Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Tunapojadili siasa za Nyerere ni budi tuangalie na wakati wenyewe na vilevile kutizama kwa undani Nyerere alikuwa ni mtu wa namna gani. Alikuwa ni mwalimu, alisoma historia na kwa hivyo alielewa misingi ya utawala na sidhani kama alikuwa mchumi, lakini aliweza kuuelezea uchumi kuliko hata baadhi ya wachumi wenyewe. Nakumbuka katika hotuba zake aliwaelezea wakulima wa pamba kule kanda ya ziwa kuwa ili kununua lori moja la isuzu tani 7 tunahitaji tani 7 za pamba. Hii iliweza kumwelewesha mkulima aongeze juhudi katika uzalizaji wa pamba. Leo hii tunapojadili siasa za Mwalimu tunaangalie theory za uchumi na siasa kuliko mambo halisi yaliyokuwapo wakati ule. Ghana ilianza kupata uhuru na viongozi wengi wakati huo walimadmire na kumsikiliza Kwame Nkurumah. Kwa kweli viongozi hawa wa post-independence Africa wasingeweza kuleta maajabu ila walituwekea misingi (mizuri au mibaya). Wengi tunawakumbuka waandishi wa vitabu wakati ule kama akina Cyprian Ekwensi, walikuwa wakiandika mbali na mambo mengine juu ya viongozi wakati ule waliosoma ulaya na wakaja kuziongoza nchi zao (akiwemo Nyerere) katika hali ya uchanga kabisa. Binafsi nilielewa vizuri wakati ule kwamba ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora kuliko sasa hivi ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya.
 
Kwanza hasanteni nyote mliochangia mada hii. Inanipa mori kutembelea hapa na kusoma mada zinazoelimisha badala ya kusoma vilio na malalamiko dhidi ya serikali na viongozi wake kila kukicha kana kwamba hatuna mambo mengine tunayoweza kuyaongelea. Binafsi, sina muda wa kujadili siasa za minong'ono, conspiracy, na facts za vijiweni.

Pili, kama alivyosema jemedari Mkandara, admin wa hii forum kaamua kukosea kwa makusudi: Kahamisha mada ya siasa kwenda kwenye uchumi; labda kwasababu haina vilio dhidi ya viongozi!!

Sasa nirudi kwenye mada. Siasa ni kilimo ni phrase ambayo mwalimu aliitumia sana katika hotuba zake, na nakumbuka hata vitabu kadhaa vya kiada vya shule ya msingi vilinukuu phrase hii. Definitions za siasa ziko kadhaa lakini hakuna moja inayowiana na hii phrase, hapa ndipo ninapokanganywa!!

Jingine ni hili la watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Hapa nina maswali mengi (i) Je vitu hivi vinne vinajitegemea au lazima viwapo vyote kwa pamoja ndipo nchi iendelee? Kwa mtazamo wa haraka sidhani kama vitu hivi vinajitegemea kwasababu, lazima kuwe na ardhi ndipo kuwe na watu, lazima kuwe na watu + ardhi, ndipo kuwe na siasa (aidha siasa chafu au safi). Lazima kuwe na watu + ardhi + siasa safi, ndipo kuwe na uongozi bora, maana hakutakuwa na uongozi bora pasipo siasa safi, kadhalika kusingekuwa na uongozi bila siasa.

Kwa mantiki hii, ardhi na siasa safi tunaweza kuviondoa kwenye list kwasababu watu watakuwapo tu endapo kuna ardhi, na 'siasa safi' itakuwapo tu endapo kuna 'uongozi bora.' Vinavyobakia ni watu na 'uongozi bora', hivyo basi mwalimu ange make sense kusema ili tuendelee tunahitaji 'uongozi bora'.

(ii) Aliposema siasa safi alimaanisha nini? Siasa safi ni siasa za namna gani? Do we have transferable 'siasa safi'? Nchi gani ina siasa safi? Kiongozi gani ana siasa safi? Siasa safi zinapimwa kwa kigezo gani?

(iii) Uongozi bora ni uongozi wa aina gani? Nchi ipi leo ina uongozi bora? Ubora huu unapimikaje? Je kipimo cha ubora, kama kipo, ni universal?

Maswali haya kwapamoja yanaunda swali moja kuu: Je kusema kwamba ili nchi iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, ni development theory?
 
Heshima kwa wote,

Wakati ndugu zangu wa CCM wanajiandaa kutumia mamilioni mengine (nadhani haitafika mabilioni) nadhani ni wajibu wangu kuwakumbusha wanajambo kitu muhimu ambacho utanzania wa sasa usingependa kikumbukwe.

Siku ya tarehe 5 februari 2007 wale tunaoamini umuhimu wa Tanzania "ya kizamani" kama wzasemavyo wenzetu waliouvaa usasa, tunapaswa kuadhimisha miaka Arobaini (40) tangia Kutangazwa kwa Azimio la Arusha.

Mazingira na mahitaji ya nyakati hizi yanaongeza umuhimu wa kwetu sote kujaribu kukutana kwa njia mbalimbali kutafakuru hali ya Tanzania yetu kwa kukumbuka tamko hilo ambalo pamoja na Ahadi Kumi za TANU ndizo zimejenga utanzania ambao hadi leo tunafaidika nao.

Makamarade wa mlimani, Kaka Shivji na wengine wanategemea kufanya maadhimisho makubwa ya siku tatu.

Nasi sote tunawajibu wa kuanzisha mjadala humu ndani na katika maeneo mengine kuhusu undani, mafanikio na changamoto ya Azimio la Arusha ambalo mimi binafsi naamini ndilo limeweza kutulinda na madhara ya unyang'au unaojitutumua miongoni mwetu na ndio pekee unaoweza kutukumbua kutoka kwa changamoto tunazopambana nazo wakati huu na tunazo kuja kupambana nazo hapo baadae

Kama wasemavyo waheshimiwa sana wa nchi yetu,

Nawasilisha hoja

Tanzanianjema
 
Mwalimu Nyerere alisema kuwa alikuwa anatembea na kitabu cha Azimio la Arusha na hadi anakufa hakuwahi kukikana! Ukweli wa hoja zake ulikuwa bado dhahiri. Licha ya mapungufu ya hapa na pale wazo lake bado linasimama!! CCM wa leo hawawezi kuangalia kijitabu hicho bila kuona haya!!
Kwa vile wana CCM wengi na vijana wengi wa miaka hii wameanza kulisahau Azimio Hili bado nimeambatanisha hapa ili kuwakumbusha: Labda kwa kuwadokeza tuweke hapa Imani ya Tanu ambayo wale wa kizazi kama changu watakumbuka jinsi tulivyolazimka kuikariri!!

Kwa kuwa TANU inaamini:-
(a) Kwamba binadamu wote ni sawa;

(b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;

(c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
Mikoa hadi Serikali Kuu;

(d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;

(e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa
mujibu wa Sheria;

2
(f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
kutokana na kazi yake

(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
kwa vizazi vyao;

(h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
muhimu za kuukuza uchumi; na

(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
na siasa ya watu wote kuwa sawa.
 

Attachments

(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
kwa vizazi vyao;

kweli nani amfufue mchonga ,hapa anatuambia utajiri wetu kwa pamoja ni wetu woote wadanganyika,kama kifungu hapo juu kinavyosema,lakini sasa angalieni uongozi wa leo unavyofuja utajiri wetu sisi tunambulia 3%
bora mwalimu alikataa akasema utajiri wetu hauozi,tusubiri wazalendo waweze kuchimba.leo hii kule mererani,mara,buhemba na kwingine ni vilio tu ,nchi yoote mali asili inaporwa ,,shamba la babu!!!

AZIMIO LA ARUSHA LILIHITAJI MABADILIKO KIDOGO TU,ukiangalia AZIMIO LA ZANZIBAR ni kinyume cha la arusha ...nani ana azimio la zanzibar atuwekee hapa?
 
This is pathetic, very pathetic.

Labda mimi sijui historia ya nchi yangu, lakini natambua kwamba failure moja wapo ya mwalimu ilikuwa hili Arusha Declaration (AD) ambalo kwa mawazo yangu ni taboo kuliongelea. Taboo kwasababu limeifanya Tanzania iwe masikini wa mwisho duniani na kudumaza business class ya wananchi huku ikisababisha kushamili kwa magendo na rushwa baina ya viongozi wa utawala wa mwalimu na wajanja wachache wenye asili ya kiasia.

AD ndio lililodumaza ujasilimali kwa kunyang'anya mali muhimu za wajasilimali waliokuwa wameanza kuchipuza baada ya uhuru. Mwalimu akatulazimisha tuwaite wajasilimali hao "makupe" "wanyonyaji" "maadui wa ujamaa" "mabepari" na majina chungu mbovu, yaliolenga ku dismantle capitalist class. Matokeo yake, wajasilimali wakawa na option mbili tu: kutekeleza AD, au kuondoka nje ya nchi. In fact tunaweza kusema kwamba hizi hazikuwa options bali ni nia haswa ya Nyerere.

AD ndio iliyowapa wahindi wajanja utajiri na kuifanya Tz iwe na rotuba ya Rushwa. AD ndio chanzo halisi cha rushwa Tz, rushwa ambayo hadi sasa imeota mizizi na kunawiri. Wakati mwalimu ananyang'anya mali za watu binafsi na kufanya kila bihashara iwe bihashara ya umma, huku akizuia ulimbikizaji binafsi wa mali, wajanja (wakiwemo viongozi wake) wakawa wana illegal monopoly za production and distribution of goods and services. Yani hapa AD ikaandaa mazingira safi ya rushwa.....Nyerere nazani hakusoma "game theory" kabla ya kutangaza AD. Maana siasa za ujamaa na AD zinaendeleza nchi tu pale kila kiumbe anapo conform na siasa hizi, any deviation kwa wachache ni bingo kwao.

Baada ya AD kuzaa rushwa, mwalimu akaona akaze uzi kupiga vita rushwa ambaye yeye mwenyewe ni mjenzi, ndipo Moringe wa Sokoine alipouawa kiajabu ajabu, katika jitihada zake za kukomesha rushwa. It is very dangerous and difficult to destroy what you had created, for you created to last. Nyerere alipoona moto alioanzisha unamshinda kuzima, akaamua kubwaga manyanga chini na badala yake ku focus kwenye vita vya uhaini na kutunza amani. Polepole lugha ya AD ikawa inafifia, na vita dhidi ya rushwa ikazikwa pamoja na Moringe Sokoine, wajanja wakafungua champagne kusherekea.

Kila mwenye uchungu na nchi yake hapaswi kutonesha madonda ya AD. Wale tulio wanyang'anya mali na kuwaita "makupe" sasa tunawabembeleza waje na tunawaita "wawekezaji" na kuwapa kila kivutio. AD inanikumbusha mbwa wangu pale kijijini, kipindi cha mavuno na uwindaji tunapobahatika kula "simba na yanga" (wali kwa nyama ya swala) na mbwa kumrushia mifupa iliyoambatana na minofu, mbwa wetu alikuwa na tabia ya kusambaza kinyesi bila utaratibu. Tukawa tunamuadhibu kwa viboko na kutompa chakula, the less we knew, mbwa alikuwa anakula kinyesi chake alipokosa chakula. Kinyesi alichokisambaza kilikuwa chakula adimu wakati wa njaa. Kadhalika AD Tz, tuliwafukuza capitalist class na sasa tunakula kinyesi chetu. Tunawaimbia nyimbo zote nzuri na kuwapa kila kishawishi waje....pale kijijini kwangu tabia hii tunaita "upumbavu wa mbwa wa kula kinyesi chake."

Leo hii tunawaita wawekezaji huku tunawapiga vita wawekezaji kutoka nje kwamba wanatuibia. Kwanini wasiibe? Kwani wawekezaji ni maparoko? Lakini tujiulize, kama tusingewafukuza wawekezaji wetu kama tulivyofanya wakati wa AD hivi leo tungeomba wawekezaji wa nje? With all due respect to Mwalimu (r.i.p) the AD failed us completely. If anything it made us so dependent on the government, it also discouraged business initiatives for our own good.

Sasa tunaposema ati turejee kwenye AD kwakweli mimi inanishangaza mno. Maana AD ndio ulikuwa mwanzo wa rushwa, ubepari, na hatimaye umasikini wetu. Hizo nguzo za AD mnazoziongelea ni sawa na sheria za ndoa ambazo hazina policy wa ku-reinforce. (i) Nguzo inayosema binadamu wote ni sawa, ni nguzo ya kisheria (legal right), wala sio nguzo ya kiuwezo. Mbona AD haisemi kwamba binadamu wote wanauwezo sawa? Mana uchumi na access to public services inakuwa determined na uwezo, wala sio nguzo ya kisheria...hivyo basi kama hakuna policy inforcement, huwezi ku-ntranslate legal right iwe economic equality.

