NMB juzi mlifungua makao makuu mapya katika jengo la Nyumba Ya Sanaa . Ni vizuri kwa branding ni mahala au sehemu strategical kabisa kwa branding.

lakini juu ya hayo wasi wasi wangu ni gharama za kukodi jengo hilo lote . jee risk mangers na budget planner wenu kweli wamzingatia cost ya kukodo jengo lote ?
jee hapa faida ya bank yote inaenda kwenye kodi ?

hili jengo nathani lina gorofa 5 na kwa wastani kila floor ni wastan wa sqmts 1200 ambapo kodi ya kawaida ya CBD ni $ 23sqmt so 23x1200x5 =138,000 x 12 =1,656,000

kwa miaka mitano =$ 8,280,000.
sasa kibiashara hizi pesa ni nyingi mno na ufujaji hizi hapa Mjini unapata Kiwanja kwa bei ya chini ya $2-3m na mnaweza kujenga jengo la kwenu pekee kwa anothe $ 2-3 m hivyo na chengi inabaki.

uamuzi wenu sio biashara labda kama hilo jengo mume kodi $ 5/sqmt !!!!!

Nafikiri hawaruhusiwi kujenga jengo lao, kuna mtu aliwahi kuniambia hivyo kuwa BOT lazima itoe kibali karibu kwa kila kitu mnachonunua ama kutumia. Nasikia kuwa hata vijiko lazima upate " No objection" kabla ya kununua
 
HI, NMB
mwaka 2008 nilikopa pesa ambazo deni lilipaswa liishee 2010. ikiwa deli limesalia kama miezi mitatu hivi kwisha nilienda kukopa tena 2010.

Mkopo niliopewa walikata deni lote lililosalia la 2008. nikaelezwa kuwa ili kuwa na makato ya mkopo moja tu wamekata kiasi cha fedha kwa ajili ya deni lilotangulia na hivyo nitaanza kukatwa deni jipya tu.

but makato ya deni la zamani yaliendea kwa muda mrefu na nilipouliza niliambiwa yatalipia deni jipya. baada ya muda mrefu kwa hesabu zangu deni liliisha but waliendelea kukata zaidi ya sh.300000/= na 2010 Octoba nilienda kupata ufafanuzi tawi la Mkawakwani Tanga kwa afisa mkopo. (namkumbuka mpaka leo kwa sura) baada ya kumueleza afisa mkopo akanipeleka kwa meneja wa kike (namkumbuka na sitamsahau) yule meneja aliangalia kwenye comyuta na akachapisha karatasi ambazo zinaonesha makato ya kila mwezi mpaka deni lilipokomea na akaniambia hakuna fedha iliyokatwa ya ziada.

kimsingi sikuridhika but kwa sababu kuna karatasi alizichapisha zinazoonesha makato yangu nikaona nitazisoma mwenyewa nyumbani kupata uhakika. nilipojumlisha makato yote nikaaona nilikatwa zaidi ya sh 300000. bahati mbaya kabla sijarudi bank nikasafiri nikarudi octobar 2011. nikaenda tena kwa afisa mkopo yule yule na makaratasi yangu niliyopewa na meneja 2010. nilimweleza afisha mkopo nikamwonesha na ushahidi wa fedha zilizokatwa za zaidi. baada ya kukokotoa akasema hata yeye anaona kuna fedha ilikatwa kimakosa, lakini siku hiyo meneja hakuwepo, hivyo akachukua no yangu ya cm na akaahidi kunipigia simu meneja akirudi.

Baada kama siku mbili hivi nilipigiwa cm na yule afisa mikopo na kwa unyenyekevu mkubwa akanifahamisha meneja amerudi na hivyo nikamuone. Siku ya pili nilirudi pale Bank nikiwa na karatasi zangu mkononi. Nilipofika yule afisa mkopo alinipeleka kwa meneja na yeye akatoka nje nikabaki mimi na yule meneja wa kike.

CHA AJABU YULE MENEJA ALIANZA KUNIULIZA MIMI NI DINI GANI?, KABILA GANI? NATOKA WILAYA GANI? UNAFANYA KAZI GANI WEWE? na nilipokataa kujibu hayo maswali kwa kuwa hayahusiani na shida yangu yule mama alinitupia maneno ambayo siwezi yaandika hapa. kifupi niliona shetani ameshuka na kuendelea kukaa pale huenda kungepelekea kumjibu vibaya na hivyo polisi walio nje wakatumika. kifupi niliona bora kupoteza zaidi ya sh. 300000/= kuliko kuingia kwenye mtego wa ugomvi ambao sijui hasa nini kiliharibika.

