Mkuu naona umepanga hoja zako vizuri, sasa tusaidie please weka nodo kwa kueleza in details unayo yafahamu maanake mpangilio huu si bure, utakuwa umeufanyia utafiti siku nyingi tu - tusaidie FAIZA kututoa matongo tongo machoni - watu wana kiu ya kujua mengi kuhusu Ndugu yetu huyu ambayo yalikuwa yamefungiwa kwenye closet.
Pitia tu hii nyuzi, mengi yatajitokeza.
Unajuwa sababu kubwa ya kuuweka huu uzi ni double standard iliyopo sasa hivi.
Namba 1.
Nyerere hakupigania Uhuru na alidai Uhuru tena akiwa si peke yake, wazee wa Dar walimpokea na akashirikiana nao kwa hali na mali katika kutimiza hilo, wazee wa Dar walifurahi sana kupata kijana msomi aliyesoma hukohuko kwa wazungu kuwa kaja kuwatafuta na kuwanao bega kwa bega, walimheshimi sana Nyerere. Rejea kitabu cha
Mohamed Said, The Life and
Times of
Abdulwahid Sykes (1924-68). Utaona jinsi Nyerere alivyoishi na hao watu wa Dar., na mikakati yao iliyofanyika ya kudai Uhuru.
Cha kushangaza hao wazee aliowatafuta mwenyewe Nyerere Dar., na waliompokea na waliokuwa naye bega kwa bega kudai Uhuru, leo wamesahauliwa kabisa katika historia na ili ionekane ni jitihada za Nyerere pekee basi limtungwa neno "kapigania Uhuru" na si "kadai Uhuru".
Leo neno hili linazuwa mapya, sasa kuna chama cha kisiasa kina sera za "wapiganaji", ukiwauliza mnapigania nini? majibu ni "kuikomboa Tanzania". Kuikomboa kutoka kwa nani?
Cha kushangaza zaidi, wale waliopigania kujiweka huru na utawala wa kikoloni na waliomwaga damu zao, rejea vita ya majimaji, vita ya Mkwawa, vita ya Bushiri. Hao wote hawatajwi kupigania na hata majina yao hayajulikani na walipoteza roho zao kwa kutaka wasitawaliwe. Kulikoni?
Tunataka historia iwe ya ukweli na vizazi vijavyo viuelewe ukweli na si historia ya kupindishwa pindishwa.
Ntakuja na maelezo mafupi kwa mengine. Kila tunavyoendelea.
Hizo point nimeziweka makusudi ili watu waje wafunguke. Kuna wachache waliokwenda sshule wameliona hilo na wanafunguka ki aina yao, lakini "majority" wanaacha hoja wananishambulia binafsi, nilitegemea hilo pia lakini nnawaona ni misukule wasiojuwa walinenalo na zinawashika hasira mpaka povu linawatoka na wanasahau kuwa hata Nyereree mwenye alisema, yeye si malaika na yale aliyokosea tuyaache.
Sasa hapa waje na yale ambayo si makosa ya Nyerere tuyashike na yale tunayoona kuwa ni makosa tuyazungumze ili tuyaache tusiyarudie.