Nipo South Africa hapa Hakukaliki

Nipo South Africa hapa Hakukaliki

Pole mkuu, nadhani kama umeishi miaka 10 ushakuwa msauzi hawawezi kukugundua toka inje act kama unaandamana nao afu jiengue mdogomdogo.
Kuwa makini sana bado tunakuhitaji tz, maana huku ajali nazo zinatumaliza.
 
Nipo Johannesburg,South Africa hapa mitaa ya Jeep street tumejifungia ndani toka saa 10 jioni wenye nchi yao wanapiga wageni,kuwaua na kuwachoma moto kama kuku.Wanapita mtaa kwa mtaa wakikuona mgeni hakuna kuuliza ni kipondo bila huruma.

Wanachoma matahiri barabarani na kuyachoma moto magari ya wageni wote kwenye nchi yao cha ajabu sasa wanaowapiga ni watu weusi wenzao na sio wazungu,wachina au waarabu mpaka unajiuliza hawa hawataki wageni au hawawataki wageni weusi.

Kesho natakiwa kurudi kwangu Cape Town maana nilikata ticket ya go & return hapa najiuliza nitaenda vipi uwanja wa ndege na kurudi kwangu Cape Town maana kule hakuna fujo za kijinga na kipuuzi kama hivi
Kwani ni lazima ukaishi kwa wabaguzi?waachieni nchi yao.mbona kuna nchi nyingi tu africa za kukufanya ukawa na maisha bora
 
J'burg niijuayo mimi kuna mobile court twenty four hours in almost part of the city. Na jiji hili lilivyo linazidi majiji mengi tu ya Ulaya (kwa uzuri na infrastructure). Police ni wa kumwaga,blacks, indians, whites etc kwa nini mleta mada asijisalimishe kwa hawa?
Nafikiri unyama unafanyika kwa wazamiaji.

Ni zuri kuzidi hayo mengine ya ulaya mana huko ni ulaya pia na sio africa,
Mana aliyeko huko ni mzungu ndo kalijenga kama asingekuja huko kweli wangeweza kupajenga kama palivyo
 
waambie jaman mi natokea TANDALE KWA MTOGOLE labda watakuelewa
rudi kwenu achen ushamba kila ki2 SOUTH sasa wamewachoka Wa TANZANIA wengi huko ni wezi.
Nasapot hyo muvment
 
Dah! Very badly hapo itakuwa kunamkono wa makaburuu,, pia napenda kusema ivii wale ni vibakaa
 
no mkuu nina nyumba bongo ipo kibada ila huku ndio biashara zangu zilipochanganya na mke wangu pia ni msouth africa na watoto pia na tabia za watu wa nchi hii sio rahisi kumshawishi kwenda kuhishi nje ya nchi yake tena nchi yenyewe ikiwa kama Tanzania...ndio maana nimeng'ang'ania ndani ya nchi hii ili wanangu wakue kue nirudi nao nyumbani siwezi kumuachia huyu mwanamke hawa sio waleaji wazuri
Mdau wewe Komaa huko
 
Pole sana, endelea kujifungia humohumo mpaka uhakikishe vurugu zimeisha hiyo ticket wala isikusumbue uhai wako kwa sasa ndicho cha muhimu. tatizo serikali ya Zuma nayo ni legelege hivi watu wanauwaje wenzao kama vile hakuna polisi.
Kwa kuwa Unafanya biashara huko fikiria mara mbili je wakivamia na kupora biashara yako si watakuwa wamekurudisha nyuma sana. Kama vipi vurugu zikiisha funga virago urudi nyumbani kuliko kuishi kwa mashaka huko South.

Zuma ni mshenzi mno na ana sapoti huu ujinga...hapa hata mtu akikamatwa anaiba super market basi zitakuja gari za police 10 na helicopter juu angani ila leo waafrica wenzake wanauliwa uoni gari za police wala helicopter kuweka doria
 
Kwa hiyo mnaongeleshwa kizuru au wanawafahamuje msio wa huko?

tofauti ipo kubwa mno mkuu...wanajua wenyewe kwa wenyewe na hata ile kiroho tu ukiona mambo namna hii lazima ukose ujasiri hata kama unajua kizulu
 
We ng'ang'ania huko huko tu, wakikula kichwa itakua bahati mbaya tu
 
nilifikiri unapanga kurudi bongo kumbe unakwenda cape town halafu unakusifia cape town utadhani haipo ndani ya South Africa. Kwa mtazamo kama huu wako mtakula kipondo na kuchinjwa sana. Maana unachukulia nchi ya watu kama yako. kauli ya PM ipo kazini WAPIGWE TU

amna mkuu Cape Town anapaita kwangu kwa sababu ndio familia yangu ilipo...mke wangu wa Ki-Xhosa na watoto wawili naanzaje kuwaacha na kurudi bongo haraka namna hiyo
 
S.A wamesahau walikotoka. Hawa hawa waafrica wenzao weusi ndo waliowasaidia kuwatoa gizani kwa makaburu leo hii ndo wamekuwa maadui

Waswahili hawakukosea waliposema,"Mfadhili nyani umpe boga binadamu atakuroga"
 
Mkuu Cape Town yote hakuna vurugu?
si nimesikia hadi cape town?
 
We mvivu wa kufikiri badala ya kurudi nchi yako Tanzania yenye amani na upendo pamoja na mafisadi kibao unalaumu kuchelewa kurudi Cape town!! inafaa wakuvunje miguu kabisa.

Mtumie nauli basi... halafu aje ale na kula kwako na fujo zikiisha umrudishe south
 
Nilikuwa nawakubali saana Wa Sauzi ila katika hili nimeanza kuwaona Vilaza
Yani afazali wange wafanyia vurungu wazungu kidoogo ninge waelewa

Nilichogundua Wa sauzi waneanza kujiona black amerika
Sababu ya maendeleo waliyo nayo.
 
Back
Top Bottom