Makampuni ya mawsiliano kuachwa yaendelee kutoa mikopo ya kausha damu Serikali imebariki wananchi kufilisiwa kwa maslahi ya kikodi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,774
Kukua kwa teknolojia kumeyavuta makampuni ya Simu kuanza kufanya biashara ya huduma za kifedha ambazo hapo awami zilikuwa zinafanya na taasisi za fedha tuu kama benki.

Katika kufanya biashara hiyo makampuni ya simu yameanzisha huduma mbalimbali ya muda mfupi za kifedha ikiwemo kuwezesha miamala, kutunza fedha na kutoa huduma za mikopo.

Sina shida na wao kufanya Huduma hizo ila tatizo linakuja pale ambapo huduma hii hasa za mikopo kugeuka kuwa mnyonyaji na mkamuaji kwa wananchi Kwa kutoa mikopo yenye tiba kubwa ambazo zinajukioana kama mikopo ya Kausha Damu.

Miaka ya hivi karibuni kulitokea malalamiko ya kuibuka kwa utitiri wa taasisi za kifedha za binafsi ambazo zilikuwa zinatoa mikopo kwa riba za kijambazi na kupelekea malalamiko kwenye jamii na Serikali kuingiliwa kati. Kwenye kilele cha malalamiko walikuwepo walimu na wakinamama wa vikoba nk.

Serikali iliingia na kuja na kanuni ambazo zimepunguzwa kwa sehemu kubwa mikopo ya Kausha Damu ambayo ilipelekea watu kujinhonga na Ndoa kuvurugika au watu kufilisika Kwa Mali zao kupigwa mnada.

Sasa limejitokeza Wimbi jipya la mikopo ya kausha Damu Kupitia makampuni ya Simu mfano Vodacom wao Wana Huduma za mikopo kedekede na zote hizo ni kausha Mathalani;
  • Songesha
  • Nipige tafu
  • Mgodi
  • M Pawa
  • M Koba
  • Chomoka nk

Huduma zote hizo ni za kijambazi na kausha Damu kiasi kwamba imegeuka kuwa unyonyaji mpya kwa wananchi huku wao wakipatwa faida kubwa ambazo ndio hutoa sehemu yake kama gawio kwa Serikali na kuifumbia macho huu wizi.

Wanakuambia kiasi cha kukopa ukikopa wanakata pesa yao kabisa kabla ya matumizi, na ukienda kutoa wanakata tena kwenye salio na mbaya zaidi riba inaendelea kuongezeka kadiri mda wa kulipa ambao ni ndani ya mwezi mmja tuu. Huu ni wizi na haikubaliki.

Ukiacha wizi huu wa Kausha Damu, haya makampuni yamekuwa na wizi mwingine kwa wananchi kwa kutumia bando na dakika ambapo husisha mapema zaidi kabla ya mada ukiuliza unaambiwa ni matumizi yako.

Swali la kuniuliza, ni kwanini Serikali iko kimya kwa wizi huu wa wazi licha ya malalamiko ya mara kwa mara? Je, Serikali Imebariki wizi na kufukarisha Wananchi wake kwa maslahi ya Kikodi?

Tuwaombe Wabunge na baadhi ya watu ambao huwa wanasimama kutetea maslahi ya wananchi ili wakawakalie kooni Mawaziri Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba kwa kuifumbia macho ambapo kwa sehemu kubwa huenda wanapata 10%.

Shime Wabunge wafuatao chukueni hii hoja mkawapiganie wananchi Bungeni;
  • Mwita Waitara
  • Getere
  • Musukuma
  • Festo Sanga
  • Jumanne Kishimba
  • Luhaga Mpina
  • Hamis Tabasamu
  • Civid 19

Piga kelele komesha wizi naamini Mh. Rais akisikia atawa summon wahusika na hatua zitachukuliwa kuliko kukaa kimya.

Pia soma 👇
 
Duh who cares,wakati mabenki yenyewe ndo kinala wa huu unyonyaji,mimi nimekopa nmb shilingi 8M,kwa miaka 5 riba ni sh ,7M,no difference.

Lakini pia haya makampuni ya simu yanasaidia sana,kuliko kwenda kufedheheka kwa mtu ,unajipimia mwenyewe tu,mimi songesha yangu inasoma laki 2 ,mgodi inasoma 100,000 ,sasa kama ninashida si natatua shid yangu mapema tu
 
Inasikitisha sana ,ndio maana wabunge niliowataja hapo Juu watusaidie
 
H
Hakuna aliewahi lazimishwa kukopa hio mikopo,

Kingine ukikopa ukalipa ndani ya mwezi mmoja riba sio kubwa, shida mtu anakaa na deni miak 2 halafu anategemea asipigwe na riba za ajabu
Huwezi elewe wewe, kuna hao Tigo na bustisha yao. Walikata mkopo wao wakabakisha deni la 0.02tsh, kujaribu kulipo hiyo 0.02 ikakataa. Baada ya siku 5 wakakata 338tsh wakasema nimalizie mkopo uliobaki wa tsh 0.02 kuepuka riba wakati salio lilikuawepo la kutosha kwanini hawakukata mkopo wote. Nikapiga 100 huduma kwa wateja jamaa akasema mtandao uko chini hivyo hawezi kufikia account yangu, nipige baada ya nusu saa. Tangu hapo mpaka leo namba 100 iko bize. Kama sio wizi ni nini.
 
