June Holliday Nostalgia: A Night in Konka Sowetto Nightclub, South Africa

Espoir_jnr

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
450
1,755
Natumai mko vyema ndani ya hili jukwa pendwa la Jamii Forums. Ngoja niende moja kwa moja kwenye shina la huu uzii.

Chapter 1 Namibia.
Toka mwaka uanze nilikua nimebanwa sana na majukumu ya utafutaji ukizingatia sisi tuliochukua njia za kujiajiri huwa tunapitia mengi sana wakati mwengine kuhakikisha biashara inasimama na usimamizi unakua madhubuti ili uendeleze majukumu yako kuhudumia familia kama baba, biashara zangu nafanyia katika mjii maarufu nchini Namibia na ndipo makazi yangu yalipo.

Basi mwezi wa sita nilipata kidogo ahueni kutokana na mambo kwenda sawa nikaamua kumtafuta rafiki yangu mkubwa sana ambae yupo Richard bay, South Africa ili nikapate mapumziko na mimi pia nijikumbushe kuwa ni binadamu kama walivyo watu wengine.

Na pia hii ni sehemu yangu pendwa kwenda niki hitaji utulivu kila nipatapo muda wa ziada.
basi tulikubaliana na huyu swahiba wangu juu ya safari yangu na kila kitu kilikuwa vyema.

Chapter 2 Durban &Richards Bay.

Usafiri ninaoutumia kufika Richard Bay ni Ndege, ambayo inatoka moja kwa moja kutoka Windhoek mpaka Durban kwa kuwa Richards bay hakuna International Airport yenye forodha ya uhamiaji. Niliagana na familia yangu pale Hosea kutako Airport na moja kwa moja nili elekea kucheck inn na kusibiri kuondoka.
Niliwasili majira ya saa 18:35 CAT

(CAT) means Central African Time, na kumkuta swahiba wangu kashafika kunipokea pale Airport ya King Shaka Durban, tulichukua Taxi mpaka Kwake Richards bay ambapo huchukua masaa ma 3 au 4, tulifika kwake majira ya saa 21:30 CAT na kupokelewa kwa bashasha kubwa sana na shemeji yangu wa ki - Xhosa pamoja na watoto wao wawili.

Nilikua nimechoka sana lakini hili halikuzuia kujibu maswali niliyokuwa nina ulizwa na wale uncle zangu wadogo wakitaka kujua wenza wako wapi, kwa kuwa sisi tuna utaratibu wa kutembeleana mimi na swahiba wangu na mara nyengine anakuja yeye Namibia na familia yake na mara nyengine naenda mimi na familia yangu kule kwao, ilibidi ni ingie WhatsApp nimpigie wife na kuongea na watoto na pia niwape wale uncle zangu waonge na rafiki zao.

Chapter 3 Johannesburg.

Nilitumia Wiki yangu yote ya kwanza na siku 3 nikiwa Richards bay, nikiogelea kwenye fukwe ya bahari, kupata vinywaji na chakula Safi pamoja na mazoezi.

Na pia kukutana na waswahili wenzangu ambao hatujakutana muda kujiliana hali na pia kufanya networking na watu wapya.

Wakati wa kurudi Flight nilikua napandia Johannesburg hivyo nika agana na swahiba wangu vizuri pamoja na familia yake, and on top of that walinifungashia zawadi za kuwapelekea familia nyumbani na pia kwakuwa sikuwa na mtu Johannesburg alini connect na rafiki yake mmoja ambaye yeye ni Raia wa hapa hapa na kuniambia atakupokea na utakaa nae siku izo zilizo salia ukisubiri Ndege ya kurudi Namiba pia akaniambia ni mtu poa na anapenda sana vibe na club.

Niliwasili Johannesburg usiku kwa Bus nikitokea Durban kweli nilikutana na yule jamaa kama nilivyo ahidiwa, jina tutamita (Mabena)

Mabena alinipokea pale Mtn Taxi Rank akiwa na Taxi yake au ofisi kama mwenyewe alivyokuwa anasema, kwa muda ule alikua anasikiliza nyimbo za Amapiano huku akiwa na chupa yake kubwa ya Black Label. Kwakuwa nilikua nimechoka na safari sikua na maswali mengi sana, tulifika kwake maeneo ya Vlakfontein, nilienda kuoga na moja kwa moja nililala bila hata kula.

Chapter 4 Konka Night Club.

Mabena alikua mtu poa sana yeye alikua ni Dereva Taxi na pia anafanya upande wa Bolt pale CBD Johannesburg, alikua anapenda sana wanawake na Pombe. na akipata free time anasema huwa anakesha club.

Basi siku zikiwa zimebaki siku mbili nikaribie kurudi Namibia, akaniambia na nukuu "Let's go and enjoy the night life with the riches of Johannesburg."

Na pia akasema atakuja na wanawake wakuspend nao time.

Siku iliwadia nakumbuka night saa mbili aliwahi kurudi na pia alikua na wanawake matata wa 4 na washkaji zake wa 2, alinitambulisha na moja kwa moja alinipatia mmoja wa wale wanawake aliokuja nao huyu tumpe jina "Thandiwe" alikua mzuri tu kama mjuavyo watoto wa ki- Zulu wako matata sana.

Final Chapter.

Tulitoka huku nikiwa sijui tunaelekea club gani na ilikua ni Saturday, njiani tulikua tunasikiliza nyimbo huku wao wakiongea ki-zulu ambacho nilikua nafahamu maneno machache sana, huku mwenyeji mabena akiwaambia waonge English na mimi nichangie mada huku akiwatisha kuwa tuta anza kuongea kiswahili mimi na yeye na wao wasielewe kitu, generally ilikua ni utani tu na maneno ya hapa na pale, basi tulitoka kule mpaka sehemu mmoja inaitwa Pimville katika mtaa wa Modjaji.

Nilikaribishwa na magari makali sana ya kifahari mwengine sijawahi kuyaona na walimbwende walionawiri na kupendeza, huku kwa juu kukiwa na Bango kubwa lililoandikwa KONKA.

Tulifika kila mtu na mwanamke wake kana kwamba tunafahamiana sana kumbe hakuna lolote, kwa wakati ule nilikua karibu sana na mwenyeji wangu mabena kutokana na kama tujuavyo South muda mwengine usalama hakuna lakini alinitoa wasiwasi na kuniambia hapa wanakuja Vibopa na wasanii wakubwa na Watu wenye pesa zao Mjini na ulinzi upo wa kutosha.

Basi Mabena alilipia pale entrance fee sikujua kiasi gani lakini inavyonyesha ni ghali kidogo tukapatiwa meza yetu na kuanza kupata vibe la KONKA.

Kwa siku ile Dj nakumbuka alikua anaitwa Kabza de small walisema ni msanii marufu sana wa nyimbo za Amapiano, alitukosha moyo pale huku Watu wakianza kumiminika ndani.

Bei za vinywaji kwa kweli pale zilikua super expensive sababu ya hadhi ya ile sehemu ninachokumbuka ni ile hookah au (Shisha kwa nyumbani)/ ilikua ni (R1500) = 200,000Tzs na zililetwa 4 kulikua na Heineken pamoja na Savannah hizi wadada wa South wanazipenda sana pia zilikua za kutosha, zile zilikua (R25) = 3300Tzs binafsi nilitumia Wine ambapo zililetwa 8 (R300) each = 40000Tzs, na soseji, nyama choma hivi sikujua bei gani mwenyeji wangu aliniambia hapa kuna Pombe mpaka za (R300,000)= 40M Tzs, nilistaajabu lakini ya kaisari nilimuachia kaisari.

Vibe lilikua kubwa sana kulikua na wanawake wazuri kupitiliza wazuri haswa nikisema hivi nadhani kwa mtu ambae kafika South Africa anaelewa.

Sijawahi kuona lile vibe kwa kweli, na watu waliokuwa mule ndani walikua ni watu mashuri kweli na wenye pesa zao.

Mfano kwa siku ile kulikua na Kabza De Small ndio Dj, Daliwonga nk. wafanya biashara wakubwa wa pale Town, wachezaji mpira wa club kubwa za South Africa nk.

Saa 2:00PM ndio mwisho ile Club huwa ina fungwa basi tulitoka pale tuliongozana na kila mmoja alitokomea kichaka chake binafsi sikuenda mbali nilitafuta Hotel karibu nikaenda kulala na Thandiwe, kama mjuavyo ulevi ukishafika kichwani.

Kwa Mabena na wale wengine sikujua walikwenda wapi, asubuhi ilivyofika nikampigia simu Mabena mpaka saa 6 alikuja pale hotel na tukaelekea kwake niliachana na yule mwanadada na tukabadilishana contacts.

Nilivyofika nililala mpaka jioni nika amka na kumkuta Mabena ndio anatoka kazini.

Tulipiga story na mikasa ya jana usiku na huku nikijianda na safari ya kurudi.

All ni all kama mtu akipata nafasi ya kufika Johannesburg atembele hii club japokuwa ni Expensive lakini options zipo unaweza pata vitu affordable, I rate it 8/10 izo 2 ni sababu ya sehemu kuwa sio kubwa sana.

Monday jioni Mabena na mmoja wa rafiki zake wa kiume tulioenda nae KONKA usiku wa juzi walinisindikiza Airport Kurejea nyumbani niliwashukuru na kuwachia kiasi kidogo nilichokua nacho kama zawadi niliwapatia ($600) kama shukurani na kuwachia ahidi ifikapo December nitarejea tena mungu akipenda.

Kwa kweli ilikua break nzuri sana na nilipata refreshment na nguvu mpya nilivyorudi nyumbani.

Asanteni Sana na poleni kama nitakua nimeruka any detail's coz siwezi elezea kwa asilimia mia kila kitu na nina karibisha maswali kama yapo.

It was on June 6 - 19 2023.
 
Kunjani...! Stori kali sana Malume, always stori za bondeni zinakuwaga za moto sana 😂
 
Nilienda kujiridhisha kama kweli kuna KONKA. Na mitaa ya palmville aisee ni balaa na kisanga hayo magari bongo sijawahi kuyaona 🙌🤔
 

Attachments

  • Screenshot_20240121-162450.png
    Screenshot_20240121-162450.png
    1.7 MB · Views: 11
  • Screenshot_20240121-162427.png
    Screenshot_20240121-162427.png
    1.2 MB · Views: 7
  • Screenshot_20240121-162400.png
    Screenshot_20240121-162400.png
    460.1 KB · Views: 9
Back
Top Bottom