Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Kwa hiyo haya ndiyo maoni yako uliyowasilisha kwenye marekebisho ya katiba? Tunataka Tanzania mpya yenye kusonga mbele wewe unaleta ngonjera za kijinga kwa vile mnamchukia Nyerere?
 
Nakubali kutokukubakiana na maoni yako. Leta kwanza vielelezo mujarabu na vithibitisho kwamba yeye ndio chanzo cha tatizo...vithibitisho kama takwimu, taarifa za utekelezaji etc. Na pia toa sababu za kwanini unadhani hivyo.
 
marais wanaokuaja sasa wanajiamulia wao. kama sheria Inasema kunyonga wa hawanyongi sababu ni marafki zao. watu wanapesa huko uswiswi wanasema warudishe harafu wasamehewe!. je ndio misingi yetu tuliyojiwekea?.


mazingira gani zaidi ya ya hili hapa chini? kwanini lilifutwa na kutokomezwa? nani alilitokomeza? tujilaumu sisi wenyewe alitukabidhi tukalizika siyo yeye nahumo kulikuwa na miiko na maadili yote..

Unaifahamu miiko na matakwa yaAzimio la ARUSHA? hili lilijumuisha kila kitu.
 
FaizaFoxy nimewahi kuisikia hotuba moja ya Nyerere redioni aliitoa baada ya Mwinyi kuwa madarakani,

Unajua alisema nini? Alikuwa amekasirishwa kwa nini Watz wanajenga shule za sekondari kwa wingi....
Alitaka sekondari ziwe chache sana na za msingi ziwe nyingi, pia akadai kuwa Watu wengi wakisoma
eti wataenda maofisini na miti itakatwa yote kutengenezea fenicha za maofisini, pia akadai kua
watu wote wakisoma hakuna atakaye lima....
Hii hotuba ilinisikitisha sana na ilinifanya niamini kua kweli Nyerere hakupenda kuona watu wanaelimika...
Na ndio maana ameweza kuwafanya asilimia kubwa ya Watz kuwa mazuzu na kumuabudu

Shirikisha vizuri halimashauri ya ubongo wako kutafsiri na kuelewa mambo.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Huu ni unafiki na upotoshaji mkubwa na ni uchochezi. Thibitisha madai yako. Bandiko namba 145.
 
Ndio nini hicho? au Kiswahili ni lugha adimu kwako?

Hapo ujue watu wameshachanganywa no hoja ndio maana wanakosea kiswahili mpaka mantiki haieleweki. anyway yafaa tujifunze na kuelewa philosopy. nyerere alikuwa either awafate wazungu west block au wachina na russia east block.
 
Una kibali cha viongozi wako kusema uliyosema? Ni kweli Nyerere alishindwa kwenye maeneo fulani lakini mimi namwona kama hero aliyesimamia yale alyoamini. hakuwa na price tag usoni kama walivyo baadhi ya viongozi. Aliwapenda watu wake na nchi yake na aliweza kuwatetea toka kwa vibaraka wa nje. Hakuwa mwoga kwamba wakuu wa Magharibi watamtenga... alikuwa mkweli japokuwa alichochagua (siasa ya ujamaa na kujitegemea) ilishindwa katika utekelezaji. Atabaki kuwa baba wa Taifa kwani hata wewe FF huwezi kumnyooshea kidole cha kukosa uadilifu kama ambavyo sasa viongozi wengi wanatajwa kujihusisha either directly or indirectly na biashara chafu wawapo pale patakatifu
 
Mkuu, unaelewa maana ya MSINGI lakini?

Fundi paa anaweza kuweka msingi?

We jamaa una akili za mbayumbayu sasa kama unajua msingi wa nyumba ni mbovu kwanini uendelee kuezeka? Fundi mzuri ni yule anayejua kujenga na kubomoa, ninachoshukuru Team lumumba mnakiri kwamba serikali ya ccm imeshindwa ingawaje mnakiri kwa njia ya indirect wenye akili tushaelewa!! Cdm wanataka kujenga misingi ambayo awamu zote nne zmeshindwa emu wapeni support muone!!
 
Nadhani umepoteza dhana halisi ya maisha yako, ya babu na babu wa bibi yako nadhalia asilia ya wapi ulikotoka na maendeleoa kiuchumi nk.

Je babu wa babu na babu yako alikuwa dini gani? uislam au ukristu umekuja hivi karibuni lakini babu zetu zama zile waliishi kwa imani zao na maisha yalienda.

Hebu tuambie kwanini hulalami kwamba

1. walikula matunda mabichi, mizizi na hawakuswali wala kutawaza nani aliweka misingi ya maisha yao? Nyerere?

2. kama walifanya makosa mbona FaizaFoxy umestaarabika na kumgeukia mtume? vipi hujabaki kulalama kwa wale wasiojuwa kutawaza wala kuenda misikitini?

Wewe mwanamke FaizaFoxy nimpumbavu unaendeshwa na kuwashwa na udini! chuki za kijinga
zisizo na base wala misingi yoyote zaidi ya unafiki na ufedhuli kufanya uchochezi watu waanze malumbano yasiyo natija.

adolay,

Naona umehamaki sana bila sababu, badala ya kujadili hoja umeamua kumshambulia mleta mada.

Nyerere, alikuwa rais wetu wa kwanza hakuna ubaya kumjadili, kuna mazuri na mabaya mengi kafanya, itakuwa kichekesho kuwafunga watu midomo wasijadili, wakati wewe hapo pamoja na wengine mnapata nafasi ya kuyajadili mabaya ya marais waliopita Mwinyi, Mkapa, Kikwete.

Nyerere, siyo malaika alikuwa binadamu nadhani kumjadili kama kiongozi hakuna tatizo.
 
Last edited by a moderator:
marekebisho yake ni azimio la zanzibar?kama sikosei!
Nakushauri kamanda bora huwe msomaji kwenye huu uzi utapata faida, ukiulizwa Azimio la Zanzibar ni nini utajibu kweli.
 
Ndio maana nimekuwa nikiwaambia washabiki wa serikali tatu kuwa likipitishwa hilo tu inabidi tujiulize Nyerere tunamuenzi kwa kipi maana Ujamaa na Kujitegemea tulishaupungia mkono siku hizi tunajivunia misaada na ubepari. Ndio maana tunaona vyama vinavyoahidi mabadiliko vikipokea rundo la pesa toka Ujerumani za kuendesha shughuli zake. Nyerere alihamasisha vyama viendeshwe na michango ya wanachama.

Umoja wa kitaifa ndio kilichobaki ambacho kwa kuleta serikali tatu tunakuwa tumeshauvunja rasmi umoja huo.

Uongozi kwa maslahi ya Umma siku hizi unaonekana ni ushamba na ujinga, uongozi siku hizi ni kwa maslahi binafsi hata wagombea Urais wanaweka vigezo kuwa wahakikishiwe pesa iwapo watashindwa uchaguzi la sivyo hawashiriki!

Je, legacy gani ya Nyerere itabaki?

Serikali ya sasa inamuhenzi nyerere namna gani? kwa kukimbiza Mwenge?
 
Huwezi kujadili challenge za nchi zilizoko kwa sasa na kuangalia positive solution za miaka ijayo bila kuangalia historia ya matukio ya zamani na jinsi yalivyoshughulikiwa kwa sababu kutokufanya hivyo, kutakuwa na uwezekano wa kufanya makosa yaleyale.

Utawala wa Mwl. Nyerere ni mojawapo ya historia ya nchi yetu na katika utawala huo kuna mambo mengi mazuri na mabaya ya kujifunza ili tupate solution ya matatizo yaliyopo na yajayo. Maendeleo yoyote yale chanya mara nyingi yanapatikana kwa kujua udhaifu wa kilichoko na hasa tangu kilipoanzishwa na kutafuta solution ya kukibadilisha katika hali chanya.

Historia ya taifa letu ipo kwa ajiri ya kutuasaidia kujitambua wapi tumetoka na pia inatusaidia kufahamu mabadiliko yaliyotokea kama ni mazuri au mabaya. Ndiyo maana hata Katiba tunayohangaika kuitafuta kama taifa, misingi yake mikuu imekuwa based on our Nation history.

Mbona kuna watu huwa wanapandwa na midadi na hasira pale tu historia ya utawala wa Mwl. Nyerere inapoangaliwa katika macho hasi lakini ni hao hao pia wanapatwa na furaha sana pale inapoangaliwa katika macho chana.

Kama yeye mwenyewe alishawahi kusema kuwa hakuwa "malaika", kwa nini baadhi ya watu wanataka jamii imuone kama alikuwa "malaika" katika macho ya kinafiki. Tujenge nguvu ya hoja na siyo hoja za nguvu kama baadhi ya watu wanavyopenda iwe.

Jamii bado inaangalia na kuzichambua athari za vita vya dunia (1,2) na pia athari ya utawala wa Adolf Hitler kama ilivyo kwa watanzania ambao wanaangalia na kuzichambua athari za kikoloni katika dunia na hii ikiwa ni pamoja na Tanzania. Why not Mwl. Nyerere legacy?.

We can't have Mwl. Nyerere positive legacy without having negative legacy. Huu ndiyo ukweli. Let's talk openy as Jf motto.
Mkuu Ng'wamapalala,

Umendika maneno mazito sana tena yenye ujenzi, huwa inashangaza sana kuona Nyerere anasifiwa midomoni tu, lakini waangalie hao wanaomsifia matendo yao.

Katiba tunayoitumia hivi sasa ndiyo inaonekana ina makosa mengi inampa mamlaka makubwa rais, lakini linapokuja suala la Nyerere na hii katiba hakuna tatizo.

Angalia unafiki mwingine kuhusu huu muungano aliouzisha alikuwa Nyerere na Karume, lakini hawamtaji kama alifanya makosa wao wanailalamikia CCM tu.

Vipi msimamo wa Nyerere kuhusu muungano hao wanajifanya kumlilia Nyerere wanafuata msimamo wa Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni kosa kubwa sana kati ya makosa yaliyowahi kufanywa na kiongozi wa nchi. Usilitaje wala usilikumbushe.



unataka tujadili katika misingi gani kwa hutaki hata kusikia kilo AZIMIO LA ARUSHA. Hebu ainisha hayo makosa makubwa uyaonayo ili tujadili pamoja bila kuwa bias. Tusijadili kitu ambacho hajawekwa ktk uwazi.
 
Mkuu Ng'wamapalala,

Umendika maneno mazito sana tena yenye ujenzi, huwa inashangaza sana kuona Nyerere anasifiwa midomoni tu, lakini waangalie hao wanaomsifia matendo yao.

Katiba tunayoitumia hivi sasa ndiyo inaonekana ina makosa mengi inampa mamlaka makubwa rais, lakini linapokuja suala la Nyerere na hii katiba hakuna tatizo.

Angalia unafiki mwingine kuhusu huu muungano aliouzisha alikuwa Nyerere na Karume, lakini hawamtaji kama alifanya makosa wao wanailalamikia CCM tu.

Vipi msimamo wa Nyerere kuhusu muungano hao wanajifanya kumlilia Nyerere wanafuata msimamo wa Nyerere.

Nadhani mkuu una nafasi kubwa tu ya kusaidia nchi hii kutoka hapa ulipo. Katiba inakuruhusu kugombea hata uraisi ukatekelza maono yako. Sioni faida ya kumhukumu mtu aliyeondoka madarakani miaka 20 iliyopita. Marekani imejengwa ma maraisi mbalaimabli wala sio raisi mmoja. Huku kunaitwa kutojiamini kusingizia kuwa makosa yako ni sababu ya mtu fulani
 
Hebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.

-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari

-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....

-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?

-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.

-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu

-Mbuga za wanyama na maliasili

Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?

-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)

Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.
kila wakati na mambo yake..wakati wa nyerere jeshi limeasi,majaribio mawili ya mapinduzi,vijana wameteka ndege na kuipeleka londoni,etc
 
Sihui ni kwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, LAKINI
Nahisi watanzania tunaweza kuwa tunaongoza kwa kuwa wanafiki bila kujali tumelinganishwa na nani.
Watu wengi ambao wamekua wakitusi UJAMAA pamoja na AZIMIO LA ARUSHA
i. ndio hao hao wanaolalamikia watoto na wadogo zao kukosa mikopo ya ELIMU YA JUU.
ii. Ndio hao hao wanaolalamikia kukosekana kwa huduma bora za AFYA kwenye vituo vya afya na hospital za UMMA.
iii. Ndio hao hao wanaolalamikia kuuzwa kwa makampuni na mashirika ya UMMA kwa wageni.
iv. Na hawaachi kuimba kama sio juhudi zake Nyerere na hayo yote yangetoka wapi.

Na kila kinachopiganiwa hapo ni misingi iliyopo kwenye UJAMAA, sasa sijui ndio tunaimba UBEPARI lakn tunataka kucheza UJAMAA
Hofu yangu ni kwamba watanzania hatusomi maandiko ya Nyerere na wanafalsafa wengine ili tujue malengo yao yalikua ni nini, badala ya kuangalia utekelezaji uliofeli kama kigezo cha kuwakosoa. Serikali ni Mfumo, na kama ni mfumo kufeli kwake hakuwezi kuhusianishwa na mtu mmoja moja kwa moja bila kuangalia wengine walihusikaje kufika tulipofika.
Mwacheni mzee wa watu apumzike, na sie tusalie na uvivu wetu wa kufikiri.

Watanzania hatujui tunataka nini.
 
Mkuu, umesema kweli.

Ninachoona mimi ni UNAFIKI kwa watu wetu. Mashabiki wa serikali tatu
ndio haohapo wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Wanaonunua kura
wakati wa uchaguzi ndio haohao wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu.
Vinara wa kuomba misaada nje ya nchi ndio haohao wanaojidai kupigania
legacy ya Mwalimu. Mabepari ndio hao hao wanaojifanya kupigania legacy
ya Mwalimu.

Huu ni UNAFIKI.

Huwezi kusema ugombei Urais mpaka uahidiwe pesa nono kama mshahara wa
mbunge halafu ukajifanya unapigania legacy ya Mwalimu.

Huwezi kusema chama chako hakihitaji wanachama Zanzibar halafu ukajidai
unapigania legacy ya Mwalimu.

Lets be true,

Legacy gani ya Mwalimu tunaishi nayo leo?

Dr. una hoja nzuri lakini kwa kua mada hii imeletwa na kada mwenzio wa Lumumba basi unataka kuuma kwote kwote, pia unachanganya na hisia za chama zaidi, hapo ndipo unapoharibu dr na kua Dr. Manyau Nyau
 
mkuu . sio kwamba watu hatusomi/hatujui ujamaa na siasa za kujitegemea. ni kwamba hivyo vitu haviwezekani kwa
raisi asiye na msimamo au asiejua context of the world politics and economics kama nyerere. nyerere hakua na maono.

Tatizo sio JKN, tatizo ni sisi wenyewe esp. waafrika. Ni nchi nyingi jirani zetu na nyinginezo za afrika zilichagua mrengo wa siasa tofauti na za JKN lakini zipo nyuma yetu kiuchumi na kiubora wa maisha ya mwananchi wa kawaida. Kwa maana hiyo je ni sahihi kusema kwamba siasa za JKN zilikuwa bora kulinganisha na za hao marais wa nchi nyingine za afrika?
 
Back
Top Bottom