Yaani, mmetachi my very soul kwa hizi picha.
Kama unakidate chako unasubiri siku ya mnada/soko, nao ulikuwa once per month
Unasugua ndala zako zinawaka, kanga yako ya njano, gauni vitambaa polyster au japan, umesuka tano kichwa
Kazi unafanya fasta ili uruhusiwe kwenda sokoni
Unakikuta kidate njiani, kama ni babu kubwa kina baskel swala au phonex
Kina radio ndogo almaarufu duduprufu, kimefungua BBC au dochiwele, full kingereza
Kinakupalift, mtazunguka siku nzima
Kinakupeleka for lunch
Ni chai na vitumbua, wakati mwingine vya unga wa mahindi, au maandazi
Matawi sana unanunuliwa soda na biskuti
Mnamalizia na desert lenu la maana la miwa
Na hiyo miwa haikatwi ni kila mtu wake mrefu
Ili msifike nyumbani mapema, mnarudu taratiibu huku yy anasukuma baskeli yake
Hizi mnazoitwa water and pillow fights, kwa enzi zetu ilikuwa ni anakunyangánya kanga
Sababu its a taboo kigori kutembea bila kanga kiunoni,
Unaanza kumkimbiza, anailaza baskeli yake pembeni mwa njia
Mtakimbizana kimbizana wee, mara akusubiri, unamshika unaanza kuivuta vuta kanga
Mara anakutishia kukutekenya kwapani, wewe unaona aibu unakimbia tena.
I can go ON and ON andON andON
The love was PURE, PURE, haya mashule haya yanaharibu vichwa tu, tukaja mjini kujijaza taka za wazungu, nataka desert ya pina pie
Hawa jamaa lazima atakuwa Wasukuma au Wanyamwezi maaana enzi hizo walikuwa wanapenda sana kutembea na radio na baiskeli..