Nyerere alisingiziwa mengi sana

Nyerere alisingiziwa mengi sana

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,802
Nyerere wetu, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania, kasingiziwa mengi sana.

Ntaanza kuyataja hapa mambo 7 aliyosingiziwa na ntatowa sababu kwanini kasingiziwa.

1) Nyerere anasingiziwa kuwa kapigania Uhuru wa Tanganyika.

Si kweli, Nyerere hakupigania "Uhuru wa Tanganyika". Vita gani alivyopigana kudai Uhuru kama "Kapigania Uhuru"?

2) Nyerere anasingiziwa kuwa kaasisi TANU.

Si kweli, Nyerere hakuasisi TANU wala hajatowa jina la TANU.

3) Nyerere anasingiziwa kuwa ni mzalendo na anawaamini na kuwapenda Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, Nyerere hajawahi kuipenda Tanganyika. Kwanini aliifuta kwenye ramani ya dunia kama anaipenda?

Si kweli, kuwa ni mzalendo. Nyerere hajawahi kumuamini mtu yeyote mwenye asili ya Kiafrika, Nyerere alimuamini mtu mmoja tu katika maisha yake yote, nae ni Mzungu aliyekuwa katibu wake mpaka kufa kwake.

4) Nyerere anasingiziwa kuwa ni Daktari.

Si Kweli, Nyerere alishindwa kwenye sayansi na akaamuwa kuchukuwa masomo ya sanaa, Nyerere ni msanii.

5) Nyerere anasingiziwa kuwa ni msomi wa kwanza kutokea Tanganyika mwenye "Masters Degree".

Si kweli, kuna Watanganyika waliokuwa na udaktari "Phd" kabla yake, ushahidi ni akina Muhimbili, Sewa Haji, Kibasila na wengi wengineo.

6) Nyerere anasingiziwa kuwa ni kipenzi cha Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, hakuna kiongozi Tanzania hii aliyewahi kutaka kupinduliwa au kuuliwa mara nyingi zaidi ya Nyerere.

7) Nyerere anasingiziwa kuwa hajaiba,

Si kweli, BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Kama si Nyerere aliyeiba basi ni Mtei wa Chadema, aje hapa Mtei bado yuko hai, ni vipi BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu?

Mengine malizia wewe, mimi nikirudi naonesha jinsi alivyo singiziwa mengi mengine.

Nikirudi narudi na mengine saba aliyosingiziwa Nyerere.
 
Hiyo namba 6 ndio umeonesha ulivyo ajuza na mjane mjaa laana!

Waliotaka kumpindua si vibaraka kama wewe.

Waliozuia mapinduzi ndio watanganyika wa kweli.

Naona hauelewi kuwa Nyerere alishapinduliwa na ujumbe ukapelekwa kwa U Thans, aliyekuwa mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo. Na aliyeyageuza mpinduzi hayo na aliyemuokoa Nyerere na utawala wake ni kati ya hao wajaa "laana".

Unalijuwa hilo?

Nimefurahi kuwa hujakataa kusingiziwa huko kwa Nyerere.
 
7) Nyerere anasingiziwa kuwa hajaiba,

Si kweli, BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Sasa kama BOT iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, kwa nini unauliza nani alichukuwa? Nani alichukuwa nini kama hakuna senti moja iliyobakia?

Kamasi Nyerere aliyeiba basi ni Mtei wa Chadema, aje hapa Mtei bado yuko hai, ni vipi BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu?

Hata mantiki nyepesi tu zinakushinda! Unasema BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu halafu kwa wakati huo huo unadokeza kwamba huenda Nyerere aliiba. Nyerere ataibaje vitu vyote vilivyoteketezwa na moto? Aliiba majivu?
 
wafuatiliaji tunaomba hoja kwa hoja ili kuweka kumbu kumbu sawa
 
Hivi mtu unapata faida gani kumsimanga marehemu....mtu ambaye hakusikii wala hakuoni...mtu ambaye hataguswa na maneno yako kamwe....kuendelea kumjadili au kumsimanga marehemu...ambaye ni mwanadamu kama sisi...ni kuupoteza muda ambao ungetufanya turekebishe pale ambapo tunahisi alikosea kama mwanadamu na kuyaenzi yale mazuri aliyotuachia....
 
Aisee Tindu Lissu ameanzisha mengi sana yamuhusuyo nyerere
 
Hii umeisahau Nyerere alisingiziwa kupora shule za secondary za wakristo kama mazengo, pugu, minaki, kigonsera nk ili watanzania wote bila kujali dini zao wasome.
Malizia si kweli.............
 
FaizaFoxy

Tunaendelea
8. Walimsingizia eti alizilinda rasilimàli za taifa (madini),si kweli kwani madini yote aliwagawia Wazungu na akina Mwinyi ndio waliorudisha hizi rasilimali mikononi mwa Watanzani.

9.Wanasema aliasisi sera za uchumi wa kujitegemea kwa kuanzisha viwanda vingi kwa msaada wa washirika wake mataifa ya kijamaa (China,Cuba,USSR), si kweli hakuna kiwanda chochote kilichojengwa enzi za utawala wake kwani viwanda vimejengwa enzi za akina Mwinyi.

10.Wanasema eti utawala wa Nyerere haukuwa na madeni makubwa,si kweli kwani utawala wake uliandamwa na madeni lukuki na tawala zilizofuatia ndizo zilizopunguza madeni ya taifa hasa utawala wa Kikwete.
 
Last edited by a moderator:
Nyerere wetu, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania, kasingiziwa mengi sana.