Hakuna aliewahi lazimishwa kukopa hio mikopo,

Kingine ukikopa ukalipa ndani ya mwezi mmoja riba sio kubwa, shida mtu anakaa na deni miak 2 halafu anategemea asipigwe na riba za ajabu
Mipasho majibu haya!! Na wao hawakulazimishwa kufanya biashara, kinachopingwa ni "EXCESSIVE INTEREST" biashara lazma ifuate haki na sheria siyo ku take advantage ya wateja.
 
Ukivuka muda uliopangiwa kulipa ndio riba inaongezeka,
Mfano songesha ukilipa ndani ya week ina riba ndogo sana, ila jichanganye ukae miezi mingi ndio riba inapanda sana,
Na hii inachangiwa na penalties unazopigwa kwa kuchelewesha
 
Kukua kwa teknolojia kumeyavuta makampuni ya Simu kuanza kufanya biashara ya huduma za kifedha ambazo hapo awami zilikuwa zinafanya na taasisi za fedha tuu kama benki.

Katika kufanya biashara hiyo makampuni ya simu yameanzisha huduma mbalimbali ya muda mfupi za kifedha ikiwemo kuwezesha miamala, kutunza fedha na kutoa huduma za mikopo.

Sina shida na wao kufanya Huduma hizo ila tatizo linakuja pale ambapo huduma hii hasa za mikopo kugeuka kuwa mnyonyaji na mkamuaji kwa wananchi Kwa kutoa mikopo yenye tiba kubwa ambazo zinajukioana kama mikopo ya Kausha Damu.

Miaka ya hivi karibuni kulitokea malalamiko ya kuibuka kwa utitiri wa taasisi za kifedha za binafsi ambazo zilikuwa zinatoa mikopo kwa riba za kijambazi na kupelekea malalamiko kwenye jamii na Serikali kuingiliwa kati. Kwenye kilele cha malalamiko walikuwepo walimu na wakinamama wa vikoba nk.

Serikali iliingia na kuja na kanuni ambazo zimepunguzwa kwa sehemu kubwa mikopo ya Kausha Damu ambayo ilipelekea watu kujinhonga na Ndoa kuvurugika au watu kufilisika Kwa Mali zao kupigwa mnada.

Sasa limejitokeza Wimbi jipya la mikopo ya kausha Damu Kupitia makampuni ya Simu mfano Vodacom wao Wana Huduma za mikopo kedekede na zote hizo ni kausha Mathalani;
  • Songesha
  • Nipige tafu
  • Mgodi
  • M Pawa
  • M Koba
  • Chomoka nk

Huduma zote hizo ni za kijambazi na kausha Damu kiasi kwamba imegeuka kuwa unyonyaji mpya kwa wananchi huku wao wakipatwa faida kubwa ambazo ndio hutoa sehemu yake kama gawio kwa Serikali na kuifumbia macho huu wizi.

Wanakuambia kiasi cha kukopa ukikopa wanakata pesa yao kabisa kabla ya matumizi, na ukienda kutoa wanakata tena kwenye salio na mbaya zaidi riba inaendelea kuongezeka kadiri mda wa kulipa ambao ni ndani ya mwezi mmja tuu. Huu ni wizi na haikubaliki.

Ukiacha wizi huu wa Kausha Damu, haya makampuni yamekuwa na wizi mwingine kwa wananchi kwa kutumia bando na dakika ambapo husisha mapema zaidi kabla ya mada ukiuliza unaambiwa ni matumizi yako.

Swali la kuniuliza, ni kwanini Serikali iko kimya kwa wizi huu wa wazi licha ya malalamiko ya mara kwa mara? Je, Serikali Imebariki wizi na kufukarisha Wananchi wake kwa maslahi ya Kikodi?

Tuwaombe Wabunge na baadhi ya watu ambao huwa wanasimama kutetea maslahi ya wananchi ili wakawakalie kooni Mawaziri Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba kwa kuifumbia macho ambapo kwa sehemu kubwa huenda wanapata 10%.

Shime Wabunge wafuatao chukueni hii hoja mkawapiganie wananchi Bungeni;
  • Mwita Waitara
  • Getere
  • Musukuma
  • Festo Sanga
  • Jumanne Kishimba
  • Luhaga Mpina
  • Hamis Tabasamu
  • Civid 19

Piga kelele komesha wizi naamini Mh. Rais akisikia atawa summon wahusika na hatua zitachukuliwa kuliko kukaa kimya.
Mtag Lucal Mwashambwa,KABENDE MSAKILA, JIDULABAMBASI nk,MIKOPO hiyo safi sana,tunaipongeza Serikali kwa kuturahisishia mambo,fasta Mtu unapata Mkopo wako
 
Ukivuka muda uliopangiwa kulipa ndio riba inaongezeka,
Mfano songesha ukilipa ndani ya week ina riba ndogo sana, ila jichanganye ukae miezi mingi ndio riba inapanda sana,
Na hii inachangiwa na penalties unazopigwa kwa kuchelewesha
Kwa nini riba ziwe za kuvizia na haziko wazi?
 
Kuna alizamisha kukopa huko? Mbona ni kiherehere cha mtu?

Sent from my 2201117TG using JamiiForums mobile app
Usiwe mpuuzi, biashara ya Mikopo lazima ifiate Taratibu ndio maana nikakuyolea mifano ya taasisi za kukopesha binafsi zimezuiwa kuweka riba za wizi.

Ndio nauliza Hawa makampuni sheria za Kuzuia mikopo umiza haziwahusu?
 
Lazima ukope? Bado nauliza tuu. Sii kila kitu kitakufaa. Ukifika baa achana na pombe za laki 5 kwunywa balimi za kiwango chako.... Kalale

Back
Top Bottom