Nipo Mwanza, haijanivutia kabisa

Nipo Mwanza, haijanivutia kabisa

Habari zenu wadau,

Ni siku yangu ya pili hapa Rock City (Mwanza) kama inavyo julikana na wengi.

Kwa wale wanaotamani kufika Mwanza ambalo lish tunukiwa sifa ya jiji miaka kadhaa sasa lakini jina hilo haliendani na sifa ambayo linapewa.

Saa yangu inaonyesha ni saa 1:23 usiku ndani ya Dar lux tunaingia Mwanza, moyo unashtuka baada ya kuambiwa Nyegezi stand ndo mwisho wa safari, wakimaanisha tushafika Mwanza.

Ni giza kila sehemu stand ya Nyegezi kama dampo jamani hakuna taa barabara imejaa mashimo, taa za barabarani haziwaki.

Tunatoka Nyegezi tunaelekea Nata ambako ndio mwisho wa gari jamani city centre mashimo, viroba vya taka vimetupwa katikati ya barabara.

Hiyo ndio Mwanza unayo isikia, pana pambazuka asubuhi najiandaa kwa ajili ya mishe ilo nifikisha uwiii! Daladala zimechoka, na zinajaza balaa, vituo havieleweki kama vile hakuna mkandarasi wa jiji.

Je, mkuu wa mkoa hayupo au hajifunzi kutoka kwa Makonda?
Kama umedanganya muda hata ulichomaaanisha utadanganya tu. Hivyo umekosa uaminifu unadanganya
 
Back
Top Bottom