(ii) kwamba kila mtu anastahili heshima...do we have policy enforcement on this? Nani alifungwa kwa kuto mpa heshima mwenzake? (iii) Uhuru wa kutoa mawazo yake....mbona waliokuwa na mawazo ya mfumo wa vyama vingi wakati wa AD waliitwa wasaliti? (iv) malipo ya haki kutokana na kazi yake....mbona wakulima wa mazao walikuwa wanalipwa bei ya hasara? (v) Kwamba raia wote ni wamiliki wa utajili wa nchi.....if so, how do we deal with the problems of public goods? Do we have enforcements with regards to this? Je kumiliki huku ni kwa lazima?

Ukiangalia nguzo zote utagundua kwamba ni virutubisho tosha vya rushwa na umasikini, maana zinapeleka madaraka makubwa kwa viongozi kwa kisingizio cha manufaa kwa jamii. Huu ni upumbavu husiopimika, show me people's empowerment in AD.
 
mgonjwa wa ukimwi,
hapa umenivuta hata na mimi niliyekuwa pangoni,
kwanza ningependa kukufahamisha mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na seminar nchi moja ya ulaya ikijadili kuhusu siasa ya ujamaa na azimio la arusha,
actually walikuwa wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kuchukua mambo waliyoona yana wafaa kutoka kwenye ujamaa na azimio la arusha ili waweze kuimplement kwenye policy zao, na believe me or not at this time siasa ya jamaa is among a hot topic in western countries na inaingizwa katika mitaala ya wanafunzi wa chuo, watu wana fanya reseach kuangalia ni jinsi gani ujamaa ulishindwa kuinua hali ya maisha.

sasa nikianza kujibu hoja zako,
i am sorry to say that you must be "crazy"
you should never put yourself in the level of julis nyerere ,incourruptible,humble,a true son of tanzania and a hero of africa, much respected in the world to date.
utakuwa mtu wa ajabu sana kumlaumu mwalimu kwa kutaifisha mali za umma,
kumbuka mwalimu alikuwa na vision, na vision yake ili kuwa ni kuwaona watanzania wenyewe taking charge of their own country,
hivi kungekuwa na maana gani ya kupata uhuru halafu uchumi unashikiliwa na watu weupe, basi haina maana ya kuwa na huo uhuru, ni bora tungekubali kuendelewa kutawaliwa.
swali ambalo mwalimu alishwawahi kuulizwa "kama watanzania hawakuwa tayari kujitawala kwanini uliharakisha kupata uhuru??"
mwalimu akawajibu kuwa wajerumani na waingereza wametutawala zaidi ya miaka 60 lakini wametuachia wahandisi wawili na madaktari wasiozidi 5, sasa mnataka tusubiri kwa mda gani zaidi??
zaidi ya hapo kumbuka mapambano ya kudai uhuru ilikuwa sio Ambition ya mtu kutaka madaraka bali ilikuwa kitu kutoka ndani, watu waliona wananyanyasika kwenye nchi yao, wanafanywa watumwa kwenye nchi yao, na wao kama binadamu mwingine yeyote mwenye akili lazima wajikomboe,
baada ya kupata uhuru shule nyingi zilikuwa ni za kikristu na zilikuwa haziruhusu waislam kujiunga na shule hizi, sasa kungekuwa na maana gani ya kuacha ubaguzi huu kuendelea na kujiita nchi huru??
baada ya uhuru mashamba yote makubwa yalikuwa chini ya wazungu, viwanda vyote vilikuwa chini ya watu weupe na watu weusi walikuwa ni kama vibaraka tu, sasa nini maana ya uhuru kama hali hii ingeendelea??
alichokifanya mwalimu ni sahihi sana labda tuwe vipofu na viziwi wa akili kutokujua ukweli huu,
unachekesha zaidi pale unapo "shangilia" umalaya wa taifa letu kwenda kujiuza kwa wazungu kuja kuchukua mali zetu kwa jina la "kuwekeza".
fact ambayo unashindwa kuilewa ni kuwa uwekezaji huu unatokana na ukweli kuwa sisi tumeshindwa kufanya uzalishaji hapa kwetu na hivyo serikali imekosa mapato ya kutosha,huu ni ujinga wa mtu mwafrika na sio siasa ya ujamaa au azimio la arusha.kitu ambacho hufahamu ni kuwa kuna nchi nyingi za afrika ambazo hazikuata siasa ya ujamaa wala azimio la arusha na mpaka leo ni masikini wakutupwa, hata hapa tanzania tuna afadhali. sasa unaweza kuleta explanation kwanini hizo nchi bado ni masikini wakati hazikufuata azimio la arusha??
i cant continue to argue with u any more,it is true your very narow minded and dont know your own history.
our beloved father julius nyerere rest in peace.AMEN
 
MgonjwaUkimwi,

Tafadhali mkuu nakuomba usome tema Azimio la Arusha linasema nini badala ya kuchukua matokeo ya mfumo wa kiuchumi wakati wa vita baridi na kuutumia hapa. Azimio hili linaweza kufanya kazi ktk mfumo wowote ule wa kiuchumi leo hii ama kesho. Hii ni Dira ya kitaifa ambayo inaweza kufanya kazi ktk mifumo yoyote ile ya kisiasa iwe ya Communist, Capitalist ama Socialist na chini ya chama chochote kile iwe CCM, Chadema ama CUF maadam tu utaelewa walengwa ni akina nani.
 
Quarz:

Nimetafuta majibu ya hoja zangu katika posting yako, sijaona japo chembe...ila umejitahidi kuonyesha mapenzi yako kwa baba wa taifa, ambaye hata mimi nampenda kuliko raisi wowote duniani.

Ni vyema ukajibu nilichoandika na kukielewa kama nilivyokiandika. Inasikitisha naposoma kwamba "you should never put yourself in the level of julis nyerere ,incourruptible,humble,a true son of tanzania and a hero of africa, much respected in the world to date." Wapi kwenye posting yangu nilijaribu kujiweka kwenye level ya Nyerere? I question your wisdom.

Sasa nitarudia kwa njia ya maswali point zangu, na nitafurahi endapo utajibu swali hadi swali, maana sasa unanishawishi nione kwamba nikiandika in paragraphs inakuwia vigumu kuelewa.

(A) Kanusha. Arusha Decralation (AD) haikujenga mazingira ya rushwa na umasikini kwa ku-dismantle the most vital class in economic growth: capitalist class.

(B) Kanusha. Wajanja wachache wakiwamo wahindi na viongozi wa ngazi ya juu (except Nyerere na Sokoine) walikiuka misingi ya AD na hivyo kujitajirisha na kufanya vita dhidi ya rushwa ishindikane, huku ikisababisha kifo cha Sokoine.

(C) Kanusha. Misingi ya AD haitekelezeki kwasababu haina reinforcement yeyote, na kwamba inawapa viongozi utajiri na kinga dhidi ya rushwa. Umiliki wa umma wa mali na utajiri wa taifa hautekelezeki (refer to game theory).

Nijibu hapo kwanza.

Pia hii historia ya darasa la saba uliyoileta hapa inanoga tu kuwaeleza wanafunzi husika. Haya mambo ya kusema kwamba mara baada ya uhuru mali zote zilimilikiwa na wachache, na kwamba shule nyingi zilimilikiwa na wakristo, ati kukazuka makupe, wanyonyaji, ati mashamba yote makubwa yalikuwa chini ya weupe na kadhalika, ni historia ya kujidhalilisha na haina misingi yeyote ya kiuchumi....ndio maana inaishia darasa la saba.

Ni historia ya kujidhalilisha. Kwenye nchi zilizoendelea, huko wanakotoka wazungu, ni wazungu wangapi wanamiliki mabenki? Ni wazungu wangapi wanamiliki mashamba makubwa? Ni wazungu wangapi wanamiliki mashule? Ni wazungu wangapi wanamiliki maduka makubwa kwenye nchi zao? Nini kazi ya serikali kama sio kutoza kodi kutoka kwa wachache wanaomiliki utajiri/mali na ku-compansate majority? Nini kazi ya serikali kama sio ku-regulate mazingira ya bihashara ili kuleta usawa? Serikali yetu ilishindwa vipi kutekeleza haya?

Pili, sikutegemea kwamba ungesema kwamba nchi ambazo hazikuwa na AD na ujamaa bado ziko masikini zaidi yetu. Kwani nani alisema kwamba ili nchi iendelee tunahitaji AD na siasa za ujamaa? Nilichosema mimi ni kwamba kama tunsingekuwa na AD tungekuwa tumepiga hatua, tusingekuwa hapa tulipo. Na nikatoa sababu kwamba tungekuwa na capitalist class na tungekuwa empowered na kuchukuwa initiatives za maendeleo yetu wenyewe pasipo kutegemea serikali. Wala sikutunga economic theory ambayo ni generalizable kwa nchi nyingine.....nadhani unatatizo la kuelewa, unaelewa kile unachotaka kuelewa, sio unachotakiwa kuelewa.

Halafu hili suala la kufikirika la uhuru uliloliingiza hapa nalo halina maana. Unauongelea uhuru kana kwamba ni mchana na usiku, kana kwamba uhuru ni kitu rahisi kama 1+1, kana kwamba uhuru wako ni sawa na uhuru wa mtu mwingine. Kana kwamba uhuru alioudai Nyerere ni sawa na uhuru walioutaka wapemba au washirazi. Soma historia hiyo hiyo ya darasa la saba utakuja kugundua kwamba yapo makabila ambayo hayakutaka uhuru na yakaupinga sana, wapo watemi ambao hawatajwi vitabuni ambao walipinga vita vya kudai uhuru...wala uhuru haukuwa sauti ya kila Mtanzania.

Hivi nikuulize: Uhuru una maana gani kwa wananchi wanaomiliki rasilimali zote huku wakifa kwa njaa, umasikini, ujinga, na dhuluma? Uhuru una maana gani kwa wananchi wanaoishi kwa maisha ya afadhali kwa wastani, huku wachache wakimiliki rasilimali zote? Majibu ya maswali haya yatakupa mabaya ya AD.
 
MgonjwaUkimwi,

Tafadhali mkuu nakuomba usome tema Azimio la Arusha linasema nini badala ya kuchukua matokeo ya mfumo wa kiuchumi wakati wa vita baridi na kuutumia hapa. Azimio hili linaweza kufanya kazi ktk mfumo wowote ule wa kiuchumi leo hii ama kesho. Hii ni Dira ya kitaifa ambayo inaweza kufanya kazi ktk mifumo yoyote ile ya kisiasa iwe ya Communist, Capitalist ama Socialist na chini ya chama chochote kile iwe CCM, Chadema ama CUF maadam tu utaelewa walengwa ni akina nani.

Mzee mwenzangu, hapa umeteleza kabisa! Tena Umeteleza kwa kinyumenyume.

Azimio la Arusha haliwezi kufanya kazi kwenye mfumo wa capitalism. Kwa sababu azimio hili lina dismentle capitalist class. This is so clear na hii haina ubishi.

Ila point yangu, ambayo najuwa hukuisoma kwa makini kwenye posting yangu ya awali ni kwamba, azimio hili kamwe haliwezi kufanya kazi kwa sababu ya tatizo la prisoners dilemma. Kwa mantiki kwamba, ili lifanye kazi kila kiongozi lazima atekeleze, na viongozi wasiolitekeleza wanafaidika mara dufu ya wale wanaolitekeleza. Hivyo basi ili iwe win win situation, kila kiongozi ataamua kutolitekeleza...this situation is what is refered as prisoners dillema (exactly happened in Tz). Hapa ndipo azimio la arusha lilipogeuka kichekesho!
 
Mgonjwa Ukimwi,
Rushwa haikuletwa na Azimio la Arusha. Hata kama tungeanza kama mabepari rushwa ingekuwepo tu. Angalia jirani zako Kenya.
 
Mkandara
Huyu jamaa amesema anaumwa Ukimwi. Mwili ukiugua sana muda mwingi hupelekea hata akili kuchoka . Si kawaida ukiwa na akil timamu na ukawa huumwi ukimwi ukajiita Mgonjwa wa Ukimwi hili pekee linakupa urahisi wa kujua unaongea na mtu wa aina gani .

Mimi naangalia nondo zenu bado ushauri wa bure huo sitaki malipo.
 
MgonjwaUkimwi,

Sii vizuri kwangu kuanza kubisha kitu bila kuelewa unazungumza kitu gani...
Hivyo basi nakuomba unitolee Kipande chochote ktk Azimio ambacho kina dismentle Capitalist Class kwa sababu navyofahamu mimi nchi kama za Nordic zina maazimio kama hayo na bado wanaendesha U -capitalist. Kumbuka SIASA safi haina Ukomunist, Ukapitalist ama Usoshalist kama nilivyosema inategemea na wakati pamoja na mlengwa. Imesemwa tu siasa safi ambayo inaweza kutoka upande wowote ule.
Azimio sio Mfumo wala Sera sasa labda wewe nipe somo mwenzangu!
 
mgonjwa wa ukimwi,
unajua mimi ninapojibu hoja najaribu kuangalia factors nyingi na ninakuwa abstract na wakati huo huo nina acha space for you to digest more,
mfano umekuja na kusema kuwa ujamaa ni siasa ya darasa la saba blah blah..., wakati mwanzoni mwa message yangu nimegusia kuwa wenzetu nchi za magharibi kwenye vyuo vikuu sasa hivi wanasoma ujamaa, na nilialikwa kuhuzuria semina moja inayohusu ujamaa na jinsi gani europeans wanaweza kufaidika nayo.

kitu cha pili nilipokuambia usijilinganishe na mwalimu, nilikuwa na maanisha kitu muhimu,unajua mwalimu kabla haja implement hizi policy alifanya utafiti wa kina, si kwamba alikurupuka tu, kama utakumbuka baada ya kuwa rais alifanya ziara katika nchi za magharibi na baadae akaenda china, kwahiyo niliposema hiyo message nilikuwa nikimaanisha kuwa tusifanye kama vile mwalimu hakuyafikiria hayo unayo yaona wewe sasa hivi,tofauti ni kuwa mwalimu alichagua njia ambayo aliiona ni bora kwa taifa hili kutoka na mazingira ya wakati huo.

mfano unaongelea capitalism katika nchi za magharibi, kumbuka kitu kimoja,capitalists wa magharibi ni raia wa nchi zile, mfano bill gates ni raia wa marekani na pesa zake ziko kwenye benk za marekani na serikali ya marekani inafaidika na pesa zake,

sasa watu tuliokuwa nao hapa tanzania wakati tunapata uhuru walikuwa wanyonyaji au makaburu,interest yao kubwa ilikuwa ni kupata resources na kupeleka kwenye nchi zao, na hata pesa zao walikuwa hawawekezi hapa.
kwahiyo kama unaongelea capitalists be carefull on interest,
you have capitalists with different interests,
kama tungekuwa na capitalists wa kitanzania wengi ambao ndio wangekuwa wana viwanda,mashamba na wana weka pesa zao hapa tanzania na pia wanatoa ajira na kuheshimu haki za binadamu sidhani kama wangetaifishwa,
kwahiyo chazo cha kutaifisha ilikuwa unyonyaji,unyanyasaji unaofanywa na hawa makabaila.
baada ya haya maelezo naomba sasa nijaribu kukujibu maswali yako

(A) Kanusha. Arusha Decralation (AD) haikujenga mazingira ya rushwa na umasikini kwa ku-dismantle the most vital class in economic growth: capitalist class.
jibu:
azimio la arusha lilitokana na ukweli kuwa tanzania ilikuwa(na bado) ni taifa la watu masikini, unapokuwa na watu milioni 20, halafu watu milioni 15 ni masikini wanaoishi vijijini na katika hao milioni tano wapo milioni moja ambao ni matajiri sana na wengi wao ni wazungu, wahindi, waarabu nk na zaidi wana wa exploit wale milioni 15 kama kundi la wanyama , unategemea nini? huu ndio uhuru unao utaka wewe??kwahiyo azimio la arusha lilikuwa ni kurealiize kuwa hili ni taifa masikini na haliko tayari kuwalinda watu wachache kuishi kwa jasho la watu wengi.kwahiyo sioni mazingira ya rushwa unayoyaongelea yametokea wapi,
infact nchi yetu imeengia kwenye wimbi la rushwa baada ya hao viongozi wenu wa siku hizi kwenda zanzibar na kutuletea azimio la zanzibar,kuanzia miaka ya 90 ndio tumeanza kushuhudia wimbi la viongozi kutajirika kupindukia.
ku prove hili nipe mfano mmoja wa rushwa uliotekea wakati wa mwalimu na kama wahusika wamegundulika hawakuchukuliwa hatua kali,
lakini angalia kipindi cha mwinyi, mkapa na kikwete, kuna maskendo mangapi yametokea na hatua gani zilichukuliwa?

