Mfahamu vizuri mwenza wako kabla ya Ndoa

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Huenda wewe ni miongoni mwa vijana wanaokaribia kuoa au kuolewa lakini haulewi ni mtu wa namna gani wa kuingia nae kwenye ndoa.

Mbali na kuangalia uzuri wa sura, umbile, kipaji au hali ya kiuchumi ya yule unaetarajia kumuoa au kuolewa nae kuna jambo lingine muhimu kuliko yote ambalo unapaswa kuliangalia kwa jicho la pekee.

Tabia ni jambo la muhimu kulipa kipaumbele wakati wa kuchagua unayetaka kuingia nae kwenye ndoa.

Inawezekana ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya wanandoa wenyewe hawakutumia vizuri muda wao kuelewa tabia za wenza wao na kujipima wenyewe kama wanaweza kuishi pamoja kwa amani wakadumu.

Mshauri wa maisha na ndoa kutoka nchini Marekani Sarah E Stewart aliwahi kusema ndoa hubadili kila kitu hivyo wahusika wanapaswa kujiandaa kabla ya kuchukua maamuzi ya kuoa au kuolewa.

Leo nakuletea baadhi ya tabia ambazo ni muhimu kuzitambua kutoka kwa mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa.

Kwanza kabisa wahusika wote wawili wanapaswa kujuana kila mmoja kuhusu historia yao ya maisha ya uhusiano wa mapenzi kabla ya wao kukutana.

Kufanya hivyo kutawasaidia kila mmoja kujua mwenzake alipitia mambo gani na kuweza kujua namna gani ataishi nae pasipo kukwaza au kukwazwa.

Inatokea kuna ndoa huvunjika kwa sababu mwanaume amesikia mke wake aliwahi kuhusiana na mwanaume fulani mwenye maradhi hatari, iwapo wakajuana mapema mgogoro huu hauwezi kutokea.

Pia mwanaume hapaswi kuoa mwanamke ambaye ameshiriki kwenye mahusiano na wanaume wengi ndani ya eneo husika na kutegemea waishi hapohapo mbeleni inaweza kutokea dharau na kusababisha ndoa yao kuvunjika.

Iwapo itatokea ndoa ya namna hii basi wahusika wanashauriwa kuhamia eneo lingine la mbali wakaishi huko.

Usioe au kuolewa na mtu ambaye tabia zake huwezi kuvumilia, kwa mfano kama wewe hupendi ulevi na huwezi kuvumilia kuishi na mlevi basi hupaswi kuolewa au kuoa mtu mlevi ambaye huwezi kumbadilisha.

Usioe au kuolewa na mtu ambaye hujui kipimo chake cha hasira, watu wengi hawazingatii jambo hili ambalo linaweza kugharimu hata maisha ndani ya ndoa.

Ikiwa utaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hujui akikasirika anakuwaje na ni namna gani naweza kumtuliza ndoa yenu haitofika mbali itakuwa kituo cha migogoro.

Chunguza misimamo na imani ya mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa hii itakupa maelekeo sahihi kujua ni namna gani mna gani mnaweza kuishi kwa kutambua mwenza wako anapenda hiki na hapendi kile.

Utofauti wa misimamo umevunja ndoa nyingi sana, kuna ndoa huvunjika kwa sababu tu ya wahusika kutofautiana wapi waishi kijijini au mjini.

Tambua kinachompa furaha mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa, mfano kujua anapenda nini ili awe na furaha.
Kama anapenda mchezo wa mpira wa miguu ujiandae kuvumilia utani wa mchezo huo na mabishano yake.

Si hivyo tu mchunguze ujue tabia zake zote zisizofaa kisha muandae kisaikolojia ili aweze kubadilika kabla ya ndoa.

Pia jiandae kukutana na tabia mpya ambazo haukuweza kuziona kwenye uchumba hivyo jipe ujasiri na uvumilivu kwa lolote jipya linaloweza kutokea.

Peter Mwaihola.

Photo_1708448225112.jpg
 
๐—›๐—ฎ๐˜†๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐—บ๐˜‚๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜‡๐—ผ ๐˜€๐—ฎ๐—ต๐—ถ๐—ต๐—ถ ๐—น๐—ฎ๐—ธ๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐—ป๐—ถ ๐˜ƒ๐˜†๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ต๐—ฎ๐—บ๐˜‚ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฎ๐—ฑ๐—ต๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐˜๐—ฎ๐—ฏ๐—ถ๐—ฎ ๐˜‡๐—ฎ ๐—บ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜‡๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ผ,, ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—ฎ๐˜€๐—ถ ๐—™๐˜‚๐—น๐—ฎ๐—ป๐—ถ.
 
Unawezaje kujua kopimo cha hasira ya mtu ambae hujawahi kushuhudia akikasirika to the max??? Maana kuna wengine hata wao wenyewe hawajui their own boiling point...

Au ndo inabidi watu wachokozane ili wajuane vizuri?๐Ÿ™„
Kama ni mlevi ngoja alewe halafu mtie kidole
 
Huenda wewe ni miongoni mwa vijana wanaokaribia kuoa au kuolewa lakini haulewi ni mtu wa namna gani wa kuingia nae kwenye ndoa.

Mbali na kuangalia uzuri wa sura, umbile, kipaji au hali ya kiuchumi ya yule unaetarajia kumuoa au kuolewa nae kuna jambo lingine muhimu kuliko yote ambalo unapaswa kuliangalia kwa jicho la pekee.

Tabia ni jambo la muhimu kulipa kipaumbele wakati wa kuchagua unayetaka kuingia nae kwenye ndoa.

Inawezekana ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya wanandoa wenyewe hawakutumia vizuri muda wao kuelewa tabia za wenza wao na kujipima wenyewe kama wanaweza kuishi pamoja kwa amani wakadumu.

Mshauri wa maisha na ndoa kutoka nchini Marekani Sarah E Stewart aliwahi kusema ndoa hubadili kila kitu hivyo wahusika wanapaswa kujiandaa kabla ya kuchukua maamuzi ya kuoa au kuolewa.

Leo nakuletea baadhi ya tabia ambazo ni muhimu kuzitambua kutoka kwa mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa.

Kwanza kabisa wahusika wote wawili wanapaswa kujuana kila mmoja kuhusu historia yao ya maisha ya uhusiano wa mapenzi kabla ya wao kukutana.

Kufanya hivyo kutawasaidia kila mmoja kujua mwenzake alipitia mambo gani na kuweza kujua namna gani ataishi nae pasipo kukwaza au kukwazwa.

Inatokea kuna ndoa huvunjika kwa sababu mwanaume amesikia mke wake aliwahi kuhusiana na mwanaume fulani mwenye maradhi hatari, iwapo wakajuana mapema mgogoro huu hauwezi kutokea.

Pia mwanaume hapaswi kuoa mwanamke ambaye ameshiriki kwenye mahusiano na wanaume wengi ndani ya eneo husika na kutegemea waishi hapohapo mbeleni inaweza kutokea dharau na kusababisha ndoa yao kuvunjika.

Iwapo itatokea ndoa ya namna hii basi wahusika wanashauriwa kuhamia eneo lingine la mbali wakaishi huko.

Usioe au kuolewa na mtu ambaye tabia zake huwezi kuvumilia, kwa mfano kama wewe hupendi ulevi na huwezi kuvumilia kuishi na mlevi basi hupaswi kuolewa au kuoa mtu mlevi ambaye huwezi kumbadilisha.

Usioe au kuolewa na mtu ambaye hujui kipimo chake cha hasira, watu wengi hawazingatii jambo hili ambalo linaweza kugharimu hata maisha ndani ya ndoa.

Ikiwa utaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hujui akikasirika anakuwaje na ni namna gani naweza kumtuliza ndoa yenu haitofika mbali itakuwa kituo cha migogoro.

Chunguza misimamo na imani ya mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa hii itakupa maelekeo sahihi kujua ni namna gani mna gani mnaweza kuishi kwa kutambua mwenza wako anapenda hiki na hapendi kile.

Utofauti wa misimamo umevunja ndoa nyingi sana, kuna ndoa huvunjika kwa sababu tu ya wahusika kutofautiana wapi waishi kijijini au mjini.

Tambua kinachompa furaha mwenza wako kabla ya kuingia nae kwenye ndoa, mfano kujua anapenda nini ili awe na furaha.
Kama anapenda mchezo wa mpira wa miguu ujiandae kuvumilia utani wa mchezo huo na mabishano yake.

Si hivyo tu mchunguze ujue tabia zake zote zisizofaa kisha muandae kisaikolojia ili aweze kubadilika kabla ya ndoa.

Pia jiandae kukutana na tabia mpya ambazo haukuweza kuziona kwenye uchumba hivyo jipe ujasiri na uvumilivu kwa lolote jipya linaloweza kutokea.

Peter Mwaihola.

View attachment 2910478
hakunaga hizi habari
 
Back
Top Bottom