NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Duh waTanzania tunahitaji kubadili mfumo wetu wa uendeshaji wa serekali huu utaratibu wa kumwachia waziri mamlaka makubwa kiasi hiki tusipokuwa makini tunaweza kujikuta hakuna nchi inayoitwa Tanzania.

Waziri anataka kukabidhi bandari miaka 45 halafu kuna mijitu ya hovyo kabisa inamtetea.

Wewe ulitakaje mkuu

maana kuna hiyo ya miaka 45 na kuna gharama ya mradi US$500MILION badala ya US$ 300 MILION?
 
Hakuna maneno mengi, Nundu ni mwizi au ni jambazi, angalieni kwa ufasaha maneno ya kwenye mkataba, tunakopa mkopo wa milioni mia sita na baada ya miaka mitatu tunaanza kulipa asilimia mbili ambazo ni milioni 12 dola za kimarekani kwa kila mwaka. Ukiendelea kutoa zinazokuwa zimelipwa na kuweka riba ya 2% kwa muda wa miaka kama kumi tutakuwa tumelipa tu kiasi cha milioni miamoja, maana yake tutalipa deni hilo kwa miaka karibu 50, na wakati huo mkataba unasema wao wachina wata-operate, na wata-own terminal 13&14. Hakuna wala ubia na TPA ila wamekabidhiwa tu.

Swali ni kwanini sisi ndiyo tukope na kulipa wakati ni mtaji wa wengine? Kampuni kama inatoka china na Exim Bank ni branch ya China kwa nini isiwe kama inavyokuwa katika ujenzi wa barabara, mwenye kampuni ndiye anayeomba mkopo na atarudisha kwa kulipwa kwa gharama zilizokubaliwa.

Kuwapatia bandari kwa miaka 45 (kwa hakika Nundu atakuwa hayupo hai vinginevyo aishi miaka mia!!!) ni zaidi ya ujambazi. Pesa hizo zingekopwa na TPA na TPA wakatoa tender kwa mtindo wa kushindanisha ili tujue nani analeta quotation yenye unafuu. Lakini hii ya kukutana na watu kimya kimya huyu kakutana na CCCC na huyu kakutana na hiyo ya Nundu naona kote kuna dalili za rushwa na hata hiyo gharama anayosema Nundu ameokoa hajaokoa chochote badala yake amegawa zaidi maana miaka 45 halafu sijui ndo iweje!!!! Maana mkataba haujasema.

Wanasheria wa wizara jamani kuweni wazalendo nawe Werema sijaona kama hata ulipewa nakala ya mikataba hii!!!! Hata hivyo naomba wanasheria mnitafsirie hii ya mwisho kwamba Part B shall Build, Own, Operate and Transfer (BOOT) sasa hiyo Transfer ni ya pesa ziptokanazo na mapato wakati waki-operate au ni kurudisha gati na. 13&14 baada ya miaka 45? ? ? Sijaelewa hapo.
 
Mamlaka mengine mawaziri hawa hawana! Mashirika ya UMMA yana sheria yake inayoyaanzisha ambayo pamoja na mambo mengine inaeleza wazi yanavyopasa kujiendesha kwa kutumia Boards zake za Wakurugenzi. Kwa nini wanasiasa wetu wanaachwa kuenenda hivi sijui!
 
Kwani lazima tujifunge kwenye us 500 mil au us 300 milioni.Mkuu wangu tunaweza kuanza upya na kwa uwazi zaidi nakuhakikishia gharama zitashuka mpaka ushangae kinachopiganiwa hapa ni maslahi makundi kuna kundi moja limesha lamba dume na kuna kundi linatafuta ulaji wangeelewana mapema hizi kelele tusingezisikia hata kidogo.

Mkuu engmtolela nataka uwazi na uwajibikaji zaidi mikataba inayogusa rasilimali za watanzania haiwezi kufungwa na mtu mmoja au kikundi kidogo cha wanasiasa nilitegemea maoni ya wataalamu wa uchumi,usafirishaji na wanasheria yangepewa nafasi kubwa badala yake majina ya akina Mkullo,Nundu .... yamechukua nafasi kubwa.

Kwanza TPA wana management yao na Bodi yao waziri Nundu anaingiaje hapa ?.

Wewe ulitakaje mkuu

maana kuna hiyo ya miaka 45 na kuna gharama ya mradi US$500MILION badala ya US$ 300 MILION?
 
Nasubiri Tamko kutoka Ikulu kwamba Rais asihusishwe or hana Taarifa kwa kipande cha nchi yake kupewa wageni kwa karibia nusu karne (miaka 45).Bravo JK na watendaji wako!
 
Kwa viwango vyovyote vile ni wazi kuna triangle ya uchafu kati ya wizara ya Nundu, wizara ya Mkulo na TPA.
Hata sioni kwa nini tujadili nani msafi wakati ukweli upo kwenye makaratasi hayo.

Nundu anamtuhumu naibu wake hadharani, je amepata kupeleka tuhuma hizo kwa JK??
Kama hajapeleka kwa nini hajafanya hivyo???
Na kama amepeleka je hajaridhika na hatua zilizochukuliwa na JK???
Kama hajaridhika na hatua alizochukua JK, kwa nini bado ameshikilia uwaziri badala ya kujiudhuru???

This is just an ice-breaker, utamu bado unakuja.........

Hapa ni Wizara nzima kusafishwa, kama Waziri anamtuhumu Naibu hadharani, hapa hakuna tena Wizara. Hata kama anajidai ni safi, Nundu tayari ameonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi. Kwanza hana busara hata kidogo na mkurupukaji. Huwezi kuzungumza aliyoyazungumza ukitegemea kuendelea kuwa mbunge, wala si tu Waziri.

Unawatuhumu wabunge wa kamati, ambao ni wengi, bila ya ushahidi wowote!! Unamtuhumu Katibu mkuu na mamlaka na bodi bila aibu na bila kuwa na ushahidi, kwa nafasi yake hapaswi kuzungumza kwa hisia, angewaachia watu wa chini kabisa kuzungumza aliyoyasema si yeye kama Waziri. Ni Tanzania tu haya yanatokea. Wote wang'oke, hata Waziri na Naibu na Katibu Mkuu abadiliswe.

Hii Tanzania, mtu anafanya madudu anakomaa tu, eti anataja wengine, hivi kumtaja Naibu kuwa mchafu ni kuongeza tu idadi ya wachafu si kujisafisha.
 
Wapo wapi wasomi wetu wanaojitapa kila siku humu JF watusaidie wanaingiaje hii mikataba ya hii nchi kijinga namna hii.
Yuko wapi kiongozi mkuu wa kisasa hapa nchini ambao wengi wa wanaoingia hii mikataba ama kawateua kwa kuwafahamu au kaletewa majina.

Na anachukuliaje hali kama hii wakati hao wateule wake wanaendelea kutafuna mbegu wakati mvua zaendelea kunyesha shamba liko tayari ila hakuna upandaji wowote? Tutavuna nini? majani? Tutapata wapi chakula kwa watoto na wajukuu zetu kama mbegu zote zitakuwa zimetafunwa na mwenye maamuzi ya kuwakataza wale yupo anawachekea?
 
Ni aibu kubwa sana kwa serikali; Nundu kama huhusiki na hii dili basi ujiuzulu kwa kushindwa uongozi na unafiki. Kwanini unasema leo jambo hili. Pasco nilikuona jana ukiwa na Mhe.Nundu ukimshauri namna ya kushusha hizo nondo
 
Yaani nipo HOI kwa hiyo MOU ya miaka 45 kwa mpango wa BOOT.

Ina maana kwa umri wangu huu nitakufa bado jamaa wanaendelea kumiliki GATI!!!!!!!!

Na watoto wanaozaliwa leo watafikisha miaka 45 au kufa kabla ya mkataba haujaisha.

BALAA!!!!! NCHI INAUZWA HII JAMANI TUAMKE!!!!!!!!!

VINGINEVYO NCHI INABAKIA KAMA PICHA HII HAPA

Skeleton.jpg

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hakuna maneno mengi, Nundu ni mwizi au ni jambazi, angalieni kwa ufasaha maneno ya kwenye mkataba, tunakopa mkopo wa milioni mia sita na baada ya miaka mitatu tunaanza kulipa asilimia mbili ambazo ni milioni 12 dola za kimarekani kwa kila mwaka. Ukiendelea kutoa zinazokuwa zimelipwa na kuweka riba ya 2% kwa muda wa miaka kama kumi tutakuwa tumelipa tu kiasi cha milioni miamoja, maana yake tutalipa deni hilo kwa miaka karibu 50, na wakati huo mkataba unasema wao wachina wata-operate, na wata-own terminal 13&14. Hakuna wala ubia na TPA ila wamekabidhiwa tu.

Swali ni kwanini sisi ndiyo tukope na kulipa wakati ni mtaji wa wengine? Kampuni kama inatoka china na Exim Bank ni branch ya China kwa nini isiwe kama inavyokuwa katika ujenzi wa barabara, mwenye kampuni ndiye anayeomba mkopo na atarudisha kwa kulipwa kwa gharama zilizokubaliwa.

Kuwapatia bandari kwa miaka 45 (kwa hakika Nundu atakuwa hayupo hai vinginevyo aishi miaka mia!!!) ni zaidi ya ujambazi. Pesa hizo zingekopwa na TPA na TPA wakatoa tender kwa mtindo wa kushindanisha ili tujue nani analeta quotation yenye unafuu. Lakini hii ya kukutana na watu kimya kimya huyu kakutana na CCCC na huyu kakutana na hiyo ya Nundu naona kote kuna dalili za rushwa na hata hiyo gharama anayosema Nundu ameokoa hajaokoa chochote badala yake amegawa zaidi maana miaka 45 halafu sijui ndo iweje!!!! Maana mkataba haujasema.

Wanasheria wa wizara jamani kuweni wazalendo nawe Werema sijaona kama hata ulipewa nakala ya mikataba hii!!!! Hata hivyo naomba wanasheria mnitafsirie hii ya mwisho kwamba Part B shall Build, Own, Operate and Transfer (BOOT) sasa hiyo Transfer ni ya pesa ziptokanazo na mapato wakati waki-operate au ni kurudisha gati na. 13&14 baada ya miaka 45? ? ? Sijaelewa hapo.
.
Yaani kwa kweli inasikitisha!

.
 
Nathani hujasoma vizuri au kiingereza kinakupiga chenga CCC iliandika proposal na ku-solicit funds (a soft loan with 3% interest with grace period of 3 years after construction is completed) from Exim Bank China kupitia serikali yao! yaani wanaaminika huko kwao na wana experince kampuni ya tano kwa ukubwa duniani kwenye uendeshaji wa bandari! sasa unapouliza uwazi wa tender hii ulipaswa kuulizia pia hao China Merchant ltd wana uwazi upi huo wa kwenda behind the scene kujaribu kumshawishi waziri kuvunja makubaliano na CCC ambao washasaini MOU na wame-secure funds! Au hasara ya fidia kutokana ujuha wa kuvunja mikataba kiholela bado hazijawafunza kitu nyie mambumbumbu? Hayo mengineyo sitaki kukujibu maana umeandika upuuzi na bali jua tu Nundu ni mwizi sura yake haijalishi....!

Kuna vitu nilikuwa sitaki kuzungumza humu: Kwanza nikufahamishe kwamba mimi nimesoma Uingereza na nimekaa huko zaidi ya miaka saba, nimefanya kazi na Wachina zaidi ya miaka kumi na ushee kwa hiyo najua Modus Operandi ya Wachina wa siku hizi, la tatu Mh.Nundu anijuhi na wala sijawahi kukutana naye; mambo mengine hayaitaji kusomea mambo ya sayansi ya roketi kutambua ni akina nani wanao pania kunufaika na mradi huu mzima by hooks and crooks wana inflate thamani ya mradi husika wanafikili hatuna akili.

Analytical mind ya kawaida tu inakudhilihishia wazi ni nani ana Uzalendo wa kweli kati ya Mh.Nundu na group lililo mkalia kooni kwa kutaka kichwa chake - hivi mzalendo wa kweli anaweza kuafiki mkataba ambao huko open ended bila kuwa na check and balance, mpaka Dogo Mnyika alipo nusuru jahazi na Mh. Nundu kuhafikiana naye, unataka kutueleza kamati hilo walikuwa awalioni!!!!!! Alafu muadishi wa post hii amekasirika as if naye anafanya kazi wizarani-WHY?

China kuna makampuni lukuki ambayo ni mahili katika mambo ya ujenzi, why pick CCCC; kampuni ambayo inazunguka zunguka tu hapa Tanzaini kufanya lobbing na ku-exploit weakness za wazalendo wasiokuwa na uaminifu - kwa nini awakai kwao wakasubiri atima ya tenda yao, some Chines are very cunning; waulize TTCL ilivyo ingizwa mkenge kwa kushikizwa na Wachina kwenda mfumo wa CDMA wakati makampuni yote ya simu nchini ni GSM.

Mwisho nataka kuwaelezeni kwamba ni mara chache ma-injinia kujihingiza katika mambo ya ajabu ajabu-wao wanalidhia kuona projects zao zina take off na kukamilika na kuona zinafanya kazi kama walivyo kuwa wanafikilia, mambo ya pesa na hujuma ni secondary kwao. Mimi namuomba Mh.JK ampe rungu Mh.Nundu a-deal na watu hawa kwa nguvu zake zote bila kuogopa mtu yeyeyote-Watanzania wengine wamekubuhu katika kufanya mambo ya fitina, uzushi na kuaribiana sifa na hii ndiyo inayofanyika katika Wazari hii, Waziri asipokuwa makini anaweza kuyumbishwa sana - chain of command aziheshimiwi hata kidogo.

Mh Nundu futilia mbali mambo ambayo unayaona hajakaa sawa na umuombe mweshimiwa Raisi afanye mabadiriko makubwa kwenye Wizara hii nyeti, asihishie hapo hata TPA wanapashwa kushughulikiwa. Nataka nimkumbushe Mh.Nundu kwamba wewe ndiye umepewa dhamana ya ku-run Wizara kwa hiyo don't you be wobbly au kuwa-controlled remotely, historia ndiyo itakuhukumu. Just read between the lines kwa huyu anayenipinga humu ndiyo utajua unakazi ya ziada-wamejipanga kweli kweli. Mungu akulinde.
 
Pamoja na tuhuma alizopewa Waziri Nundu kuna kitu kimoja namuunga mkono kwamba inabidi sisi wenyewe tufanye upembuzi yakinifu nu kiasi gani kinahitajika kwa sababu wengi tumejikita kwenye hoja huu mwingine utachukua miaka 12 na huu mwingine miaka 45 inawezekana wote wanatupiga changa la macho kwa sababu huu sio mradi wa kwanza wanafanya hivyo tunao wataalamu na vyombo ambavyo vinapaswa kujua gharama halisi kabla ya kuanza kutafuta wawekezaji
 
Serikali yetu imeshindwa hata kujihifadhia nyeti zake je itaweza kulindea nyeti za wengi?

Tuanzie hapo, tunamlaumu mtu asiyestahili kulaumiwa kutokana na ukweli kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu tuliyompa. Nundu na wengine kuanzia juu na yale wanayoyafanya yote ni makosa na hata wamlete Mungu awasafishe... hakika bado dhambi zao zitakuwa nyekundu kuliko damu! Na ni dhahiri kuwa hata tukimpa Kikwete miaka mia ya kuweza kuvunja na kuunda mabaraza mengine ya mawaziri au kuwaonya hataweza kupata baraza lililokwa maslahi ya umma.

Ni vyema kuendelea kuanika uozo huu ila mwisho wa siku lengo liwe ni kuuamsha umma ili ufanye mapinduzi takatifu yasomwaga damu.

Nawasilisha maoni yangu na ASANTE SANA JAMII FORUM kwa kazi nzuri
 
siasa za tanzania zina tapisha mara watu wana washa moto baada ya mda wapepoa aaaaaaaaaaaaaaa kama maji ya mtungi.....sijui hii siasa ni PEPO??
:lalala:
 
jamani hakuna namna hii mikataba yote ya serikali inayoingiwa na wawezeshwaji (wawekezaji) kuwa wazi?
mbona hizi barua zinaandikwa siri? inauma, inauma, inauma, inauma........inauma sana.
 
Back
Top Bottom