Ninauguliwa na baba watoto wangu

Ninauguliwa na baba watoto wangu

Status
Not open for further replies.
Mimi bana utanisamehe siwezi kukupa pole kwakuuguliwa na jambazi huyu. Umeandika uzi wako ili uweze kuonewa huruma na Watanzania kwakuwa ni watu wa ajabu sana eti wanajifanya wanahuruma na mtu aliyetelekeza watoto wako tena wanne kwa miaka yote hiyo, huruma hii inatoka wapi, anafaida gani huyu mtu aliyeacha watoto ili wawe chokoraa pasi na wewe kujifunga kibwebwe. Hata wewe na kina mama wote nawashangaa sana huwa mnahurma za ajabu sana, wewe ulipaswa kuja hapa kuomba msaada tukusaidie kusomesha watoto ningekuelewa na kukusaidia kwa moyo mmoja, lakini baada ya miaka kadhaa ya kuteseka kusomesha watoto bila mume, leo huyu jamaa anaibuka eti anaumwa, mwache tu afe wamekufa watu muhimu kuliko yeye ambaye amepotezea watoto wako. Mimi nawashauri watu msitoe mchango, si kwamba kila mtu akiomba mchango lazima tumpatie eti kwakuwa tunamfahamu bila kuangalia kuwa hizo sababu ni juftiable. Kuna watoto yatima wengi wanapatashida, hawana ada, hawana vyakula, mavazi wanahitaji msaada pelekeni huko lakini si kwahili baba lililotelekeza watoto wake mwenyewe. Sorry kama nimewakwaza naomba tu tujifunze kukubali kutofautina hoja na tuliheshimu hilo. Sikupi pole kwahili.

Nimekuja kwenu rasmi kuleta taarifa hii ya kuuguliwa na bwana ambaye nimezaa naye watoto wangu wote wanne.

Kweli tulifikia mahali kimaisha tukatengana tokea 2001. Kila mmoja akiwa na maisha yake huku nikiwa na changamoto kubwa na kali za kulea watoto ambao ilibidi nibaki nao, hayo kwa sasa tuyaweke pembeni.

Hadi ninavyoandika huu uzi hakuna mtoto hata mmoja ambaye ameshapata kibarua wote wapo kwenye kuhangaika kutafuta kazi.

Ilipofikia mwaka jana mwishoni nikapata taarifa ya kuwa yule bwana niliezaa naye anaumwa, nikajuwa ni homa za kawaida tu.

Leo kaka yake ndo ananipigia simu na kusema kuwa mdogo wake amezidiwa sana na alikuwa amezimia ila kazinduka tena juzi.

Kwangu hiki kitu ni kikubwa nimeshindwa kukibeba.

Kwenu wana jamii kwa upendo wenu ninaomba mnichangie nauli ili niweze kwenda huko Mbeya kumwona huyo mgonjwa. Kama mnavyojua mahali penye ugonjwa mkubwa pia panahitajika hela ya matumizi mengineyo.

Kwa wana jamii wa Mbeya mnaweza kwenda kumuuona nyumbani ni Sae.

Naomba tu msinitukane maana nitalia;
[/QUOTE]Sema wewe mkuu. Atleast angekuja humu kuomba msaada namna wanawe watapata ajira, lkn kuchangiwa nauli ukamuuguze mume aliyekutelekeza way back, mbaya zaidi ameoa na ana familia yake! Kweli wanawake wengine akili zao ni .......
 
Nafikiri hujasoma kifungu kwa kifungu, amepigiwa simu na shemeji yake, kwa maana nyingine ameitwa
Hata kama mkuu, hao mashemeji walikuwa wapi wamkumbuke leo ndg yao anaumwa ndo waone umuhimu wake? Si ajabu hao hao shemeji hawajawahi kuchangia japo ada ya watoto waliotelekezwa, mama wa watu kahangaika peje yake hadi kuomba mtandaoni mpaka watoto wamefika chuo. Leo kaka yao tia maji tia maji ndo akumbukwe mamdenyi? Hapana aisee
 
Wacha akachunwe ngozi huko.hayo mambo hayamuhusu.hv anaenda kumuuguzaje kwanza? Nani anamtaka huko by the way?
Eti shemeji kampigia simu kumpa taarifa za ugonjwa.... Kweli tunatofautiana akili na maamuzi. Hii haimuhusu hata robo, labda mara mia angesema anaomba msaada wa nauli ya watoto wakamuone baba yao mgonjwa, hii ingeleta maana sana kuliko hilo la yeye kwenda.
 
17yrs huyo ex hajaoa mpaka sasa? Hana ndg wa kumuuguza? Huyo shemeji kwa nn asikupe nauli uende ukamuone kaka yake

Pole sana
Hayo ni maisha ndani ya fikra zako, ila yapo mengine mengi tu nje ya box. Kuna watu wanakufa baada ya ukoo kukosa laki ya matibabu. Ijueni Tanzania. Msaidie ukiwa nacho.
 
Hayo ni maisha ndani ya fikra zako, ila yapo mengine mengi tu nje ya box. Kuna watu wanakufa baada ya ukoo kukosa laki ya matibabu. Ijueni Tanzania. Msaidie ukiwa nacho.
Shida sio kusaidia, point unamsaidia nani? Umetelekeza mke na watoto kwa miaka 17, umeenda kuoa mke mwengine. Uliyemtelekeza kahangaika na watoto kwa shida, miaka yote hiyo, mpaka watoto wamehitimu chuo, leo hii uko hoi unaumwa ndio uone umuhimu wangu? Utakuwa unaumwa mavi wewe, bora ukanye tu
 
Watu wengi wenye majibu kama haya no wale waliozaliwa familia za kimasikini mmekuja mjini kwa shemeji zenu mmeanza kulalia godoro na kuficha chenji za jikoni mnunue vocha alafu mnakuja kujivimbisha humu ngoja dada yako aachike urudi kijijini ndo utaelewa kwanini watu wanaombaga msaada!
Amekwambia amewaomba kwanza wakamnyima au unabuni tu?

Acha kunipa mambo ya laana ili kunitisha,ooh "dunia tunapita",sijui nini....thats all bullshit mzee!

Hoja zake kwangu hazija make sense,unanilazimisha sasa?

Hivi unajua ifike mahali watu waachwe wafate wakitakacho...wewe hujawahi nyima mtu msaada?Hebu acha kudanganya watu wazima wenzio!

Hoja za kuweka matatizo yako binafsi hadharani ili upewe pesa ni selfish act ya hali ya juu,maana sisi hatuna shida kama zako?Why zako ziwe ndio zenye thamani zaidi ya za kwetu?
 
Hata kama mkuu, hao mashemeji walikuwa wapi wamkumbuke leo ndg yao anaumwa ndo waone umuhimu wake? Si ajabu hao hao shemeji hawajawahi kuchangia japo ada ya watoto waliotelekezwa, mama wa watu kahangaika peje yake hadi kuomba mtandaoni mpaka watoto wamefika chuo. Leo kaka yao tia maji tia maji ndo akumbukwe mamdenyi? Hapana aisee
Ndg. Maisha ya watu walioshea shuka achana nayo kuna wakati watu wanalazimika kutengana kwa jambo flani lkn kuna mambo mazuri mtu hukumbuka kwa mwenzi wake. Mimi naona anafanya jambo la kiungwana kwenda kumwona na kuchangia matibabu.
Hii itampa amani ya kudumu endapo mwenzi wake ataenda njia ile ya ulimwengu wote. Kadhalika watoto wake watajifunza msamaha kupitia mama yao.
Ni vyema kujenga daraja kuliko ukuta.
Bora kusamehe kuliko kujenga uadui.
Wakristo tunakumbushwa kuwatendea mema maadui na waliotuudhi.

Mamndenyi ametupa somo zuri sana kuwa kusamehe ni jambo linalowezekana hata kama umeudhiwa kwa kiasi gani
 
Acheni kufikirisha akiri kidogo, huyo ni mzazi mwenzie. Kila awaonapo watoto wake fikra hujirudia pia, alishamuachia hiyo zawadi ya watoto, uadui mwingine hauna nafasi, inawezekana mgonjwa yuko ktk wakati wake wa mwisho, yanini Kukumbuka mabaya?

Watoto labda wanataka at least waione sura ya baba yao, unajua wameumiaje kulelewa tofauti na wenzao? Kuna maamuzi ya ujana na mengi hayajazwi na hekima. Tuuvae uhusika, ni mtu mzima huyu.
 
Salaam sana wana MMU wote;

Nimekuja kwenu rasmi kuleta taarifa hii ya kuuguliwa na bwana ambaye nimezaa naye watoto wangu wote wanne.

Kweli tulifikia mahali kimaisha tukatengana tokea 2001. Kila mmoja akiwa na maisha yake huku nikiwa na changamoto kubwa na kali za kulea watoto ambao ilibidi nibaki nao, hayo kwa sasa tuyaweke pembeni.

Hadi ninavyoandika huu uzi hakuna mtoto hata mmoja ambaye ameshapata kibarua wote wapo kwenye kuhangaika kutafuta kazi.

Ilipofikia mwaka jana mwishoni nikapata taarifa ya kuwa yule bwana niliezaa naye anaumwa, nikajuwa ni homa za kawaida tu.

Leo kaka yake ndo ananipigia simu na kusema kuwa mdogo wake amezidiwa sana na alikuwa amezimia ila kazinduka tena juzi.

Kwangu hiki kitu ni kikubwa nimeshindwa kukibeba.

Kwenu wana jamii kwa upendo wenu ninaomba mnichangie nauli ili niweze kwenda huko Mbeya kumwona huyo mgonjwa. Kama mnavyojua mahali penye ugonjwa mkubwa pia panahitajika hela ya matumizi mengineyo.

Kwa wana jamii wa Mbeya mnaweza kwenda kumuuona nyumbani ni Sae.

Naomba tu msinitukane maana nitalia;
POLE SANA ATI USITUKANWE
 
Duh..mamdenyi kumbe ni mhengaa....!!?? 2001 ndo uliachana na mme...! Na tayari ulikuwa na watoto 4,yaani km ulizaa kwa wastani wa miaka 2.9,ina maana umeolewa kati ya 1989 au 1990. Me wakati huo nasoma darasa la 4 au 5. Hakika we Dada yangu, lazima nikuchangie mhenga!!!!
HATA WEWE UTAKUWA MUHENHA HAKUNA LA AJABU NI SAWA UMCHEKE MAREHEMU ILHALI NA WEWE UNAELEKEA HUKO UJINGA HUU........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom