Dua,
kuhusu UPEO nimekuletea makala ina-quote watu waliofanya kazi na sokoine. nadhani umejionea kwamba alikuwa mtu wa mtulinga, asiyefanya tafakuri ya kina kabla hajatoa uamuzi.
Kuhusu kuruhusu bidhaa toka nje, ni kweli Sokoine ndiye aliyefikia uamuzi huo. kabla ya hapo alikataa pendekezo la kufungua milango ya uchumi, na kuendelea kuwaletea mateso wananchi. hivi umesahau kwamba sokoine huyo huyo alikuwa akiwasweka watu jela kwa kuwa wamepatikana na colgate, kimbo toka kenya?
kwa kifupi mwalimu na sokoine waliwanyanyasa na kuwadhalilisha wale waliokuwa wakipendekeza mbinu tofauti na zao kuhusu kuokoa uchumi miaka ya 1980. wako waliolazimishwa kuacha kazi, wapo waliopikiwa majungu ili waonekane wabaya mbele ya jamii.
kitu cha kushangaza baada ya mambo kuharibika kabisa mwalimu na sokoine wakaanza kutekeleza yaleyale waliyoyakataa mwanzo. halafu bila haya, wala soni, wanajaribu kuchukua credits zote.
Kuhusu ubavu wa kumweleza mwalimu matatizo yaliyokuwepo....ni kweli mwalimu alimsikiliza sana sokoine, tatizo ni kwamba, sokoine alikuwa hana idea ya chanzo cha matatizo ya wakati ule, na wala mikakati[nguvu kazi,wahujumu uchumi]
Sokoine alikuwa waziri mkuu bora mpaka bale alipojitwisha jukumu la kutoa muongozo wa uendeshaji uchumi tanzania. sokoine alikataa kata kata ushauri mzuri ambao ungeokoa uchumi wetu miaka ya 1980. hiyo ndiyo sababu inayonifanya nimpe maksi mbaya.
Mwalimu aliona mawazo ya sokoine hayafai na ndiyo maana akaachana na kampeni ya uhujumu uchumi. kampeni ile ilikuwa ikikiuka misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.
Unahitaji ushahidi upi kwamba nchi ilimshinda Mwalimu zaidi ya hali mbaya ya uchumi aliyotuachia alipotoka madarakani?
Mwalimu alitufanyia mengi mazuri, lakini ktk uchumi kwa kweli......mhhh