Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 945
MHE. JANEJELLY NTATE AIBANA SERIKALI KUHUSU SHERIA YA KUTUMA NYARAKA ZA SERIKALI SEHEMU ISIYOHUSIKA HUSUSANI MAGROUP YA WHATSAPP
"Sasa hivi kuna utaratibu wa viongozi au maafisa kufungua group la WhatsApp na kutumiana nyaraka za kiserikali ndani ya group. Sheria ya TEHAMA mliyoitunga inazungumzia humo? Kama haimo na hairuhusiwi mnafanya nini ili sheria ijumuishe ili kuwaepusha wanaotumia huo mtandao wasije kupatwa na matatizo ya kuhukumiwa kwa kukutwa na nyaraka za Serikali sehemu zisizohusika?" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam
Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
MSITUME NYARAKA ‘WHATSAPP’ NI MARUFUKU
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema sheria inayosimamia nyaraka za Serikali inaelekeza kuwa mawasiliano ya Serikali yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo.