NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Pasco hapa ndipo unapoweza kumaliza hasira za Boss wako, hakuna kulala mwambie Lowasa akupe details zote anazozifahamu lete mwaga hapa na from there indio utakuwa mwisho wa matumizi ya neno kujivuwa gamba.

Kuna storm kubwa inakuja ambayo cha kusikitisha mpaka sasa Watanzania wameshindwa kusoma alama za nyakati kwamba Mungu ameamuwa kujidhihirisha upande wa Wananchi lakini cha kushangaza taasisi za kiraia na kidini ziko kimya juu ya swala hili.

Kwa hakika huu ndio wakati muhafaka wa kuing'oa serikali ya Kikwete madarakani, hatuna sababu ya kusubili mpaka 2015 maana hata JK akisema avunje baraza lake leo atapata Mawaziri kutoka miongoni mwa Wabunge wepi? Lusinde!!??....

hapo kwenye red, mkuu acha tu hizo taasisi zikae kimya, wakizungumza upande mmoja watasema ni CDM, tunahitaji kura zakutosha toka ukanda wa pwani 2015, kwa sasa ngoja wasitibue mambo, hope umenielewa, upande mmoja wa hizo taasisi utapingana na upande mwingine pasipo hoja kwa sababu tu ya shule kuwa ndogo.
 
makubwa 45 years hata kama ni China ni wehu uliopita kiasi fikirieni kabla ya kupokea misaada mingine
 
CEO/MD/DG wa TPA anasemaje? Mwenyekiti wa Board ya TPA ana maoni gani? Ni lini uwekezaji huu ulihamia wizarani? Kwa taratibu zipi?
 
Wakati wa Waziri mwingine kwenye wizara hii na Wizara ya fedha kulitokea zengwe kama hili kuhusu Fibre Optic Cable kama ICT infrastructure Ya nchi nzima.

MoU zilisainiwa baadhi ya wataalamu hawakuhusishwa ilikuja kujulikana wakati wa negotiation ya mkopo wakati wengine wanazungumzia feasibility study kumbe MoU imesaininiwa na mkataba upo tayari kwa kigezo cha kukidhi matakwa ya mkopo.

Anayoyasema Nundu ni common practice isiyokubalika (ambayo haimtoi kwenye hatia)

Kinachouma

1. Kutumika vibaya kwa wataalamu

2. Mchezo wa kila siku wa mawaziri kuteuliwa kwa sababu kuna dili linaiva

3. Kutekwa nyara miradi bila usimamizi wa kuhakikisha kuwa kusudio lililobuni mradi linafikiwa.

4. Cheapness ya watumishi kulipiwa gharama za usafiri na posho uchwara kubariki huu ubazazi na upuuzi.

5. Taratibu vurugu ambazo si rahisi kumkata mtu mmoja na kumwajibisha

Way Forward

1. Kutofautisha uongozi wa kisiasa na wakitaalam kwa kuweka mipaka ya wazi. PS ndiye accounting officer wa wizara lakini kama alivyosema katibu mkuu fedha amekuwa reduced kupendekeza/kumshauri waziri.

2. PS asiteuliwe kisiasa kwa sababu accountability ni suala la kitalaam ambalo kwa sasa halipo kwenye utawala unaoongozwa na CCM kwa maslahi ya kifisadi.

3. Watumishi wawe screened properly kwa sababu wanawekwa kimikakati kutekeleza haya madudu wakiwa wakala wa mafisadi kwa kujua au kutokujuwa.

4. Uongozi wa mashirika ya umma yasiteuliwe kisiasa kwa maana utawala wa CCM kwa sababu mashirika mengi kazi zake ni specialised wanasiasa wanajuaje ubora na utaalamu wa kiongozi kama wa bandari kama si kimaslahi binafsi.

HITIMISHO

Mfumo wa serikali umeuawa pole pole toka awamu ya pili kwa kuondoa taratibu proffessional za kuendesha serikali eg Makatibu wakuu / wakurugenzi hawakuwa wanasiasa na hawakuteuliwa kisiasa.

Kuna haja sisi sote tumiliki serikali kama inavyosema katiba ya nchi kwa kukemea na kuonyesha wazi serikali inapokwenda kombo. Maana yangu maisha yetu ya kawaida, mitaala ya elimu kwa ngazi zote hata elimu ya ngumbaro ilenge kujenga utaifa na kuithamini serikali kuwa ni nyetu na siyo kukurupuka na mkakati wa JKT pekee au kuwaachia wabunge kazi za ziada za kupambana wao kwa wao kwa uzembe wa watu waliokasimiwa madaraka.

Tuunge mkono kwa gharama yo yote mkakati unaoendelea wa kuiwajibisha serikali, wala tusisikilize porojo za akina Nundu kwa sababu wanavyotaka kutuaminisha wanadhihirisha umbumbu wao wa kiutawala na kutokuwa na uzalendo kwa taifa.

Iwe fundisho kuwa utaratibu wetu wa kuwapata watawala una kasoro hadi wezi na mafisadi wanaingia hadi ngazi ya juu kabisa ya uongozi.

TUSILILIE TULIPOANGUKIA BAADA YA KUJIKWAA, TUBAINI TULIPOJIKWAA TUONDOE KISIKI
 
Unajua kuna kitu ambacho mpaka sasa najiuliza kama nimesoma nikaelewa, au macho yangu yananichezea; MOU inasema kampuni ya China ina "build, own and operate, na ku-hand over baada ya miaka 45". Wakati huo huo mkopo toka Exim unachukuliwa na Tanzania, na pia kulipwa na Tanzania kwa interest ya asilimia 2%.

Hivi ni macho yangu au hizo ndio facts za huu mradi?
 
Nundu ameonyesha udhaifu katika uongozi wake maana kama alijua ni naibu wake ana matatizo kwa nini hakusema
 
Tanzania ni balaa, sasa huo mradi alioukata yeye wa wazili mwenzake wa $542,000,000 ambao wawekezaji hao wataendesha bandari kwa miaka 15, kisha unarudi serikalini-TPA, yeye wakwake wa bei nafuu ni $300,000,000, wawekezaji wataendesha mradi kwa miaka 45...... yupi nafuu kati yao?
 
Yuko wapi kiongozi mkuu wa kisasa hapa nchini ambao wengi wa wanaoingia hii mikataba ama kawateua kwa kuwafahamu au kaletewa majina.

Na anachukuliaje hali kama hii wakati hao wateule wake wanaendelea kutafuna mbegu wakati mvua zaendelea kunyesha shamba liko tayari ila hakuna upandaji wowote? Tutavuna nini? majani? Tutapata wapi chakula kwa watoto na wajukuu zetu kama mbegu zote zitakuwa zimetafunwa na mwenye maamuzi ya kuwakataza wale yupo anawachekea?

Yupo ila anasubiri UPEPO upite......

Kuweni wavumilivu kidogo, the ship is on the right course.
 
Kumbe CCCC ni ya RA jamaa anatisha sana

"Politicians are often accused by their opponents of claiming to be honest and seek the truth while using spin tactics to manipulate public opinion"..... RA hapa munamleta kujenga chuki. Kwa taarifa yenu RA katulia sana sasa.... labda ataibukia Kagoda, makaburi yatakapofukuliwa soon. Hapa jibuni HOJA
 
"Politicians are often accused by their opponents of claiming to be honest and seek the truth while using spin tactics to manipulate public opinion"..... RA hapa munamleta kujenga chuki. Kwa taarifa yenu RA katulia sana sasa.... labda ataibukia Kagoda, makaburi yatakapofukuliwa soon. Hapa jibuni HOJA

Kwa hiyo mkuu unaona haiwezekani CCCC kuwa mikononi mwa RA?
 
Unajua kuna kitu ambacho mpaka sasa najiuliza kama nimesoma nikaelewa, au macho yangu yananichezea; MOU inasema kampuni ya China ina "build, own and operate, na ku-hand over baada ya miaka 45". Wakati huo huo mkopo toka Exim unachukuliwa na Tanzania, na pia kulipwa na Tanzania kwa interest ya asilimia 2%.

Hivi ni macho yangu au hizo ndio facts za huu mradi?

Sio macho yako kiongozi, huo ni utaratibu waliojiwekea hii serikali ya ccm. Yaani ni sawa na mtu ukope bank kujenga nyumba, bank ikukuposhe hela za ujenzi, bank hiyo hiyo ikuletee mkandarasi na kukulazimisha umchukue, kama haitoshi bank hiyo hiyo ihamie kwenye hiyo nyumba na kufanya shughuli zake kwa muda wa miaka 45, lakini wakati huo wewe mkopaji unalipa riba! Lakini kumbuka ardhi/kiwanja ni chako wewe muombaji! Hivi kuna mkopo kweli hapa?

Ninachoweza kusema ni kwamba watanzania tuwe macho na mikopo ya kichina kuanzia serikali hadi makampuni ya watu binafsi toka China. Pia ni vizuri tutambue kuwa hiyo 2% ya riba inaonekana kama ni mkopo wa bei nafuu, lakini wanachofanya hawa wachina ni kwamba wanapotoa mkopo i.e $300 milioni, wanakuwa tayari wameshaongezea cha juu hivyo kushusha riba 2%.
 
Acheni uvivu wakuu,kama mnatumia simu sawa, ila hapo kuna file Invisible ameattach mautamu yote yapo humo, kabla ya kucomment angalie kwanza maana amesema hapo inabidi u download hataki kumwaga mtama kwenye kuku wengi....
Mimi nadhani hapa shida sio kudownload hilo file, hapa shida lugha iliyotumika ndo tatizo.
 
Haya ndiyo yalikuwa yanasemwa bungeni.
Hapa Invisible una maana gani kuwa Nundu ni msafi?

Heading ya hii thread ni 'Nyaraka:Je, Omar Nundu ni msafi?'

Kuna alama ya kuuliza hapo. Ukisha soma nyaraka hizo ndio ujibu hilo swali.
 
Nini kosa la Nundu hapo? Nundu amezuia kampuni moja isipewe huu mradi kwani wao ndio wapange bei, wafanye utafiti, wapewe kazi nayo ni CCCC na hayo ni kabla Nundu hajawa Waziri. Kwa hiyo afukuzwe kwa kuzuia ubadhirifu?

Mnaelewa mnachokisoma na kukisema?

Usiwe mpuuzi wewe......kama hujui mambo kaa kimya.........Waziri Nundu anadai kuwa hajui mpangao wa serikali TPA na CCCC....hii tu pekee inamfanya HAFAI................pili umesoma hiyo MoU ilivyo........umesoma barua ya hao wachina kwa waziri Nundu.........hivi wewe unajua haya mambo yanatakiwa yaende vipi.......Hivi JK alienda Brazil kufanya nini.......
stop being fool.........kwa kupenda chongo
 
Tanzania ni balaa, sasa huo mradi alioukata yeye wa wazili mwenzake wa $542,000,000 ambao wawekezaji hao wataendesha bandari kwa miaka 15, kisha unarudi serikalini-TPA, yeye wakwake wa bei nafuu ni $300,000,000, wawekezaji wataendesha mradi kwa miaka 45...... yupi nafuu kati yao?
kwanza huo mradi wake wa kuiweka nchi rehani kwa miaka 45 sio uhaini huo? si inatakiwa kupita katika baraza la mawaziri? au ndio ticts nyingine inaingia, kwa uwezo wa waziri sifikiri kama ni busara kusaini mkataba wa zaidi ya miaka 5, la sivyo aombe kibali cha baraza la mawaziri, kwa baraza lote kuuchambua huo mradi na kuona faida na hasara zake.
 
Hili suala zima ni kizungumkuti.. Kama Mh. Nundu alikuwa anayajua haya alioyasema jana.. kwani alicilipeke kwa boci wake na katika vikao vyao vya mawaziri..? Pale Mlimani city ninacikia wana mkataba wa miaka 30.. Sasa kama hii gati itamilikiwa na jamaa kwa miaka 45 itakuwa balaa.. Ina maana kwa umri wangu cintobahatika kuona sherehe ya kulirudisha kwa serikali gati letu hilo..! Kweli Tanzania ni shamba la bibi..
 
Huyo Nundu anachekesha watu walioenda shule. Baada ya kuona deal limebumburuka ndio "ANAJINASUA". Na yeye yumo kwenye hiyo issue. Wakina - Zito endelea....
 
Back
Top Bottom