Salaam JF,
Hivi karibuni Mhe. Rais Samia alifanya ziara nchini Kenya lengo likiwa kurejesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na kujenga zaidi ushirikiano baina ya hizi nchi ili kuipa uimara Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kilichonishtua ni kuona namna haya mahusiano yanavyokwenda kwa kasi ukizingatia kenya wamekuwa na urafiki wa mashaka na kimaslahi zaidi na Tanzania hadi kufikia kutukejeli na Rais wetu kwenye suala la korona na kutuchongea kwa mabeberu ambao kihistoria wamekumbatiwa sana huko Kenya na kuendesha mambo ya uchumi na uwekezaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa.
Kwa hulka hii ya kukumbatia mabeberu na ubeberu kenya waliunga mkono Serikali ya makaburu dhidi ya mtu mweusi.
Hivi karibuni Kenya wamepiga marufuku mahindi ambayo yalikuwa tayari kuingizwa kutoka Tanzania kwa kisingizio cha sumu kuvu huku hayo mahindi wakiwa wanayatumia kwa miaka lukuki. Utafiti ukionyesha kwamba huo msimamo umetokana na kutaka kuikomesha Tanzania kama njia ya kulipa kisasi kutokana na Tanzania kuja na njia mbadala za kuendesha uchumi wake na kukuza uwekezaji na ajira.
Hivyo, naomba chonde chonde Serikali ichukue tahadhari kubwa katika mashirikiano dhidi ya Kenya.