Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Asante mkuu...ila Mimi ni Mwanamke na huyo nilie taka umcheck ni mwanaume!!
 
Wewe ni mwenye asili ya upepo wa kawaida yaani pumzi na yeye ana asili ya udongo wa mwekundu nyie wawili mnaendana kwa asilimia 40% tu na hiyo ni kwa sababu nyote wawili mmechangia sayari moja katika hali zenu ambapo inapelekea kuwa vizuri katika;
1: Mawasiliano na Utambuzi wa akili = 80%
2: Hisia = 55%
3:Kusaidiana na kuthaminiana =40%
Lakini kwenye uaminifu na tendo la ndoa ni 2% kitu ambacho kinabeba mahusiano na ndoa huwa ni uamiifu na tendo la ndoa ambacho kwenu kimebeba asilimia 60% hiyo ni kwa sababu kila mmoja kati yenu anasifa ya kutawaliwa na akili mbele hisia nyuma sasa.

Hapo ndio mwisho wenu hutokea zinapoanza kufanya kazi akili zaidi kuliko hisia.
Na hata mahusiano yenu yanavyoanza utaona kila mmoja anakuwa na doubt kuhusu mwenzie
Yeye ni mtu anaekuchukulia wewe kama ni mtu ambaye akili yako haijakomaa yaani anakuona mdogo kiakili haijalishi kama kawahi kukwambia au la hilo ndio linaloendelea mara kwa mara katika akili yake.
Tukirejea kwako utamchukulia au unamchukulia kama mtu ambaye mfano wake ni fimbo iliyochomekwa kwenye tope yaani habadiriki kimawazo wala maamuzi yaani kiswahili rahisi unaweza kuanza kumuona kama kisiki.
Njisi yeye anavyotumia akili yake katika kukuchambua na kukutakia mambo wewe utakuwa unaona kama ni mtu ambaye hakujali.

Yeye ni mtu utamuona mwenye kutaka sana kutizamia mifano ya maisha ya watu na mitizamo yake huwa tofauti na wewe.

Nae anapokutizamia wewe anaona ni mtu mwenye maisha ya juu juu na mwenye kupenda kupoteza muda katika mambo ya kijamii kama mitandao ya kijamii.

Na pia yeye ndio hujiona muhimu zaidi inapokuja kwenye mtizamo wa wewe na yeye wakati wewe unakuwa ni mtu usiye na busara inapokuja kwenye swala hilo.
Shauku yenu kwa kila mmoja itakuwa ni ya chini na maisha yenu ya kingono(tendo la ndoa huanza kupooza mapema tu.
Na wewe utaanza kuangalia nje.
Kama kawaida yako kiroho wanakuita sura mbili.

SEHEMU ZA HISIA:
Ukitaka kuwa nae hivyo hivyo basi fahamu sehemu zake za hisia ni tumbo mtekenye tekenye tumboni na kumpa parapanda hapo hata kama umemkosea ama umemnunisha utamuona anaanza kucheka na kufurahi na hupenda sana kushikwa kwa vidole tumboni wakati wa tendo.
Na kupitishiwa ndimi sehemu ya mstari wa tumbo uzazi pia mkono wako kushika tumbo lake kwa ulaini wakati wa tendo ni kitu kinachomfanya akuone kama mfalme.

Fanya hayo kumfurahisha lakini hutampenda nje ya hapo ndivyo kama nilivyokueleza

Rakims
Mimi Me 12/08 J
yeye Ke 08/12 V
 
Mahusiano haya yeye anaonekana ni mwenye nguvu, mamlaka na mwenye uwezzo wa kutoa usalama kwako ambaye mara nyingi unakuwa na asili ya kuyumba yumba, Pia yeye ni mtu anaeweza kukuongezea mawazo ya ubunifu kwa kuwa wewe una asili ya ubunifu,

Wewe pia utamletea tabia ya kumjali, na pia kwake yeye utakuwa ni mwenye kujiachia, mkiwa pamoja basi mtahakikisha kuyaweka sawa mapenzi yenu na kuwekana sawa ikiwa ni pamoja na kurekebishana, nyote ni wenye mapenzi ya dhati katika mahusiano haya na wenye hisia kali, ingawa wewe ni mwenye hisia kali zaidi na na tabia yeke yeye ya kutaka kujiweka kuwa mtawala basi hukufanya kujihisi kama kakulinda na kukulindia mapenzi yako.

wakati utawala wake hukufanya wewe kujihisi umelindiwa mapenzi basi ndivyo inavyokuwa kwa maana anakuwa ni kweli kalinda mahusiano yenu na vile vile itafikia sehemu utahisi na kuona kakutosheleza na hutahitajia mwingine tofauti na yeye.

Ikiwa yeye atajirekebisha na kitabia chake cha kutaka usaliti kichini chini basi ni mtu ambaye mnaendanana nae pia katika mahusiano haya.

rakims
Thanks
Sijaona uongo wowote ni hakika

Asante sana mkuu.
 
Wewe ni kondoo unakurupuka tu unaoa mwanamke ambae ni simba ni lazima atakuwa juu yako. Na KILA kitu chako kitavurugika. Ujaona mtu baada ya kuoa au kuolewa tu ataandamwa na mabalaa uchumi unashuka, biashara imekufa.
 
Rakims nini maana ya hayo maneno mkuu kuna movie nilikuwa nachek nikaona hayo maneno hapo.
 

Attachments

  • 20230202_222636.jpg
    20230202_222636.jpg
    1.8 MB · Views: 15
Me: N 02/Jan
Ke: A 08/July
Kati yenu kuna mvuto mkubwa sana wa kingono na pia mnaendana vizuri na kimtizamo mnaendana vema sana kwa maana yeye ni maji ya bahari na wewe mchanga wa bahari hivyo mna mtizamo mmoja katika mambo yenu mengi na mnaendana kwa asilimia nyingi;
Kama mtaweza tu kuwezana tabia zenu basi moja kwa moja mtakuwa na mahusiano yenye bahati na mafanikio makubwa kindoa mfano wake utasikia watu huyu kaoa leo nyota yake imeng'aa au mafanikio yake yamefunguka yupo vizuri kwa kila sekta hii ni kwa maana kuwa hata mkiingia kindoa mnapatikana katika mlango wa 12 yaani mzunguko mzima wa nyota 12 unakuwa pamoja na nyinyi bega kwa bega na kila mmoja wenu anakuwa kayapatia maisha na hakuja haja ya kuhofia riziki kwa maana kwenu mkiwa pamoja kila jambo huenda vizuri na kwa ufasaha zaidi.
Lakini kwenye mlango wa kazi pia unatakiwa sana ujitahidi kumuachia yeye pia afanye kazi na kama ni biashara mpe nafasi ya yeye kuisimamia utaona maajabu ya Mungu kwa maana wewe asili yako ni mazingira ya nyumbani na yeye ni mtafutaji mzuri na ana nyota ya mafanikio na ndio bahati yako imelalia kwake usije kumvuruga wala kumuharibia muelekeo kwani huyu unaweza kutembelea nyota yake pindi utakapofunga nae ndoa na ukitaka kuthibitisha hapa kwa watu kwamba haya mambo sio kubahatisha basi muoe siku ya jumatatu kama sio saa 1 asubuhi saa 8 mchana na kama sio hapo basi saa 3 usiku utajiuliza ulichelewea wapi kwa maana usiku wa kwanza tu mmeanza kuitumikia ibada ya ndoa matunda yake siku inayofuata hadi kuingia usiku utaona matokeo na hapa nazungumzia ndoa sizungumzii uhawara.
ni mtu sahihi kwako na ana maslahi mengi na hutaamini ukiwa nae.
na pia ni mtu ambaye anaweza kukukamilishia all the attention you need. Na vile wewe ni mtu wa aibu na mwenye hisia kali na kupenda kukosoa basi huyu kwako ni sahihi;-
Mtizamo unaonyesha wewe ni mtu wa aibu,hisia na mwenye kutaka affection wakati yeye ni mtu wa kuondoa aibu,kuponya maumivu ya hisia na kutawala ndio sifa zake basi popote utakapo hisi you are down she will lift you up haijarishi kipesa mawazo au hisia.
Tofauti zenu zinaweza kuwa kubwa sana ambazo zitaleta furaha za muda mrefu, yaani hapo ni mfano wewe ni hasi na yeye ni chanya. Perfect Match.

Rakims
 
Ke: 10/11 S
Me: 11/02 A

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
MTIZAMO WAKO KWAKE;

Wewe ni mtu mwenye tabia za maji na yeye ni mtu mwenye tabia za udongo kwa mjumuiko huu unaonyesha kabisa nyinyi kuendana ni vigumu na hata kama mnapendana vipi itakuwa dhoruba tu ndani.
Kwa mtizamo anaonekana yeye ni mtu wa kupenda utawala na ukubwa kwa kuongoza mambo/kupelekesha- ambapo wewe unaonekana sio mtu wa kupelekeshwa na hautakubali hilo.
Pia wewe ni mtu wa kuhitaji mabadiriko,anuwai,matukio ambapo hayo humfanya yeye kujihisi tofauti na wewe kwa kuwa yeye ni mtu wa ambaye hujifanya ni mjuaje na incharge wa mambo yanavyokuwa yanakwenda katika miliki yenu na kujiona ni mtawala mzuri wa tabia za nyumbani na hujiona ni mwenye hekima na heshima na imani zaidi kuliko wewe;-
yeye anakuwa ni mtu wa kutaka kufanya mambo ambayo teyari yana uhakika na kutaka kufanya mambo yenye uhakika,
wakati wewe unakuwa upo teyari kufanya chochote kinachowezekana.
Na pia wewe ni mtu wa kusema chochote kinachokujia na nimtu wa kumdondoshea maneno tu randomly yanayokujia kichwani kwa fikra yako ambayo humfanya kuanza kujawa na hasira taratibu. Pia kuna tatizo la pesa katika mahusiano yenu, hiyo ni sababu wewe unataka kuzalisha pesa kwa yanayowezekana leo hali ya kuwa yeye anawaza kuhusu mambo ya kesho (ukifa unaniachaje)
Mna muda mfupi sana kwenye mahusiano yenu.

MTIZAMO WAKE KWAKO:
Mapenzi yenu yanaweza kwenda kama tu ataweza kujikaza vizuri kuwa na wewe au kukuvumilia kwa maana mtizamo wake kwako wewe ni mtu ambaye huvumiliki. wote mnavutiwa zaidi kwa muonekano wa mwenzi wake, kwa tamaa zake yeye alizonazo katika kufanya tendo anakuwa anavutiwa zaidi na ufanyaji wako. Lakini ni mtu inamuwia ugumu katika kuvumilia tabia yako ya kupepesa macho na kutizama mambo mapya(wanawake wa nje) wewe ni mtu wa kuchukulia kila jambo poa poa na rahisi rahisi inapokuja katika maswala ya mahusiano na tendo la ndoa wakati yeye ni mtu muda mwingi anataka kuwa serios kwenye mahusiano na kutawala. hali ya kuwa wewe ni mtu ambaye hutaki kutawaliwa kimapenzi na mtu yoyote hakuna baya kwenu lakini ni watu wenye kupishana mara kwa mara uhawara kwenu inakuwa ni starehe kuliko ndoa. maana mnaweza kukaa kwenye uhawara miaka ila mwezi tu ndoa ikawa ndoana.
Mahusiano yenu ya ndoa yatakuwa ni vichekesho tu.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.
Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake

Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe ikiwa atajua kucheza na mapaja yako yako basi ataweza kukupeleka mbali sana kihisia hisia zako siwezi kukwambia sana kwa maana wewe unamtizamia yeye.

UTAMVUTIA VIPI:-
Yeye kwanza sio mtu wa papara ni mtu anapenda kama ni utafiki ama mahusiano basi yaanze taratibu kama vile unajenga nyumba mapenzi kwake anataka uanzie msingi kwanza hivyo inakutaka kuwa ni mtu mwenye subira kuweza kummudu kimapenzi na subira wewe muda mwingine ni kitu huwa,
Mbinu;
kwanza kabisa kama ndio unaanza nae basi hakikisha kuwa unakuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta na usiende nae kwa pupa kama hujagusa katika kujifanya ni mtu mwenye subira sana basi moja kwa moja hutampata kwa maana kama ni wa dada wazamani huyu atakwambia nisubiri miezi 9 nikufikirie.
Muonyeshe kuwa upo radhi kuwepo muda wote pale anapokuwa anakuhitaji na ujionyeshe kuwa wewe ni mtundu mtundu. Yeye hupenda mtu anaekuwa taratibu taratibu na kama unaweza kumsababisha kucheka cheka basi huna muda mrefu unayoyataka utapata. Pia utaanza kumuona nae ni mtu anautundu utundu na kupenda utani utani na anapenda mtu mwenye kumvutia kwa yale anayoyafikiria akilini kwake yaani unatakiwa kujipendekeza kuuliza unataka niwe vipi?

Tabia zake za kero ndogo ndogo ni mategemeo yake uzifurahie na ujifanye kucheka anapoongea upumbavu au jambo lisilo na maana kwako.
Na kama akisema kwa utani ukajibu kwa utani basi moja kwa moja anakufungulia moyo wake na kuona hakuna mtu kama wewe duniani hapa na anaweza kukuganda kama kupe pia utani wa kimwili kama kumgusa mwili na kumminya minya ni vitu anapenda kama ni mke wako basi jaribu leo hata akinuna ukifanya hivyo anakaa sawa. Ni mtu kama unataka kumtoa basi anapendelea sehemu za hadhi ya juu kidogo na anapenda sehemu anayoenda kuwe kuna watu wanaojua nini wanafanya hasa wapishi. Mnunulie kinyaji kisichokuwa na kilevi ndio mapenzi yake kama sio mlevi lakini kama ni mtumiaji basi utakuta ni mpenzi wa wine.

Mazingira ya nyumbani ukimpikia hata chochote tu hujihisi special sana na hataskia la mtu kuhusu wewe valia mavazi ya kupika unapomuandalia chakula na hakikisha muonekano wako uwe ni safi mfanyie hivyo hata mara moja kwa mwezi utaanza kuona anatoa machozi
Ikiwa mazungumzo yanachelewa basi jitahidi asikushinde kimaongezi na wala usikwame katika kuzungumzia mnayoyapenda hasa akianza kuongelea pesa muhimu tabaka hili ni mwanamke mwenye kupenda pesa na kuigiza hajali pesa.

Pia tengeneza account mbili tatu za bank ili akitizama aone kabisa ni mtu mwenye kushughulika na mambo ya saving hata kama huna pesa atatambua ukipata utatunza.
Usihodhi mazungumzo.
anapoanza kuzungumza usimkatishe na usiwe mzembe katika kutoa sifa akifanya kitu hata cha kipuuzi nyumbani,kwenye gari yake,mapambo ni watu wenye kupenda kusifiwa wanapofanya mambo madogo.

Rakims
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom