Nipo kinyume na kwenda kasi kwenye kurudisha mahusiano na Kenya

Dunia ni watu inatakiwa utafute watu ili ujifunze ya watu ili ufanikiwe vile vile maendeleo huletwa na watu.. Sio kujifungia ndani eti upate maendeleo hakuna Dunia ya hivyo
 
Huu mtego alioweka kenyatta kwamba watanzania wanaruhusiwa kufanya biashara na kazi kenya bila zuio lolote unalenga kuiingiza serikali kingi nayo iruhusu wakenya waje kufanya biashara, uwekezaji na kazi Tanzania. Hii itapelekea wakenya kuwekeza Tanzania huku wakiajiri wakenya wenzao kwenye makampuni yao na kuwaacha vijana wa kitanzania kuwa machinga wa kuuza bidhaa zao......huu upuuzi unaotaka kuletwa na wakenya hauwezi kuvumiliwa, kila mtu akae kwenye mipaka yake alinde maslahi yake.
Kwa wale ambao hawafahamu Tanzania inachukua 52% ya eneo zima la afrika mashariki, ikiwa na watu zaidi ya mil.60 na rasilimali lukuki zinazoambatana na ukubwa wa eneo lake. Kwa hiyo Tanzania inaweza single-handed kujenga uchumi imara bila kufanya ziara za kujipendekeza kwa wakenya na hivyo kuweza kujenga ushawishi zaidi kwenye eneo zima la E.A....
 
Back
Top Bottom