Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Je unahisi i am not clear-headed?
Just for not agreeing to what you believe?
Fungua milango kwa mawazo ya watu wengine ambao hawaamini to divine power or let me say "divine personal"
Sitaki kusema una mawozo mgando kwani nina respect michango na urgements zako katika forum hii. lakini juu siku moja hat wewe ukitoka kwenye madaraka hata kama ulitoa utu wako kwa ajiri ya nchi yako wapo watu watakusema tu hilo huwezi epuka swaiba
 
Je unahisi i am not clear-headed?
Just for not agreeing to what you believe?
Fungua milango kwa mawazo ya watu wengine ambao hawaamini to divine power or let me say "divine personal"
Sitaki kusema una mawozo mgando kwani nina respect michango na urgements zako katika forum hii. lakini juu siku moja hat wewe ukitoka kwenye madaraka hata kama ulitoa utu wako kwa ajiri ya nchi yako wapo watu watakusema tu hilo huwezi epuka swaiba

we fuata mlolongo wa mada hii utagundua naongea na ole na si weye!

kumbuka kuwa ni weye uliyesema...."nadhani atakujibu"

au nawe uko na ndito hapo karibu unashindwa ku-concentrate!

anywayz....hayo mengine ulosema....tuseme sijayaona...tuendelee!
 
Viongozi wengi Afrika wadaiwa kuwa ni walafi
Na Mwandishi Wetu, Arusha

WENGI wa viongozi waliotawala Afrika baada ya uhuru
walikuwa walafi na hivyo wamechangia mno kukwama kwa
maendeleo ya bara hilo, imeelezwa.

Mchumi na mtunzi maarufu wa vitabu wa Ghana, George
Ayitteh, alisema hapa jana kwamba kati ya marais 204
waliotawala Afrika baada ya uhuru, ni wachache, tena
hata 20 hawatimii, ambao hawakufilisi nchi zao.

“Ukiondoa wachache, Kwame Nkrumah (Ghana), Julius
Nyerere (Tanzania)... yupo pia Nelson Mandela, tena
hata 15 hawatimii, wengine wote walikuwa wezi
wakiendesha mifumo ya serikali iliyokuwa ikiishia
kuweka fedha za wizi katika benki za Uswisi,” alisema.

Alikuwa akizungumza katika mada: “Tutazame nyuma ili
kutazama mbele” katika mkutano wa teknolojia, wabunifu
na wasanii (TED) uliofanyika mjini hapa kwa siku ya pili
jana.

Aliongeza Ayitteh: “Katika Afrika serikali ni
matatizo. Ni huko tu ambako serikali zinafilisi watu
wake. Baada ya kuwafilisi hutembea na bakuli kubwa
zikiomba omba. Lakini bakuli hilo nalo huwa halijai kwa
kuwa limetoboka, linavuja.”

Alisema ili kubadili mambo, hakuna budi kurejesha
uwezeshaji katika sekta zisizo rasmi na zile za jadi
ambako ndiko waliko Waafrika wengi wenye kufanya kazi
za kujizalishia maendeleo.

“Tunaposema tunataka kuisaidia Afrika tuangalie ni
Waafrika kina nani hawa ambao tunataka kuwasaidia.
Tutawapata hao kwenye sekta zisizo rasmi na za jadi,
wao ndio wakulima. Hiyo itatupunguzia mzigo wa kutumia
kila mwaka dola za Marekani bilioni 20 kuagiza chakula
nje. Na tutaziba mwanya wa fedha inayopotea katika
rushwa na uoza mwingine zipatazo dola za Marekani
bilioni 148 kwa mwaka,” alisema.

Mkutano huo wa TED ni wa kwanza kufanyika Afrika na
unawashirikisha mamia ya raia wa mataifa mbalimbali
duniani tangu wasomi hadi watu wa kawaida, wabunifu na
watu ambao wamefanikiwa katika maisha kwa kujituma na
kutumia fursa za kujiendeleza.
 
HIVI KWANINI HAWATAKI KUHESHIMU MATAKWA YA MWALIMU?
ALIPOKUWA HAI HAKUTAKA KUTUKUZWA LAKINI LEO HII KILA KITU WANAKIPA JINA LA NYERERE

NA SASA HIVI MPAKA MIJISANAMU YA MWALIMU INAJENGWA KAMA UYOGA JAMANI MAMBO HAYA VIPI?

d1.jpg
 
HIVI KWANINI HAWATAKI KUHESHIMU MATAKWA YA MWALIMU?
ALIPOKUWA HAI HAKUTAKA KUTUKUZWA LAKINI LEO HII KILA KITU WANAKIPA JINA LA NYERERE

NA SASA HIVI MPAKA MIJISANAMU YA MWALIMU INAJENGWA KAMA UYOGA JAMANI MAMBO HAYA VIPI?

d1.jpg


...unakumbuka weye nicknames ngapi ulizikataa lakini bado watu wakaendelea kukuita....na hiyo ulikuwa hai!
 
Hivi hii nimekua nikiangalia na kusoma kwa shauku historia fupi ya kikwete toka alivyokuwa kijana mpaka sasa hivi , malengo yake haswa ya kuingia ccm yalikuwa ni nini , kwanini alikataliwa kugombea uraisi mwaka 1995 na mambo mengine kem kem

Pamoja na kusoma haya maandishi yote nimekuja kugundua Nyerere hakuna na uhusiano mzuri na kikwete pamoja ya yeye mwenyewe kikwete anavyojitapa anapotembelea maeneo mbali mbali nje za nchi na jinsi anavyojifnaya kumwabudu nyerere .

Mwaka 1995 wakati wa kuchagua watu watakaogombea uraisi kwa tiketi ya CCM , majina mengi yalipelekwa lakini wa mwisho alikuwa ni Kikwete na jamaa wengine hakuna aliyekuwa anajua kama mkapa kweli atachaguliwa au la , nah ii ni kutokana na mkapa mwenyewe msimamo wako tokea akiwa mwanafunzi wa makerere , mwandishi wa habari mpaka alivyokuwa waziri historia yake ilimweleza ni mtu wa aina gani

Watu wengi haswa huko CCM walikuwa wanataka DAMU changa ambayo wanafikiri ingeendana na Mwinyi au tofauti kidogo ambayo ingeleta mapinduzi katika Nchi husika lakini hapo hapo nchi iendelee kuliwa kidogo kidogo .

Ndio hapa Nyerere aliingilia kati na kuamuru MKAPA agombee na kumwacha Kikwete solemba , Baba wa taifa alikiri mwenyewe hayuko tayari kumwona Kikwete akiongoza nchi wakati yeye akiwa Hai kwa sababu alishajua kile kikwete na jamaa zake wengine wanachotaka hichi ambayo wanakifanya sasa hivi .

Hapo tukampata mkapa , kwa kweli mkapa alifanya kazi na kubadilisha mambo mengi katika nchi hii , mpaka pale Nyerere alipoaga dunia , CCM ikawa haina mbabe , kigogo aliyebaki ambaye hakuonyesha kiburi wakati nyerere akiwa hai ni mkapa , hapo ndio mkapa akaanza kuwa mjasiriamali

Ndio historia ya Mkapa kufanya biashara wakati akiwa Bado kiongozi wa nchi inapoanzia ingawa alikuwa akifanya lakini kwa siri haswa na maswahiba wake wa Uganda na vigogo wengine aliosoma nao chuo kikuu cha makerere .

Kama nilivyosema hapo juu Mkapa ni mtu Mkimya lakini Jeuri sana , wakati nyerere akiwa hai alionyesha Ukimya wake na pengine nyerere asingefariki mkapa asingefanya hizo biashara na hujuma zingine ambazo amezifanya kwa nchi hii kwa sababu kungekuwa na mtu wa kumuuliza na kuhoji .

Mwaka 2005 ukafika mambo ya kuchaguana yakafanyika tena , wakati huu watu waliongezeka kidogo lakini ambao walivuta hisia ni Kikwete yule yule na Salim , kama unavyojua waandishi wetu wa kitanzania ni vipofu hawakuweza kuhoji wala kudadisi ni nini haswa kilimkosesha Uongozi kikwete 1995 ?

Bado waandishi wetu wa habari hawataki kutuambia ukweli waliendelea kumlamba kikwete miguu yake , kumsifia na kumpamba na mambo kibao ambayo hayana msingi wowote , kikwete aliweza kuwanunua mpaka wachungaji wa makanisa ambao tunawaheshimu wamsaidie kumpigia kura makanisani na misikitini .

Mbaya zaidi alifanikiwa mpaka kutengeneza ubaguzi wa rangi pale alipomtuhumu salim yeye ni mwarabu ,na mmoja wa ndugu zake ni offisa wa jeshi huko Arabuni , lakini la kutisha zaidi inasemekana kikwete alihusika na mauaji ya mmoja wa walinzi wa Salim huko Addis Ababa , sina uhakika kuhusu hili na waandishi wa habari wamejaribu kuficha sana kadhia hii .

Lakini faulo zake zilianza pale alipoanza kwenda Mwanza ndege imejaa babu zake wa bagamoyo , washirikina na wanga ambao walikuwa wanaenda nae safari nyingi kuhakikisha wanafanya mazingira mpaka apate ushindi hapo ndipo kasheshe zilipoanza .

Ni ukweli usio fichika kwamba Nyerere alishajua kabisa kwamba Kikwete sio chaguo la wananchi wala la mungu wala la mtu wowote alishatoa utabiri wake sema watanzania wengi sio wadadisi na sio wazalendo wangehoji tangia mwanzo

Huu ni mwaka mmoja na nusu , tangia kikwete raisi hajafungua barabara yoyote , hajafungua mradi wowote ule mkubwa na wala hajaafanya lolote la maana ambalo litamfanya akumbukwe hata akitutoka sasa hivi sijui ana malengo gani na nchi hii ?

Uwanja wa taifa ulitakiwa ufunguliwe toka aprili mpaka leo haujafunguliwa kwa sababu ambazo raisi anazijua mwenyewe , BOT makao makuu ilitakuwa ifunguliwe nayo mpaka sasa hivi hatujui nini kinachoendelea zaidi ya kashfa na bilali wake ambaye ni kiongozi pale BOT .

Ni kweli Nyerere alijua haya ?
 
Kikwete ana jibu fupi na zuri sana: "Kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala."
 
"KELELE ZA MLANGO HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KULALA"Sawa,Hata Sadam Hussein hakuwahi kufikiri kuwa angeishia hapo.
 
Pamoja na kuwa Nyerere hakumuunga mkono Kikwete mnamo mwaka 1995,Kikwete tayari alikuwa ameshajikita vizuri ndani ya chama na alikuwa na wafuasi wengi kama kura zilivyodhihirisha wakati huo.Mwalimu hakuwahi kutamka jambo lolote baya kuhusu Kikwete ukiachilia mbali kigezo cha umri ambacho ndicho pekee kwa wakati ulekilichotumiwa na Mwalimu. Siyo siri pia kuwa Mwalimu alimsifu sana Kikwete katika kukubali kwake kushindwa na kumwambia asubiri zamu yake.
Katika mwaka 2005 Kikwete alikuwa Tsunami,hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi kuliko yeye.Hii ilijidhihirisha kwa idadi ya kura alizozipata Chimwaga.
Ni dhahiri kuwa hata Mwalimu angekuwa hai asimgethubutu kwenda kinyume na nguvu aliokuwa nayo tayari amejipatia kwa wananchi.Sisi wengine tulikuwa kando tunatafakari na kuchunguza sifa za wagombea wote lakini hatukuona mtu ambaye angeweza kiukweli kabisa kupambana naye.Kikwete alikuwa kishajisafishia njia kwa sababu ya umahiri wake katika kushawishi na kujenga mahusiano na watu.Aliwavuta watu wengi na jumuiya nyingi zikiwemo makanisa,misikiti,wana ccm na jumuiya zake na hata watu binafsi kama mimi tulimuunga mkono mapema kabisa na kuweza kumpa ushindi mnono.Pamoja nahayo yote JK alikuwa na mahasidi hasa wafanya biashara wakubwa katika maeneo mengi ya nchi.Kwa hapa Mwanza watu wazito walijitahidi kuwashawishi wajumbe wa mkutano Mkuu wa uchaguzi wakiyamwaga mapesa yao ili kumsaga lakini kuna kitu ambacho hawa jamaa walikuwa hawakijui.Kikwete alikuwa tayari amejijenga kwa watu amabo tangu 2004 walikuwa tayari wamejiheasabu kama marafiki wa Jk.Hwa ndiyo waliokuja baadaye ku outsmart matajiri wa Mwanza na sehemu nyinginezo kwani mahusiano yao na wapiga kura.

