#COVID19 Dunia inatakiwa ije kujifunza Tanzania kuhusu Covid-19

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani (lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi, wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita, tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje!

Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashqngilia?
 
Jana kwa mara ya kwanza Mimi na mke wangu, for the first time tulikaa rasmi kama familia tukijadili COVID/CORONA.

Tulijadili:-

1. Vaccine types
2. Vaccine time experiment
3. Vaccine side effects
4. Vaccine time of negatives effect
5. Why nchi iliopata vaccine kwa kiasi kikubwa imepoteza uhai wa watu wengi kwa COVID/CORONA
6. Why Dr alie shiriki kutengeneza VACCINE alimuandikia barua USA president barua akishauri kusimmaishwa kwa chanjo.
7. Why USA ili tengeneza kitengo cha Emergency ili kupitisha hizo VACCINE, na CDC ikaamua kujitoa kuhusika na chanjo kwaajili ya CORONA.

Agghhhhhhh...

Mwisho wa siku, tuliishia kukosa majibu na tukaanza kujadili ada ya watoto tutailipaje next term
 
Agghhhhhhh.....
Mwisho wa siku, tuliishia kukosa majibu na tukaanza kujadili ada ya watoto tutailipaje next term
Ile kamati ilitakiwa ijibu hayo maswali yako lakini wamekuja na mapendekezo ya hovyo kabisa.
 
Shida pekee nnayoiona ni mahitaji ya kidunia kwa Watanzania watakapokwenda Mataifa ya watu.

Juzi nmeona waliotaka kwenda kuhiji walitakiwa kuwa na chanjo ya Covid.

So kuna uwezekano mambo mengi huko mbele yakahitaji chanjo zaidi so tukisema tuikataze kabisa kuna fursa nyingi kama nchi ama raia mmoja mmoja tunaweza kuzikosa.

So Tanzania kama sisi sidhani kama. Tuna shida internaly ila huko Duniani ndio kutatupelekea kukubaliana na baadhi ya vitu.

Wazo langu mimi Chanjo iwe ihari ya mtu kutokana na mahitaji yake na shughuli zake za kiuchumi.
 
Shida pekee nnayoiona ni mahitaji ya kidunia kwa Watanzania watakapokwenda Mataifa ya watu

Juzi nmeona waliotaka kwenda kuhiji walitakiwa kuwa na chanjo ya Covid.
So kuna uwezekano mambo mengi huko mbele yakahitaji chanjo zaidi so tukisema tuikataze kabisa kuna fursa nyingi kama nchi ama raia mmoja mmoja tunaweza kuzikosa.

So Tanzania kama sisi sidhani kama.tuna shida internaly ila huko Duniani ndio kutatupelekea kukubaliana na baadhi ya vitu.

Wazo langu mimi Chanjo iwe ihari ya mtu kutokana na mahitaji yake na shughuli zake za kiuchumi.
Lakini dunia inatakiwa ije kujifunza Tanzania mbinu tunazotumia kukabiliana na corona.
 
Chadema wanafuraia kwa sababu wanaona CCM tumeuingia mtego kiurahisi na wananchi hawata ikubali chanjo hapo ndioo mtifuano utaanza na wao watapita kati kuchukua nchi manake watu wote watawa support wao.
 
Tukichanja haya ma chanjo tutapukutika kama india usikute wanakuja kutupandikiza kirusi kipya bila kujijua manake hiki cha kuambukizwa na mate kimefeli.
 
Lakini dunia inatakiwa ije kujifunza Tanzania mbinu tunazotumia kukabiliana na corona
Unaweza kuwa sahihi mkuu waje kujifunza huku kwetu Ila tukiangalia hlo ni rahisi kutokea kwa sasa?

Wao wameshafanya research mbali mbali na kutengeneza chanjo za aina mbali mbali sidhani kama watakua tayari wapoteze hzo gharama kwa kumwambia jifukize na unywe Tangawizi wakakuelewa.

Bahati mbaya sana hao ndio wanaoendesha uchumi wa Dunia katika nyanja mbali mbali na mbaya zaidi tunategemea vitu vingi sana kutoka kwao so hatuko kwenye advantageous position kwa sasa.

Muhimu anaetaka achanjwe asietaka asichanjwe basi.
 
Naaam kulingana na mahitaji ya muhusika basi na achanjwe kama kuchanjwa ni muhimu katika hitajio lake.
 
Shida pekee nnayoiona ni mahitaji ya kidunia kwa Watanzania watakapokwenda Mataifa ya watu

Juzi nmeona waliotaka kwenda kuhiji walitakiwa kuwa na chanjo ya Covid.

So kuna uwezekano mambo mengi huko mbele yakahitaji chanjo zaidi so tukisema tuikataze kabisa kuna fursa nyingi kama nchi ama raia mmoja mmoja tunaweza kuzikosa.

So Tanzania kama sisi sidhani kama.tuna shida internaly ila huko Duniani ndio kutatupelekea kukubaliana na baadhi ya vitu.

Wazo langu mimi Chanjo iwe ihari ya mtu kutokana na mahitaji yake na shughuli zake za kiuchumi.
Chanjo ni hiyari ya mtu, hakuna sehemu yoyote au ambapo watu wanalazimishwa chanjo. Hawa wafuasi wa jiwe wanasema kama vile Samia atalazimisha watu chanjo, akili hawana.
 
Corona ndio imemuua Magufuli, kijazi, Maalim Seif, Balozi Mahiga na watanzania wengine wengi. Lile zee la propaganda lilikuwa likiwadanganya eti maombi yameodoa Corona, tangia lini maombi yakatibu janga? bahati nzuri amekufa
 
Mbona magari ,malaria , Ukimwi ,njaa vinaua kila siku?
 
chanjo ni hiyari ya mtu, hakuna sehemu yoyote au ambapo watu wanalazimishwa chanjo. Hawa wafuasi wa jiwe wanasema kama vile Samia atalazimisha watu chanjo, akili hawana
Kuna chanjo ya hiari? Ni nchi gani wamechanjwa kwa hiari?
 
Mabeberu wameanza kutubu kwa Magufuli
Screenshot_20210706-104836_millardayo.jpg
 
Back
Top Bottom