Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.
Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.
"Kwamba tumependa kutoliita koleo kwa jina lake."
Maajabu ya Mussa.
Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?
Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.
Maisha yanaendelea kama vile kila kitu ni sawa.
Ya nini kutoambiana ukweli wote tukajipanga kukabiliana nalo ana kwa ana kama nchi?
Kwenye tahadhali zilizotolewa na wizara katika namna za kujikinga, kutogusana nayo imo. Inawezekana namna gani kwenye maisha yetu ya kawaida watu kutokugusana masokoni, magulioni, mashuleni, makanisani, misikitini, kwenye mabasi au kwenye madala dala?
Ebola si ya maji tiririka, barakoa, michaichai, matango pori wala upigaji nyungu.
Walioyasikia ya kwetu wameshtuka kuliko sisi wakati sisi tukichukulia poa. Dhidi ya gonjwa hili dunia tayari inatunyanyapaa.
Angalia Rwanda, The New Times - Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak
Angalia mabeberu, BBC News - Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania
Coverage zao ni makini na kamilifu (extensive and focussed). Kwetu wenge la awamu ile na njama za mabeberu bado lingalipo.
Kwanini watu wasiambiwe ukweli wote kukiwa kungali mapema? Ya nini kujidanganya?
Magonjwa haya si vita (vya kiuchumi). Ebola si corona ambayo kuuwa kwake kulikuwa hadi 2%. Hiyo hata ikihusianisha uzee na uwepo wa magonjwa mengine pia.
Kwa hakika kwenye ugonjwa huu tusipoamka mapema, usanii wetu uliozoeleka utatuumbua.