NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

According to the Chinese country's criminal law….it is an offence for Chinese companies and Chinese nationals to bribe foreign government officials. The law applies to companies organized under Chinese law and would include Chinese companies overseas and wholly foreign-owned enterprises in China. This is according to a World Bank statement issued in Washington in July 29[SUP]th[/SUP]/ 2011…when the WB announced the debarment of China Communications Construction Company (CCCC) Limited, and all its subsidiaries, for fraudulent practices under the Phase 1 of the Philippines National Roads Improvement and Management Project.

Under the sanction, CCCC is ineligible to engage in any road and bridge projects financed by the World Bank Group until January 12, 2017. This action was based on recent changes in the World Bank sanctions system to clarify that successor organizations- through purchase or reorganization –will be subject to the same sanctions applied to the original firm.

My take:
This is the same company involved here in TZ and already under this very suspicious deal….involving the current transport ministers from the TZ government. I will take the said paid for trip to China involving Minister Mfutakamba as bribery offered by the CCCC Ltd for the port's deal……no wonder minister Nundu is trying to isolate himself from this fiasco……something is very fishy here…..we could be in for another Richmond….or Buzwagi or Kiwira here…..very sad that this is again happening under JK's government……these guys seem not to learn from their past mistakes……kweli sikio la kufa halisikii dawa…….

Source: Read about this from here: http://www.worldbank.org/en/news/20...imited-for-fraud-in-philippines-roads-project
 
As I noticed all the documents attached are classified, thus the truth is, not only Mr. Nundu should go,
but the whole secretaryship of his ministry should also be sacked. However, it is obvious that the documents
were released by the Mfutakamabas' camp, thus why they misses documents that implicates him in this scam.
Please Mr. Invisible, disclose the other side of the coin so as we may reasonably and fairly conclude the matter.
 
Katika Nipashe ya leo Nungu akiongea na waandishi wa habari jana alisme maneno haya nanukuu

"Aidha, Nundu alisema shutuma kwamba kampuni ya China Merchant ni yake ni uongo na kwamba hajawahi kuingia nayo mkataba wa kibiashara (MoU) kwa ajili ya ujenzi huo kama inavyiodaiwa na wabaya wake hasa kamati ya Bunge"

Sasa anataka kutuambia kuwa nyaraka hizi ni za uongo? Hawa viongozi wetu sifuri kabisa.
 
Nundu hajasafishika kwani mbona hakusema haya kabla hajaambiwa kujiuzulu, kilichopo naibu alimzidi spid ila wote walikuwa kwenye mbio za ufisadi.
 
kinachooneka kwa Nundu au uvimbe,mwizi akiibiwa hulalamika sn.aweazidiwa na naibu au vp haijalishi.WOTE WEZI 2.
 
nimesoma nyaraka hiz nikagundua yafuatayo:

1.. waziri nundu sio msafi,

2..yeye ndio waziri wa wizara husika..hakika alikuwa anajua kinachoendelea ila nadhani alitofautiana namwenzake kwenye hiyo 10%.

3. kuna barua ya wachina inaelekezwa kwake..ina maana hata hiyo barua hakuipata?..huyu waziri ni mvivu na mzembe na anakubali kuburuzwa na kugeuzwa kama chapati kwenye kikaango.

4..kwa nini analia leo kuwa hawajui ccc na kusema kwamba naibu waziri wake ndio amehongwa na hapatani nae? kwa nini asingesema mwanzo kama alivyofanya jana kuwaita waandishi wa habari? hii inaonyesha kwamba huyu waziri anajua kitu ila yamemkuta sasa anatafuta pa kujinasulia

5. haiwezekani yeye kama waziri barua na nyaraka zote hizi yeye asiwe ameipata hata moja...kama waziri alipaswa kuwa ameshaziona hizi nyaraka...

mwisho nasema anapaswa kuachia ngazi kwa uzembe wake....

'' na msimu huu wamekula maembe yakiwa bado mabichi''
 
"KUJIHUDHURU" ndo nini? kingereza sawa sio lugha yetu, lakini jamani hata kiswahili kinatushinda?

Mkuu Dr. Wangesamila watanzania wengi ni vuguvugu hawakiwezi kiswahili wala kiingereza ama lugha nyingine yoyote hata lugha za kienyeji. Tupo tupo tupo kila kitu tunajitahidi na siyo kwamba tunaweza.
 
Last edited by a moderator:
Omary Nundu inawezekana ni kiongozi dhaifu kuliko wote serikalini. Sikutegemea kuona anayasema aliyosema halafu eti nitaendelea kuwa waziri. Nundu anatakiwa ahojiwe na vyombo vya dola mara moja. anaweza kutusaidia, kumbe anajua mengi ananyamaza na analinda wezi? Je wasinge msulubu angesema haya? Nundu nilitegemea baada ya kusema aliyoyasema mwisho angemwaga manyanga, Uwaziri na Ubunge awe raia wa kawaida.
 
Hizo ni mbinu za Nundu kutaka washirika wake CMHI wapate ulaji na vile vile ni mbinu ya kutaka kujiepusha na kitanzi.

Kama unaamini maneno ya Nundu kwamba hawa CMHI wangewekeza kwa nusu ya gharama za CCC, tuwekee ushahidi(document) kuonyesha hicho kiwango anachosema Nundu.

Na kama Nundu alikuwa mzalendo, baada ya kupata barua ya wachina wake kwamba wizara ya fedha inashirikiana na wachina wengine katika mradi huo huo, alichukua hatua gani? kuwasiliana na wizara ya fedha!? Kama kweli aligundua kwamba naibu wake amemzunguka alimripoti kwa mkubwa wao? au amesubiri uozo wake umeanikwa ndipo anakuja kujipapatua? katika hili Nundu hatoki hata afanye nini.

Moja ya maazimio ya kamati iliyochunguza tuhuma za katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini(Jairo), ilikuwa ni kutazama upya muundo wa wizara. Point iko hivi,katika hizi wizara,yakupasa uelewe chain of command haiko kama unavyofikiria,kuwa waziri ndie incharge wa maamuzi yote ya wizara,la hasha. Rejea ripoti ile kabla ya kumhukumu waziri Nundu. Huyu waziri Nundu amezungukwa na watendaji wengine wizarani kwake kwa kushirikiana na wizara ya fedha kutokana na muundo wa wizara ulivyo wa hovyo. Na hili ndio jambo la msingi la ku-address. Tusikimbilie njia ya mkato ya kumstaafisha kazi waziri kwa kufikiria ndio tunatatua tatizo. Tutatue kwanza tatizo la msingi la ku re-structure muundo wa wizara zote ili tuondokane na matatizo haya moja kwa moja. Kwa nini hamtaki kusikia kitu kingine zaidi ya Waziri Nundu kujiuzulu wakati hana kosa? Why all Tanzanian are being played by the media?
 
kwanza ukisoma hizi docs, si waziri nundu peke yake...hapa ni kusafisha waizara nzama na huko TPA na kwingineko..kote kuna wezi....tatizo kiti cha rais kimewekewa koti jeusi...
 
Ukisoma madudu yote haya, hawa wote wanatakiwa kufikishwa mahakamani, na mwingine muhimu ni Mh Lukuvi aliyekuwa akitoka mapovu kutetea kuwa ni uongo huyu anatkiwa kujiuzuru uwaziri, na kujiuzuru ujumbe wa kamati kuu ya CCM na kufikishwa mahakamnio kwa kuudanganya umma, kwani ni mshirki wa wizi
 
kwa ninavyo angalia bunge serikali yote imeooza kwa wizi hata spika labda kina zito wana juwa wanamfichia siri japo nilisoma mahali kuna mashine ya printing press ilinunuliwa haikufanya kazi
 
As I noticed all the documents attached are classified, thus the truth is, not only Mr. Nundu should go,
but the whole secretaryship of his ministry should also be sacked. However, it is obvious that the documents
were released by the Mfutakamabas' camp, thus why they misses documents that implicates him in this scam.
Please Mr. Invisible, disclose the other side of the coin so as we may reasonably and fairly conclude the matter.

Hapa hakuna kambi. Kama kuna kambi, wanaojua ni wanaosema, na Nundu alipoenda kwenye Kamati ya Bunge bila document alikuwa kambi gani?

Mfutakamba naye abanwe kama amekula rushwa ili apambane na Waziri wake ambaye naye amevuta kupinga mradi ulioanzishwa na Kawambwa (ambaye naye kama kala walete docs).... Lakini hapa utaona Naibu Waziri hana kazi katika mchakato, labda kupiga debe ama kumhujumu Waziri, kwa hiyo hata hao waliomnunua Mfutakamba waliingizwa mjini, lakini wenye ushahidi watoe naye ashughulikiwe. Haoa utaona mchakato ulishaanza tokea 2008 kwa hiyo mtu ambaye anaweza kubanwa kuwa amevuta ni Katibu Mkuu, Chambo ambaye Nundu nadhani anaogopa kutoa siri zake kwa kuwa naye anajua zake.... maana hata hiyo kampuni nyingine Chambo nayo anaonekana alikuwa akiijua lakini alikuwa akikwepa kwa kuwa enzi za kawambwa alishiriki pia.

Sasa kama kuna uchafu Nundu asiume ume maneno aseme wote bila kumuogopa yule anayeona atamuumbua.
 
Mh. Nundu kakosea nini hapa! Actually yeye ndiye anataka kunusuru nchi yetu kutoka kwenye hujuma hisiyo kifani, what is CCCC, kwani Exim Bank China imetoa fedha na shinikizo la kusema lazima CCCC ndiyo ipewe tender ya kujenda maghati, one may ask why pick on CCCC; kwa nini pasiwepo na ushindani uliyo wazi huko Uchina, tenda ikatangazwa huko Uchina na kampuni itakayo shinda iweze kujenga maghati. Waziri anachezewa kama mtoto mdogo na watu walio chini yake maanake nini, wanaondoka kwenda safari bila kutoa taharifa kwa Waziri na nyinyi mnaona hilo sawa.

