Naweza kusema jambo moja kuhusu corona ila lisiwafanye watu wabweteke

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,804
18,532
Watu wasibweteke ni muhimu kuchukua tahadhari zote zinazoshauriwa

Inaonekana sasa kwa namna fulani yale yaliyosemwa mwanzoni kabisa kuhusu waafrika na corona pengine yana ukweli fulani. Kwamba virus vya corona vinaweza visiwaathiri waafrika sana kutokana na hali ya hewa Afrika na kinga mwili za waafrika.

Ni kwamba kwa mahesabu (mathematical modelling) ya mwezi February/March ilitarajiwa kuwa hali ya corona ingekuwa ya kutisha mno Afrika ifikapo May yaani sasa. Ila kulingana na taarifa za nchi nyingi bado maambukizi ni machache ukilinganisha na nchi za Ulaya ilivyokuwa March/April (kumbuka maambukizi yalifika Afrika takriban mwezi mmoja baada ya Ulaya).

Kwa mfano maambikizi yote ya nchi za Afrika ni ~80,000 yaani hayajafikia ya nchi moja tu kwa mfano Peru (88,000 cases). Kama ukiichukua Afrika kama nchi moja basi sasa tupo namba 13 kwa maambukizi, namba 1 ni Marekani yenye visa zaidi ya 1,500,000.

Sababu zinazoweza kuchangia hali kutokuwa mbaya kama ilivyotabiriwa:

1. Kiwango kidogo cha upimaji. Nchi nyingi za Afrika zimepima watu wachache sana zikiongozwa na Tanzania
2. Kuficha ukweli. Baadhi ya nchi zinaweza kuficha uhalisia wa mambo (maambukizi na vifo) kwasababu za kisiasa na kiuchumi. Hili linawezekana sana katika nchi zilizo dhaifu na zisizo na demokrasia imara kama ilivyo Afrika
3. Hali ya hewa ya Afrika. Nchi nyingi za Afrika zina joto na unyevu mwingi. Imesemwa hivi karibuni kuwa hali hii hufanya virus visikae kwa muda mrefu kwenye hewa au vitu
4. Matumizi ya dawa za kienyeji. Kuchelewa kwa maambukizi kufika Afrika kumewafanya watu kujiandaa na kuanza kutumia "kinga" za vyakula kama tangawizi, pilipili, vitunguu, malimao na kujifukiza (nyungu). Afrika ina mimeadawa (medicinal herbs) mingi na bado waafrika wengi hutegemea mitishamba hii.
5. Kinga imara dhidi ya magonjwa. Waafrika wa Kusini mwa jangwa la Sahara wanafahamika kwa kuwa na kinga imara ya asili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Mafua yanayoweza kumuua mzungu yanaweza hata yasimpate mwafrika.

Ila ikumbukwe kwamba maambukizi ya corona Afrika bado hayajafikia kilele (peak) au uwanda (plateau), bado idadi inaongezeka lakini inaonekana kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotabiriwa. Hivyo corona inaweza kubaki Afrika kwa muda mrefu zaidi kuliko sehemu nyingine duniani kwani inaonekana watu wengi hawaoneshi dalili (symptoms) na hivyo huendelea kuambukiza watu wengi zaidi.

Mahali kama Afrika pengine kila mtu ataambukizwa corona wakati fulani ukifika, lakini watakoathirika vibaya ni wachache (wazee au wagonjwa). Hivyo yawezekana kwamba tukalazimika kuishi na corona kwa muda mrefu hadi chanjo itakapopatikana.
 
Tunamshukuru sana Mungu
Mungu ameamua kutudundisha kupitia Civid19 that we have to be proud of our race.
 
Points zako za sababu zinazoweza kuchangia hali kutokuwa mbaya zinajicontradict!

Point no 1 na 2 (negatives) zinapingana na points no 3, 4, na 5(positives)

Jipange tena!
 
Jambo la muhimu ni kuendelea kuchukua tahadhari zinazoshauriwa, nilichojifunza watanzania ni wepesi sana kupuuzia tahahari, mtu atavaa barakoa siku mbili, tatu anatupa kule, ashajiona yeye mjanja kuliko wale waliovaa.......tuwekeze sana kwenye elimu angalau kila kijana afike kidato cha nne hii itasaidia IQ za vijana waweze kujitambua.....
 
Back
Top Bottom