(B) Kanusha. Wajanja wachache wakiwamo wahindi na viongozi wa ngazi ya juu (except Nyerere na Sokoine) walikiuka misingi ya AD na hivyo kujitajirisha na kufanya vita dhidi ya rushwa ishindikane, huku ikisababisha kifo cha Sokoine.

hii sio sababu tosha ya kudiscredit azimio la arusha,hiyo ni sawa na kusema kwasababu kuna amri ya Mungu inasema usiibe na kwasababu kuna watu wanakiuka amri hiyo basi ni unasema ni bora amri hiyo iondelewe.
kusababisha kifo cha sokoine?? hizo ni speculations, ukweli tunaoujua ni kuwa sokoine alikufa kwa ajari ya gari morogoro, kama kuna kitu unauhakika nacho tutafurahi ukituwekea wazi.

(C) Kanusha. Misingi ya AD haitekelezeki kwasababu haina reinforcement yeyote, na kwamba inawapa viongozi utajiri na kinga dhidi ya rushwa. Umiliki wa umma wa mali na utajiri wa taifa hautekelezeki (refer to game theory).

hii nayo sio kweli,
misingi ya azimio la arushwa ilitekelezwa na ilikuwa reinfoced.viongozi walikuwa hawaruhusiwi kujitajirisha kwa njia za rushwa na matokeo yake tulikuwa na serikali makini,
the fact ni kuwa mataifa ya magharibi yalikuwa yanaupinga mfumo ule kwasababu wazungu waliathirika na wakatuwekea masharti mengi ndio maana tulishindwa kutoka, more than that, kumbuka kwenye kundi la watu wengi kuna mengi pia, kwahiyo ni kweli kulikuwa na watu walioendelea kutumia mianya mbalimbali na kujitajirisha.
vilevile kumbuka hato nchi za magharibi viongozi wao pia wana code of conduct ambayo sio azimio la arusha lakini semantics ni sawa,kwa maana ya kwamba rushwa haivumiwili katika jamii.

kwa kumalizia nasema kuwa azimio la arusha bado liko "valid" na nafikiri ni muhimu likatekelezwa wakati huu wa uwekezaji kuliko wakati mungine wowote.
tunatakiwa tufanye mabadiriko kadhaa mfano tunahitaji kuwapa wazawa uwezo zaidi wa kumiliki mali, mfano pale reginald mengi alipotakana kununua kilimanjaro hotel halafu akanyimwa,ule ndio ulofa wenyewe,pale mzawa anapoonyesha nia ya kuwekeza ndio tuwape kipaumbele kwanza,
pili tunataka wawekezaji katika sekta ya kilimo na viwanda sio majambazi hawa wanaofata resourse zetu kama madini,gesi nk hivi vitu vikiisha na wao hao wanaondoka zao wanatuachia mashimo.
 
Unajua nini kinafurahisha zaidi hapa?.. kwamba sisi ndio tunazungumzia Azimio la Arusha!!! Kwa kuadhimisha miaka 30 ya CCM kwanini hawakuandaa kongamano la kujadili "Azimio la Arusha -Umuhimu wake"?
 
Mshikamano na JK kuwa sponsored CCM wanna test how much are still supported hata baada ya uchafu wao huu ambao wengi wa huko hawaujui.Walala hoi sherehe kwao ni nadra sasa watatumia nafasi hii kujirusha na vikofia na pesa zimeliwa na muda umepotea lakini CCM watakuwa wamesha jua how much are still support hata baada ya nondo zetu hapa . Hawana lolote .
 
Quarz,
I admire your patience. There must be a teacher in you.
 
Back
Top Bottom