Kuhusu mambo ya kubeba timu ya waganga na kuja nayo kanda ya ziwa
 
....kama imeanza tuambiane!

....ila haitafanikiwa,hilo wala halina ugumu wa kulifahamu!kama ilivyofahamika kitambo kuwa atakuwa rais!

....naona mchele umegaiwa watu wauchambue upikwe!

....nasubiri kula tu!
 
"KELELE ZA MLANGO HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KULALA"Sawa,Hata Sadam Hussein hakuwahi kufikiri kuwa angeishia hapo.

Swadakta! acha Saddam Hussein tuu, mnamkumbuka Ceausescu na 'nyodo' zake na ubabe aliishia wapi? Kelele za mlango na mwenye nyumba hashtuki? ANAKASORO HUYO.
 
Sasa Jamani Tufanyaje!!?

Hakujua haya!! Kwani Nyerere alikua na e-mail?
we Una fikiri Nyerere ange kuwepo hata hii Jamboforum ange ishitukia? au labda Ungekua rafiki Yake!!
 
Swadakta! acha Saddam Hussein tuu, mnamkumbuka Ceausescu na 'nyodo' zake na ubabe aliishia wapi? Kelele za mlango na mwenye nyumba hashtuki? ANAKASORO HUYO.

.............interesting
 
Sasa Jamani Tufanyaje!!?

Hakujua haya!! Kwani Nyerere alikua na e-mail?
we Una fikiri Nyerere ange kuwepo hata hii Jamboforum ange ishitukia? au labda Ungekua rafiki Yake!!


Umenivunja mbavu sana....
 
Wajumbe wenzangu,
Mara kwa mara nimekuwa ninasikia kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mjengaji mahiri wa hoja na kwamba hoja zake zilikuwa makini na mpaka leo bado zinahusika (relevant). Najua aliandika vitabu kadhaa ambavyo vinapatikana kiurahisi kama mtu unavitaka. Kitu ambacho hakipatikani kwa urahisi ni hotuba zake (video au audio). Nimejaribu kila kona ya kwenye mtandao lakini nimeambulia kidogo sana. Hata tovuti ya taasisi yake hawana nyingi na walizonazo zinachukua muda sana kuzishusha. Hata Youtube hawana!! Za Nkrumah na wengineo zinapatikana yuotube. Kuna mtu yeyote humu anayejua wapi zinapatikana? Na je Nyerere aliwahi kushiriki katika mdahalo wowote ule na kuwashinda washiriki wa huo mdahalo kwa hoja?
 
Wajumbe wenzangu,
Mara kwa mara nimekuwa ninasikia kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mjengaji mahiri wa hoja na kwamba hoja zake zilikuwa makini na mpaka leo bado zinahusika (relevant). Najua aliandika vitabu kadhaa ambavyo vinapatikana kiurahisi kama mtu unavitaka. Kitu ambacho hakipatikani kwa urahisi ni hotuba zake (video au audio). Nimejaribu kila kona ya kwenye mtandao lakini nimeambulia kidogo sana. Hata tovuti ya taasisi yake hawana nyingi na walizonazo zinachukua muda sana kuzishusha. Hata Youtube hawana!! Za Nkrumah na wengineo zinapatikana yuotube. Kuna mtu yeyote humu anayejua wapi zinapatikana? Na je Nyerere aliwahi kushiriki katika mdahalo wowote ule na kuwashinda washiriki wa huo mdahalo kwa hoja?

Naamini Radio Tz Dsm zitakuwepo. Jaribu ku-check nao.
AF.
 
Back
Top Bottom