Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Sio kwamba alikuwa hana muuono; baada ya 9/12/1962 Baba wa taifa alikuwa na muuono wa kuendelea lakini sio kwa Tanganyika tu bali kwa kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla (Umajumui wa kiafrika) ambapo yeye alikuwa tayari hata kutumia rasilimali za nchi yake kupigania muungano wa Afrika Mashariki na hatimaye Afrika kitu ambacho wenzake hawakunacho na daima hakukiona kwao yeye alizidi kutumia rasilimali zetu kupigania wengine wakati taifa likiwa halina cha kututosheleza kitu ambacho kilituangusha sana hasa pale ambapo hata lile soko dogo la bidhaa zetu (EAC)lilipoanguka hatukuwa na namna ya kufanya biashara yoyote kwa ufanisi na vita iliyofuata (Kageran War) ambayo ilitumaliza kabisa kiuchumi ambapo inasemekana aliposema miezi kumi na nane ya kufunga mkanda alificha uhalisia ambapo kiuhalisia ilikuwa ni miaka 18 ya kufunga mkanda!

Kiukweli Mwalimu alijenga misingi thabiti ya uongozi katika nchi hii na kuisimamia vilivyo kuliko kiongozi yeyote katika historia ya nchi hii hadi leo. alituunganisha watanzania wote akiwa na nia ya kutengeneza taifa la Tanzania na sio vitaifa vidogo vidogo ndani ya Tanzania kitu alichofanikiwa kwa kiwango kikubwa na sehemu ya matunda yake tunayaona leo. Alisimamia thabiti, upatikaji wa elimu hadi kwa watu wazima na hata wale maskini kabisa ambao hawakuwa na tumaini kwa watoto wao kupat elimu walisoma na kusomeshwa katika shule na taasisi kubwa za kielimu ndani na nje ya nchi bure kabisa kwa nia ya kuja kujenga taifa kiasi kwamba Tanzania ikaongoza Afrika kwa watu wanojua kusoma na kuandika na mengineyo mengi...

Kwa mimi namwona Nyerere kama kiongozi jasiri mwenye kukemea pasipo kujali wewe nani, msema kweli, mhalisia, mwanadiplomasia mahiri na kiongozi aliye kiri wazi kuwa anaondoka madarakani baada ya kuona kuwa sera zake zimeshindwa na hakuwa tayari kuzipa nafasi sera kandamizi za kimagharibi akiwa yeye madarakani akaona bora apishe mtazamo mpya.Ni kiongozi gani Afrika anayeweza leo kufanya hivi?

Kimapungufu Mwalimu alibana sana uhuru wa kujieleza hadi ikafika mahali kukosoa serikali ilikuwa kama kufuru, aliweka kizuizini waliotofutiana na mitazamo yake, na hakuweza tambua haki za binadamu katika katiba ya nchi, aliifanya serikali na viongozi wake waogopwe na watu na hakuruhusu juhudi binafsi na ubunifu katika kutafuta maendeleo.

Zaidi ya yote ndo maana kaitwa Mwalimu anatufundisha na sisi tunaiga kwake; hivyo tuyaige yale yake mazuri na kuachane na yale mabaya aliyotenda enzi za utawala wake!. vita ya kagera ilituua kiuchumi na ilikuwa na umuhimu mkubwa , vita ya kukomboa nchi zingine zilikuwa na umuhimu sana tu. lakini nyerere alitakiwa awe na akili kwamba sio watu wote/nchi zote zinamawazo kama yake ya kuunganisha africa (hakuwa na Maono ).

NAWASILISHA HOJA!
ni kiongozi mjinga anaejaribu kuachieve a national dream katika utawala wake. alitakiwa kujua kwamba umoja wa africa hauwezekani wakati nchi ndo inapata uhuru. alitakiwa kujua kuna watu grreedy kama IMPLA, UNITA , UNITA NA RENAMO. hakuwa na maono
 
ofisi za chama nchi nzima!

Mkuu, umesoma ulichoandika lakini?

Hivi kweli Mwalimu ameongoza nchi miaka 23 na kitu unachoweza kukumbuka kumuenzi ni kuweka ofisi za Chama Cha Mapinduzi nchini?

Nyinyi maadui wa Mwalimu sijui mna matatizo gani?!! Najua sasa hivi mnapigania serikali tatu ili msimame kushangilia kuwa Mwalimu's last legacy is gone!!!
 
Hivi kweli &haifu ameweka misingi gani hiyo imara ya kutufikisha popote? Ufisadi, madawa ya kulevya, ujangili wa akina Kinana, uuaji wa kina nchemba, rushwa mpaka jeshini, bila shaka hiyo ndo misingi imara ya Kikwete.
 
Mkuu, umesema kweli.

Ninachoona mimi ni UNAFIKI kwa watu wetu. Mashabiki wa serikali tatu ndio haohapo wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Wanaonunua kura wakati wa uchaguzi ndio haohao wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Vinara wa kuomba misaada nje ya nchi ndio haohao wanaojidai kupigania legacy ya Mwalimu. Mabepari ndio hao hao wanaojifanya kupigania legacy ya Mwalimu.

Huu ni UNAFIKI.

Huwezi kusema ugombei Urais mpaka uahidiwe pesa nono kama mshahara wa mbunge halafu ukajifanya unapigania legacy ya Mwalimu.

Huwezi kusema chama chako hakihitaji wanachama Zanzibar halafu ukajidai unapigania legacy ya Mwalimu.

Lets be true,

Legacy gani ya Mwalimu tunaishi nayo leo?
mkuu kwa hoja yako hii unataka kuniambia kwamba legacy ya mwalimu haieleweki. au watanzania hatuielewi legacy ya mwalimu (naamni hilil kwanza zaidi).
 
Kwa ufupi sana labda niseme msingi wa mkuu wa AZIMIO LA ARUSHA ulikua ni "uchumi kumilikiwa na SERIKALI" .... hebu tujikite ktk hili.... bila kuwaudhi kwa maelezo marefu ya kisiasa ngoja nitoe mifano ya kimaelezo ....!

Mwaka 2008 uchumi wa DUNIA nzima ulianguka na sio IMF wala WB waliokuwa na jibu ila lililo kutokea km ndio tatizo dhahiri ilikuwa BIASHARA HURIA hivyo wakuu wa nchi zenye Uchumi mkubwa walikaa (G20) na katika mwaka huo walikaa mara mbili badala ya moja kwa mwaka km kawaida yao... kubwa walilokua wanalifanya ni kutunga sera zenye kuhakikisha serikali zinaweka udhibiti ktk Biashara (Huria)
Serikali ya Marekani ilinunua hisa za Mabenki yote (4) Makubwa ... serikali ya Uingereza iliyatwaa Mabenki yote makubwa (9) ... Hali ya Uchumi ilirejea ktk ukuaji wa kila mwaka na sasa hali ya uchumi wa kidunia unakua vyema

Katika nchi ambayo serikali ilimiliki njia za Uchimi km China na karibuni Venezuela hazikuathirika na kutokukujua kwa uchumi wao. Uchumi wa China ukiendelea kujua kwa kati ya 8% na 12%

AZIMIO LA ARUSHA likihimiza umiliki wa nji kuu za uchumi kumilikiwa na serikali..... Sera hii ndio iliyotumika kuuokoa Uchumi wa DUNIA na pia kuuliza Uchumi China na Venizuela....!

Mwaka 1986 Mwl. Nyerere alimhakikishia Regan na Thecher kuwa sera ya Biashara huria ni kosa Iliyoasisiwa mwaka huo...miaka 22 baadae hakuna anayebisha kuwa Biashara huria kuwa ni kosa.... Tumelitupa Azimio ambalo ni jibu la mengi ya mambo yasioende vizuri km taifa.
 
Mkuu, umesema kweli.

Ninachoona mimi ni UNAFIKI kwa watu wetu. Mashabiki wa serikali tatu ndio haohapo wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Wanaonunua kura wakati wa uchaguzi ndio haohao wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Vinara wa kuomba misaada nje ya nchi ndio haohao wanaojidai kupigania legacy ya Mwalimu. Mabepari ndio hao hao wanaojifanya kupigania legacy ya Mwalimu.

Huu ni UNAFIKI.

Huwezi kusema ugombei Urais mpaka uahidiwe pesa nono kama mshahara wa mbunge halafu ukajifanya unapigania legacy ya Mwalimu.

Huwezi kusema chama chako hakihitaji wanachama Zanzibar halafu ukajidai unapigania legacy ya Mwalimu.

Lets be true,

Legacy gani ya Mwalimu tunaishi nayo leo?
Wanafiki wakubwa katika legacy ya Mwl. Nyerere ni viongozi wetu wa kisiasa katika vyama vyote vya siasa na asasi zingine.

Ukigusa negative legacy ya Mwl. Nyerere wanakuwa wa kwanza kusema hayo yamepita tugange yaliyopo na yajao. Ukigusa legacy yake katika hali chanya, wanakuwa wa kwanza kusema, lazima tumuenzi Mwl. Nyerere na uongozi wake.

CCM wako happy kumuona Mwl. Nyerere kama baba wa Taifa na kumuenzi wakati legacy zake wanaziondoa kisiri siri moja baada ya nyingine kwa maana kuwa HAZIFAIi. Cha kushangaza mpaka sasa katiba ya nchi inasema nchi iko kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea.

Vyama vingine vya upinzani navyo vinapenda vijishikize katika legacy za Mwl. Nyerere ili kupata kura wakati policy na misingi ya utawala wao iko mbali kabisa na maono, utawala na utendaji wa Mwl. Nyerere. Walichofanya, wanachofanya na kukitenda mpaka sasa kiko mbali kabisa na misingi ya utawala wa Mwl. Nyerere.

UNAFIKI ni kitu kibaya sana.
 
Kwanza; unapojadili tuende kipengele kwa kipengele naomba upitie upya maelezo yangu kisha kwa kila kipengele jadili

ukilinganisha na hawa wasasa na pia kosowa udhaifu wa JK nyerere usitowe majibu ya jumla ambayo hayaleti maana halisi

Pili unataka kuniambia elimu ya sasa ni bora kwasababu ni ya malipo kwa failure ya 90%?
mi naenda point by point. mkuu.elimu ya kulipia ni bora kuliko ya bure kiukweli.ila nyerere hakutujengengea misingi ya kujua hilo , sijui ni makusudi au hakuwa na maono. hebu we niambie niambie leo hii
elimu ya kulipia na bure ipi bora?.sitaki kusema kwamba mtu anayekuwa rais wetu anatakiwa kuwa nabii!, hapana. hapana, ila anatakiwa kuwa na missions zinazoendana na cotext of the world.
 
Mkuu, umesoma ulichoandika lakini?

Hivi kweli Mwalimu ameongoza nchi miaka 23 na kitu unachoweza kukumbuka kumuenzi ni kuweka ofisi za Chama Cha Mapinduzi nchini?

Nyinyi maadui wa Mwalimu sijui mna matatizo gani?!! Najua sasa hivi mnapigania serikali tatu ili msimame kushangilia kuwa Mwalimu's last legacy is gone!!!
Nimekuandikia wewe na dada yako mleta thread msome!

Maadui wakubwa wa mwalimu ni ninyi mnaomtetea chekbobu kila kukicha!Mwalimu alisema wazi kuwa jamaa hafit!
 
Tofauti iliyopo kati yetu ni kwamba wewe unaifananisha Tanzania na Kenya, Uganda, Rwanda etc.
Mimi naifananisha na Marekani, Uingereza, Japan na Uswisi
. Kwanini unadhani Tanzania imekuwepo duniani ili kuwa na kiwango cha Kenya, Uganda, Rwanda? Hizo nchi zina viwango vya chini mno na havifai kuchukuliwa kama reference. That is where most of you guys do mistakes. Nchi haiwezi kupiga hatua ya maana kama reference point yetu itaendelea kuwa Kenya. There is NOTHING in Kenya to emulate. To try to emulate Kenya, Uganda or Rwanda is a sign of lack of vision!!!


1. Ili vitu vifananishwe lazima viwe na sifa flani/vigezo kufananishwa

-Nipe vigezo vya kufananisha/kulinganisha nchi ya ulimwengu wa kwanza (marekani) na nchi ya ulimwengu wa tatu?

2. Mpaka kufikia sasa marekani imefikisha marais wangapi? na kwanini tanzania ina wanne tu. unazitofaushaje kwa hili hata uzilinganishe?

