Nipo kinyume na kwenda kasi kwenye kurudisha mahusiano na Kenya

Salaam JF, hivi karibuni mh. rais alifanya ziara nchini kenya lengo likiwa kurejesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na kujenga zaidi ushirikiano baina ya hizi nchi ili kuipa uimara jumuiya ya afrika mashariki...
Hakuna ushahidi wowote
 
Hapana,, sijasema hivyo, nimesema nilikuwa nakuonyesha kuwa jeshi letu bado linatakiwa kuajili zaidi kwani hata udogo tunaoutaka halijaufikia.
Nchi yetu inatakiwa iwe na jeshi la nchi kavu, jeshi la maji na jeshi la anga...
Hoja yako inamashiko ndugu kongole
 
Sisi ndio tulikuwa miamba,mahodari na mashujaa wa huo urafiki wa mashaka,na kuwa geuza maadui wetu,sababu sisi ni wavivu na walk niwachapakazi said yetu ,unabisha angalia uwekezaji wao kwetu, hata tukanaribu kuwazuia.
Nimeshudia mara kadhaa wakenya wako na uelewa na makini kwa kazi. Nilimpa fundi kutoka Kenyaanitengenezee gari jinsi alivyokomaa na uaminifu wake nilfurahishwa akikuambia bei ni ya uhakika. Watz kazi kidogo mhh
 
Kuna wakenya wengi wanajifanya watanzania ndio wanaongoza kukupinga angalia magazeti wanayomiliki kama citizen na mwananchi yanavyoshangilia ni swala la muda watakapoleta wakenya halafu watanzania watawekwa kando ndipo watafunguka akili
 
Salaam JF, hivi karibuni mh. rais alifanya ziara nchini kenya lengo likiwa kurejesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na kujenga zaidi ushirikiano baina ya hizi nchi ili kuipa uimara jumuiya ya afrika mashariki...
Mama anasema alivutiwa na Rais Uhuru kusimamisha khutuba na kupisha Adhana.

Hiki kitendo kimemfanya Mama aamini Kenya ni majirani wema.

Huyu ndio Rais wa JMT.
 
Mama anasema alivutiwa na Rais Uhuru kusimamisha khutuba na kupisha Adhana.

Hiki kitendo kimemfanya Mama aamini Kenya ni majirani wema.

Huyu ndio Rais wa JMT.
Sitaki kuamini kwamba hii ndo sababu, lakini ni vizuri kutahadharisha hii fast-track approach kwenye integration na kenya. Wakenya wangekuwa wanajali mashirikiano na majirani zake jumuiya ya afrika mashariki isingevunjika mwaka 1977, mara zote wamekuwa karibu zaidi na wazungu na wanatafuta kukuza ushawishi kwenye eneo zima la E.A kupitia kukuza uwekezaji na kujenga uchumi imara kwa kuzitumia nchi jirani kwa ajili ya masoko na kupata malighafi na nishati rahisi, mfano mradi wa bomba la gesi uliosainiwa majuzi na hii itawasaidia kuendelea kukuza ajira kwa watu wao...
 
Salaam JF, hivi karibuni mh. rais alifanya ziara nchini kenya lengo likiwa kurejesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na kujenga zaidi ushirikiano baina ya hizi nchi ili kuipa uimara jumuiya ya afrika mashariki...
Hakukuwa na mashaka yoyote ya mahusiano kati ya Kenya na Tanzania. Tatizo lilikuwa kati ya Kenya na Magufuli.

Wakati utawala wa Magufuli ulipotaifisha ng'ombe wa wakenya 4,000 kwa kukanyaga ardhi ya Tanzania, Wakenya walikamata ng'ombe 9,000 wa Watanzania waliokutwa kwenye ardhi ya Kenya. Utawala wa Magufuli ulitaifisha ng'ombe 4,000 wa Wakenya. Kenya aliwarudishia Watanzania ng'ombe wao 9,000. Wakati wa kurudisha, Gavana wa Kenya alisema:

'Utawala ya Magufuli ni aibu kwa Afrika nzima. Wakenya wanalia, Watanzania wanalia. Wamasai ya Kenya na masai ya Tanzania, ni ndugu. Tunawarudishia ng'ombe zao. We Magufuli unajifanya kifua mbele, kifua mbele na hiyo umaskini yako, utapeleka wapi?"

Sote tunajua kuwa tatizo halikuwa kati ya Watanzania na Wakenya, bali Rais Magufuli na Kenya. Ndiyo maana mara baada ya yeye kuiendea hukumu, mahusiano na Kenya yanarudi kwa kasi.
 
Watu kama nyinyi Mh. Suluhu amewaongelea kule bungeni. Watu kadhaa walio na choyo na fikra finyu za kuendeleza chuki baina ya wananchi wa pande zote mbili. Na hamtaweza kwani mwendo ni wa 5G sahi. Urafiki, undugu, ushirikiano na ujirani mwema kwa pande zote mbili husika ndio jambo muhimu sahi na mbeleni ili kuimarisha uchumi na hali ya maisha kwenye ukanda huu. 🇹🇿 + 🇰🇪 = Prosperity
Subiri. Bado hujaona kitu kwani hapo ni kama unaota tu ndoto na huyo Samia wako.

Yamewashinda wenyewe kwa wenyewe ndani ya Kenya, yeye Samia ndiye atayaweza yatakapoletwa Tanzania?

Vuta subira.
 
Salaam JF, hivi karibuni mh. rais alifanya ziara nchini kenya lengo likiwa kurejesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na kujenga zaidi ushirikiano baina ya hizi nchi ili kuipa uimara jumuiya ya afrika mashariki...
Na tuwe makini ile njia ya barabara mpakani iliyofungwa na Nyerere,ili watalii watokao Kenya wapitie Namanga TUSILEGEZE ule msimamo wa Nyerere!,kwani Marais wote waliofuata walishikilia msimamo huo.
 
Niambieni Rais gani aliyemaliza muda wake bila kukutana na Mambo ya Nongwa kutoka Kenya? Wakenya ni wepesi kujifanya wao ni wema kwetu lkn ni ukweli usiopingika Wakenya si watu wakuamini hata siku moja always They after Profit Maximization.
 
Watu kama nyinyi Mh. Suluhu amewaongelea kule bungeni. Watu kadhaa walio na choyo na fikra finyu za kuendeleza chuki baina ya wananchi wa pande zote mbili. Na hamtaweza kwani mwendo ni wa 5G sahi.

Urafiki, undugu, ushirikiano na ujirani mwema kwa pande zote mbili husika ndio jambo muhimu sahi na mbeleni ili kuimarisha uchumi na hali ya maisha kwenye ukanda huu. 🇹🇿 + 🇰🇪 = Prosperity
Wee wala hujamwelewa. Kuna watu wanakupenda tu kama wanakufaidi. Ukitaka urafiki wa kufaidiana wanakuona mtu mbaya. Hao ndio kenya.
 
Niambieni Rais gani aliyemaliza muda wake bila kukutana na Mambo ya Nongwa kutoka Kenya? Wakenya ni wepesi kujifanya wao ni wema kwetu lkn ni ukweli usiopingika Wakenya si watu wakuamini hata siku moja always They after Profit Maximization.
Nyinyi ndio hamtaki profit kwenyu au wasemaje?
 
Biashara kati ya Tanzania na Kenya mbona ipo miaka mingi mkuu, ninachohofia ni hizi moves zinazoharakishwa ambazo zitaipa kenya advantages zaidi za kiuwekezaji nchini kwao huku wakifaidika kwa kutengeneza ajira zaidi na kuifanya Tanzania kuwa soko tu la bidhaa zao jambao ambalo litaendelea kuua ajira za watu wetu.

Kenyatta anaposema watanzania wanaruhusiwa kufanya kazi na biashara kenya bila zuio lolote kuna mtego mkubwa ndani yake, ndo maana wengine tunatahadharisha kwamba haya mahusiano yaendelee kwa kasi iliyokuwepo au iliyozoeleka, maana kuna watu wanataka twende kwa kasi ya 5G kwenye integration na kenya, jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa mustakabali wa nchi na watu wetu.
Sawa. Nimekuelewa. Suala la msingi hapo ni kuweka mazingira rafiki kwa wote, wakenya na Watanzania. Japo Always usawa hakuna. Mfano USA na Canada Wanafanya kama sisi tunavyotaka kufanya. Sasa cha msingi hapo kuweka mazingira rafiki badala ya kutunishiana misuli.
 
Watu wengi wanaoponda mahusiano yetu kurudishwa na wakenya,hawajishugulishi chochote na wakenya
Utakuta mijitu hiyo imekaa tu maofisini au sebuleni kwa shemeji zao ndy ina cmnt maupuzz haya

Ova
 
Back
Top Bottom