Mh. Nundu ndiye kapewa dhamana ya kuongoza Wizara na Raisi, Waziri ana uwezo wa kufutilia mbali mambo ambayo hayakukaa sawa; mimi niliangalia ubishi uliyokuwepo kati ya mwenyekiti wa Kamati, Waziri na Mh.Mnyika mtu mwenye akili timamu unaona wazi wazi kwamba hoja anazo zitoa mwenyekiti hazija kaa sawa, watu walikuwa wamepania kumdhalilisha Mh.Nundu aonekane hafahi, kisa maghati; lakini Mh. Nundu alipo simama na kutoa ufanafanuzi watu tulig'amua ni kundi lipi lenye matatizo, mtu kama analitakia mema Taifa hili hasingesita kukubali kurekibisha kipengele kilicho kaa vibaya katika mambo ya mikataba kilekebishwe, hizo small prints ndizo zimeli-cost Taifa Dearly.

Mh. H. Rashid alitoa onyo la kweli kwamba Wachina wengi wa siku hizi siwa enzi za Mao na nikweli, Wachina wengine hawaogopi hata kidogo-leo hii Raisi wa Uchina apate habari kwamba kuna kampuni kutoka China inawapa ma-trip yasiyo na kichwa wala miguu viongozi wa Wizara inayotoa tenda za kujenga maghati, hilo likijulikana Wachina hao watapigwa risasi adhalani - wenzetu wako serious na mambo haya.

Mimi siko overly concern na uharaka wa kusema eti wapewe CCCC kwa kuwa Wakenya wanajenga Bandari/maghati Lamu, sijuhi Msumbiji nini -visingizio chungu mzima. Namuomba Mh.JK amuache Mh. Nundu afanye kazi zake kwa amani, mtu hata ukimwangalia usoni Mh.Nundu unamuona yuko sincere, wasilete mambo ya kumvuruga wizara kwa ajili ya maslahi yao yasiyo na tija kwa TAIFA, mimi naona kitu cha kufanya ni kubadirisha watendaji wakuu pale wizarani na TPA; wapewe kazi nyingine nje ya wizara, bila kufanya hivyo Waziri atapata wakati mgumu - watu hawa wako well organised.

Mkuu umeandika mengi lakini hatutuelezea Public Procurement Act, 2011 inaemaje kwenye maswala ya manunuzi? Ni kampuni gani kati hizo mbili ime comply with the respective act to the letter? Ya Mh.Nundu naona inataka kukwepa kufuata utaratibu wa jinsi sheria yetu ya manunuzi inavyotaka. Na kama unaona huo ndio uzalendo basi kuna tatizo. Mh.Zitto juzi alisema kamati yake inapendekeza eyes on hands off. Tuache wahusika wa Procurement Management Unit wakiongozwa na katibu mkuu wafanye kazi na mawaziri kazi yake iwe ni kuwa watch dogs ili mambo yasonge mbele. La sivyo tutabaki kuwaonea huruma wanaotoa machozi ya kinyonga
 
According to the Chinese country's criminal law….it is an offence for Chinese companies and Chinese nationals to bribe foreign government officials. The law applies to companies organized under Chinese law and would include Chinese companies overseas and wholly foreign-owned enterprises in China. This is according to a World Bank statement issued in Washington in July 29[SUP]th[/SUP]/ 2011…when the WB announced the debarment of China Communications Construction Company (CCCC) Limited, and all its subsidiaries, for fraudulent practices under the Phase 1 of the Philippines National Roads Improvement and Management Project.

Under the sanction, CCCC is ineligible to engage in any road and bridge projects financed by the World Bank Group until January 12, 2017. This action was based on recent changes in the World Bank sanctions system to clarify that successor organizations- through purchase or reorganization –will be subject to the same sanctions applied to the original firm.

My take:
This is the same company involved here in TZ and already under this very suspicious deal….involving the current transport ministers from the TZ government. I will take the said paid for trip to China involving Minister Mfutakamba as bribery offered by the CCCC Ltd for the port's deal……no wonder minister Nundu is trying to isolate himself from this fiasco……something is very fishy here…..we could be in for another Richmond….or Buzwagi or Kiwira here…..very sad that this is again happening under JK's government……these guys seem not to learn from their past mistakes……kweli sikio la kufa halisikii dawa…….

Source: Read about this from here: World Bank Applies 2009 Debarment to China Communications Construction Company Limited for Fraud in Philippines Roads Project

Mkuu big up kwa kutupa ushahidi wa rushwa ya hili kampuni. Kuna articles fulani nilisoma mwaka jana (I believe in "The Economist") kuhusu madudu yao hawa na Sinopec (kampuni yao ya mafuta) kuhusiana na rushwa katika uchimbaji wa mafuta huko Angola. Sijafanikiwa kuzipata online.

Nimeshauliza hapa, kama hawa watu wanajulikana kabisa kwa rushwa mpaka wamekuwa listed hivyo na World Bank, kwa nini tufikiri Tanzania hawakutembeza rushwa? Kulikuwa na open tender? Kuna transparency kiasi gani katika process yote?
 
Back
Top Bottom