuwepo Bongo. Tunachojua ni kuwa Bongo tulipata matatizo ya vitu vinavyotoka nje basi na kiuchumi sidhani kama ingesaidia kitu.

Leo hii uchumi wetu una nafuu ipi ikiwa kila supermarket imejaa mali za nje! si ndiyo ya Zimbabwe hayo yaani tukifungiwa tu kuingia vitu nchini tumekwisha! mpango wa kuwa na taifa Tegemezi...Zimbabwe walitegemea kila kitu toka kwa Makaburu wa South na hali hii waliyojifunga wao likuwa ni lazima itokee kwani waliuza uhuru wao kwa Kaburu na Muingereza pale walipokubali kuweka mkataba! Hata kulima walisha acha wakajikita ktk elimu na kutafuta kazi mijini wakitegemea mzungu atawalisha!.. mzungu mwenyewe Kaburu ambaye juzi tu mlikuwa mkiuana kama wanyama.
Wakati wa Nyerere tunachoikumbuka zaidi ni kupanga mawe kwa ajili ya njaa iliytoingia na rais wtu alipo declare emergency, tulizalisha kuliko uwezo wetu na vyakula vilioza mashambani. wakati wa Nyerere ni visa ya nchi moja tu naikumbuka nayo ni US lakini kote tulikuwa tukipeta tu na ganda lako la kijani!..
Kwanza habari za kutoka nje Ukimbizi sijui kutafuta meli hazikuwa somo kabisa kwa vijana wengi wa nje ya mikoa ya Pwani na Zanzibar.
Matatizo gani ndugu yangu wee umekusikia Zimbabwe ama unafanya mzaha!... Nimetaka kununua mali fulani ktk biashara zangu visa yangu imekataliwa na serikali ya hapa kwamba siruhusiwi kununua wala kupeleka kitu Zimbabwe!.. sasa nambie mchezo huo unafikiria mdogo!.. jamani acheni maneno hamjakutwa na zahma nyie!
 
Ninaifanyia kazi hotuba ya mwalimu ya Mei Mosi 1995 kule Mbeya. Hotuba hii ni hotuba ambayo mwalimu alitumia muda wake kuzungumzia mambo mengi yaliyolihusu Taifa hasa mwelekeo wake. Nimeisikiliza tena jana na nikajikuta mwili unasisimka kwa kuguswa na ukali wa hoja zake.

Akizungumzia suala la viongozi wetu kukubali mashauri ya IMF na World Bank without a fight Mwalimu alisema:

"Mtu mwenye akili akikujua na wazo la kipumbavu, na akijua wewe una akili, nawe ukalikubali wazo hilo, atakudharau".

Pia akikema kitendo cha serikali kufuta haki ya raia kuchaguliwa (kwa kukataa wagombea binafsi) Mwalimu alisema:

"Serikali haina uwezo wa kufuta haki za raia"!

Na hapa alikumbushia mfano wa Chief Sarwat aliyembwaga mgombea wa TANU licha ya mgombea yule kupigiwa debe na Mwalimu mwenyewe.
 
Jioni ya leo niliweka muda wa kutosha kusoma baadhi ya maandiko ya Nyerere. Nilikwenda maktaba pale chuoni na kukaa hadi walipofunga. Niliweza kusoma baadhi ya hotuba zake na kushangaa kwa nini sikuizielewa hotuba zile wakati yeye mwenyewe yuko hai. Kwa bahati mbaya sikuweza kuandika notes zozote, ila yale yalinonitachi zaidi yalihusu matumizi ya madaraka na matumizi ya raslimali za nchi:
  1. Matumizi ya madaraka: Mwalimu ni mtu pekee aliyekaa madarakani kuiongoza nchi yetu kwa miaka 26. Waingereza walitutawala kwa karibu miaka 40 lakini katika kipindi hicho tulikuwa na magavana 9 ambao walikuwa wakidumu miaka minne tu isipokuwa magavana watatu tu ambao vipindi vyao havikuzidi miaka kumi. Gavana wa kwanza Sir Horace Byatt alipitisha vipindi viwili na kudumu kwa miaka 8 kuanzia mwaka 1916 hadi 1924. Gavana pili Sir Donald Cemeron naye alizidi miaka minne kwa kukaa madarakani kwa miaka 6 kuanzia mwaka 1925 hadi mwaka 1931. Magavana waliofuata wote hawakutawala zaidi ya miaka minne isipokuwa gavana wa nane, Sir Edward Twining, liyedumu vipindi viwili kuanzia mwaka 1949-1958 na hivyo kuongoza miaka 9. Hata wale magavana wanane wa kijerumani waliotutawala kwa miaka 34 kuanzia mwaka 1885 hadi mwaka 1919, hakuna aliyezidi zaidi ya miaka mitano. Kwa hiyo, katika karne nzima ya 19 na karne ya 20, ni Nyerere pekee aliyeongoza nchi yetu kwa zaidi ya miaka 10.

