Nyerere alisingiziwa mengi sana

Nyerere alisingiziwa mengi sana

Hivi mtu unapata faida gani kumsimanga marehemu....mtu ambaye hakusikii wala hakuoni...mtu ambaye hataguswa na maneno yako kamwe....kuendelea kumjadili au kumsimanga marehemu...ambaye ni mwanadamu kama sisi...ni kuupoteza muda ambao ungetufanya turekebishe pale ambapo tunahisi alikosea kama mwanadamu na kuyaenzi yale mazuri aliyotuachia....
Adolf Hitler mpaka kesho anasimangwa na kuchukiwa.
 
Umejaa chuki kali kwa Mwl Nyerere ambayo haita kufaidisha kwa lolote ndugu.

1. Mwl Nyerere ndiye kipenzi cha wa Tanganyika. Hakuna kitu au mtu ataweza geuza ukweli huu. Iwe kwa chuki za kidini au siasa.

2. Jumuiya ya kimataifa ilimweshumu sana JK na bado inamuheshimu hadi leo.

3. Faiza nakushauri ujipime na kuuondoa uchungu na chuki kali uliyonayo kwa Mwl Nyerere.
Ni kikao kipi tulichokaa na kukubaliana kwa pamoja kuwa wote tunampenda, sisi ni wale tuliomuita Haambiliki, Mchonga na mengineyo.
Wewe si msemaji wetu, jisemee nafsi yako.
 
Sijawahi kuwa na chuki na Nyerere, ila yote aliyosema huyu mama ni kweli.
 
Nyie mnaomtukana nyerere ndio mnafanya mafisadi wanaoiibia nchii hii wajione wapo sahihi.
Maana wanaona mbona nyerere alikuwa muadilifu na bado watanzania wanamtukana.
Wapi katukana Mzee, punguzeni mihemuko ili akili zenu zifanye kazi vizuri
 
Nyerere wetu, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania, kasingiziwa mengi sana.

Ntaanza kuyataja hapa mambo 7 aliyosingiziwa na ntatowa sababu kwanini kasingiziwa.

1) Nyerere anasingiziwa kuwa kapigania Uhuru wa Tanganyika.

Si kweli, Nyerere hakupigania "Uhuru wa Tanganyika". Vita gani alivyopigana kudai Uhuru kama "Kapigania Uhuru"?

2) Nyerere anasingiziwa kuwa kaasisi TANU.

Si kweli, Nyerere hakuasisi TANU wala hajatowa jina la TANU.

3) Nyerere anasingiziwa kuwa ni mzalendo na anawaamini na kuwapenda Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, Nyerere hajawahi kuipenda Tanganyika. Kwanini aliifuta kwenye ramani ya dunia kama anaipenda?

Si kweli, kuwa ni mzalendo. Nyerere hajawahi kumuamini mtu yeyote mwenye asili ya Kiafrika, Nyerere alimuamini mtu mmoja tu katika maisha yake yote, nae ni Mzungu aliyekuwa katibu wake mpaka kufa kwake.

4) Nyerere anasingiziwa kuwa ni Daktari.

Si Kweli, Nyerere alishindwa kwenye sayansi na akaamuwa kuchukuwa masomo ya sanaa, Nyerere ni msanii.

5) Nyerere anasingiziwa kuwa ni msomi wa kwanza kutokea Tanganyika mwenye "Masters Degree".

Si kweli, kuna Watanganyika waliokuwa na udaktari "Phd" kabla yake, ushahidi ni akina Muhimbili, Sewa Haji, Kibasila na wengi wengineo.

6) Nyerere anasingiziwa kuwa ni kipenzi cha Watanganyika na Watanzania.

Si kweli, hakuna kiongozi Tanzania hii aliyewahi kutaka kupinduliwa au kuuliwa mara nyingi zaidi ya Nyerere.

7) Nyerere anasingiziwa kuwa hajaiba,

Si kweli, BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Kama si Nyerere aliyeiba basi ni Mtei wa Chadema, aje hapa Mtei bado yuko hai, ni vipi BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu?

Mengine malizia wewe, mimi nikirudi naonesha jinsi alivyo singiziwa mengi mengine.

Nikirudi narudi na mengine saba aliyosingiziwa Nyerere.
We bibi agent wa DP World, umeamua kumchafua Nyerere?? Hapa nasoma kitabu 38 Reflections of Mwalimu Nyerere, jamaa alikuwa kichwa sana
 
Back
Top Bottom