Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 60,721
- 100,252
Katika mambo ambayo yameigharimu sana Tanganyika na kuidumaza huenda hata sio siasa ya ujamaa zaidi bali siasa za kikanda(geopolitics) za Nyerere ambazo hazikuzingatia maslahi ya uchumi wa Tanganyika wakati huo na ya muda mrefu.
Ukitafakari kwa kina katika fikra huru ni jinsi gani tulivyonufaika kama nchi kuzisaidia kwa jasho na damu nchi za SADCC kama South Africa, Namibia, Zimbabwe, Msumbiji na Angola kupata uhuru ni vigumu sana kupata jibu lolote lenye mashiko kuthibitisha kunufaika kwetu.
Muungano wa Jumuiya ya Africa Mashariki nao hakuwa na umuhimu wowote kabisa kiuchumi miaka ya 1960's kwa nchi zetu changa ambazo hazikuwa na bidhaa za kuuziana sisi kwa sisi. Nyerere alitakiwa kuzingatia zaidi Bilateral relationships kuliko Jumuiya za OAU, SADC na EAC.
Vita vya Uganda navyo huenda vingeweza kuepukika na kuepusha hasara kubwa ya kiuchumi kama Nyerere angempuuza Iddi Amin na kuwaacha Uganda wafanye siasa zao wenyewe wanavyojua wao.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar nao ni kizungumkuti kikubwa mpaka leo ambapo dola ya TANU na CCM haijawahi kuwa na hoja za maana za kuonyesha Tanganyika inanufaikaje nao.
Kiujumla ukitazama wote Tanganyika tuliowasaidia katika harakati zao au kuungana nao walitupa au wana manufaa gani kwa Tanzania mpaka sasa hivi hakuna jibu kwa hakika.