    Nyerere uzoefu wake wa kuongoza nchi hii ulionyesha kuwa kwa nchi hii ya Tanzania ni rahisi sana kwa viongozi kulewa madaraka na kuyatumia vibaya kujinufaisha. Kwa hiyo ni lazima sana tufahamu nia ya mtu anayetaka kuwania uongozi. Wale wote wanaotaka kupata madaraka ili wayatumie vibaya kujifuaisha, ni watu ambao lazima waogopwe kama UKOMA.

    Matokeo ya maneno haya ni kama leo tunavyojadili swala la Rais Mkapa kufanya biashara ikulu na kutumia ofisi ya Ikulu kuomba mikopo wenye mabenki ambayo yao chini ya uongozi wake. Matokeo yake ndiyo haya tunayoona viongozi wanaingiza nchi kwenye mikataba ya ajabu ajabu huku wakiangalia manufaa yao tu. Nyerere alijua sana mikataba iliyoandikwa na akina Chief Mangungo na Carl Peters na matokeo yake; yeye aliingia madarakanai siyo by default ila kwa kupignania uhuru wetu. Alikuwa anaona hatari za watu kuingia madarakani by default na matokeo yake kama tunavyoona leo hii.

  2. Matumizi ya Raslimali Zetu: Mwalimu alipokea nchi hii kutoka kwa wakoloni ambao walikuwa wameshafanya survey ya raslimali za madini zilizouwapo ambazo walikuwa tayari kuzichimba. Makampuni kama Lonrho yalikuwa yameshajizatiti sana kuchimba madini nchini kama walivyokuwa wanafanya Rhodesia wakati huo (Zimbabwe). Mwalimu akaona kuwa tukiwaachia jamaa hawa kuchimba madini haya na kuyachukua kwao huku tukijua kuwa ndiyo raslimali pekee tuliyonayo na ambayo ndiyo ilikuwa imewafanya watutawale in the first place, nchi hii itakuwa kama bado ni koloni ingawa linaongozwa na mtu mweusi. Ni kutokana na kuona hali hiyo ndipo yeye kwa kushirikiana na rafiki yake Kwame Nkrumah walipoingiza msamiati wa neo-colonialism (Ukoloni Mamboleo). Akasema kuwa tutaziacha raslimali hizi bila kuzigusa hadi sisi wenyewe tutakapoweza kuzitumia. Hatuwezi kujifanya tuko huru huku tukiwaachia raslimali zetu mchukue bila sisi wenyewe kufaidika nazo. Ndiyo maana investmet yake kubwa ilikuwa kwenye watu kusudi waje wazitumie raslimali hizi. Akatoa elimu ya bure na huduma ya afya ya bure kusudi tutakapofungua macho na kujua kutumia raslimali tulizonazo, zitufae.

    Ukweli unaotokana na maneono haya ndio tunaounona leo. Kwa bahati mbaya ndoto yake haikufanikiwa kwa vile wale wachache waliopata nafasi ya kusimamia raslimali hizo baada ya yeye wakaamua kuzitoa kwa kujenga ukoloni mamboleo huku wakiwaondoa watanzania wasizitumie raslimali hizo kinyume kabisa na plani ya Nyerere. Watu waliofukuzwa Merereni, kufukiwa Bulyankulu, na migodi mingineyo ndio watu Nyerere aliokuwa na matumaini nao kwa nchi lakini kwa bahati mbaya walizimwa. Watu wa nje wanachukua mchanga mzima bila hata kuusafisjha ili wakasafishie kwao; ni jambo la aibu kweli. Nimeishi marekani zaidi ya miaka kumi na ninajua kuwa wao wana mipango ya kutochimba baadhi ya mafuta yao kwa sababu zao za kitaifa, badala yake wanafuata mafuta ya nje kama yale ya Iraq, saudia, Nigeria na kwenngiko; sisi tulikosaje subira wakati watu wetu walikuwa wameshaanza kuchimba madini yale? Je kwa kuleta makampuni ya nje kuchimba madini yale kumeongeza nini katika masiha ya watu wetu?

    Nyerere aliona haya, je leo hii hatuna viongozi wanaoweza kuona hayo pia?
 
Mzee Mkandara, heshima yako Baba

Binafsi, nadhani tulikuwa na misingi mizuri katika nyanja za Michezo, Elimu, Viwanda, Siasa, Uchumi, Madini na Mali Asili nyingine. Misingi yote katika hizi nyanja ilihitaji kuimarishwa kwa kufanya marekebisho ya kuondoa dosari zilizojitokeza mara kwa mara. Sikuona haja ya kuvunja nguzo au misingi muhimu katika baadhi ya hizi nyanja kwa lengo la kuanza upya. Nafikiri tulifanya makosa makubwa ya kiama ambayo gharama yake haina kifani.

Hizi sera mpya za “utandawazi/globalization” ni mithiri ya mafuta ambayo tunayatumia kujikaanga wenyewe. While the “utandawazi” has been engineered to create the illusion that it is creating wealth, in fact it is about concentrating a declining pool of real wealth into fewer and fewer hands. Tanzania’s real wealth is increasingly appropriated and ravaged by makampuni ya kigeni ambayo yanakuwa more aggressive extracting what remains. Ni kweli unavyosema, ama tuyakorofishe haya makampuni yaondoke alafu sisi tuanze mtafaruku kama Zimbabwe, au resources za nchi yetu zikauke alafu yatimue mbio. Lazima kitu kimoja kati ya hivyo viwili kitatokea. Anyway, time will tell.

Mzee Kichuguu, heshima yako Mkuu

Unaongelea maswala ya wananchi kufukiwa kwenye mashimo? Who cares anyway? Of course, as mining corporations engage in the extraction of non-renewable mineral resources to provide often momentary pleasures for the already well off, they create a double tragedy. Ukiacha watu kufukiwa au kuhamishwa bila mafao, we have seen our traditional lands irreversibly damaged by these mining corporations. Hakuna kitu cha maana tunapata kutoka katika haya makampuni.

Nadhani wengi tulisoma hadithi za Alinacha. Nafikiri Alinacha hakuwa mjinga hata kidogo. Alikuwa na mipango mizuri ya maisha lakini akaipiga teke mwenyewe. Nchi yetu imeazima busara za Alinacha. Haiwezekani misingi yote aliyotuachia Nyerere ikawa na makosa kiasi cha kuipiga teke. Historia itatuhukumu.
 
Kyoma,
Hiyo na Alinacha nayo ina afadhali, mimi naona tumekuwa kama Abunuasi aliyekuwa akikata mti aliokalia mwenyewe na kwa akili zake katu haikumwingia kuwa ataanguka.

Hii ndio reasoning ya viongozi wetu kwa kila hoja na inashangaza sana wanaposhindwa kuona mbele... hivi kweli hawa watu hawana vision ama wanafanya makusudi fulani maanake wamesoma tena shule KUBWA ambazo sisi akina yakhe tunasoma mabango yake tu kwa nje!.
Shukran sana usiwe unapotea kiasi hicho mkuu wangu maanake tunazikosa taaluma zako!
 
Mzee mkandara, Heshima yako Mheshimiwa

Hivi wewe huwa ni comedian? Manake wakati mwingine vijembe vyako huwa vinaniacha hoi nikicheka. Umenikumbusha hadithi za Abunuasi, sina mbavu kabisa!

Ndugu yangu we! Viongozi wengi wametwanga shule kweli kweli, lakini wanacheua fyongo nyingi mno. Hata hivyo, hiyo isikukondeshe. Education level measures only the number of years an individual attended school, not how much the individual learned in school. Thus, asking hawa viongozi wetu waheshimiwa how many years of school they completed does not help us predict their literacy skills. Mantiki nyingine ya kuelezea vihoja vya hawa viongozi wetu ni kuwa they are very educated but sadly never cultivated.



 
Mwanakijiji,
nimecheka ulipoelekeza kwamba Baba wa Taifa aliikemea serikali kwa kukataa wagombea binafsi. hivi ni kwanini yeye alipokuwa madarakani alizuia si wagombea binafsi tu, bali pia vyama vya upinzani?

mambo mengi ya Mzee wetu huyu yanapendeza kuyasoma tu on weekends, lakini matokeo ya utekelezaji wa mawazo yake siyo mazuri sana.
 
Mwanakijiji,
nimecheka ulipoelekeza kwamba Baba wa Taifa aliikemea serikali kwa kukataa wagombea binafsi. hivi ni kwanini yeye alipokuwa madarakani alizuia si wagombea binafsi tu, bali pia vyama vya upinzani?

mambo mengi ya Mzee wetu huyu yanapendeza kuyasoma tu on weekends, lakini matokeo ya utekelezaji wa mawazo yake siyo mazuri sana.


Joka kuu umewahi kusikia kuhusu Chief Sarwat wa Mbulu.. au na wewe unaamini kuwa "alizuia wagombea binafsi". Hiyo myth nyingine.
 
mkjj,
suala chief sarwatt nalielewa. hii sheria ya kufuta demokrasia ya vyama vingi na hata wagombea binafsi haikuanzia wakati wa utawala wa nyerere?
 
jokakuu, Chief Sarwat aligombea kama mtu binafsi sivyo? hivyo maneno yako "kwamba Baba wa Taifa aliikemea serikali kwa kukataa wagombea binafsi" hayana ukweli. Rais alitokea Mbeya hadi kwenda Mbulu kumpigia debe mgombea aliyependekezwa na TANU lakini alishindwa, na Mwalimu alifanya nini? alimtimua Sarwat?

Suala la vyama vingi au kimoja, tafuta hotuba ya Mwalimu akielezea suala hilo na kile alichokiita demokrasia ya chama kimoja. leo hii ukifikiria sana utaona kuwa kulikuwa na demokrasia zaidi kwenye chama kimoja kuliko mazingaombwe tunayoyaona sasa. Sisemi kuwa ilikuwa inafaa zaidi.
 
suala linabaki palepale kwamba, aliyeidhinisha sheria ya kutokuwa na wagombea binafsi ni Julius Kambarage Nyerere.

wakati wewe unaangalia yanayojiri wakati huu, mimi naangalia ya wakati ule na haya ya sasa. kama kungekuwa na vyama vingi: je, bunge lingekaa kimya wakati wananchi wanaswagwa mikoa ya kusini kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa? je, bunge lingekaa kimya wakati serikali inasuasua kuchukua hatua za haraka kurekebisha uchumi?
 
suala linabaki palepale kwamba, aliyeidhinisha sheria ya kutokuwa na wagombea binafsi ni Julius Kambarage Nyerere.

wakati wewe unaangalia yanayojiri wakati huu, mimi naangalia ya wakati ule na haya ya sasa. kama kungekuwa na vyama vingi: je, bunge lingekaa kimya wakati wananchi wanaswagwa mikoa ya kusini kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa? je, bunge lingekaa kimya wakati serikali inasuasua kuchukua hatua za haraka kurekebisha uchumi?

sheria gani hiyo?
 
Back
Top Bottom