Hivyo baada ya kurushiwa maneno mabaya nilisimama na nikaondoka. Mwaka 2013 nilirudi tena na nikataka kufanya jaribio la kumuona meneja tena. but niliishia kukaa kwenye foleni na kuondoka niliogopa huenda akanijibu vibaya na uvumilivu wangu ukapotea. uvumilivu ukipotea waweza leta shida zaidi.

Ni zaidi ya miaka mitatu sasa bado najiuliza kulitokea nini mpaka meneja wa bank tena mama akaanza kunishambulia ofisini kwake kwa maneno kakasi Vile? Au yule afisa mikopo labda alimueleza nini? Na kwa nini afisa mikopo alitoka mara tu ya kunifikisha kwa meneja?
 
Nimechukua kadi mpya na kubadili namba ya siri lakini nikienda kwenye menu ya Nmb mobile inaomba pini ya zamani mpya hawaitambui why?
 
tunaomba NMB muwe mnatuwahishia mikopo yetu hasa sisi wafanyakazi maana tunapata shida sana, mfano mimi nliomba mkopo sasa hv wiki inaisha sipewi
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta ? Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe ?Siri?)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Kwakweli NMB huduma zenu zinaridhisha sana ukiacha mapungufu madogo madogo ya baadhi ya wafanyakazi.

Matawi yenu mengi mmeweka wakudumu wakuwasaidia watu hiyo ni nzuri sana kwani tatizo la kitaalam likitokea huripotiwa na kushughulikia kwa haraka.
 
Asanteni sana NMB kwa kuja kwenye hili jukwaa kutatua kero za wateja wenu.

Sasa mi nilikuwa naomba kujua je sisi ajira mpya mwalimu 2015 tunaweza pata mkopo.asante
 
NMB mnaudhi sana. Eti ili nipate faida kwenye akaunti yangu lazima niache humo milioni tano mpaka mwisho wa mwaka kweli??

Nitakuwa nahamisha kila mshahara wangu ukiingia kwenda benki nyingine ambako nitawekewa faida hata kama kuna laki 5.
 
Duuh, mbna napata mashaka juu ya hii bank, Natumia NMB huu mwezi wa tatu sasa bt sijawahi kupata tatizo la kunifanya niwachukie ila huko ninapoelekea naona ukungu
 
Naomba kujuwa kuhusu ukweli wa utoaji mikopo kwa watumishi wa umma nimesikia kuwa zoezi hilo mmesitisha na kama ndy je? Huduma hii itaanza kupatikana lini?
 
Nmb je? Ni kweli mmesitisha utoaji wa mikopo kwa watumishi wa umma? Kama ni kweli je?ni kwa mda gani?
 
Leo mmepata aibu mmetoa pesa nyingi kwa ajili ya sherehe ya wabunge na rais baada ya kuhutubia bunge. Mnashindwa kusaidia huduma za kijamii.

Hongera Magufuli kupeleka pesa yenu hospitali ya Muhimbili ikanunue vitanda ili wagonjwa wasilale chini. Aibu kwa benki yenu.
 
Mimi waliniudhi maana sipendi kabisa kuzenguliwa, nikawa siendi, waliponistua kuwa bado siku kumi tu wafunge account, nikaamua kusamehe. lakini Tz tunamatatizo sana, sijui lini tutabadirika!
 
Hivi nyie mnajisikiaje kuwa Benji ya mwisho kwa huduma bora?... Ni aibu bora NMB ingefutwa tu
 
mimi nina tatizo moja nilikuja nikakosea siku moja namba yngu ya siri ya NMB MOBILE lakini baadae nikawa nimeikumbuka, nilipoingiza haikukubali tena mpaka leo nina siku nyingi. Kwa hyo naomba msaad nifanyeje jmn nisaidieni ndg!!!!!!!!!!
 
Naomba kujua km usajili wa pikipiki mpya yaani numberless km ni wa ghali sana. Naomba ushauri kwa anayejua please!!
 
Badilikeni Leo tumekaa ATM za Mbalizi road ambapo ndiyo zonal office 2hours mashine inatoa mojatu. Halafu ni mwisho wa mwezi.
 
Back
Top Bottom