Je, upungufu na kupanda bei ya mchele, mahindi na sasa petroli unatokana na bidhaa hizi kuuzwa Kenya kwa TSH?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Nchi jirani yetu ya Kenya imekumbwa na matatizo makubwa ya balaa la njaa tangia lock downs za COVID na ukame mfululizo.

Pia tangia vita vya Ukraine imekubwa na balaa la upungufu na kupanda sana kwa bidhaa ya mafuta ya petroli na dizeli.

Machafuko yanayoendelea sasa nchini Kenya yanatokana na hali hiyo.

Tanzania kwa kiasi kikubwa imekuwa mwokozi wao kwa kuruhusu ku export kwenda Kenya mchele na mahindi yetu kwa malipo ya Tanzania shilling badala ya angalao USD ili ku boost foreign currency reserve ya benki kuu yetu.

Hii imesababisha bidhaa hizi muhimu za chakula nchini kwetu kupanda bei kwa kiwango cha 200% ikilinganishwa na ile ya mwaka 2021 wakati wa covid 19.

Pia ilisababisha mara kadhaa upungufu wa chakula na kulazimika Tanzania ku import vyakula hivi kutoka Korea au Zambia kwa pesa ya USD kutoka foreign currency reserves za BoT yetu. Kitendo hiki kimesababisha uhaba wa dollar.

Hivi karibuni kwa busara za Mama yetu, bei ya mafuta ya petroli na dizeli nchini mwetu zimepungua kiasi. Kwa upande wa Kenya zimepanda sana.

Kama kawaida matenka ya mafuta kutoka Tanzania yamekuwa yakipeleka bidhaa hii Kenya kwa bei ya Tsh 5,000 kwa lita. Hayapelekwi kama transit goods bali hushushwa kwenye vituo vya mafuta vilivyo jirani na Kenya, hususani huko Arusha, Moshi, Tarime na hata Mwanza.

Je, kuna haja kweli kuendelea kuwasaidia hawa ndugu zetu wakenya kwa mtindo huu unaotuumiza sisi? Ingalikuwa kama ni sisi tumepata shida hiyo hawa rafiki zetu wangalitusaidia kweli kihivyo?
 
Kwa uweledi wa kawaida nchi hu export bidhaa ambazo ina ziada au haizihitaji. Hu export surplus baada ya kukidhi mahitaji ya ndani. Hata kwenye ngazi ya familia ni kukosa weledi kuuza chakula karibu chote ulichovuna shambani kwako na baadaye unajikuta unalazimika kununua chakula kwa ajili ya familia yako kwa bei ya zaidi ya maradufu ya bei ya ile uliyouzia chakula ulichovuna shambani kwako.
 
Ndo matatizo ya kuchelewesha kuanzisha nchi moja ya Afrika mashariki, ingeleta sarafu na soko la pamoja na kupunguza migogoro kama hiyo inayoendelea Kenya, Nyerere alikuwa sahihi.
 
Nchi jirani yetu ya Kenya imekumbwa na matatizo makubwa ya balaa la njaa tangia lock downs za COVID na ukame mfululizo.

Pia tangia vita vya Ukraine imekubwa na balaa la upungufu na kupanda sana kwa bidhaa ya mafuta ya petroli na dizeli.

Machafuko yanayoendelea sasa nchini Kenya yanatokana na hali hiyo.

Tanzania kwa kiasi kikubwa imekuwa mwokozi wao kwa kuruhusu ku export kwenda Kenya mchele na mahindi yetu kwa malipo ya Tanzania shilling badala ya angalao USD ili ku boost foreign currency reserve ya benki kuu yetu.

Hii imesababisha bidhaa hizi muhimu za chakula nchini kwetu kupanda bei kwa kiwango cha 200% ikilinganishwa na ile ya mwaka 2021 wakati wa covid 19.

Pia ilisababisha mara kadhaa upungufu wa chakula na kulazimika Tanzania ku import vyakula hivi kutoka Korea au Zambia kwa pesa ya USD kutoka foreign currency reserves za BoT yetu. Kitendo hiki kimesababisha uhaba wa dollar.

Hivi karibuni kwa busara za Mama yetu, bei ya mafuta ya petroli na dizeli nchini mwetu zimepungua kiasi. Kwa upande wa Kenya zimepanda sana.

Kama kawaida matenka ya mafuta kutoka Tanzania yamekuwa yakipeleka bidhaa hii Kenya kwa bei ya Tsh 5,000 kwa lita. Hayapelekwi kama transit goods bali hushushwa kwenye vituo vya mafuta vilivyo jirani na Kenya, hususani huko Arusha, Moshi, Tarime na hata Mwanza.

Je, kuna haja kweli kuendelea kuwasaidia hawa ndugu zetu wakenya kwa mtindo huu unaotuumiza sisi? Ingalikuwa kama ni sisi tumepata shida hiyo hawa rafiki zetu wangalitusaidia kweli kihivyo?
Tunawasaidia vipi? Kwani tunawapa bure?
 
Kama kawaida matenka ya mafuta kutoka Tanzania yamekuwa yakipeleka bidhaa hii Kenya kwa bei ya Tsh 5,000 kwa lita. Hayapelekwi kama transit goods bali hushushwa kwenye vituo vya mafuta vilivyo jirani na Kenya, hususani huko Arusha, Moshi, Tarime na hata Mwanza.
Unasema mafuta yanapelekwa Kenya lakini hapo hapo unasema mafuta yanashushwa vituo vya mikoa jirani na Kenya.
Hapo nyoosha maelezo kwamba mafuta yananunuliwa na wakenya ndani ya ardhi ya Tanzania. Na manunuzi yanayofanyika ndani ya Tz huwa ni kwa Tzsh.
Kuna kosa gani hapo?

Hata kwenye kununua mazao wakenya huja na Tzsh kufanya manunuzi.
 
Hiyo torosha ya mafuta italeta uhaba hapa nchini. Serikali isiwafumbie macho hao wafanyabishara wa mafuta. Kwenye uchumi wa kibepari mfanyabiashara anaendeshwa na jambo moja tu, faida! Ni wajibu wa serikali kulinda maslahi ya wananchi/ walaji.
 
Back
Top Bottom