Mtengeneza kahawa

ashurabakari272

New Member
Jun 19, 2023
2
1
Habari zenu.

Leo ngoja nishee story yangu kwa ufupi

Nakumbuka mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu tulishauriana kwenda South Afrika kutafuta maisha tukiamini kwamba huko maisha ni marahisi sana, basi ikabidi tuanze kutafuta nauli kipindi hicho ilikuwa nafanya biashara ya kuuza nguo za mtumba kwa bahati nzuri biashara ilikuwa sio mbaya kwa kipindi hicho, basi baada ya kupita miezi kadhaa tulifanikiwa kupata nauli na pesa ya kutengezeza passport.

Baada ya hapo tukaianza safari mimi na rafiki yangu kuelekea South Africa, safari wala haikuwa ngumu sababu tulijipanga na tukiamini baada ya kufika South maisha yetu yatakuwa mazuri.

Tulifanikiwa kufika South Africa katika mji wa Johanesburg, kiukweli tulivyofika ni tofauti na tulivyotegemea, maisha kwetu yalikuwa magumu mno bora hata Tanzania basi yule mwenzangu akaamua kurudi nyumbani baada ya kukaa miezi 3 bila ya muelekeo.

Nikamwambia wewe nenda mimi nitakomaa yeye ilimbidi arudi sababu alikuwa na Familia, basi baada ya mwaka mmoja maisha kuzidi kuwa magumu ikabidi nihame mji nikahamia mji mwingine ambao unaitwa Cape Town, baada ya hapo maisha kidogo yakaanza kubadilika baada ya kukutana na mkaka mmoja ambae ni mkenya akiwa anatafuta watu wa kwenda kufanya kazi kiwandani yeye alikuwa msimamizi pale katika kiwanda.

Basi nikaona haina jinsi sababu nipo kwenye utafutaji ngoja nifanye kazi, sasa kiukweli alitokea kunipenda kwa sababu tunaongea lugha moja nikafanya kazi kama miaka 3. Kuna siku yule mkenya akanambia kuna kazi ya kuosha vyombo katika Duka la kahawa sehemu moja mjini.

Akanambia kama utakuwa tayari basi inabidi twende wote kila Jumamosi kama deiwaka, basi kwa vile nipo kwenye kupambana ikawa sichagui kazi nikamwambia sawa kwa hiyo ilikuwa nafanya kazi sehemu mbili Jumatatu hadi Ijumaa kiwandani na Jumamosi naenda kuosha vyombo kwenye duka la kahawa, kiukweli maisha kwangu yakaanza kuwa mazuri japo sio sana ila ilikuwa sikosi pesa ya kula na kulipa kodi

Miaka ikasonga hapo nishazoea kazi na nishajifunza lugha ya kingereza ili nisipate shida kwenye maeneo ya kazi maana ndio lugha inayotumika, nikafanya kazi kama miaka mitano kwenye duka la kahawa hiyo ni deiwaka kila Jumamosi tu bila ya kujua kwamba kuna siku nitakuja kuajiliwa kabisa

Basi kuna siku naenda kazini yule boss anayemiliki duka la kahawa ni mzungu kabisa akanambia unaonaje tukikuajili kabisa maana tumependezwa na utendaji wako wa kazi wa kila Jumamosi. Kiukweli niliona kama ndoto sababu kama mnavyojua kazi za kiwandani zilivyo malipo yake na pale ilikuwa nalipwa vizuri japo ni kila Jumamosi. Nikajisemea mwenyewe je wakiniajili kabisa ina maana itakuwa nimevuka hatua fulani!

Basi sikuchelewa ile ofa nikawamjibu mzungu mimi nipo tayari lakini muda huo wananiajili kama muosha vyombo na sio vinginevyo. Mwaka 2020 mimi nikapewa ajira kamili ya kwenye duka la kahawa na wakawa wananilipa vizuri kweli basi huo ndio ukawa mwanzo wa ndoto zangu

Pale kwenye Duka la kahawa walikuwa wanadili sana na kutengeneza kahawa, nikisema kahawa yani ina maana ni kahawa zote zinapatikana pale. Basi na mimi nikaanza kushawishika kujifunza kidogo kidogo kukiwa hakuna wateja nachukua muda wangu kujifunza ikiwa na ndoto kwamba ipo siku na mimi nitakua Barista mkubwa na hii ndoto ya kuwa Barista nikaifanyie katika Nchi yangu ya Tanzania.

Kufika mwaka 2022 ikawa nishajua kabisa jinsi ya kutengeneza kahawa na kuielezea kahawa ili kumshawishi mteja, ikabidi yule Boss akaniita na kuniambia kuanzia sasa inabidi uwe unatengeneza kahawa na sio muosha vyombo kama tulivyokuchukua, kiukweli nilifurahi sana sikuwahi kujua kama nitafikia hatua hii nilimshukuru sana yule Boss wangu kwa nafasi aliyonipa maana nikasema sasa nishapata kitu ambacho kitakuwa ni ndoto yangu ya kunifanya nikaishi vizuri

Basi kidogo kidogo nikaanza kununua vifaa vya kutengenezea kahawa vifaa vidogovidogo vya kahawa kama Grendar ya kahawa, vikombe, Espresso machine, na vitu ninavyohusiana na biashara ya kahawa nikiwa naamini fursa ipo nyumbani Tanzania, kwa maana nikifungua biashara nyumbani itakuwa bora zaidi kuliko huku nilipo nikiamini nyumbani kila kitu kinawezekana ukiwa na nia.

Kiukweli natamani sana nije kuwa Barista mkubwa nchini kwangu na niwe Mwalimu wa kufundisha wenzangu kuhusu biashra hii ya kahawa.

Kikubwa kilichonifanya niweze ku share story yangu sina mtaji wa kuchukua fremu ambayo ipo location nzuri ya kufanyia biashara kwa sasa hivi, kwa sababu pale ninapofanya kazi kampuni imeuzwa kwa hiyo Boss mpya anataka wafanyakazi wapya. Kiukweli natamani kurudi Tanzania naamini hili linawezekana.

Niwaombe wa Tanzania wenzangu na ambao sio Wa Tanzania naombeni ushirikiano wenu

Asanteni.

IMG-20230619-WA0030.jpg
iyo ndio kazi ya mikono yangu.
 
Hongera sana, karibu nyumbani hautafeli mapambano amini hivyo
 
haya mambo ya kapachino sijui nini, itabidi utafute mitaa ya masaki na posta utauza poa. ila uswahilini tumezoea Ile ya kakikombe kadogo chungu kama Nini
 
Ma

View attachment 2662475 iyo ndio kazi ya mikono yangu.
Maendeleo yakoje mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom