Mrejesho, Mwanza is overrated, ni kama shamba la Bibi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,784
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kustukiza Jijini Mwanza Kwa siku 4 hivi ila Cha nilichokiona kinaendelea ni masikitiko makubwa..

Ukuaji wa Jiji licha kuwa sio wa Kasi sana ila unaridhisha lakini ukuaji huo hauko regulated "Shamba la Bibi" These are my observations..

1.Hakuna mipango Miji makazi yanajengwa shaghalabaghala

2.Barabara za mitaani za lami ni chache na finyu ,huku za vumbi zimejaa mashimo na hazieleweki zinaanzia wapi na zinaishia wapi,

3.Jiji linanuka shombo ya Samaki Kila sehemu,sijui watu wa mazingira wanafanya kazi gani.

4.Robo 3 ya Jiji limejaa mabanda ya watu maskini wamerundikana huko milimani hakuna Barabara Wala mitaa Wala sewage systems.

5.Ni nadra sana Kwa Mwanza kukuta mitaa ya kishua na mitaa ya watu maskini yaani makazi yamechanganyikana humo humo tofauti na Dar,Dom,Arusha,Mbeya au Tanga.

6.Barabara za mitaa chache zilizopo hazina Taa yaani Giza Totoro mjini tofauti na Shinyanga na Tabora,Mpanda au Majiji mengine makubwa..

7.Jiji la Mwanza Bado liko nyuma sana kwenye ujenzi wa majengo marefu au hata ya gorofa kulinganisha na Arusha au Dodoma..

8.Jiji halina open spaces Wala bustani za watu ku enjoy,hata zinazoitwa beaches ni mawe matupu au ziko submerged na maji ya Ziwa..

9.Watu Bado washamba wanaongea rafudhi za kilugha,wanashangaa Wageni na hawana ustaarabu,wahudumu wa hotels na lodges hawajua castomer care kabisa unakuta wamenuna utadhani hawalipwi salary.

10.Mwisho Barabara kuu za kuingia Mwanza kutokea Mkoani zimejaa mashimo na viraka na ni nyembamba, utadhani hakuna Serikali hasa Shinyanga na Musoma Road.

Mwisho Mwanza ni Jiji zuri sana kama tuu watakomesha ujenzi holela na kuzuia kabisa kujenga makazi kwenye milima ,kinyume na hapo ni shamba la Bibi.

My Take.
Nime outline hizo observations Ili wahusika wachukie hatua Stahiki ya kulifanya Jiji la Mwanza kuwa na hadhi Stahiki..

Ni jambo la kusikitisha Jiji lenye wakazi zaidi ya 1M ila linaacha kuwa la kienyeji kienyeji kiasi hicho,inasikitisha sana..

Naiomba Serikali ijitahidi kuzuia ujenzi holela wa makazi,just imagine ndani ya miaka 5 ijayo Jiji la Mwanza litaanzia Magu na Misungwi lakini all the way to City centre ni ujenzi holela,hakuna Barabara za mitaa Wala public gardens za watu kufurahia maisha..imagine Jiji wameshindwa kujenga ngazi za kivutio pale Bismarck Rock kama kivutio Sasa unategemea nini?
 
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kustukiza Jijini Mwanza Kwa siku 4 hivi ila Cha nilichokiona kinaendelea ni masikitiko makubwa..
ndwa kujenga ngazi za kivutio pale Bismarck Rock kama kivutio Sasa unategemea nini?
Namba 5 ni ukweli mtupu, Mwanza haina mitaa kwa ajili ya wenye pesa ni full changanyikeni,

Pia umesahau Mwanza Sehemu za vyakula ni za kutafuta sana na mapishi yenyewe sasa ni shida tupu,

Ile Rockcity mall yao hakuna kitu pale watu wanaendaga kupiga picha tu, tangu nifike pale niulizie mkate wa Brwon na wahudumu kuniambia hawaujui na hawajawahi kuuona nilishangaaa sana.Mwanza ni ya kishamba sana
 
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kustukiza Jijini Mwanza Kwa siku 4 hivi ila Cha nilichokiona kinaendelea ni masikitiko makubwa..

Ukuaji wa Jiji licha kuwa sio wa Kasi sana ila unaridhisha lakini ukuaji huo hauko regulated "Shamba la Bibi" These are my eshindwa kujenga ngazi za kivutio pale Bismarck Rock kama kivutio Sasa unategemea nini?
Napataga shida sana kwa vyakula Mwanza, yaani sehemu za kupata Chakula cha maana ni chache mno, Unaweza tembea kutoka Usagara hadi Mwanza mjini hapo katikati hakuna sehemu ya maana ya kupata Chakula,
 
Namba 5 ni ukweli mtupu, Mwanza haina mitaa kwa ajili ya wenye pesa ni full changanyikeni,

Pia umesahau Mwanza Sehemu za vyakula ni za kutafuta sana na mapishi yenyewe sasa ni shida tupu,

Ile Rockcity mall yao hakuna kitu pale watu wanaendaga kupiga picha tu, tangu nifike pale niulizie mkate wa Brwon na wahudumu kuniambia hawaujui na hawajawahi kuuona nilishangaaa sana.Mwanza ni ya kishamba sana
Mall Iko vichochoroni huko yaani ni shida tupu 😁😁
 
Hivi karibuni nilifanya ziara ya kustukiza Jijini Mwanza Kwa siku 4 hivi ila Cha nilichokiona kinaendelea ni masikitiko makubwa..

Ukuaji wa Jiji licha kuwa sio wa Kasi sana ila unaridhisha lakini ukuaji huo hauko regulated "Shamba la Bibi" These are my ndwa kujenga ngazi za kivutio pale Bismarck Rock kama kivutio Sasa unategemea nini?
Public Gadern nazani ni tatizo la nchi nzima
 
Napataga shida sana kwa vyakula Mwanza, yaani sehemu za kupata Chakula cha maana ni chache mno, Unaweza tembea kutoka Usagara hadi Mwanza mjini hapo katikati hakuna sehemu ya maana ya kupata Chakula,
Kiufupi Mwanza Bado sana ila ukiwasikia huku Nje Sasa ni shida unaweza kudhani ni boonge la Jiji kumbe hamna kitu 😂😂
 
Mwanzaa nawaambiaga watu ni kubwa kwa kujengwa ila ni kwa kishamba balaa,
Huwezi Kuta kampuni za Real estates Mwanza zinatangaza blocks zilizopimwa au apartments kama Dar,Arusha au Dodoma.

Technically Mwanza inachoizidi Mbeya ni pale CBD basi ila kwingine ni Yale Yale mambo ya shaghalabaghala Bora liende 🤣🤣
 
Kama mwanza umepaona hivyo, mbeya utasemaje sasa kaka???
Bora hata Mbeya unaweza Kuta block za watu matajiri au mitaa iliyopimwa,Mwanza haina hiyo distinction..

Mbeya Ile forest Mpya na ya zamani zimepimwa,kule Iwambi nk imepimwa ila Mwanza ni Jiji zima.liko hovyo hovyo sana.
 
Hakuna mji tz ambao Hauna sehemu ambazo hazijapimwa,l/pangiliwa,kung'ang'ania kutofautisha sehemu za matajiri na mafukara no ujinga ambao wanaofikiri sawasawa watakushangaa
 
Back
Top Bottom