Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

quars umesema maneno mazito na ndiyo maana hata Mwalimu alipo kufa pale St.Thomas London kutokana na enzi hizo za maisha yake na uongozi , Tony Blair went in Public kwenye TV na kusema Tanzania and Africa has lost the leader of his time .Kwa wakati ule maamuzi ya Mwalimu yalikuwa sawa maana kama angaliachia leo mafuta na guess na mbuha zetu kungalikuwa hakuna kitu . Azimio lilikuwa na maadili ya uongozi na watu walili ogopa.Ule ndiyo uzawa wenyewe . Hapo Amsterdam kaonanen na Prof June wa Political science Dept atakuelezea ujamaa na jinsi anavyo tushangaa watanzania kwamba tumeachana na habari za Mwalimu. Niliwahi kufika hapo nasema vitabu vya Mwalimu mpaka Hotuba zake zote zimelala pale watu wanachimbua .Leo mnasemaje ?
 
MzeeShughuli Bwana,
Hawa viongozi wa sasa wanajiona wajanja. Walishamzika Mwalimu na siasa zake. Sasa wanakula sahani moja na wale waliokuwa wanatunyonya. Ili mradi wao wanapokea 10% au 30% zao hawajali kabisa. Madini yanakwenda, mbuga zinakwenda na sisi tunabaki wakata kuni na wachota maji kwa niaba ya wawekezaji. Si unamwona Mwungana akiwa bize kutafuta wanyonyaji?
 
azimio la arusha lina sehemu mbili: ya kwanza, ni suala zima la maadili ya viongozi. sehemu ya pili, inahusu uendeshaji uchumi, pamoja na umiliki wa njia kuu za uchumi. kila kipengele hapo kinamuathiri mwenzake.

Hivi miaka 18 ya utekelezaji wa azimio la arusha haikutosha kuweka misingi imara ya kulilinda? Nyerere ndiyo alikuwa incharge, akisaidiwa na mfumo wa chama kimoja. Kwanini alishindwa?

Naomba tujadili makosa yaliyotokea wakati wa utawala wa Baba wa Taifa. We can not claim that everything was perfect.
 
Joka kuu, kushindwa kwa kitu haina maana ni kibaya ila watu waliotakiwa kukisimamia na kukitekeleza walikuwa na ubinafsi sana, ambao tunaendelea kuuona hata leo, kuliko uzalendo.Na lazima tukumbuke kuwa Ujamaa(likiwemo AR)havikupewa nafasi kufanya kazi na ubepari (ikiongozwa na Marekani) ili vifanye kazi yake.Lakini vilipigwa vita kwa kuwatumia CIA(Mobutu),IMF na World Bank.
 
Nyangumi,
wakati wa nyerere tanzania ilikuwa moja ya nchi zilizoongoza kwa kupata misaada mingi toka nje. ndiyo marekani walikuwa hawapendi ujamaa, lakini wapo wengi waliokuwa na nia nzuri na nchi na siasa zetu.

robert mac-namara aliyepata kuwa raisi wa world bank alikuwa rafiki mkubwa wa baba wa taifa. kwa msingi huo basi kipo kipindi ambacho world bank ilikuwa ikimsaidia nyerere kutekeleza sera zake za ujamaa.

baba wa taifa alikuwa na miaka 18, toka 1967-1985, kulitekeleza azimio la arusha na siasa ya ujamaa na kujitegemea. je, kwanini alifeli? haitoshi kulaumu watekelezaji tu. baba wa taifa ndiyo alikuwa msimamizi mkuu. je, huyo hastahili lawama?

kama ujamaa ni mfumo bora na tena imara, kwanini utegemee huruma za mabepari[usa,cia,...] ili uweze kufanya kazi? wajamaa nao si walikuwa na vyombo vyao kama KGB,Stasi,...? mataifa yote ya kijamaa yamesambaratika!! kulikoni???
 
jasus na mzee shughuli bwana nashukuru kwa maneno yenu ya kunitia moyo,
mimi ninachosema hapa viongozi wetu wenye nia nzuri na taifa letu lazima tuwape sifa wanazostahili hata kama mafanikio yao hayaonekani moja kwa moja.
baba wa taifa pamoja na kuwa hakuweza kututoa kwenye umaskini alikuwa na nia nzuri kuona watanzania wanaishi kwa amani,upendo na umoja.
na hii imetutofautisha na mataifa mengi ya afrika,
hii tanzania ambayo wazungu waliipiga vita leo hii wanaitegemea kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuja kupumzika kwa holidays na vilevile wanaitegemea tanzania katika kutatua migogoro katika eneo la maziwa makuu.

nakubaliana na kuwa kuna haja hasa kwa sisi watanzania kufanya utafiti wa kina kwanini siasa ya ujamaa ilishindwa kutuondoa kwenye wimbi la umaskini,
there is internal factors as well as external factors. na mimi bado naendelea kufanya utafiti wa hili.
 
Mwl. Quarz, tafadhali endelea kutupa somo!
Kuna mengi tunayohitaji kujifunza kuhusu Azimio la Arusha!
Mimi binafsi nasubiri kwa hamu matokeo ya utafiti wako!
 
quars

Hatukupiga hatua toka kule kwa kuwa wale walio kuwa na mwalimu bado walikuwa na njaa ku implement mambo yale kwa Taifa was never their priority ila kuwaza namna ya kumpiga chenga Mwalimu na kujishibisha kwamba . Wakati Mwalimu walikuwa Mzalendo haswa akiwa na nia njema watekelezaji wao walikuwa wanasikilizia wapi wakaibe kwanza . Tatizo hilo ni kubwa sana hadi sasa si Tanzania pekee bali Africa . Uzawa, uzalendo haupo . Mzungu ni rafiki yako nje ya kazi na ukiingia kwenye anga zake na anajua sheria inasemaje anakusomea tu na kukuacha uamue . Sisi Kinana na sijui na Ngasongwa wanaenda kumpokea mwekezajoi hata watumishi wake wanakosa nafasi ya kumtoa airport kweli tutaondoka hapa ?

Vizazi vijavyo if we are not careful vitakuwa na swali kama lako Quars kwamba why we never moved .
 
JokaKuu,
Miaka kumi na minane is a drop in the bucket. Marekani walipata uhuru 1776. Waliamini "all men are created equal," lakini ilichukua zaidi ya miaka 170 kwa akina Martin Luther King Jr. kutokea na kuanza kusuta kutotekelezwa kwa kanuni hiyo ya "equality." Na ni leo tu ndugu zangu weusi wanajiona kuwa nao ni "equal." Mwalimu aliweka misingi. Lakini hata kabla ya misingi hiyo kuimarika wakatokea wajanja akina Mwinyi na azimio lao la Zanzibar. Badala ya ku-adapt the good parts of Arusha they threw the whole concept in the Indian ocean. Ndiyo maana leo tunaongozwa na wezi na wababaishaji.
 
Jasusi, we do still have a dream!
A dream that all men are created equal...!
Sounds like Martin Luther King Jr alikuwa anagelezea kutoka kwenye Azimio la Arusha... oops.. au Mwl Nyerere aligelezea misingi ya usawa toka kwa MLK Jr?
Lool!
Tuendelee kupiga kelele tu, iko siku tutasikiwa!
Tusipopiga kelele sisi, tutakuja kubezwa na kuzomewa na vizazi vijavyo!
Aluta continua!
 
Jokakuu,

Unajua swali hili la mikopo ya Nyerere nakumbuka kuna mtu aliwahi kuuliza kule bcstimes.
Kitu ambacho wengi tunashindwa kuelewa hadi leo ni kwamba urithi tuliokuwa nao ni asilimia 75 ya urithi wote umejengwa na Nyerere. Urithi ambao jana Mkapa kauza na kujisifia kwa mabillioni tunayotangaza kwa wananchi. Hizo IPTL, NBC, ATC, hayo ma dam ya Umeme, Tipper na nyingine kibao zote zilijengwa na mikopo hiyo hiyo mnayouliza ilitumika vipi.
Kwa mfanya biashara yeyote anafahamu kuwa Unapojenga nyumba ya kuangisha hupoteza mafedha kibao, sasa inapofikia biashara ya kupata wapangaji hilo ni somo jingine kabisa...
Kibaya hapa wengi mnatazama hesabu ya wapangaji bila kujiuliza hizo nyumba zimesimama vipi.
Hata ktk swala la ustawi wa jamii tazameni mfano wa nyumba miaka aliyotawala Nyerere kajenga nyumba nyingi za National housing kuliko vipindi vyote vya Mwinyi na Mkapa...Na kifupi hakuna kipya kilichojengwa na Mwinyi wala Mkapa chenye hadhi ya kimataifa, hata hizo barabara mpya mzazojisifia ni vichekesho vitupu huwezi kulinganisha na highway za Kenya ama Uganda zilizojengwa 1980's.
Where he failed ndio hivyo kama China waliweza kuwa na kila kitu cha serikali yao na waliweza kujitegemea kabisa lakini inapofika ktk biashara hilo tena somo jipya. - walishindwa kama sisi. Milango ilikuwa imefungwa, bad policy za kiuchumi.
Mimi naamini kabisa kuwa unaweza kuwa na milango wazi na bado ukaendeleza azimio la Arusha. nchi za Nordic na China hadi leo wana maazimio kibao ambayo ukiyasoma hayana tofauti kabisa na hayo ya Nyerere na nchi hizi zinapiga hatua kishenzi. Isipokuwa sasa hivi China kidogo wanaanza kujisahau (fedha imenoga) , gap kati ya matajiri na maskini inaanza kujitokeza tena kwa kasi ya ajabu.
Kisha nitarudia kusema Azimio la kitaifa sio kabisa mfumo wa chama ama sera za chama hata kidogo. Naweza kusema kuwa Canada ni nchi ya kibepari lakini utakuta baadhi ya majimbo yake yame/naongozwa na vyama vyenye mrengo wa kushoto. Ontario iliwahi kuongozwa kwa miaka kisha leo hii zipo manitoba na saskachewan. Ubepari bado umesimama pale pale pamoja na kwamba maazimio kama hayo yapo.

Kama alivyosema ndugu yetu Quarz, kuna tofauti kubwa sana kati ya Capitalism ya Ulaya na kwetu Afrika. Hawa wenzetu wanao matajiri tayari ndani ya nchi zao na siasa hizi mbili zinawahusu na kuwatazama wao sio kwetu Afrika unapozungumzia Capitalism unatazama nje wageni wenye mitaji (wawekeshaji) kuingia ndani.
 
Mkandara kumbe wewe kiboko kweli. Unaweka mambo yaonekane wazi. Huwa sielewei kwa nini waswahili wengi hatuoni mambo kwa mbali vile. Kushindwa kwetu kuona mbali ndiko kunakotufanya tutumiwe na wazungu kila siku.
 
kichuguu

Mkandara ni mwalimu mmoja mzuri sana.

Yaani mtu akishindwa kumwelewa Mkandara basi hawezi kumwelewa mtu ye yote. Halafu Mkandara ana mifano yake hiyo ambayo huburudisha na kufanya mada ieleweke zaidi.
 
Mkandara,
naunga mkono maelezo yako. lakini ninayo haya ya kuongezea:

baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki tanzania iliingia ktk zoezi la kuanzisha viwanda vyake yenyewe. kiongozi aliyepewa jukumu hilo nakumbuka alikuwa cleopa msuya.

walioandaa industrial master plan ya tanzania naamini kabisa walikuwa wachapakazi wazuri na walikuwa wanajua wanalolifanya. tatizo hawakupewa nafasi ya kufanya kazi yao kwa uhuru.

tatizo letu tuliingiza siasa ktk kuendesha uchumi. mameneja waliteuliwa kisiasa. chama kilishika hatamu na kuingilia katika maamuzi ya kiufundi na kiutaalamu ktk uendeshaji mashirika yetu.

matawi ya ccm wakati mwingine yaliwalinda wafanyakazi wazembe na wahujumu wa mashirika na viwanda tulivyoanzisha. nidhamu ya kazi na tija viliathirika sana kutokana na majungu ya ccm ndani ya haya mashirika yetu.

mara nyingine siasa iliingilia mpaka ni wapi kiwanda kijengwe. mfano wa siasa kuingilia maamuzi ya wataalamu ni kujengwa kwa kiwanda cha kukata almasi iringa!!

siasa chama zililazimisha mashirika haya kuingia maamuzi yasiyo ya lazima. mfano mzuri ni kudhamini mikutano ya chama, timu za soka,vikundi vya ngoma na bendi za muziki n.k.


matawi ya chama yalikuwa kama menejimenti ya pili katika haya mashirika. huo ulikuwa ni mzigo mkubwa wa gharama. kiongozi wa chama alipojisikia hamu ya kuku, au mbuzi, basi aliamua kutunga ziara kutembelea shirika la mifugo. na alipofika huku basi walimpa mbuzi watano, au hata kuku hamsini!!
ilizuka tabia ya mameneja, ili kulinda ajira zao, wakaanza kutoa zawadi na kuwakarimu viongozi wa chama.

wale waliopewa jukumu la kuendesha uchumi, wakina mtei,msuya,rweyemamu,...walipiga kelele kuhusu chama na siasa kuingilia utendaji wa mashirika ya umma. tatizo lililojitokeza ni Nyerere na kikundi fulani cha wakereketwa wa chama kukataa ushauri wa kitaalamu, na wakati mwingine hata kuanzisha hujuma na majungu ya kisiasa dhidi yao.

mgongano huo nilioueleza hapo juu ndiyo uliosababisha: kwanza ,mashirika yetu kudorora; pili; mapato ya serikali yakashindwa kuhimili matumizi yake. wataalamu wakamshauri tena Nyerere apunguze, kwa muda, matumizi ya serikali yake, na akaribishe mitaji toka nje. Nyerere alikataa vyote hivyo. Matokeo yake wafadhili wakatugomea, nchi za Nordic zilichelea kidogo, lakini nazo zikagoma kutusaidia kwasababu Nyerere aligeuka "haambiliki."

Nyerere alishauriwa ayabinafsishe haya mashirika kwa masharti yake yeye mwenyewe. Kama alikataa mpaka yakafikia kuwa magofu ni nani wa kulaumiwa? Hizi lawama ni zake Nyerere. Alipoondoka nakumbuka hazina ilikuwa imekauka na aliyetuokoa ni Robert Mugabe. Meli za mafuta ziligoma kupakua mzigo kwa sababu nchi ilikuwa mufilisi na haiaminiki tena.

Mwalimu ndiye aliyepaswa kurudisha nidhamu na ufanisi katika kuendesha mashirika yetu. Kwa bahati mbaya aliyafumbia macho au kuyaonea aibu matendo ya hujuma yaliyokuwa yakiendelea.

Mwalimu ndiye aliyepaswa kusitisha tabia ya wakereketwa wa chama kuingilia menejimenti za mashirika ktk kufanya maamuzi ya kibiashara.

Mwalimu vilevile alipaswa kuwa jasiri na kukubali ushauri wa kukaribisha mitaji toka nje, at the time when he could enforce discipline and ethics.

WE HAD A CHANCE TO ATTAIN ECONOMIC DEVELOPMENT AND WE SQUANDERED IT. UNFORTUNATELY, OUR BELOVED MWALIMU WAS AT THE CENTER OF IT.
 
Jokakuu,

Nakubaliana na wewe kwa yote uliyosema. Ila nasisitiza kuwa swali halikuwa uwezo wa Nyerere kupata wapangaji wa nyumba aliyojenga!... hoja ilikuwa kwa nini tulishindwa hali Tanzania ilichukua mikopo mingi sana wakati wa Nyerere?..Mimi nimeonyesha tu wapi mikopo ile imekwenda... sio jinsi mikopo ile ilivyoweza kuleta wapangaji ndani ya nyumba yetu..

Mikopo ilijenga mali zote ambazo leo Mkapa anataka muamini kuwa yalikuwa magofu!.. sijaona gofu likinunuliwa kwa mabillioni ya fedha bila kupelekwa museum kwa maenyesho. Kila alichojenga Nyerere kililala kibiashara kama China walivyolaza viwanda vyao. Gofu haliwezi kusimama tena kwa mguzo zake zilezile!.. Hotel ya Kilimanjaro isingefanyiwa Ukarabati kama ilikuwa gofu, IPTL,NBC,ATC, UFI Urafiki, Mwatex nambie hata kiwanda kimoja kilichouzwa na leo hii wamebadilisha kila kitu ama kutumia kiwanja peke yake?... hakuna hata kimoja!
Kwa hiyo hizo habari za magofu ni habari za Mwinyi na Mkapa kuwafungeni kamba huku wao wakichuma hizo 10%.

Je, hata mbuga zetu zilikuwa magofu maanake zinauzwa pia kwa visingizio kuwa zimeshindwa kujiendesha.
Ni kweli kabisa Nyerere alishindwa kibiashara. Alishindwa kupangisha nyumba aliyoijenga kwa Ubishi wake na kila tusi linaloweza kusemwa linamstahili ktk kipande hiki tu cha biashara na binafsi nasema policy za biashara kidunia pia zilikuwa mbaya sana.
Yet, still mali zote zilikuwepo safi zimesimama baada ya vita baridi ya kisiasa. Tulitakiwa sisi tumwonyeshe yeye jinsi gani ilitakiwa kupangisha nyumba hizo badala yake sisi tumeziuza na leo hii sisi ndio wapangaji!...tunakula mtaji na mirathi ya baba zikisha benki tumekwishaaa!..
 
Jokakuu,

Nakubaliana na wewe kwa yote uliyosema. Ila nasisitiza kuwa swali halikuwa uwezo wa Nyerere kupata wapangaji wa nyumba aliyojenga!... hoja ilikuwa kwa nini tulishindwa hali Tanzania ilichukua mikopo mingi sana wakati wa Nyerere?..Mimi nimeonyesha tu wapi mikopo ile imekwenda... sio jinsi mikopo ile ilivyoweza kuleta wapangaji ndani ya nyumba yetu..

Mikopo ilijenga mali zote ambazo leo Mkapa anataka muamini kuwa yalikuwa magofu!.. sijaona gofu likinunuliwa kwa mabillioni ya fedha bila kupelekwa museum kwa maenyesho. Kila alichojenga Nyerere kililala kibiashara kama China walivyolaza viwanda vyao. Gofu haliwezi kusimama tena kwa mguzo zake zilezile!.. Hotel ya Kilimanjaro isingefanyiwa Ukarabati kama ilikuwa gofu, IPTL,NBC,ATC, UFI Urafiki, Mwatex nambie hata kiwanda kimoja kilichouzwa na leo hii wamebadilisha kila kitu ama kutumia kiwanja peke yake?... hakuna hata kimoja!Kwa hiyo hizo habari za magofu ni habari za Mwinyi na Mkapa kuwafungeni kamba huku wao wakichuma hizo 10%.

Je, hata mbuga zetu zilikuwa magofu maanake zinauzwa pia kwa visingizio kuwa zimeshindwa kujiendesha. Ni kweli kabisa Nyerere alishindwa kibiashara. Alishindwa kupangisha nyumba aliyoijenga kwa Ubishi wake na kila tusi linaloweza kusemwa linamstahili ktk kipande hiki tu cha biashara na binafsi nasema policy za biashara kidunia pia zilikuwa mbaya sana.
Yet, still mali zote zilikuwepo safi zimesimama baada ya vita baridi ya kisiasa. Tulitakiwa sisi tumwonyeshe yeye jinsi gani ilitakiwa kupangisha nyumba hizo badala yake sisi tumeziuza na leo hii sisi ndio wapangaji!...tunakula mtaji na mirathi ya baba zikisha benki tumekwishaaa!..

Kwa post hii na ile iliyotangulia nasema this is 'The' Mkandara I know. Nimeweka 'the' kuonyesha msisitizo. Watu weusi tu wepesi mno wakusingizia historia. Kila kufanya vibaya kwetu utasikia watu wanaanza kuleta historia. Mara utumwa, mara ukoloni, mara Nyerere yaani almradi visingizio kibao. Ati leo Nyerere ni sababu ya kufali kwetu wakati enzi zake walau tulikuwa na shule, zahanati, viwanda kwa maana halisi ya misamiati hiyo.
 
Duuuuh,
Shukrani wakuu maanake hizi sifa sii rahisi kuzipata hasa toka kwa wachambuzi wakubwa wa hizi hoja!... kama vile nimesikia matokeo ya mtihani wa A level vileeee...Mkandara - chuo Kikuu!
 
Nani kakwambia unaenda Chuo Kikuu cha bei nafuu?
Mkandara.. Harvard!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ndio umuhimu wa forum hii. Kila mtu anasaidia kuchangia na kufundisha Watanzania wenzake. Mkandara, heko kwa umahiri wako, JokaKuu vile vile nakupongeza kwa mchango wako. Tuendelee kukata issues.
 
kichuguu

Mkandara ni mwalimu mmoja mzuri sana.

Yaani mtu akishindwa kumwelewa Mkandara basi hawezi kumwelewa mtu ye yote. Halafu Mkandara ana mifano yake hiyo ambayo huburudisha na kufanya mada ieleweke zaidi.

Hapo ume-sum up vizuri about MK. Huyu jamaa ni kiboko. Ushauri wa bure kwa JK:Mtafute huyu jamaa awe mshauri wako. Nakumbuka tangu enzi za BCS original (BCS iliwahi kufungwa mara mbili kabla ya kufungwa mara ya tatu for good) jinsi alivyokuwa akishusha vitu. "Kibano" alichomshushia Mtukwao sijasahau mpaka leo🙂 Sijui Munishi ameishia wapi jamani? Aliahidi kugombea uraisi..Time flies.
 
Back
Top Bottom