Ni aibu kusema Mwanza ni jiji la pili, limechoka, linachekesha, halmashauri hazina hela

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,080
2,000
Kama anakuja mgeni mwanza unamuambia eti mwanza ndilo jiji la pili Tanzania atakushangaa sana,last time nilikuwepo huko 6 years ago kulikuwa na ahueni,nipo huku sasa kwa miezi kadhaa tangu mwaka jana

Ndugu zangu ambao hamjaja mwanza muda mrefu hali ya huku ni kichekesho,ngoja niseme machache tu:

-Ukiingia mwanza ile stend ya zamani imevunjwa kwa mbwembwe ikasogezwa kwa mbele yako tu kichekesho sasas,ile stendi ya zamani hakuna kinachoendelea hata tofali moja halijawekwa ingawa ni takribani miezi minne,wanadai kuna kesi utajiuliza haraka ya kuvunja ilikuwa ni nini?hapo walipohamia sasa nakuhakikishia hata stendi ya Nanjilinji ni kali kuliko huo upuuzi hapo kwanza imekuwa ni maficho ya vibaka,ni pachafu kama li mwanza lilivyo sasa hivi

_Ukifika mjini kati sasa utacheka,soko kuu lilifungwa wale wauzaji wamesambaa pale mjini hakufai narudia tena HAKUFAI,na soko lenyewe haijulikani ni kinaendelea ni kama vile hela hakuna sijui?

-Barabara ni chafu hazisafishwi ipasavyo hapo nazungumzia za lami,taa za barabarani zile za security zipo lakini haziwashwi,uende nyasaka,igoma,nyegezi umeme ukikatika usiku inasikitisha sana ni giza tororo

-Barabara za mitaani kama kwa mbunge mabula anayejifanya mzalendo ni kituko kama siyo wale vijana wanaotupiaga vi gunia vya mchanga kuziba mashimo na baadaye kuomba hela basi hata bwana mabula ile barabara ya majengo kufika kwake angeshindwa,nimeambiwa halmashauri hazina hata hela ndogondogo maana zote zinapelekwa hazina kwa matumizi ya maana kama vile kununua mandege kwa cash

MWANZA IMEDODA<IMECHOKASANA)kwa mwendo huu wa halmashauri kukosa hata hela ya kujaza magunia ya mchanga barabarani tuendelee kusubiri miujiza ila tusirudie kujivunia kwamba ni jiji la pili ni aibu sana
 
Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,468
2,000
Hali siyo nzuri Mwanza. (1) machinga wamejazana mbele ya maduka hasa Barabara ya Nyerere na hakuna cha kuwafanya. Katika nchi iliyo na maendeleo lazima kuwe na mpangilio wa kila kitu ndiyo maana kuna Idara katika Halmashauri zetu inayoitwa Idara ya Mipango Miji. Machinga wanatakiwa wapewe sehemu yao maalum lakini hawaguswi na viongozi wa Jiji ukiwaeleza kuhusu machinga hawana la kufanya.

(2) Soko Kuu lilivunjwa kwa nia nzuri kabisa ya kujenga soko la kisasa lakini sasa yapata kama miezi mitano hakuna kinachoendelea. Labda kuna sababu ya maana lakini hata hivyo basi wananchi tungeelezwa juu ya ucheleweshaji huo.

(3) Serikali ione uwezekano wa kuwapa Halmashauri fedha za kutekeleza shida ndogo ndogo zinazojitokeza ili zirekebishwe mara moja.

(4) Soko ambalo wafanyabiashara wamehamia kutoka soko kuu linasikitisha. Kwa kweli ni pachafu na hasa Jumapili wafanyabiashara wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani. Hapa Mwanza kuna tatizo. Mwanza kunihitajika Idara ya Mipango Miji ambayo haingiliwi vinginevyo kila mtu atakuwa ndiye Afisa Mipango Miji.
 
nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,080
2,000
kiongozi siyo masihara,hiyo stendi siku basi likiingia mwanza saa saba usiku usikubali kushuka pale bora ukashukie nata au stendi ya zamani utafute lodge,ni ka uwanja fulani cha shule cha matope kukiwa na mvua pakiwa na jua ni vumbi yaani ile stendi ya makumbusho ni kali mara 1000 ya huu uchafu wa mwanza,walivunja nyegezi na soko kuu ni miezi minne sasa hata ujenzi haujaanza,mjini nako ni vurugu mabarabara machafu,barbara za ndani ni mahandaki,inatia huruma sana
Weka picha.... Bila picha sisi wa nanjilinji tutaiona VP stand

Sent using Jamii Forums mobile app
 
eyamango

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
464
500
Ok,umekuja kivingine,bila shaka uzi wako huu ~inderctly~unahusu 'batle' ya "Mwanza Vs Arusha"

Ila mjanja wewe!!!Ngoja waje wenye miji yao.

Kanyaga twende.
 
nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,080
2,000
nachukia sana watu wazima mnapohaha kurukaruka kama maharage,mnajaza mapicha ya ile mwanza safi,nishaishi sana hadi nje ya nchi,mapicha ya maghorofa hayanizuzui,ni wapi nimesema mwanza hakuna magorofa au hakuana barabara?
JIBU MASWALI HAYA?
_kwa nini taa security za barabarani haziwaki?nyasaka,igoma,nyakato,nyegezi nk
_barabara za ndani nimetolea mfano kwa mabula mitaa ya majengo ninapoishi karibu na canada sports bar kote ni mahandaki hadi california kule kwa diwani hakufai ukipanda huko nyaklazobe ndiyo utalia kabisa uingie mkuyuni ,igogo ni mayooweee,halmashauri hazina hela,hela zote zinaenda hazina
-stand ya nyegezi ni miezi mi 4 sasa wamevunja hakuna kinachoendelea,unarusha mapicha weka picha ya stendi ya mwanza sasa hivi i dare you,hakuna hat security lights,walikuwa na haraka gani kuhamia sehemu ambayo hata choo na usalama wa abiria ni shida
chukua tax au bodaboda mitaa ya kona ya nyegezi au california waambie wakupandishe majengo kwa mabula usikie jibu lao,huo ni mfano tu udongo wa mwanza sijui una shida gani ni mhandaki matupu barabara za mtaani
naomba u post na picha za wamachinga walivyojazana hovyohovyo hadi mbele ya maduka ya watu eti wana kitambulisho cha umachinga
unaweza ukaniwekea picha za wamachinga na uchafu wa mto mirongo? na kule kwa wakoma?
Halafu msiniweke kwenye ujinga wenu wa ligi ya sijui arusha na mwanza,huwa nawacheka sana ninavyoonga mnabishana kuhusu mwanza vs kisumu
yaani nyegezi ndilo lango la mtu anayeingia mwanza ila hali ilivyo kuanzia ile lami iliyojaa viraka ya shyinyanga to mwanza ni huruma sana
Kama unadhani ni ligi au unafanya kazi jiji basi nenda barabara za nyakato igoma meeco buzuruga kaone kama zinafagiliwa,yaani lami ipo lakini ni chafu imejaa mavumbi mamichanga,security lights zipo lakini haziwaki ukiongea unawekewa picha za magorofa,kama ni hivyo dar watu wasingelalamika kisa wana skyscrappers
Dont even get me started kuhusu maji utashangaa eti mita kdhaa tu kuna ziwa kubwa afrika,majuzi alikuja naibu waziri wa maji Awesso ikabidi azungukie nyegezi kona kutokea huko karibu na kwa mabula maana mitaani barabara ni mhandaki mmmekalia cheap propaganda na matusi na huyo maku aliyeniita mimi msenge akirudia tena nitakuja kumlawiti usingizini .hopeless
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,349

Kwanini hayo yote usiende kuuliza ofisi za jiji zipo mtaa wa Balewa jirani na hospitali ya Sekoe Toure au nenda ofisi za TANROAD na TARURA
 
nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,080
2,000
kama kila kitu kina chopostiwa humu ilitakiwa watu wkaulize basi kusingekuwa na posts kabisa.
Hizo pics zinaondoa ukweli gani kwamba barabara za mwanza hazifagiliwi,security lights haziwaki,barabara za mtaani ni mahandaki,stendi mpya ya mkoa ni kituko cha karne na kwamba wamachinga wame flood mjini hadi mbele ya maduka ya watu
hiyo picha ya mdau drone hapo juu ya kwanza nje ya soko sijui ilipigwa mwaka gani maana hata akienda jumapili hii ausbuhi hupati pic kama hiyo,ni vurugu na uchafu wamama wauza vitumbua hadi barabarani kwenye lami
ni vuluvulu,ndiyo maana nilianza kwa kusema mgeni akiingia mwanza leo atashangaa sana haswa ukichukuliwa lango la kuingilia ni nyegezi..hahahahahha
Kwanini hayo yote usiende kuuliza ofisi za jiji zipo mtaa wa Balewa jirani na hospitali ya Sekoe Toure au nenda ofisi za TANROAD na TARURA
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,015
2,000
nzagambadume

Acha kupaniki hovyohovyo mzee mimi kwa sasa nipo huku na hakuna wakunidanganya... Hiyo six years ago around 2014 barabara ndo zilikuwa mbovu sababu barabara nyingi za michepuko mjini ni mpya...Ile pamba road muda huo unaosemea ilikuwa mbovu hatar hadi ikabidi waijenge upya tu... Huo mwaka barabara ya airport ni njia mbili na traffic lights zilikuwa sehemu mbili tu ila sahivi kahesabu idadi yake mjini kati tu utaelewa nachokuambia... Kuhusu hilo la taa za usiku kutowaka usiku nadhani si tatizo tena maeneo ya mjini kati na baadhi ya sehemu kwan kwa sasa wanachofanya ni kuweka zile solar powered badala ya zile za kutumia umeme na utasadiki hili ukienda mjini mida ya usiku na mpango ni kuzisambaza barabara zote... Tusidanganyane mzee, mwanza ya miaka 6 nyuma ni kijiji kwa hii ya sasa... Mimi pia niliondoka huku nikarudi last year, pamebadilika mno.. Na hayo tu
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,015
2,000
kama kila kitu kina chopostiwa humu ilitakiwa watu wkaulize basi kusingekuwa na posts kabisa.
Hizo pics zinaondoa ukweli gani kwamba barabara za mwanza hazifagiliwi,security lights haziwaki,barabara za mtaani ni mahandaki,stendi mpya ya mkoa ni kituko cha karne na kwamba wamachinga wame flood mjini hadi mbele ya maduka ya watu
hiyo picha ya mdau drone hapo juu ya kwanza nje ya soko sijui ilipigwa mwaka gani maana hata akienda jumapili hii ausbuhi hupati pic kama hiyo,ni vurugu na uchafu wamama wauza vitumbua hadi barabarani kwenye lami
ni vuluvulu,ndiyo maana nilianza kwa kusema mgeni akiingia mwanza leo atashangaa sana haswa ukichukuliwa lango la kuingilia ni nyegezi..hahahahahha
Sijaweka picha ya soko lolote hapo na inaonekana hupafahamu vzr... Kwa uzoefu wangu barabara chafu ni zile za mitaa ya liberty zenye purukushani nyingi na ile iliyounganisha stendi ya dampo na mitaa ya liberty iliyokaliwa na machinga...Pia kuna ile iliyopakana na mlango mmoja kuna kipande ni kibovu ila tofauti na hapo uunatufunga kamba mzee labda hiyo sehemu sijakanyaga.
Niletee picha ya hizi barabara zikiwa mbovu nahama jf;
Musoma road,Kenyatta road,Nyerere road,pamba road,Tanesco road, mji mwema road,Airport road,Pasiasi-buzuruga road,Nyegezi-mjini road,Airport-Igombe road, Buswelu-Airport road,Isamilo road,Sekou toure road,mwaroni road.... Leta ubovu wa hizo barabara... Usidanganye.
Hakuna asiyejua stendi ya nyegezi haitumiki kwa sasa...Labda ushangae ww
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom