Mimi bana utanisamehe siwezi kukupa pole kwakuuguliwa na jambazi huyu. Umeandika uzi wako ili uweze kuonewa huruma na Watanzania kwakuwa ni watu wa ajabu sana eti wanajifanya wanahuruma na mtu aliyetelekeza watoto wako tena wanne kwa miaka yote hiyo, huruma hii inatoka wapi, anafaida gani huyu mtu aliyeacha watoto ili wawe chokoraa pasi na wewe kujifunga kibwebwe. Hata wewe na kina mama wote nawashangaa sana huwa mnahurma za ajabu sana, wewe ulipaswa kuja hapa kuomba msaada tukusaidie kusomesha watoto ningekuelewa na kukusaidia kwa moyo mmoja, lakini baada ya miaka kadhaa ya kuteseka kusomesha watoto bila mume, leo huyu jamaa anaibuka eti anaumwa, mwache tu afe wamekufa watu muhimu kuliko yeye ambaye amepotezea watoto wako. Mimi nawashauri watu msitoe mchango, si kwamba kila mtu akiomba mchango lazima tumpatie eti kwakuwa tunamfahamu bila kuangalia kuwa hizo sababu ni juftiable. Kuna watoto yatima wengi wanapatashida, hawana ada, hawana vyakula, mavazi wanahitaji msaada pelekeni huko lakini si kwahili baba lililotelekeza watoto wake mwenyewe. Sorry kama nimewakwaza naomba tu tujifunze kukubali kutofautina hoja na tuliheshimu hilo. Sikupi pole kwahili.
Nimekuja kwenu rasmi kuleta taarifa hii ya kuuguliwa na bwana ambaye nimezaa naye watoto wangu wote wanne.
Kweli tulifikia mahali kimaisha tukatengana tokea 2001. Kila mmoja akiwa na maisha yake huku nikiwa na changamoto kubwa na kali za kulea watoto ambao ilibidi nibaki nao, hayo kwa sasa tuyaweke pembeni.
Hadi ninavyoandika huu uzi hakuna mtoto hata mmoja ambaye ameshapata kibarua wote wapo kwenye kuhangaika kutafuta kazi.
Ilipofikia mwaka jana mwishoni nikapata taarifa ya kuwa yule bwana niliezaa naye anaumwa, nikajuwa ni homa za kawaida tu.
Leo kaka yake ndo ananipigia simu na kusema kuwa mdogo wake amezidiwa sana na alikuwa amezimia ila kazinduka tena juzi.
Kwangu hiki kitu ni kikubwa nimeshindwa kukibeba.
Kwenu wana jamii kwa upendo wenu ninaomba mnichangie nauli ili niweze kwenda huko Mbeya kumwona huyo mgonjwa. Kama mnavyojua mahali penye ugonjwa mkubwa pia panahitajika hela ya matumizi mengineyo.
Kwa wana jamii wa Mbeya mnaweza kwenda kumuuona nyumbani ni Sae.
Naomba tu msinitukane maana nitalia;[/QUOTE]