Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).
Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.
kwa kifupi, upinzani kwa sasa hakuna kabisa Tanzania, kuna kina sisi huku nje tunaeshangilia siasa kama mpira tuu, tukijuwa nini kinachoendelea na kuna wengi sana wenye kupandisha hasira na ghadhabu, wasiojuwa nini kinaendelea.
Narudia, upinzani kwa sasa hakuna Tanzania. Si CUF, si Chadema, Si NCCR wala si kingine chochote chenye usajili ambacho hakina viongozi ambao wapo kwenye system.
kwa kifupi, si mbowe, si lipumba, si sharif, si mrema, wote hao ni system (according to Marehem Kassim Maguto) ambae na yeye mwenyewe alikiri kuwa ni system wa miaka mingi na alinipa siri kuwa aliitwa Ikulu kuelekezwa waanzishe vyama vya upinzani na wakawa wanafundishwa kila kukicha ni nini cha kufanya na funds zote zikatoka huko, kwa vyama vyote vilivyosajiliwa.
kuna baadhi ya wanachama (wengi tuu) ambao masikini hawalijuwi hili, wapo kwa nia moja ya upinzani na wapo tayari kufa lakini masikini roho zao, laiti wangelijuwa hili nadhani wasingekuwa na hamu hata ya siasa.
Enyi kina Lipumba, Sharifu, Mbowe na Mrema wacheni dhulma hii, haya mnayajuwa lakini mtasababisha watu wauwane bure wakati nyinyi mnajuwa nini mnakifanya. Hebu rudini kwa mola wenu kabla ya watu wasiyoyajuwa haya hawajaanza kughadhibika na kumwaga damu.
Na hayo yote yalipangwa na kuanzishwa na nyerere, ndio maana ufisadi haufi Tanzania na aliyeuanzisha huo ufisadi ni nyerere.
Naapa kuwa hayo yote niliyoyasema ni kweli tupu.
Jee, hamjuwi system ni nini?