Fahamu undani wa biashara ya microfinance, hasara na faida zake

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Kuna aisiye ijua biashara hii.? Ok Kama wapo ni biashara inayo jihusisha na utoaji wa mikopo midogo midogo ya dharula.

Kwasasa ni biashara iliyo shamiri kila Kona ya Tanzania huwezi pita mji au senta flani bila kukutana na ofisi kadhaa za watoaji wa mikopo.

Walio Anza kitambo wametengeneza pesa kuliko wanao ingia sasahivi.

Changamoto kwa wale wanao ingia sasahivi nikua idadi kubwa ya wateja utakao wapata ni wale ambao tayari Wana madeni kutoka ofisi zingine hivyo wakija kwako ukawapa hela watakusumbua kukurejeshea.

Sheria na taratibu za kuanzisha biashara hii unakutaka uwe na mtaji unao anzia sh 20-milion pia uwe na vibali vyote vinavyo hitajika.

Mtindo mzuri wa kutengeneza faida kwa haraka ni ule unao mtaka mteja kurejesha kila siku.

Mfano mteja amekopa kwako 50,000 riba yake ni %20 means atakurejeshea kwa mwezi sh 60,000 lakini hii 60000 mteja atakua analeta rejesho la kila siku sh 2000.

Faida za rejesho la kila siku.

1: hukupa unafuu wa kupunguza hasara kwa mteja ambae atakimbia na deni lako atakua tayari kasha lipa kiasi flani Cha pesa.

2: kila siku utalala na hela mfano jumla ya marejesho yote kwa siku tuashumu ni 200,000/= kesho una oda ya watu wanne wanao chukua 50 kwa kila mmoja tayari unakua na pesa ya kuwahudumia wateja wako kila siku kuliko mtindo ule wa rejesho la kila wiki.

Ukitumia mfumo huu utapaa haraka ki mtaji.

Changamoto.

Idadi kubwa ya wateja wanao kuja kwako ni wale wasio na sifa za kukopesheka bank, wamama wenye mrundikano wa madeni kila kona hivyo jiandae

1: mteja kurejesha kwa kusua sua leo analeta kesho ana laza,

Asee kwenye hili wabongo ni wabishi kulipa hela za watu. Humu hua naona wadau wanalalamika kudaiwa kwa kuvunjiwa heshima hua naishia kusema kimoyo moyo huyu nae ni wale wale tu, anachukua pesa za watu afu anataka huruma. Wabongo mindset zao zimejitengeza ktm kudhurumu tu au kutapel

2: mteja kukimbia madeni na lako likiwemo. Jipange..


Ofisi zingine huweka utaratibu wa kuwapiga fain wateja wanao laza rejesho ili wawe na hofu ya kuto rejesha au kuchelewesha rejesho.

Mteja hua anaanza kwa kubeep siku za Kwanza ataleta vizuri kwa mda sahihi baadae ataanza kuchelewa atakua analeta nje ya mda wa ofisi na baadae kuanza kulaza hapa anasoma tu maafisa mikopo Kama ni wakali au wapole ukiwa mpole umeisha.


Sasa nimejifunza kwanini hii mikopo inatwa kausha damu kutokana na aina ya wateja walivyo wasumbufu kulipa hell. Ofis zikaja na mbinu za kureplace zile hasara za wateja wasumbufu.

Mwenye swali aulize
 
Hivi hamna dawa yakuwafanya wateja warejeshe pesa kwa wakati maana unajikuta badala hata yakuiombea familia yako unamwombea mdeni wako afanikiwe asikimbie na mtaji !!!
 
Yawezekana kuna nguvu za giza kwenye hiyo biashara mimi nakumbuka nilikopa 50000 mara ya kwanza ndani ya miezi mitano nadaiwa Million 1 ilitokana na Riba plus Top up.
 
Hivi hamna dawa yakuwafanya wateja warejeshe pesa kwa wakati maana unajikuta badala hata yakuiombea familia yako unamwombea mdeni wako afanikiwe asikimbie na mtaji !!!
Dawa hamna mkuu kikubwa ni kuangalia soko lako, ujue kuna wengine wanakopesha kwa kuangalia dhamana pekee lakini mm naona dhamana pekee haitoshi hakikisha awe ana chanzo kinacho muingizia fedha za cha kila siku haswaaa kiwe biashara
 
Yawezekana kuna nguvu za giza kwenye hiyo biashara mimi nakumbuka nilikopa 50000 mara ya kwanza ndani ya miezi mitano nadaiwa Million 1 ilitokana na Riba plus Top up.
Maafisa mikopo walitaka kukupiga Sasa haiwezi kufika huko kwenye milion moja mkuu
 
Wabongo sisi wagumu sana kulipa hela

Mimi ni mpole sana in real life nmekopesha watu wengi sana hela lakini wachache sana wamerudisha

Wabongo ustaarabu Ni zero kabisa yaani selfish kinoma huwazi hata kwamba aliyekukopa nae ana shida Zake
 
Kausha damu inawafanya wanawake wenye tamaa sijui niseme.. wanaliwa kizembe mnoo,, ili apate rejesho.
 
Wabongo sisi wagumu sana kulipa hela

Mimi ni mpole sana in real life nmekopesha watu wengi sana hela lakini wachache sana wamerudisha

Wabongo ustaarabu Ni zero kabisa yaani selfish kinoma huwazi hata kwamba aliyekukopa nae ana shida Zake
Mm naifanya mkuu nilicho jifunza pesa inayotoka bila ulinzi wa kisheria ni rahisi kuzurumika.

Pesa zote nilizo zitoa nje ya utaratibu huu 90% zilikua kwenye risk ya kupotea nimezipambania mpka kupata ila zote zilzo toka kwa utaratibu huu ziko salama kwa kiasi kikubwa
 
Hii biashara inatakiwa uwe kauzu na bandidu Kwa kiwango Cha lami. Kiasi kwamba hata ukimkuta mdeni amelala kitandani anaumwa hoi, wewe beba kitanda na godoro.

Your safe otherwise inakuwa kwako.
 
Back
Top Bottom