FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,802
- Thread starter
- #221
1) Unajua maana ya 'kusingiziwa' wewe?
2) Nyerere anasingiziwa na nani kuwa kapigania uhuru wa Tanganyika?
3) Neno 'kupigania' halina maana moja kama unavyotaka kuaminisha watu humu.
Hivyo, kupigania uhuru haimaanishi kuwa watu waliingia msituni na kuanza kupigana kwa mapanga na bunduki.
Haya lete namba mbili.
Usiwe na kiherehere, namba mbili tutaenda tu tartiiibu, naona hujajibu umeuliza, kwa kuwa nimetoka kulijibu swali hilo sasa hivi ngoja nikubandikie na wewe, llinakidhi kuwa jibu la maswali yako pia:
Kwanini iwe kapigania? kwanini isiwe kajitahidi sana kadai Uhuru kisiasa na kwa amani na kidiplomasia na kuweza kwa jitihada hizo katupatia Uhuru bila kupigania.
Unajuwa dhanna ya "kupigania Uhuru" anayosingiziwa Nyerere ndiyo inatumika sasa Tanzania hii na watu fulani ambao mpaka huo "upiganaji" ndiyo imekuwa kauli yao ya kawaida na pengine ni sera yao. Wanadai wanataka kuikomboa Tanzania, sasa sijuwi wanataka kuikomboa kutoka kwa nani? na wanachokipigania ni nini? na mpaka wamefikia kusema "nchi haitotawalika". Sasa hiyo ni siasa kweli? au kutishana (terrorism)?
Mpaka wanafikia kuitana wapiganaji, jee huoni kuwa hii "brain washing" ina madhara na si kutengeneza?
Fikiri vizuri na usiwe biased kwa kutaka kufundisha lugha kuwa eti upiganaji si lazima umwage damu au ukunjiane ngumi. Na ethics zipi tunazozifundisha kwa kuacha kutumia sifa kamili ya Nyerere kudai uhuru kisiasa na kwa amani na kuita kuwa "kapigania Uhuru".
Huko ni kumsingizia kubaya sana na kwa kuwa imezoweleka sasa wanatokea wanasiasa na sera za "upiganaji" na bado hatuioni athari yake.
Tafadhali tumpe Nyerere sifa anayostahili na tusimsingizie kwa matakwa yetu tu. Yeye mwenyewe sikumsikia hata mara akisema kuwa "tulipigania Uhuru", bali nimemsikia mara nyingi akisema "tulidai Uhuru".
Nimeeleza juu huko kuwa wapo wa kabla ya Nyerere waliopigania Uhuru na kumwaga damu zao na wengine kuhukumiwa kifo na Wajerumani na kuuliwa kwa kupigania Uhuru, hao tuwaandike kwa wino wa dhahabu na ni kweli walipigania Uhuru ingawa hawakufanikiwa lakini walipigania.
Nyerere kadai Uhuru kisiasa na kafanikiwa bila kukunja mgumi wala kumwaga damu, kwanini na yeye tusimwandike hivyo kwa wino wa dhahabu na tumtie hila ya kumsingizia kwa ambalo hajalifanya? Fikiri.