Nini hasa kimeondoa Corona Tanzania?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF,

Ningependa kujua out of curiosity, nini kimeiondoa corona Tanzania? Je, Nyungu ilisaidia? Watu kuhimizwa kula tangawizi na malimao?

Na watu wakachukulia serious kula tangawizi na malimao. Hivyo miili yao ikajijenga ku-fight virus? Ama watu walichukulia serious kuosha mikono na kuvaa barakoa hivyo rate ya maambukizi ikapungua? Nini hasa kilichoiondoa Corona Tanzania?

Its good to know, ili janga liingine likija, we use the same strategies.
 
Serikali huenda kuna kitu wanakijua kuhusu huo ugonjwa so wakaamua kucheza na saikolojia za watu, huku wakihimiza tahadhari ikiwa kama njia ya kufanya chochote kitu mixer maombi na nyungu.

Kusema kinga duh! Napata hofu kidogo maana hao wazungu hula vyema Sana mazoezi n.k kushinda huku ambapo wengi wao kula nini huchaguliwa na maisha na si kuchagua!.. mi nahisi kuna namna nyengine zaidi ya hizi tunazoziona kuhusu huu ugonjwa.
 
Kitendo tu cha kuficha takwimu kikupe tu jibu kuwa corona ipo sana hapa na inatafuna watu.Corona haikuwa mkondo wa upepo kwamba inapita tu na ikishapita haigeuki nyuma.

Acha tuendelee kujitoa ufahamu Ila siku ikiguza penyewe tutaanza kuipa heshima yake
 
Corona ni mradi wa watu kuintroduce mifumo mipya ya kinyonyaji baada ya hii tuliyonayo kuwa na loophole hebu fikiria toka kipindi kile papai limekitwa na corona hakuna hata mzungu au mchina mmoja aliyepatia corona hapa kwetu na kwa taarifa na wao hawachukui tahadhari kama balozi zao zinavyowataka
 
Kuna mtaalamu WHO alisema Afrika kinachotusaidia ni
1. Vyakula tunavyokula, vinatoka shamba moja kwa moja havisindikwi.

2. Maisha tunayoishi, tunafanya mazoezi bila kujua. Kutembea kwa miguu ni usafiri wa kawaida kwa wengi. Wengi hatuna excess fat.

3. Hewa safi, sehemu nyingi hazina industrial air pollution.

4. Hali ya joto.

Haya ndiyo yamesaidia tusiwe na maambukizi Kama ya Ulaya na Brazil.
 
kabla ya ujio wa ukristo na uislam wazee wetu walikua na imani zao, walipokua wakipatwa majanga makubwa daima walifanya maombi kwa imani zao majanga yalitoweka na maisha yakaendelea.

hata sisi kupitia imani zetu mungu tunaemwamini ametuondoshea corona coz yeye anauwezo na nguvu zaidi kuliko akili za madaktari, ambao hutatua matatizo yaliyo katika uwezo wa akili bt mungu hutatua hata yaliyo nje ya uwezo wa akili zetu.

nb: wenzetu waliwatumainia zaidi madaktari ambao ufaham wao unaukomo bt sisi tulimtumainia zaidi mungu ambae ufaham wake hauna ukomo ndo maana vita tumeishinda kirahisi sana.

hebu jiulize hatukufunga nyumba za ibada hata pale corona iliposhika kasi unadhani kama mungu hajasaidia hali ya maambukizi ingekuwaje? tumtumainieni sana mungu ili tupate wepesi katika mambo magum.
 
Back
Top Bottom