Hayati Rais John Pombe Magufuli akumbukwa kwenye uzinduzi wa Ikulu Mpya Dodoma.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AKUMBUKWA KWENYE UZINDUZI WA IKULU MPYA DODOMA.

Leo 10:15hrs 21/05/2023

Hayati Rais John Pombe Magufuli alituonyesha na kutufundisha ya kwamba,kuwa Rais na kufanya vizuri haihitaji uwepo madarakani miaka kumi! kazi uliyotumwa kuifanya kwa miaka 10 iliyoshindikana kufanywa kwa miaka 40 inawezekana kumalizwa kwa miaka 5,Kufikia May 17 mwaka 2021,kilipotokea kifo cha Rais Magufuli,Ujenzi wa reli ya Umeme kiwango cha SGR kutoka Dar to Morogoro Ujenzi ulifikia asilimia 90% Ujenzi wa Ikulu ya Dodoma ulifikia asilimia 60% kila wizara ilikuwa tayari imelipwa na wizara zote zilikuwa zimehamia jijini,Dodoma,jambo lililoshindikana kutolewa maamuzi na kutekelezwa tangu awamu ya kwanza ilipokubaliwa kuwa Dodoma ndio mji mkuu wa Tanzania na sio Dar es Salaam,lilitekelezwa na Rais John Pombe Magufuli kwa miaka mitano tu,ukweli ni kwamba nchi yetu ilipata bahati ya kuwa na kiongozi madhubuti,mwenye maamuzi na mtekelezaji,Rais John Pombe Magufuli,itachukua miaka kwa wengine kuligundua hilo,

Sifa za Waziri wa Ujenzi,John Pombe Magufuli ndio zilimfanya apate uraisi 2015 Chama kilikuwa kimepoteza sifa,dhoofu in hali,yupo ndugu mmoja hivi sasa ni Waziri nae alisema alikitoa chama shimoni wakati huo awamu ya nne,ukivaa uniform za CCM unapigwa mawe,nadhani kila mmoja hilo analikumbuka ndio maana hata CCM walikubali kauli mbiu "M4C Magufuli for Change" kwenye uchaguzi wa Urais 2015 wakimaanisha "vote for Magufuli bila kuitaja CCM" kwa sababu CCM ilikataliwa na wananchi ila mgombea wake alipendwa na Wananchi,nae ni John Pombe Magufuli na tuliona performance yake baada ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa hakika alitutendea haki Watanzania,Chadema 2015 walithubutu kusema , "Magufuli yupo vizuri ila wanawasiwasi na chama chake" pia wakasema "Wana wasiwas na mfumo ila hawana shaka na Magufuli" katika uchaguzi wa 2015 wapo wanachadema walihama Chadema na kumfuata mgombea wa CCM,ndugu John Pombe Magufuli.

Wakati wa tamati ya kampeni ya Uchaguzi wa Rais,Mwenyekiti wa Chadema akihitimisha kampeni hizo,aliwaambia wananchi kwamba mgombea wa CCM ni mzuri ila tatizo ni CCM,Mwenyekiti wa Chadema,ndugu Mbowe alisema ndani ya masaa 24 atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo mgombea wa Chadema,Mh Edward Lowassa atashinda uchaguzi huo,Mungu alijua na kumuandaa mtu wa kufanya kazi ya kuirudisha Tanzania kwenye mstari,hasa katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa korona uliokuwa unakuja,Mungu alimuandaa Rais John Pombe Magufuli kuiongoza Tanzania katika kipindi hiko,kwa hakika Tanzania ilipiga hatua,Rais John Pombe Magufuli alianza na vituo vya afya na kuimarisha hospital kubwa zote nchini kuwa zenye hadhi ya kutibu magonjwa yote bila Mtanzania kuomba rufaa kwenda nje ya nchi,

Kwakweli vituo vya afya kila kata ni msingi mzuri wa community health. Vikipata maji ya uhakika na umeme, mafridge ya kuhifadhia dawa na wataalamu wenye sifa. Mzigo mkubwa kwenye hospitali za rufaa ukapungua,sisi wa uswazi ndani ndani,barabara ya lami gomz to Moshi bar yenye taa na mitaro yake,barabara ya zege maji chumvi kimara korogwe hadi Ubungo external,vichochoro vyote vya Jiji la Dar na Dodoma vilipigwa lami na zege,mradi wa maji kisarawe to gomz,toka 1994 tunahamia gomz hatukuwahi kua na maji ya bomba,Chuma kimeingia mimaji kama yote, kimara,tabata hadi Kinyerezi mimaji inatoka masaa 24,baada Chuma kufariki na maji nayo yameanza kufariki,maboza yameanza kuongezeka,tembelea Kinyerezi utajionea mwenyewe,

-Kwenye shida kuu tutamkumbuka Hayati Rais Magufuli kwa ushujaa wake.

#Wakati Rais wa Marekani,Donald Trump na Marais wengine wakipambana na korona kwa nguvu za binadamu, Dr.John Pombe Magufuli alikua akipambana na korona kwa sala, maombi na kufunga,

#Wakati Marais wengine wa afrika wakichekacheka Na Mabepari, Mabeberu na wasiopenda Maendeleo, Dr.John Pombe Magufuli alikuwa akiwachana makavu dhidi ya dhuluma na uzandiki wao kwa nchi masikini hasa Tanzania,

#Wakati Dunia ikipambana na adui maradhi, Dr. John Pombe Magufuli alikuwa akipambana na adui umasikini wa Watanzania,

#Dr. John Pombe Magufuli ndiye aliyeuweza Mfupa uliowashinda wengi Tanzania na nje ya Tanzania,mfupa Wa "SERIKALI HAINA FEDHA, SISI NI MASIKINI",

#Dr. John Pombe Magufuli alipasha kwa pushapu za kuonesha uimara wake kiafya,anawaza kurejea kuendeleza miradi mikubwa ya kiuchumi nchini,

#Wakati viongozi wa vyama vya siasa afrika vikiendesha chaguzi kwa fedha za mikopo na misaada,Rais Dr. John Pombe Magufuli alikimbia aibu hii ya kuwa ombaomba kwa Mabeberu,kwa kuweza kujikimu katika uchaguzi Mkuu,2020,

#Wakati Nchi nyingine za afrika na dunia zikifunga mipaka na kuzuia raia wake wasitoke nje kwa sababu ya ugonjwa wa korona, Rais Dr. John Pombe Magufuli aliwahamasisha Raia wake kuendelea kuchapa kazi, Ili kujiletea kipato na kukuza pato la nchi,

#Wakati Marais wengine wa afrika na kwingineko duniani, wakiogopa kuirejesha mikataba tata ya rasilimali za nchi mezani kuijadili ili kupata haki ya raia iliyoporwa,Rais Dr. John Pombe Magufuli aliweza kukomaa na kampuni za kigeni za madini katika kutafuta usawa wa unufaikaji wa raia katika rasilimali zao nchini,
*Nchi ikalipwa Mabilioni na kurejesha heshima ya RASILIMALI ZA TANZANIA dhidi ya mataifa ya kibepari na kibeberu,

-Kwa miaka mitano ya Rais John Pombe Magufuli, tutamkumbuka kwa mambo yafuatayo;-

Kufufua reli ya kutoka Dar es salaam-Tanga-Kilimanjaro-Arusha

Upanuzi wa Bandari ya Dar, Tanga, Mtwara

Ujenzi wa gati Mafia

Ukarabati wa vivuko, Mv Pangani, New Mv Butiama hapa kazi Tu, nakadhalika

Mradi wa rada airport ya Dar, Mwanza, Songwe, KIA ....

Elimu bila ada

Vituo vya afya vya kila halmashauri

Hospitali za wilaya, mikoa, na kanda: Serengeti, Hospitali ya kumbuku ya Mwalimu Nyerere, Uhuru Dodoma, nakadhalika

Barabara za mitaa Dar na katika majiji mengine, na miji mingine

Ujenzi wa kota za gorofa Magomeni

Ujenzi wa masoko makubwa: Soko la Job Ndugai Dodoma, Chief Kingalu Morogoro, soko la Kisutu, soko la Magomeni, soko la Mbagala, na ya mikoa na wilaya nyingine

Ujenzi wa standi za kisasa: Mbezi Lous, Dodoma, Morogoro, Korogwe, nakadhalika

Ujenzi wa majengo ya makao makuu ya Halmashauri: Kigamboni, Mkalama, nakadhalika

Daraja la mto Kilombero, na mengine mengi

Madaraja ya waenda kwa miguu: Dar na Mwanza

Ukarabati shule kongwe na vyuo: Pugu, Galanos, Tunduru, Msalato Girls, nakadhalika

-Wafanyabiashara walikubali kulipa kodi walipoona utekelezwaji wa mambo haya,

................👇
1. JPM anajenga Reli ya Mwendo kasi – SGR.
2. JPM anajenga Bwawa la Umeme – Nyerere HydroPower.
3. JPM amenunua Ndege 13 aina tofautitofauti.
4. JPM amejenga Ikulu kule Dodoma na yale Magorofa ya Wizara kule Mji wa Serikali Dodoma ( Mtumba) Magufuli City
5. JPM amehamisha Makao Makuu ya Serikali na ameijenga Dodoma imekuwa Jiji
6. JPM amejenga FlyOver Dar es Salaam pale Ubungo na TAZARA.
7. JPM amejenga daraja la Tanzanite pale Selander.
8. JPM ametengeneza huu Mfumo wa Kompyuta wa Malipo ya Serikali.
9. JPM alikuwa anaweka umeme hadi Vijijini (kwa Tsh. 27,000/= tu.)
10. JPM ameshawishi Bomba la Mafuta kutoka Uganda lipite Tanzania.
11. JPM anajenga daraja la Kingongo Ferry Busisi kule ziwa Victoria.
12. JPM amejenga Meli kubwa mbili mbili kila ziwa, yaani Ziwa Victoria 2, Ziwa Tanganyika 2 na Ziwa Nyasa 2.
13. JPM amejenga Hospital za Kanda kubwa nne… Dodoma, Mara, Mtwara, Geita na Songea
14. JPM amejenga Hospitali za Wilaya Zaidi ya 70
15. JPM amejenga Mradi Mkubwa wa Maji ya Victoria kule Tabora
16. JPM amejenga Mradi wa Maji Mkubwa Arusha
17. JPM amejenga Barabara ya Njia Nane Dar es Salaam hadi Kibaha
18. JPM alikuwa anajenga Mizani za Kisasa kabisa Kwenye Barabara zote kubwa
19. JPM amejenga Vituo vya Afya Zaidi ya 500
20. JPM amejenga na Kununua Rada 4 za AirPort
21. JPM amejenga Viwanja vya Ndege Mara, Iringa, Mbeya, Chato, Songea na Rukwa
22. JPM amejenga Masoko ya Madini kila Mikoa yenye migodi ya madini
23. JPM amejenga ukuta wa Mirerani na kuweka Camera za Ulinzi
24. JPM amejenga Bandari Kilwa, na kuzipanua Bandari Mtwara, Tanga na Dar es Salaam
25. JPM amejenga Masoko ya Kisasa zaidi, ya maana kama Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam
26. JPM amejenga Bus Stand za Kisasa Zaidi mikoani kama Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam
27. JPM amenunua Vifaa Tiba kama MRI, CT Scan, Vifaa vya Kufanyia Oparations za Moyo pale JKCI Wagonjwa wanatoka nchi jirani kuja kutibiwa.

-Chadema ndio walikuwa wapingaji wa miradi yote aliyokuwa anaifanya Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati Rais Magufuli,!kazi yao ni kuwapumbaza wanachama na wananchi kwa ujumla waone tatizo la chadema ni Magufuli wakati Magufuli hayupo na hakuwahi kuongoza chadema,kila uzi lazima vijana wa Mbowe wataje ni kutokana na Hayati Rais Magufuli,kutokana na Chadema kufa kila mahali kwa kupoteza mvuto,viongozi wao wamebuni mbinu ya kukwepa aibu hii kwa kujificha kwa hayati rais Magufuli! Viongozi wa Chadema wakihojiwa kwa nini chama hakina ofisi watakujibu tatizo ni Magufuli,kwa nini Chadema hawataki kupata majibu kwa Mwenyekiti Mbowe badala yake mnataka majibu yatoke kwa Hayati Rais Magufuli,utagundua Hayati Rais Magufuli ni ''measuring stick'' kwa kila kitu,vilivyopo na ambavyo havipo,

Tundu Lisu akiulizwa kuwa yeye ni makamu mwenyekiti wa Chadema lakini kwa nini hafanyi kazi za Chadema? Bavichaa watakujibu chanzo ni Magufuli! Bavicha ukiwauliza kwa nini kamati kuu ya Chadema wanafanyia vikao vyao kwenye hoteli za kitalii na kuacha ukumbi wa ufipa ? Utajibiwa tatizo ni hayati Magufuli! Chadema wakiulizwa kwa nini kwenye uchaguzi mliwatosa makada wenu waliokipigania chama ,mkabadili gia angani na kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame(orodha ya chadema ya mafisadi wakuu wa nchi )?Utajibiwa tatizo ni Hayati Rais Magufuli,ndugu zangu Chadema tambueni anayepaswa kuulizwa kuhusiana na mabaya na mazuri ya Chadema ni Mbowe na Tundu Lisu hao ndio viongozi wenu mliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa sasa,Hayati Rais Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa chadema ,hivyo kukaa mnamhusisha na kuporomoka kwa chama chenu ni kupoteza muda na kuonyesha uzwazwa wa hali ya juu.

-Watanzania wana performance appraisal ya Kiongozi wao bora,nae John Pombe Magufuli.

Kundi la Wananchi masikini walioneemeka au kupata ahueni kijamii,kiuchumi na kisiasa katika awamu ya Rais Magufuli daima watamchukia mtu ambae anamsema Rais Magufuli ambae kwao alikuwa mkombozi,kitendo cha Rais Magufuli kuleta nidhamu serikalini tayari ni neema maana watu watahudumiwa ipasavyo na hakika watu walihudumiwa ipasavyo,Umeme ulikuwa stable na Umeme usipokatika unatumika na watu wote na ukiwa stable faida twapata sote,aliwaachia wamachinga uhuru wa kutengeneza vipato vyao vya halali na wakapata hela kwa kazi za halali kwa hakika Wamachinga walimpenda Rais Magufuli kwa hilo,na kwa ujumla hatuwezi kusema hakuna alieneemeka kiuchumi! Wananchi wana mfano wao wa kiongozi bora,wana performance appraisal ya kiongozi wao bora,nae ni John Pombe Joseph Magufuli,Mtu ambae amefanya kazi na watanzania bara miaka zaidi ya 20 akiwa ni Field Public Leader tangu akiwa Naibu Waziri miaka ya 1995 kisha Waziri kamili katika wizara zaidi ya tano kwa miaka ishirini na baadaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
See the pictures below;-
 

Attachments

  • IMG-20230521-WA0007.jpg
    IMG-20230521-WA0007.jpg
    45 KB · Views: 12
  • IMG-20230521-WA0006.jpg
    IMG-20230521-WA0006.jpg
    20.8 KB · Views: 12
Umemaliza kila kitu sema watanzania wazembe wa kusoma makala ndefu!.

Kwa yeyote anaye-digest mambo mwenyewe kazi ya JPM inaonekana!

Hata kama watajitahidi kufunika yote yaliyotendwa kama maandiko yasemavyo.....

"Hata kama hawa watanyamaza, basi mawe yatapiga kelele"
 
Back
Top Bottom