Ukinijibu hayo tutaendelea nakuonea huruma maana hujuwi unajadili kitugani ndugu yangu.....
 
Sijui ni kwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, LAKINI
Nahisi watanzania tunaweza kuwa tunaongoza kwa kuwa wanafiki bila kujali tumelinganishwa na nani.
Watu wengi ambao wamekua wakitusi UJAMAA pamoja na AZIMIO LA ARUSHA
i. ndio hao hao wanaolalamikia watoto na wadogo zao kukosa mikopo ya ELIMU YA JUU.
ii. Ndio hao hao wanaolalamikia kukosekana kwa huduma bora za AFYA kwenye vituo vya afya na hospital za UMMA.
iii. Ndio hao hao wanaolalamikia kuuzwa kwa makampuni na mashirika ya UMMA kwa wageni.
iv. Na hawaachi kuimba kama sio juhudi zake Nyerere na hayo yote yangetoka wapi.

Na kila kinachopiganiwa hapo ni misingi iliyopo kwenye UJAMAA, sasa sijui ndio tunaimba UBEPARI lakn tunataka kucheza UJAMAA
Hofu yangu ni kwamba watanzania hatusomi maandiko ya Nyerere na wanafalsafa wengine ili tujue malengo yao yalikua ni nini, badala ya kuangalia utekelezaji uliofeli kama kigezo cha kuwakosoa. Serikali ni Mfumo, na kama ni mfumo kufeli kwake hakuwezi kuhusianishwa na mtu mmoja moja kwa moja bila kuangalia wengine walihusikaje kufika tulipofika.
Mwacheni mzee wa watu apumzike, na sie tusalie na uvivu wetu wa kufikiri.


lakini tukubaliane kuwa nyerere hajatufikisha popote na kweli hakuwa na maono. ni kweli alijenga mshikamano wa kitaifa lakini kungine kote alikuwa anaendeshwa na emotions zaidi kul.iko kuangalia ahalisia wa mambo na dunia inakokwenda.
 
Hata kifo cha ccm kinatokana na misingi dhaifu ya nyerere?
Unapojibu zingatia:
1.Ofisi za chama na serikali
2.Viwanja vya michezo
3.mabalozi wa nyumba kumi n.k
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
 
Mengi sana Mkuu Nicholas ya kumuenzi Nyerere pamoja na makosa yake aliyoyafanya, lakini hawa Buku 7 wasaliti wa Watanzania kamwe hawayaoni wao kwao ni kumtukuza DHAIFU ambaye ni kiongozi ambaye utendaji wake ni SIFURI. Nyerere alijenga mashule ya msingi na Sekondari, Nyerere alijenga viwanda chungu nzima na hivyo kuwapatia Watanzania wengi ajira, Nyerere alijenga vyuo ambavyo viliweza kusomesha Watanzania kutoka katika familia za kimaskini ambao wasingeweza kumudu gharama za elimu bure bila kuwalipisha hata senti tano.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mumpe. Hata Mwinyi aliwahi kutamka yeye ni kichuguu inapokuja kwenye Mlima Nyerere. Utendaji wa Nyerere haukuwa perfect lakini wa kiwango cha juu sana ukilinganisha na wote waliokuja baada yake. Pamoja na juhudi zenu za kupindisha ukweli kuhusu Mwalimu lakini habari ndiyo hiyo labda mkawadanganye mambulula wenzenu wasiojua lolote kuhusu Mwalimu. Mpaka kesho kutwa ukikutana na watu wa nchi za nje wakijua tu unatoka Tanzania basi wanakuuliza kuhusu Mwalimu na kila anayemuulizia hutoa sifa kem kem kwamba alikuwa kiongozi mzuri. Hata siku moja huwezi kusikia wanamuulizia Mwinyi, Mkapa au Kikwete.


kwani taifa la Tanganyika litakuwa halina umoja wa kitaifa?Zenj sijui km watawapia chini pemba, au pemba wataungana na mombasa na Lamu au kila kitu kitakuwa km Iraq?

Nyerere kuna mengi ya kumuenzi hata yaliyoshindwa, muungano ukivunjika utakuwa umevunja mpango mmoja kukamilisha mwingine..yaani fate ya wazenj...tayari tuu wameshaanza kuuza haki ya kusajili meli..tayari ni maliberali.....na mengine mengi kufuatia ...wa unguja wanawaita wapemba wa kijijini...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, umesema kweli.

Ninachoona mimi ni UNAFIKI kwa watu wetu. Mashabiki wa serikali tatu ndio haohapo wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu.

Wanaonunua kura wakati wa uchaguzi ndio haohao wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Vinara wa kuomba misaada nje ya nchi ndio haohao wanaojidai kupigania legacy ya Mwalimu. Mabepari ndio hao hao wanaojifanya kupigania legacy ya Mwalimu.

Huu ni UNAFIKI.

Huwezi kusema ugombei Urais mpaka uahidiwe pesa nono kama mshahara wa mbunge halafu ukajifanya unapigania legacy ya Mwalimu.

Huwezi kusema chama chako hakihitaji wanachama Zanzibar halafu ukajidai unapigania legacy ya Mwalimu[/QUOTE].

Lets be true,

Legacy gani ya Mwalimu tunaishi nayo leo?


Unaonesha ufahamu wako ni wakimulugomulugo.

Hoja yetu inasema hivi; Nyerere Alifanya Makosa Makubwa..

Je hayo uloyaandika kwenye rangi nyekundu hapo juu yanauhusiano ndiyo makosa makubwa alofanya nyerere? fafaua
 
Mpaka hapo umeshathibitisha kuwa hakuwa na marafiki. Mimi nilifikiri utatataja wazee wa Musoma, Dar es Salaam, Iringa, Dodoma na kwingineko nchini!

Ukitaka kujua kuwa Mwalimu hakuna na marafiki angalia jinsi familia yake ilivyoachwa na mfumo hivi sasa. Hivi unadhani Nyerere angekuwa na marafiki mtu kama mama Maria Nyerere angeweza kudhurumiwa kiwanja?

Madingi wengi walioiga mfano wa Mwalimu wamestaafu hawana marafiki na wanaishi maisha magumu baada ya kutoka kwenye nafasi zao. Huo ndio ukweli wenyewe. Siku hizi mtu anayeishi kama Nyerere anaonekana mshamba!

Je, ni legacy gani ya Mwalimu tunayoithamini?
safari ndefu sana kujenga nchi ya usawa. unataka kuniambia mama nyerere akidhulumiwa kiwanja marafiki wa nyerere wamsaidie?.unafuata utawala wa sheria?
mama nyerere akidhulumiwa nikama mwananchi wakimasai au waloliondo amedhulumiwia.hakuna special treatment katika sheria. legacy ya mwalimu hujaielewa bado.
 
mi naenda point by point. mkuu.elimu ya kulipia ni bora kuliko ya bure kiukweli.ila nyerere hakutujengengea misingi ya kujua hilo , sijui ni makusudi au hakuwa na maono. hebu we niambie niambie leo hii
elimu ya kulipia na bure ipi bora?.sitaki kusema kwamba mtu anayekuwa rais wetu anatakiwa kuwa nabii!, hapana. hapana, ila anatakiwa kuwa na missions zinazoendana na cotext of the world.


Nitakujibu kwa swali ukilijibu utapata unachokihitaji.

Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya Tsh 1500 kwa siku.

Shule bora za kulipia ada kwa mwaka ni kuanzia 1.5 milion nakuendelea.

Swali watanzania wangapi wanauwezo wa kulipia ada hiyo?

a) wakulima na wafanyakazi wa kawaida

b) wa wafanyabishara za madawa ya kulevya, wabunge na mawazili

c) a, b, na c yote sawa?

Elezea kwanini?
 
Hili swali ungemuuliza Dr. Slaa, wakati anawafukuza uanachama wale wa kambi ya Zitto na kuwapa jina la masalia huku akimpa msamaa kijana wake Ben Saanane ilikuwa ni matokeo ya hila na ulafi ?


Aliwafukuza kwasababu hakutaka kuwa na kundi la walafi, elewa hoja yangu......Alifanya hivyo kuepuka hiyo dhambi.

Je ccm,

a) kunakambi ngapi.......kwanini watu wenyelengo moja la kushika dola, ndani pawe na makundi? (tafsiri ya chama cha siasa tafadhali..)

b) Je ccm wanawezaje kuwa na malengo tofauti ndani ya chama kilekile cha siasa (Makundi)? kwanini hawayakemei makundi?


quote_icon.png
By adolay


3. Je hudhani kwamba kambi ni matokeo ya hila na ulafi wa madaraka kwa maana ya kwamba hakuna haki ila lazima mimi nishinde? fafanua tafadhali...
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Mwalimu alikuwa kiongozi na binadamu kama binadamu wengine. Nyerere aliweka misingi mingi mizuri, kwa kipindi kile. Watu tunabadilika kila siku, na akili zetu zinachambua mambo kutokana na wakati tunaoishi. Misingi mingi iliyowekwa kipindi kile inabidi ifanyiwe marekebisho. Mfano Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umepitwa na wakati. Huu muungano unabidi uvunjwe au ufumuliwe na usukwe upya. Kitendo cha CCM kuung'ang'ania muungano ni sawa na kuturudisha nyuma. Kauli mbiu ya CCM "zidumu fikra za mwenyekiti" ndio inayotakiwa kulaumiwa badala ya kumsukumia lawama Kambarage
 
Mengi sana Mkuu Nicholas ya kumuenzi Nyerere pamoja na makosa yake aliyoyafanya, lakini hawa Buku 7 wasaliti wa Watanzania kamwe hawayaoni wao kwao ni kumtukuza DHAIFU ambaye ni kiongozi ambaye utendaji wake ni SIFURI. Nyerere alijenga mashule ya msingi na Sekondari, Nyerere alijenga viwanda chungu nzima na hivyo kuwapatia Watanzania wengi ajira, Nyerere alijenga vyuo ambavyo viliweza kusomesha Watanzania kutoka katika familia za kimaskini ambao wasingeweza kumudu gharama za elimu bure bila kuwalipisha hata senti tano.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mumpe. Hata Mwinyi aliwahi kutamka yeye ni kichuguu inapokuja kwenye Mlima Nyerere. Utendaji wa Nyerere haukuwa perfect lakini wa kiwango cha juu sana ukilinganisha na wote waliokuja baada yake. Pamoja na juhudi zenu za kupindisha ukweli kuhusu Mwalimu lakini habari ndiyo hiyo labda mkawadanganye mambulula wenzenu wasiojua lolote kuhusu Mwalimu. Mpaka kesho kutwa ukikutana na watu wa nchi za nje wakijua tu unatoka Tanzania basi wanakuuliza kuhusu Mwalimu na kila anayemuulizia hutoa sifa kem kem kwamba alikuwa kiongozi mzuri. Hata siku moja huwezi kusikia wanamuulizia Mwinyi, Mkapa au Kikwete.

Nyerere hakupendwa sana kwa vile alikuwa kikwazo kwa wenye Udini wa mwanzo kabisa....Nyerere pi alikuwa smart sana yeye km yeye ulikinganisha na hawa waliokuwa waki mblack mail...Nyerere ametishiwa sana na watanzania wanaojidaia leo kuwa walipigania uhuru..wakasema km asingewasogeza ili walingane na wengine kielimu na mitaji wangegomea uhuru(kama sensa iliyopita).

Jk amekuw akinara wa kufanya mamabo km ya Zitto..amekuwa na propaganda nyingi sana , na enzi yake ndio watu wadini wamekuwa huru sana kufanya mambo ya ajabu ..watu wana kashifu dini nyingine wanaziita za uongo, makosa yote Jk anasingizia NYerere na Mkapa, watu wake wanamvuta pengo, ....si bure na hiyo imewashika watu wote walio karibu na JK..msikie Zitto na wengine ni slanderers wazuri...na watu w akujifagilia.

kilichoharibika sana nchini kwetu ni historia yetu imepikwa sana kulinda dini ..leo hata haya matukio ya mioto, mauaji yatapita huku dini iliyo mstari wa mbele ikisalimika tena na kuingia miaka mipya as if hawakuhuisika, na wataingia m victim wanaotaka huruma huku wakidai kuwa wao ndio wamedhulumiwa..unafiki na shida walizoleta watazimeza.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom