Nyerere alisingiziwa mengi sana

Nyerere alisingiziwa mengi sana

nauchukia uongo. sijaupenda ushauri wako kwa FF kuwa akajifunze jinsi ya kuja kutuongopea, maana wengine tunapitia humu tukiacha very valuable activities. Tafadhali FF kama huo ulioleta humu ni uongo tutake radhi wa JF tafadhali.

Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwa msemo huu ningependa nipitie hoja chache tu alizotoa huyu mama Faiza Foxy kwa ajili ya kuupoteza umma ulio na Uvivu wa kufikiri manake Werevu sidhani kama wameshawishika na hoja zake zisizo na mashiko!
Kwa kuanza na hoja ya kuwa Nyerere hakupigania Uhuru kwa kigezo hakuna vita iliyopigwa ni hoja ya kitoto hasa kwa mtu mwenye kuelewa lugha ya picha "kupigania uhuru" kwa historia fupi nyerere alianzisha Tanganyika Welfare Association ambayo ilikuja kuungana na TAA ambayo mwisho iligeuzwa kuwa chama cha siasa 1954 kilichoitwa TANU ambacho mwenyekiti wake wa kwanza Alikuwa Nyerere ,Nyerere hakuasisi TAA ila aliasisi Tanganyika Welfare Association na Pia ndie alieasisi TANU,kwa taarifa angalia taarifa kutoka encyclopidia britannica kwa wale wasiopenda vitabu angalieni wikipedia.

Hoja nyingine isiyekuwa na Mashiko ni ya kuamini kuwa mtu anayeitwa daktari ni yule tu aliesomea utabibu Nyerere ni msomi mwenye shahada ya uzamili(masters degree) na pia ametunukiwa shahada kadhaa za uzamivu au udaktari wa heshima(honoris causa) kutoka vyuo mbalimbali kuvitaja vichache tu Claremont University cha Marekani,SUA na OUT vya Tanzania,Makerere cha Uganda na Forte Hare cha Afrika kusini,ni shahada hizi zilizompa udaktari wa heshima,dada yangu funguka akili usishikilie maana moja ya maneno jaribu kufikiria mbali kidogo angalau uendani na akili ya mtu wa umri wako

Hoja nyingine isiyo na mashiko ni kuwa kuna wasomi kama Muhimbili ,sewa Haji na Kibasila walipata PhD kabla ya Nyerere kwa Taarifa tu Sewa Haji Alikuwa ni Mfanyabiashara maarufu aliyefariki mwaka 1897 na hakuwa na masters degree wala doctorate(PhD) kama unavyosema na kama una ushahidi wowote tutajie chuo Alichosema kwa taarifa kuhusu historia ya Sewa Haji soma hii link kwa wanaojua kigermani wanaweza kuelewa de.wikipedia.org/wiki/Sewa_Hadji
na blog ya huyu dada itakusaidia Binti Wa Kiislamu: Sewa Haji (1851-1897) na pia Kibasila
na alikuwa na umaarufu wake ili hakuwa na elimu unayosema, epuka kuleta stori za vijiweni kama hoja zenye mashiko fanya utafiti kidogo tu dada yangu.

Nimeamua kujibu hoja chache ili kuepusha upotoshaji wa huyu dada maana kuna usemi unasema "uongo ukirudiwa ukweli husauliwa" na huyu dada ili kuonyesha maneno yake ni ya vijiweni hajaweka hata maelezo kujenga hoja zake udaktari wa Nyerere tumeweka maana yake na jinsi alivyoipata ,Elimu ya Sewa Haji tumeweka link ,na uasisi wa TANU na upiganiaji uhuru tumeweka kitabu na website ya msaada safari ijayo jaribu kuupanga uongo wako. kutudanganya kitoto ni kutukosea heshima kudhani ni mapunguani tusio weza kuchambua hoja.
 
Pia nikushukuru kwa hii link, na kwa wale ambao wataona uvivu kuifuata nawapastia humu mjisomee wenyewe.
[h=3]Sewa Haji (1851-1897)[/h]

Today, 117 years have passed and we still remember this great man.

Sewa Haji, born in 1851 in Zanzibar, Tanzania. He was a wealthy business man, who had business caravans in Bagamoyo and Zanzibar, but was also known to be God fearing and a philanthropist.

He donated a three storey building in Bagamoyo in 1892 to be used as a school. The school was the first mixed race school in Tanganyika during the German colonial era. Later on, he developed a hospital, donated many wells and land in Bagamoyo during the cholera outbreak, and a home for the lepers. He built the biggest hospital in Dar-Es-Salaam that was named Sewa Haji Hospital, later on during the british rule, the name was changed to Princess Margaret Hospital, now Muhimbili Hospital. He donated property and land to the poor, without regards to race or religion. He passed away in February 1897 in Zanzibar at the age of 46.

In Tanzania he is greatly remembered, in the new rebuilt Muhimbili Hospital, a ward is named in his honor. His school (now Mwambao Primary School) and hospital(now Bagamoyo District Hospital) still stand in Bagamoyo. The land he donated in Mombasa,Kenya is still being used as a cemetary.

May Allah grant him a high place in Jannah. He was a muslim not only by name, but also by his actions, for he understood the true meaning of serving mankind.

Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwa msemo huu ningependa nipitie hoja chache tu alizotoa huyu mama Faiza Foxy kwa ajili ya kuupoteza umma ulio na Uvivu wa kufikiri manake Werevu sidhani kama wameshawishika na hoja zake zisizo na mashiko!
Kwa kuanza na hoja ya kuwa Nyerere hakupigania Uhuru kwa kigezo hakuna vita iliyopigwa ni hoja ya kitoto hasa kwa mtu mwenye kuelewa lugha ya picha "kupigania uhuru" kwa historia fupi nyerere alianzisha Tanganyika Welfare Association ambayo ilikuja kuungana na TAA ambayo mwisho iligeuzwa kuwa chama cha siasa 1954 kilichoitwa TANU ambacho mwenyekiti wake wa kwanza Alikuwa Nyerere ,Nyerere hakuasisi TAA ila aliasisi Tanganyika Welfare Association na Pia ndie alieasisi TANU,kwa taarifa angalia taarifa kutoka encyclopidia britannica kwa wale wasiopenda vitabu angalieni wikipedia.

Hoja nyingine isiyekuwa na Mashiko ni ya kuamini kuwa mtu anayeitwa daktari ni yule tu aliesomea utabibu Nyerere ni msomi mwenye shahada ya uzamili(masters degree) na pia ametunukiwa shahada kadhaa za uzamivu au udaktari wa heshima(honoris causa) kutoka vyuo mbalimbali kuvitaja vichache tu Claremont University cha Marekani,SUA na OUT vya Tanzania,Makerere cha Uganda na Forte Hare cha Afrika kusini,ni shahada hizi zilizompa udaktari wa heshima,dada yangu funguka akili usishikilie maana moja ya maneno jaribu kufikiria mbali kidogo angalau uendani na akili ya mtu wa umri wako

Hoja nyingine isiyo na mashiko ni kuwa kuna wasomi kama Muhimbili ,sewa Haji na Kibasila walipata PhD kabla ya Nyerere kwa Taarifa tu Sewa Haji Alikuwa ni Mfanyabiashara maarufu aliyefariki mwaka 1897 na hakuwa na masters degree wala doctorate(PhD) kama unavyosema na kama una ushahidi wowote tutajie chuo Alichosema kwa taarifa kuhusu historia ya Sewa Haji soma hii link kwa wanaojua kigermani wanaweza kuelewa de.wikipedia.org/wiki/Sewa_Hadji
na blog ya huyu dada itakusaidia Binti Wa Kiislamu: Sewa Haji (1851-1897) na pia Kibasila
na alikuwa na umaarufu wake ili hakuwa na elimu unayosema, epuka kuleta stori za vijiweni kama hoja zenye mashiko fanya utafiti kidogo tu dada yangu.

Nimeamua kujibu hoja chache ili kuepusha upotoshaji wa huyu dada maana kuna usemi unasema "uongo ukirudiwa ukweli husauliwa" na huyu dada ili kuonyesha maneno yake ni ya vijiweni hajaweka hata maelezo kujenga hoja zake udaktari wa Nyerere tumeweka maana yake na jinsi alivyoipata ,Elimu ya Sewa Haji tumeweka link ,na uasisi wa TANU na upiganiaji uhuru tumeweka kitabu na website ya msaada safari ijayo jaribu kuupanga uongo wako. kutudanganya kitoto ni kutukosea heshima kudhani ni mapunguani tusio weza kuchambua hoja.
 
Dada huyo baba wawatu alikukosea nini kikubwa mpaka unakosa raha hivi kwaajili yake?

Huo uchungu ulionao dhidi ya marehemu utapunguza siku zako za kuishi huku duniani.... Hivi wajua Mungu ni pendo na aliye na upendo ni wa Mungu na asiye na upendo ni muuaji?

Relax achana na marehemu ishi kwa amani na fanya yanayokuhusu.... Mhubiri nimeona kueneze upendo!
 
Sewa Haji, born in 1851 in Zanzibar, Tanzania. He was a wealthy business man, who had business caravans in Bagamoyo and Zanzibar, but was also known to be God fearing and a philanthropist.

What was this business caravans all about, can you elaborate a little bit about!
 
Tanzania Safari Guide; 19th Century History

But further south allegiance tended towards the Al Bu’Saidi Sultan of Muscat, especially from Zanzibar and Kilwa, which was once more rising to prominence. The island state reinstated trade with the interior, and thrived especially on imports of cloth, arms, ammunition and salt, and exports of ivory, until around 1730, when they increased the export of slaves, especially to French colonies such as Mauritius and Reunion where they would work on the sugar planta

These are the people we are supposed to commend and thank for what they promoted...

Kweli ukipenda chongo huita kengeza....!
 
5) Nyerere anasingiziwa kuwa ni msomi wa kwanza kutokea Tanganyika mwenye "Masters Degree".

Si kweli, kuna Watanganyika waliokuwa na udaktari "Phd" kabla yake, ushahidi ni akina Muhimbili, Sewa Haji, Kibasila na wengi wengineo.

Ni kweli kuwa Nyerere alikuwa mtu wa kwanza kupata digrii ya Master of Arts digrii kutoka huko Scotland. Wasomi wote wa wakati huo waliokuwa wamesoma Makerere tu hawakuwa na digrii kwa vile Makerere ilikuwa inatoa diploma tu. Diploma za Makerere zilianza kutumaka kama kigezo cha kupatia digrii huko University of London mwaka 1963, yaani baadaye sana.

KIBASILA alikuwa chifu wa wazaramo, ila kuna "Dr" Kibasila aliyekuwa na diploma ya Uganga aliyopata Makerere mwaka 1958 baada ya Nyerere kuwa alishapata hiyo Masters yake. "Dr" Kibasila hakuwa na digrii hata ya bachelor

SEWA HAJI PAROO alikuwa mfanya biashara wa kiarabu na wala hakuwa Daktari. Wodi la Sewa Haji hapo Muhimbiri ni kumbukumbu tu kuwa alianzisha hospatali hiyo ya kusaidia maskini wakati huo wa utawala wa mjerumani lakini hakuwa tabibu na wala hakuwa na digrii.

MUHIMBILI: Sina uhakika na jina hilo ila kwa vyovyote hata kama alikuwa Daktari, basi hakuwa na digrii. Madaktari maarafu wa kwanza kama vile DR MWAISELA, DR Mutahangarwa, Dr Vedastaus Kyaruzi, Dr Luciana Tsere hawakuwa na digrii bali walikuwa na diploma za uganga (Assistant Medical Officer- AMO) walizopata Makerere. Mtanganyika wa kwanza kupata diploma hiyo ya Uganga (AMO) kutoka Makerere alikuwa DR Mutahangarwa aliyopata mwaka 1942.
 
Tundu lissu wakati wa kikao cha bunge la katiba alieleza sana kuhusu nyerere, kuna mpaka mashehe walilia eti anakashifiwa baba wa taifa. Mfano mdogo tu ni waraka wa muungano, lakini watu ukieleza upande mwengine wa shilingi kumhusu nyerere wamakuwa wakali kweli daaah, wakuu alikuwa binaadamu wa kawaida hakuwa mungu nae ana makosa kibao

Sijui ndugu zetu wengine ni sisimizi wanaotambaa kwenye ubongo au nini. Kwani tunajadiliana kama alikuwa na makosa au la?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Sasa jibu na hili, mbona unalikwepa swali?

BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

sasa BoT ilipoungua na hakuna senti moja iliyobakia inawezekana zote ziliungua kwenye moto? au unafikiria nini? Na sidhani kama "hakuna senti moja iliyobakia"... Umejuaje?
 
Ni kweli kuwa Nyerere alikuwa mtu wa kwanza kupata digrii ya Master of Arts digrii kutoka huko Scotland. Wasomi wote wa wakati huo waliokuwa wamesoma Makerere tu hawakuwa na digrii kwa vile Makerere ilikuwa inatoa diploma tu. Diploma za Makerere zilianza kutumaka kama kigezo cha kupatia digrii huko University of London mwaka 1963, yaani baadaye sana.

KIBASILA alikuwa chifu wa wazaramo, ila kuna "Dr" Kibasila aliyekuwa na diploma ya Uganga aliyopata Makerere mwaka 1958 baada ya Nyerere kuwa alishapata hiyo Masters yake. "Dr" Kibasila hakuwa na digrii hata ya bachelor

SEWA HAJI PAROO alikuwa mfanya biashara wa kiarabu na wala hakuwa Daktari. Wodi la Sewa Haji hapo Muhimbiri ni kumbukumbu tu kuwa alianzisha hospatali hiyo ya kusaidia maskini wakati huo wa utawala wa mjerumani lakini hakuwa tabibu na wala hakuwa na digrii.

MUHIMBILI: Sina uhakika na jina hilo ila kwa vyovyote hata kama alikuwa Daktari, basi hakuwa na digrii. Madaktari maarafu wa kwanza kama vile DR MWAISELA, DR Mutahangarwa, Dr Vedastaus Kyaruzi, Dr Luciana Tsere hawakuwa na digrii bali walikuwa na diploma za uganga (Assistant Medical Officer- AMO) walizopata Makerere. Mtanganyika wa kwanza kupata diploma hiyo ya Uganga (AMO) kutoka Makerere alikuwa DR Mutahangarwa aliyopata mwaka 1942.

Sasa FaizaFoxy anatwambia walikuwa na PhD........!!!
 
Last edited by a moderator:
Katika points 7 nilizoziweka wewe huna hata moja ya kufafanuwa nilipokuwa "wrong"? Nyani Ngabu kachaguwa mbili, zingine 5 hana comment mpaka dakika hii. Vipi wewe?

Usijipe moyo sana kuwa hizo 5 ambazo nimezipotezea ni pointi.

Nimezipotezea makusudi kwa sababu nimeziona ni pumba tu.
 
Sasa FaizaFoxy anatwambia walikuwa na PhD........!!!

Wacha uongo wewe, point yangu ilikuwa si lazima uwe na PhD ndiyo uitwe daktari nikatoa hata mfano wa Dr. Manyaunyau.

Nikimaanisha kuwa, ikiwa mtu anataka kukuita Daktari si lazima wewe uwe daktari wa kweli na wale wanaosema Kikwete anjiita Dr. nasema si kweli, ni watu wanamuita Dokta sijamsikiapo akijitambulisha hata mara moja kuwa mimi ni Dr Kikwete.

Hali kadhalika Nyerere kwa wegi waliosema hawajasikia wala kuona Nyerere akijiita Dr., nnawauliza walimsikia Kikwete akijiita Dr.?
 
Hii umeisahau Nyerere alisingiziwa kupora shule za secondary za wakristo kama mazengo, pugu, minaki, kigonsera nk ili watanzania wote bila kujali dini zao wasome.
Malizia si kweli.............

Umesahau pia kuwa hizo hizo ndio zilitusomesha kitabu cha Uhuru wa Watumwa kilichokuwa kinasema Waislam tu ndiyo walifanya biashara ya utumwa kikiwasahau Wazungu ambao bila shaka ni Wakristo waliokuwa wanunuzi wakubwa wa utumwa kuliko yeyote duniani.
 
Hapana, sikubaliani nazo bali niliziona ni za kipuuzi mno kustahili kujibiwa hivyo nikazipuuzia mbali.

Ni nini ambacho hukubaliani nacho kuwa kasingiziwa au hajasingiziwa? sikuelewi.

Tuanza na namba moja, nieleze ni nini usichokubaliana nacho:

1) Nyerere anasingiziwa kuwa kapigania Uhuru wa Tanganyika.

Si kweli, Nyerere hakupigania "Uhuru wa Tanganyika". Vita gani alivyopigana kudai Uhuru kama "Kapigania Uhuru"?
 
It seems I'm discussing with an obtuse myopic person!

My question is simple and straight forward, what is behind your mind of HATE of Nyerere and LOVE of CCM?

You can't see cha kukufikirisha may be what I'm writing is beyond your comprehension, and that is NOT your fault.

La "hate" kwa Nyerere si kweli nimeshalijibu lijibu huko juu labda hukupenda majibu yangu.

Imbecile.
 
Ni nini ambacho hukubaliani nacho kuwa kasingiziwa au hajasingiziwa? sikuelewi.

Tuanza na namba moja, nieleze ni nini usichokubaliana nacho:

1) Nyerere anasingiziwa kuwa kapigania Uhuru wa Tanganyika.

Si kweli, Nyerere hakupigania "Uhuru wa Tanganyika". Vita gani alivyopigana kudai Uhuru kama "Kapigania Uhuru"?

1) Unajua maana ya 'kusingiziwa' wewe?

2) Nyerere anasingiziwa na nani kuwa kapigania uhuru wa Tanganyika?

3) Neno 'kupigania' halina maana moja kama unavyotaka kuaminisha watu humu.

Hivyo, kupigania uhuru haimaanishi kuwa watu waliingia msituni na kuanza kupigana kwa mapanga na bunduki.

Haya lete namba mbili.
 
hapa sijaona hoja ya maana, kutumia neno kupigania inaweza kuwa na maana kujitoa na kuhakikisha unafanikiwa kwa kile unacho kitaka na kukiamini. mara ngapi tunasikia na kutumia neno alijitahidi kupigania maisha yake, ila ndo ivyo tena hatunae. wewe ulitaka kupigania hadi kuwe na kurushiana ngumi na kutoana damu.

kadri siku zinavyoenda msamiati hubadirika kwa iyo usishangae neno KUPIGANIA kuwekwa kwenye kundi la wale wanaoweka juhudi zao kupata kitu flani.

= hubadilika

Hilo la "kupigania maisha yake" mimi kwa Kiswahili sijawahi kulisikia.

Kwanini iwe kapigania? kwanini isiwe kadai Uhuru kisiasa na kwa amani na kidiplomasia na kuweza kutupatia Uhuru bila kupigania.

Unajuwa dhanna ya "kupigania Uhuru" anayosingiziwa Nyerere ndiyo inatumika sasa Tanzania hii na watu fulani ambao mpaka huo "upiganaji" ndiyo imekuwa kauli yao ya kawaida na pengine ni sera yao. Wanadai wanataka kuikomboa Tanzania, sasa sijuwi wanataka kuikomboa kutoka kwa nani? na wanachokipigania ni nini? na mpaka wamefikia kusema "nchi haitotawalika". Sasa hiyo ni siasa kweli? au kutishana (terrorism)?

Mpaka waanafikia kuitana wapiganaji, jee huoni kuwa hii "brain washing" ina madhara na si kutengeneza?

Fikiri vizuri na usiwe biased kwa kutaka kufundisha lugha kuwa eti upiganaji si lazima umwage damu au ukunjiane ngumi. Na ethics zipi tunazozifundisha kwa kuacha kutumia sifa kamili ya Nyerere kudai uhuru kisiasa na kwa amani na kuita kuwa "kapigania Uhuru".

Huko ni kumsingizia kubaya sana na kwa kuwa imezoweleka sasa wanatokea wanasiasa na sera za "upiganaji" na bado hatuioni athari yake.

Tafadhali tumpe Nyerere sifa anayostahili na tusimsingizie kwa matakwa yetu tu. Yeye mwenyewe sikumsikia hata mara akisema kuwa "tulipigania Uhuru", bali nimemsikia mara nyingi akisema "tulidai Uhuru".

Nimeeleza juu huko kuwa wapo wa kabla ya Nyerere waliopigania Uhuru na kumwaga damu zao na wengine kuhukumiwa kifo na Wajerumani na kuuliwa kwa kupigania Uhuru, hao tuwaandike kwa wino wa dhahabu na ni kweli walipigania Uhuru ingawa hawakufanikiwa lakini walipigania.

Nyerere kadai Uhuru kisiasa na kafanikiwa bila kukunja mgumi wala kumwaga damu, kwanini na yeye tusimwandike hivyo kwa wino wa dhahabu na tumtie hila ya kumsingizia kwa ambalo hajalifanya? Fikiri.
 
Back
Top Bottom