Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwa msemo huu ningependa nipitie hoja chache tu alizotoa huyu mama Faiza Foxy kwa ajili ya kuupoteza umma ulio na Uvivu wa kufikiri manake Werevu sidhani kama wameshawishika na hoja zake zisizo na mashiko!
Kwa kuanza na hoja ya kuwa Nyerere hakupigania Uhuru kwa kigezo hakuna vita iliyopigwa ni hoja ya kitoto hasa kwa mtu mwenye kuelewa lugha ya picha "kupigania uhuru" kwa historia fupi nyerere alianzisha Tanganyika Welfare Association ambayo ilikuja kuungana na TAA ambayo mwisho iligeuzwa kuwa chama cha siasa 1954 kilichoitwa TANU ambacho mwenyekiti wake wa kwanza Alikuwa Nyerere ,Nyerere hakuasisi TAA ila aliasisi Tanganyika Welfare Association na Pia ndie alieasisi TANU,kwa taarifa angalia taarifa kutoka encyclopidia britannica kwa wale wasiopenda vitabu angalieni wikipedia.
Hoja nyingine isiyekuwa na Mashiko ni ya kuamini kuwa mtu anayeitwa daktari ni yule tu aliesomea utabibu Nyerere ni msomi mwenye shahada ya uzamili(masters degree) na pia ametunukiwa shahada kadhaa za uzamivu au udaktari wa heshima(honoris causa) kutoka vyuo mbalimbali kuvitaja vichache tu Claremont University cha Marekani,SUA na OUT vya Tanzania,Makerere cha Uganda na Forte Hare cha Afrika kusini,ni shahada hizi zilizompa udaktari wa heshima,dada yangu funguka akili usishikilie maana moja ya maneno jaribu kufikiria mbali kidogo angalau uendani na akili ya mtu wa umri wako
Hoja nyingine isiyo na mashiko ni kuwa kuna wasomi kama Muhimbili ,sewa Haji na Kibasila walipata PhD kabla ya Nyerere kwa Taarifa tu Sewa Haji Alikuwa ni Mfanyabiashara maarufu aliyefariki mwaka 1897 na hakuwa na masters degree wala doctorate(PhD) kama unavyosema na kama una ushahidi wowote tutajie chuo Alichosema kwa taarifa kuhusu historia ya Sewa Haji soma hii link kwa wanaojua kigermani wanaweza kuelewa
de.wikipedia.org/wiki/Sewa_Hadji
na blog ya huyu dada itakusaidia
Binti Wa Kiislamu: Sewa Haji (1851-1897) na pia Kibasila
na alikuwa na umaarufu wake ili hakuwa na elimu unayosema, epuka kuleta stori za vijiweni kama hoja zenye mashiko fanya utafiti kidogo tu dada yangu.
Nimeamua kujibu hoja chache ili kuepusha upotoshaji wa huyu dada maana kuna usemi unasema "uongo ukirudiwa ukweli husauliwa" na huyu dada ili kuonyesha maneno yake ni ya vijiweni hajaweka hata maelezo kujenga hoja zake udaktari wa Nyerere tumeweka maana yake na jinsi alivyoipata ,Elimu ya Sewa Haji tumeweka link ,na uasisi wa TANU na upiganiaji uhuru tumeweka kitabu na website ya msaada safari ijayo jaribu kuupanga uongo wako. kutudanganya kitoto ni kutukosea heshima kudhani ni mapunguani tusio weza kuchambua hoja.