Ntaanza kuyataja hapa mambo 7 aliyosingiziwa na ntatowa sababu kwanini kasingiziwa.

1) Nyerere anasingiziwa kuwa kapigania Uhuru wa Tanganyika.

Si kweli, Nyerere hakupigania "Uhuru wa Tanganyika". Vita gani alivyopigana kudai Uhuru kama "Kapigania Uhuru"?

Nina uhakika lugha ya Kiswahili unaijua vizuri kabisa. Ila inaonekana maana pekee ya "kupigania" uliyonayo ni kukunjiana ngumi au kumwagiana risasi. Kama hii ndiyo maana uliyonayo sidhani kama kuna watu ambao wanaweza kusema kweli "walipigania" uhuru wa nchi yetu.

2) Nyerere anasingiziwa kuwa kaasisi TANU.

Si kweli, Nyerere hakuasisi TANU wala hajatowa jina la TANU.

Mbona hili hajasingiziwa. TANU bila Nyerere si TANU. Labda tumtafute Rais wa kwanza TANU tumuulize.

3) Nyerere anasingiziwa kuwa ni mzalendo na anawaamini na kuwapenda Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, Nyerere hajawahi kuipenda Tanganyika. Kwanini aliifuta kwenye ramani ya dunia kama anaipenda?

Si kweli, kuwa ni mzalendo. Nyerere hajawahi kumuamini mtu yeyote mwenye asili ya Kiafrika, Nyerere alimuamini mtu mmoja tu katika maisha yake yote, nae ni Mzungu aliyekuwa katibu wake mpaka kufa kwake.

Kwanini alitakiwa kuiipenda Tanganyika? Aliipenda Tanzania zaidi bila ya shaka. Sidhani kama kulikuwa na mzungu aliyekuwa Katiba wake mpaka kufa kwake. Katibu wake hadi mauti yanamkuta alikuwa Mtanzania.

4) Nyerere anasingiziwa kuwa ni Daktari.

Si Kweli, Nyerere alishindwa kwenye sayansi na akaamuwa kuchukuwa masomo ya sanaa, Nyerere ni msanii.

Hilo kweli wanamsingizia; hakuna mahali popote katika Historia Nyerere alitajwa kuwa ni Medical Doctor. Ila kwamba alipata shahada kadhaa za heshima za Udaktari hili mbona halina mjadala.

5) Nyerere anasingiziwa kuwa ni msomi wa kwanza kutokea Tanganyika mwenye "Masters Degree".

Si kweli, kuna Watanganyika waliokuwa na udaktari "Phd" kabla yake, ushahidi ni akina Muhimbili, Sewa Haji, Kibasila na wengi wengineo.

Hakuna mtu yeyote anayejua historia yetu kama taifa anayeweza kusema hivyo. Ila Nyerere ndiyo anashikilia rekodi ya kuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Uingereza (University of Edinburg). Lakini pia anashikilia rekodi ya kuwa Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya uzamivu (Masters degree) Hili siyo kumsingizia. Inawezekana wanahistoria wamekosea sasa hivyo ili usahihishe unatakiwa useme Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo cha Uingereza alikuwa nani na wa kwanza kupata Masters alikuwa nani. Then mjadala unanoga au historia inasahihishwa.

Hao wote uliorusha majina yao hujatuambia nani alisoma wapi na alihitimu mwaka gani ili tulinganishe. Kurusha majina tu hakufanyi kitu kiwe kweli. Inakuwa kama yule msomi mwingine wa histohisia ambaye historia ilimshinda.
6) Nyerere anasingiziwa kuwa ni kipenzi cha Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, hakuna kiongozi Tanzania hii aliyewahi kutaka kupinduliwa au kuuliwa mara nyingi zaidi ya Nyerere.

Sasa hicho ndiyo kipimo cha mapenzi. Mbona kuna wazazi wanaopenda na watoto wao wengine wote isipokuwa kichaa mmoja; sasa utasema hawapendwi kwa sababu kichaa mmoja alitaka kuchoma nyumba? What kind of reasoning is this?

7) Nyerere anasingiziwa kuwa hajaiba,

Si kweli, BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Kamasi Nyerere aliyeiba basi ni Mtei wa Chadema, aje hapa Mtei bado yuko hai, ni vipi BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu?

Sijui mantiq umesoma wapi mwenzetu; kama nyumba imeungua na kila kitu kikapotea sasa kinachoibwa kinabiwa vipi? kikiwa majivu?

Mengine malizia wewe, mimi nikirudi naonesha jinsi alivyo singiziwa mengi mengine.

Nikirudi narudi na mengine saba aliyosingiziwa Nyerere.

Hadi hapa hakuna lolote ambalo umefanikiwa kuonesha kuwa alisingiziwa. Labda uje na orodha mpya tuione.
 
Twajua huwa wamdhihaki kwa kila jambo, sijajua dhumuni hasa la huu uzi maana wewe ni zaidi ya haya. Unajielewa na kujitambua.
 
Umejaa chuki kali kwa Mwl Nyerere ambayo haita kufaidisha kwa lolote ndugu.

1. Mwl Nyerere ndiye kipenzi cha wa Tanganyika. Hakuna kitu au mtu ataweza geuza ukweli huu. Iwe kwa chuki za kidini au siasa.

2. Jumuiya ya kimataifa ilimweshumu sana JK na bado inamuheshimu hadi leo.

3. Faiza nakushauri ujipime na kuuondoa uchungu na chuki kali uliyonayo kwa Mwl Nyerere.
 
Back
Top Bottom