NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Ivi waziri akilidanganya bunge azabu yake ni nini?
Maana Nundu alisema hakuna MOU ambayo mesigniwa na akasema kamati imereport uongo!
This is to much now!With these facts huyu Nundu has to go!
 
Waziri Nundu hawezi kujitetea katika hili.

Kama kweli alikuwa na uchungu na nchi yake na alikuwa anataka haki itendeke basi angetafuta Kampuni ambazo zingefanya upembuzi yakinifu na kutoa ushauri wa gharama kwa serikali siyo Kampuni mbadala.

Alichofanya yeye kinaonyesha kabisa alikuwa na maslahi binafsi. Kwanini hakufanya hayo aliyokuwa anajitetea bungeni na kwa waandishi wa habari?
 
Mmmmmmmmmmmh mambo ya BOOT yaani build, own, operate and transfer kwa kweli kazi kwelikweli. Accountability is what we Tanzanians need.
 
Ama kweli huu ugonjwa wa Uwajibikaji na kuheshimu utaratibu wa utendaji kwa mujibu wa kanuni na sheria umewapita pembeni wengi wetu.

Toka Invisible aweke hii kitu hewani wachangiaji kila moja anavutia kamba upande wake kama wabunge walivyofanya mjegoni.(CCCC vs China Mechant/waziri Nundu vs Mtangulizi wake)

Badala ya kuweka msisitizo kuwa wote hawa wametenda nje ya Mfumo wa kisheria, unaowataka kutangaza Tenda kwa umma ilikuleta ushindani na kutuepusha na haya yanayoendelea ya kila mhusika kuwa na Kampuni yake ya Mfukoni.
 
Mkuu wangu pengine mimi sikusoma vizuri lakini sioni hata hiyo ya kwanza imefuata kitu gani..nakuomba soma hoja namba 10 ya n00b kuna mahala imeeleza wazi kwamba ni CCCC walioonyesha interest ya kujenga mradi huo mwaka 2009, haikuonyesha ufuatiliaji wa Public procuament za wakati ule.

Mkuu kwa hiyo ya kwanza kutokufuata sheria au utaratibu kuna halalisha ya Pili nayo kufanya hivyo au sijakusoma vizuri!
 
Nchi imeoza.

Pande zote 2 kuna tatizo. Kwanza ni kwa nini hiyo kazi isitangazwe wazi kampuni zishindane kama taratibu zinavyotaka.

Inakuwaje wizara 1 inakua na makundi mawili kila moja linakimbiza dili kivyake hii pia ni dalili kuwa kuna harufu mbaya kwenye dili nzima.

Lakini huyu Nunda ndio ametia fora hata aibu hana. Yuko tayari kukabidhi mradi pekee unaozalisha kwa wageni kwa miaka 45 kwa pesa ambazo naamini mradi ukikamilika gharama za ujenzi zinaweza kupatikana ndani ya mika 10.

Kichekesho zaidi ni jinsi ujinga huu ulivyo wazi lakini mamlaka husika zimeshindwa kuwawajibisha wahusika.

Kwa ushahidi huu naelewa sasa kwa nini hata magogoni wanajikanyaga.

Kwa sasa hatima ya nchi hii ipo kwa Watanzania wenyewe. Hakuna tena uongozi jahazi la nchi linazama.
Asante mkuu.
Hii kipande nilikuwa sjakisoma.
Nashangaa sana watu wanazungumzia Nundu! Nundu!,wakati Mradi kwa ujumla wake ulikuwa si halali kisheria.Nitapata kuamini kama atakuja mtu na hoja kuwa kampuni ya mwanzo ilitumia utaratibu fulani wa kisheria kufikia hatua ya kupewa kazi hiyo.
 
Hapa naona Tunatwanga maji kwenye kinu. Nyaraka zinajieleza, watu wanapaswa kujibu yaliyomo katika hizi nyaraka angalao kwa data kama nyaraka hawana, lakini si kwa kutoa tuhuma nzito ambazo yeyote anaweza kuzitoa. Hata wapo ambao wanasema mtu wa karibu na wakubwa ndiye aliyempeleka Nundu China lakini kwa kuwa tuhuma hizo hazina ushahidi, watu wanajadili nyaraka zilizopo, leo Nundu anasema Naibu katumwa na wakubwa kwa sababu tu kapewa ruhusa na PM kwenda China wakati taratibu za serikali zinataka Naibu na Waziri wote waombe kibali kwa PM wanaposafiri!!!
 
Back
Top Bottom