Nini hasa kimeondoa Corona Tanzania?

Nini hasa kimeondoa Corona Tanzania?

Nauza kiwanja kigamboni Avic town kwa mbele bei ni kama bure nilinunua 4 mil Ina nauza chini na apo Nina shida documents za mauziano zipo ukubwa wa eneo miguu 27 kwa 22 pia ni mita400 kutoka barabara kuu, Kwann nauza Nina shida muhimu check me kama unahitaji 0652502236 hii ni watsap number ama nipigie 0787326227
We Fala Wwe Yaan Sie Tunajadili Corona Wwe Unauza Kiwanja

manina Zako..
 
Huku tunazika kijana mdogo tu alikuwa akihudumu katika hospital fulani hivi, wanasema corona imemuondoa ila hatujajua kama ni kweli au lah..!
 
Hakuna lolote na hadithi kama hizi tumezizoea.

Vifo na ugonjwa havifichiki kama gongo na ndiyo maana umesema mama Muuza alipokufa ukasikia kuhusu kifo chake na mengi yamhusuyo yeye.

Jiulize au waulize wenzio wamefiwa na watu wangapi kwa COVID-19? Au wamelazwa hospital ndugu na majirani zake wangapi toka huu ugonjwa uingie nchini?

Mnachotaka kusikia kikitokea hakijatokea na hakitokei kama mnavyotaka, acheni roho ya kupenda majanga na mauti.
Uko sahihi sana,ukiangalia idadi ya watu wanaovaa barakoa na kutumia sanitizer na kufuata masharti ya social distancing ni wachache mno,hii ni kuonyesha hao wengi ambao hawafuati masharti ni kuwa huko kwenye familia/jamii zao wanakotoka cases ni chache au hakuna kabisa,hakuna mtu ambaye angeona watu wanaendelea kufa/kupukutika halafu asifuate masharti,kwahiyo kwa jinsi hali ilivyo ni almost kama umeisha.
Vyuo vimefunguliwa na shule zote zimefunguliwa hatujasikia mpaka sasa hivi case yoyote kwa wanafunzi wetu,kwahiyo sidhani kama kuna mzazi yuko tayari kuachia mwanae aende shule wakati watoto wanakufa,hakuna mzazi wa hivyo wala hajazaliwa,mtoto anauma ndugu zangu sikieni tu ,cha muhimu ni kuendelea kumuomba Mungu wetu aendelee kutupigania...
 
Hello JF,

Ningependa kujua out of curiosity,nini kimeiondoa corona Tanzania? Je, Nyungu ilisaidia? Watu kuhimizwa kula tangawizi na malimao?

Na watu wakachukulia serious kula tangawizi na malimao. Hivyo miili yao ikajijenga ku fight virus? Ama watu walichukulia serious kuosha mikono na kuvaa barakoa hivyo rate ya maambukizi ikapungua? Nini hasa kilichoiondoa Corona Tanzania?

Its good to know, ili janga liingine likija, we use the same strategies.
Kilichoaidia kwanza viongozi marais africa kila mauti ya corona ni usd za kutosha unapewa kutoka china ashukuriwe Mungu mzee Magu ana hofu ya Mungu kakataa sasa ukikataa wanawapa wenzako magu akawafuatilia polepole akawatumbua wote ukaja mchezo wa sanitize corona ikswa humo mzee baba akashtuka Akafukuza,mapsmbano ya nyungu limao tangawz ndio vita ya ukweli ndio mana tumeshinda....souz amefanya bidii sana kufuata masharti lkn ndio wanaongoza kwa kufa na maambukz hii ni vita ya kiuchumi kutumaliza viva Magu best prezda Africa.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kitendo tu Cha kuficha takwimu kikupe tu jibu kuwa corona ipo sana hapa na inatafuna watu.Corona haikuwa mkondo wa upepo kwamba inapita tu na ikishapita haigeuki nyuma.

Acha tuendelee kujitoa ufahamu Ila siku ikiguza penyewe tutaanza kuipa heshima yake
Hapo umenena sahihi kabisa
 
MWENYEZI MUNGU, OUR BELOVED FATHER, THE KING OF THE KINGS, ALPHA NA OMEGA.
...HAKUNA MWENGINE,yeye ndiye anatufanya hata sasa tunaishi kwa amani.kama hili suala lingekuwa siasa tusingeyaona yanayofanyika Tanzania kama sasa CCM kufanya vikao vyao kwenye kumbi sealed huku hakuna hata mmoja aliyevaa barakoa,refer kikao kikuu Dodoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali huenda kuna kitu wanakijua kuhusu huo ugonjwa so wakaamua kucheza na saikolojia za watu, huku wakihimiza tahadhari ikiwa kama njia ya kufanya chochote kitu mixer maombi na nyungu.

Kusema kinga duh! Napata hofu kidogo maana hao wazungu hula vyema Sana mazoezi n.k kushinda huku ambapo wengi wao kula nini huchaguliwa na maisha na si kuchagua!.. mi nahisi kuna namna nyengine zaidi ya hizi tunazoziona kuhusu huu ugonjwa.
Mkuu usikariri,kula burger na soda au juice ya kopo na mkate siyo kula vizuri.Waafrika hasa Watanzania kila tunachokula kinaweza kuwa dawa kwetu,ukila ugali na mboga mboga hai zilizo fresh kutoka shambani kwa kiasi fulani umeshaongeza kinga za mwili,ukila bamia,ukila nyanya chungu baadhi yetu tukila vyakula vyetu vya asili vilivyopikwa na vitu kama magadi nk kuna faida fulani tunaipata kiafya.

Waafrica zimetuokoa shida na umasikini wetu,pale mtu hela ya kununua soda hana anakunywa juice ya miwa,hana access ya kupata burger au mkate akachemsha mihogo au viazi akala tayari ameshajihakikishia kuingiza kitu mwilini so ktk hali ya kawaida huwezi kujua hadi utafakari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom