Habari zenu wadau
Ni siku yangu Ya pili hapa Rock City (Mwanza) kama inavyo julikana na wengi
Kwa wale wanao tamani kufika mwanza ambalo lisha tunukiwa sifa ya jiji miaka kadhaa sasa lakini jina hilo haliendani na sifa ambayo inapewa
Saa yangu inaonyesha ni saa 1:23 usiku ndani ya dar lux tunaingia mwanza, moyo unashtuka baada ya kuambiwa Nyegezi stand ndo mwisho wa safari, wakimaanisha tusha fika mwanza
Ni giza kila sehemu stand ya nyegezi kama dampo jamaaaani hakuna taa barabara imejaamashimo, taa za barabarani haziwaki
Tunatoka nyegezi twaelekea Nata ambako ndio mwisho wa gari jamaaaani city centre mashimo, viroba vya taka vimetupwa katikati ya barabara
Hiyo ndio mwanza unayo isikia
Pana pambazuka asubuh najiandaa kwa ajili ya mishe ilo nifikisha uuuuuwiiiiii daladala zimechoka, na zinajaza balaa, vituo havieleweki kama vile hakuna mkandarasi wa jiji
Je mkuu wa mkoa hayupo au hajifunzi kutoka kwa Makonda