Huwa unafanyaje kurudisha uhusiano mzuri na baba yako, kipindi nguvu ya chuki inapokuwa kubwa zaidi?

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Habari za jioni Wana forum, nimeleta kwenu changamoto yangu angalau nipate busara zenu za kiushauri, najua humu Kuna watu wazima, wenye busara, hekima na waliopitia changamoto mbalimbali za kimaisha nisingependa kuona vijana wenye mihemko ya matusi na wale wasio na busara kutumia Uzi huu kutoa matusi, masimango ama kejeli. Japo nimeandika kwa kirefu lakini ningeomba tusome ili muweze kunipa ushauri vizuri.

Mimi ndiye kijana pekee na wa kwanza ( 30aged kwa sasa) katika familia yetu ya watoto watano, wanne wote ni wa kike, binafsi naipenda Sana familia yangu, naipenda mno na kiukweli linapokuja suala la familia yangu huwa sina mjadala nipo tayari kufanya lolote ili tu iwe na furaha. Kwa miaka kadhaa familia inapitia changamoto kubwa Sana inayonifanya mda mwingine nimchukie Sana baba yangu, sikuwahi kuwaza kumchukia mzazi katika maisha yangu ila kiukweli baba yangu sijui ni nini kimemkuta.

Nimezaliwa na kukulia kijijini na wazazi wangu wote , huku maisha yetu yakitegemea zaidi kilimo Cha jembe la mkono mwanzoni mwa miaka ya 2000 baba alisafiri kwenda Arusha kutafta maisha, akituacha Mimi, mama na wadogo zangu wanne kijijini mwaka uliofuata mama na wadogo zangu walimfuata baba huku Mimi nikibaki kwa bibi kijijini nikiendelea na masomo. Nilipomaliza elimu ya msingi niliungana na wazazi wangu kabla ya kueendelea na masomo yangu ya sekondari mkoani Dar, kiukweli maisha hayakuwa mazuri Sana japo baba alikuwa amenunua kiwanja na kuanza kujenga nyumba za kuunga unga ( chumba kimoja kimoja). Baba alikuwa mpiganaji Sana ambae hakupenda kuona watoto wake tukipitia magumu,..alipambana kwa kila namna ili tuweze kusurvive kwa kipindi kile chapo hali haikuwa nzuri kivile. Kwa kipindi hicho nilishuhudia baba yangu akijatahidi sana kuihudumia familia kwa kila alivoweza, alifanya kazi yoyote ilimradi apate pesa ya kuhudumia familia.

Nikiwa kidato Cha pili maisha ya baba yalibadilika ( mifereji ya pesa ilianza kuonekana) akanihamisha nikapelekwa shule ya private ambako nilimalizia elimu yangu ya O'level, Nikafaulu kwenda Advance kabla ya kubadili na kuenda chuo DITnikisomea kozi ya uhandisi, kipindi hiki mzee wangu alikuwa ameshauaga umaskini alikuwa ashajenga nyumba nyingine nzuri tu pembeni mwa ile ya mwanzo ya kuunga unga iliyokuwa inajengwa kwa chumba kimoja kimoja ikiwa na vyumba 8 pamoja na gari 2 za kutembelea.

Baba yangu alibadilika Sana kwa kipindi kifupi baada ya pesa kuanza kumtembelea ilikuwa ni starehe na yeye, yeye na starehe na Wala hakutaka ushauri ilikuwa akipata pesa anachukua gari haonekani mpaka ziishe akawa mzee wa totozi Sana, binafsi nilijaribu kumshauri awekeze miradi ya kumuingizia pesa zaidi but niliishia kutukanwa na kudhalilishwa, lakini mda mwingine nikawa nakumbuka mateso aliyopitia mzee kuzitafta pesa nikaona ni sawa tu acha ajilawaze lakini changamoto ikawa kuanza kudharau familia na kutokuthamini sisi watoto wake, kipindi hiki watoto wote walikuwa wanasoma private school kasoro wa kike anaenifuata mm ( yeye alikataa mwenyewe akisema hana akili ya kusoma), hivyo akawa anapambana na biashara zake.

Mwaka 2009 nilipata ajira serikalini, na mwaka 2012 nikawa na mpenzi wangu aliyekuwa mjamzito akiwa anasoma chuo cha utumishi wa ummai ngazi ya diploma mwaka wa mwisho, alipopata mimba tu tulitambulishana na kuanza kukaa wote Kama mke na mme.

Nilipangiwa kazi mkoa tofauti na Arusha hivyo nilikuwa mbali na Wazazi kidogo lakini mda mwingi tulikuwa tunawasiliana, mipango mingi ya mzee kwa kipindi hiki akiwa ameanza kupata pesa alikuwa hanishirikishi hivyo nilikuwa nasikia tu baba yako kanunua hiki, kafanya kile mimi nilikuwa nikimpigia simu nampa moyo tu aendelee kupambana.

Nilimaliza mwaka sijarudi kuonana na Wazazi japo nilikuwa nawasiliana nao Sana, na mzee japo nilikuwa namshirikisha mipango yangu karibia yote nae akawa ananipa moyo nipambane nilipojaribu kumuuliza maendeleo yake hakuwa anaiweka wazi, japo kwa pembeni nikawa napigiwa simu na baba wadogo naelezwa baba kakutwa baa kanywa hajiwezi kaibiwa pesa, Mara anatembea na watoto wadogo rika za wadogo zangu bila kificho... Mzee ni mkali ilikuwa ni vigumu kwangu kumshauri masuala Kama haya, hivyo sikuwa na namna zaidi ya kutulia na kipindi hiki nyumbani ilikuwa ni vurugu kila siku mzee anaanzisha ugomvi tu, kiukweli nikaaanza kumuona baba akiwa amebadilika sana, nyumba ikaanza kuwaka Moto kukawa hamna amani tena hata marafiki zake, ndugu zake wakawa wanatukanwa maskini hawana hadhi ya kufuatana nae ikabidi nimpigie niongee nae Kama kijana wake mkubwa lakini niliishia kutukanwa Sana, sikuwa na namna zaidi ya kutulia.

Mzee akawa ni mtu wa matumizi bila mipango, hapa hata familia ( wadogo zangu) wakawa hawajaliwi tena siku moja mama akanipigia simu kunieleza hali na maisha aliyokuwa nayo baba kwa mda huo ( hii ilikuwa Mara ya kwanza mama kunipigia simu kunielezea masuala ya mzee), akaniambia mzee ana hali mbaya na pesa kwa mda huo sio Kama mwanzo hivyo maisha ya nyumbani kidogo sio mazuri, ilibidi nichukue likizo ya mwezi nirudi nyumbani kuongea na baba na kuona namna ya kuokoa jahazi.

Nilipofika nyumbani kwa kweli nilikuta hali ya uchumi sio nzuri kwa baba, mzee wangu sio yule niliyemzoea akifika sehemu anachoma mbuzi mzima na kula na marafiki zake sio huyu tena, Tuliongea mengi na mzee na akawa anasema ni kipindi tu kimebadilika na pesa imekuwa ngumu kwake tena alikuwa anaongea kwa busara sana na akanipa wazo lake la biashara lilikuwa zuri sana nililipenda na nikaona Kama akilifanya kweli litazaa matunda na akadai ni kwa vile hana pesa kwa Sasa angelifanya, nikamwambia mzee usipate shida kwa vile alikuwa anapiga mnada gari zake nikamwambia mimi naenda kukopa bank nimpe pesa, nikiwa najua akiwa na miradi wadogo zangu watasoma, nyumbani watakula bila hivo Mimi mwenyewe sitoweza kuhudumia familia yote hii ikiwa na mimi nina mke na mtoto sasa, mzee akanipa uhakika kabisa na kuniahidi nikashampa pesa nitakazokuwa nimekopa kila mwezi atanitumia pesa itakayotokana na faida ya miradi atakayofungua ili na Mimi niweze kumudu gharama za maisha, nikamwambia haina shida baba, usiku huo nikaenda kukata tiketi na kesho asubuhi nikasafiri kurudi kwangu kuchukua baadhi ya document ili nianze taratibu za kuomba mkopo, nilifanikiwa kuomba mkopo wa 24m ambao ningekatwa kwa kipindi Cha miaka 5 nikarudi arusha nikawa nasubiri mkopo uingizwe kwenye account.

Ni siku mbili zilikuwa zimepita nilikuwa sijamshirikisha mama nini nimeongea na baba, na baba pia hakumwambia mama.. nilivomweleza mama akashtuka, akasema pesa mpe ila usimpe pesa zote hizo kwa tahadhari, mimi nikapingana sana na mama nikamuona kama hapendi nimpe baba pesa, baada ya mabishano mama hakuwa na lingine zaidi ya kuniambia "sawa endeleeni". Nilibaki pale nyumbani ili nihakikishe namkabidhi pesa baba mbele ya familia kabla sijaondoka kurudi kazini.

Baada ya wiki2 nilipigiwa simu na watu wa bank kuelezwa pesa yangu ishaingizwa kwenye account yangu , nikaenda kuchukua niliporudi nyumbani nikamkibidhi baba 19mill. Mbele ya familia na kipindi hicho alikuwa ameuza gari zake 2 kwa jumla ya Tsh 12mill. Hivyo akawa na 31mill. Watoto walikuwa wanadaiwa Ada akatoa palepale 4m akampa mama akawalipie shuleni mmoja alikuwa kidato Cha tatu mwingine mwingine Cha kwanza, hivyo akabaki na 27mil.

Kesho asubuhi, mzee aliondoka kwenda Mkoani tayari kuanza taratibu za kufungua miradi yake Kama tulivokubaliana na Mimi nikaondoka kurudi kazini na mke wangu nikiwa na 4.6mill nilizobaki nazo, nilipofika Wala sikutaka kumsumbua mzee nilikaa kimya ili nimpe mda aandae mipango yake vizuri, baada ya kuwa nimekaa na ile 4.6mill kwa MDA na nisijue niifanyie nini mke wangu akanishauri tutafte kiwanja na akanishauri kwa sababu mzee ni mzoefu nimtumie pesa atununulie, nikaongezea 1.4m ikawa 6m nikamtumia ili atununulie viwanja viwili vya 3m kila kimoja, nikampa mapendekezo yangu nataka kiwanja kimoja kiwe Mwanza kingine Morogoro, Basi baada ya mda akaniambia ashanunua nikamwambia basi naziomba hati nizikute nyumbani kwa mama... Hapa ndipo matatzo yalipoanza sasa.

Hati zikapelekwa nyumbani kwa mama kupitiwa moja inaonesha shamba limenunuliwa heka laki nne mwanza, kiwanja kingine Morogoro 500k imelipwa 1m deni halafu vyote majina ni ya baba na si yangu mashahidi wote wananwake na siwajui, kumuuliza baba imekaaje akasema mradi ulikula pesa nyingi hivyo aliongezea kule na kuhusu majina haina shida, sikuwa na wasiwasi kabisa kwa sababu yule ni baba tena mzazi... Kadri siku zinavyoenda mzee Yuko kimya haniambii maendeleo ya uwekezaji Wala mama hajui kinachoendelea, Kuna siku alinipigia simu akanieleza uwekezaji umekamilika asilimia kubwa ila amepungukiwa na 4m nikatafta na zilizopungua nikakopa kwa watu binafsi kwa riba nikamtumia.

Siku zikaenda, nyumbani mama wanalia hali ngumu wananiomba niwatumie pesa na Mimi linapokuja suala na nyumbani na familia sijiulizi Mara mbili mbili Kama nina pesa, nikawatumia. Lakini nikataka kufahamu ni kivipi mzee asitume matumizi wakati alichukua pesa kwenda kufanya uwekezaji, nikamuuliza mzee anasema uwekezaji ndio umeanza faida bado ndogo ikabidi niwe mpole na kwa changamoto za biashara zilivyo sikuweza kubishana nae ilibidi niwe mpole....huko Mkoani mzee alikuwa tayari amenunua kiwanja mjini hivyo Kama ni suala la uwekezaji wa biashara hakuhitaji eneo tena.

Kuna siku mama alinipigia simu, baada ya kusalimiana akaanza kunieleza "Baba yako alikuja kuchukua ile hati ya kiwanja Cha Mkoani akisema inahitajika manispaa, lakini Kuna watu wameniambia huko amejenga nyumba na sehemu za biashara halafu kuna hawala yake alikuwa bamedi walikutana baa huku kamhamishia hapo na kamumilikisha nyumba na kampa hiyo hati" haya maneno yalikuwa mazito Sana kwenye masikio yangu kwanza sikutaka kuyaamini nikamwambia "mama wewe acha wivu baba hawezi kufanya hivo anatupenda Sana yaani huthamini hata juhudi zake kipindi kile akiwa fukara anashindia juani kwa ajili yetu tupate kula, baba ana akili timamu hawezi kufanya hivo, huo ni wivu tu hebu kaa mama angalia familia inakutegemea Sana usiweze kuyumba kwa vitu visivyo na ukweli" mama akaendelea kunisisitizia huo ndio ukweli na nikiukataa siku Moja nitakuja kuujua, baada ya kuagana na mama nikapuuzia yale maneno yake na Wala sikutaka hata kuulizia hiyo habari na hata sikuweza kumuuliza mzee mwenyewe kwanza naanzia wapi.

Siku zilivokuwa zinaenda sioni mrejesho mwaka ukapita na mimi niko mbeya kikazi, wadogo zangu wakafunga shule mmoja ndo akawa anaingia kidato Cha nne mwingine Cha pili, nikampigia simu baba kuhusu ada za watoto wakifungua shule, hapa ndipo nilipogundua kuna hali ya utofauti alinijibu, " Sina pesa warudie madarasa au waache shule" nikamuuliza ina maana hayo madarasa wanarudia bure, mzee akasema yeye hana pesa na hataki kusikia hiyo habari..nikahisi kichwa kuanza kuniuma Sasa na jasho kuanza kunitoka taratibu, sikutegemea majibu Kama haya kutoka kwa baba, baada ya mda nikakumbuka Kuna viwanja vyangu viko huko nilimuagiza aninunulie nikampigia tena kumuomba aniuzie hivyo viwanja ili anitumie pesa nikalipe ada za wadogo zangu, akajibu sawa lakini viwanja viliuzwa na sikuambulia kuiona hata Mia tano yake hapa pesa zote alikula za viwanja vyangu.

Ikabidi nianze kufuatilia kwa ukaribu zaidi, nikagundua kupitia kwa baba wadogo na mashangazi kweli mzee ana mke walikutana baa kipindi mke akiwa mhudumu wa baa na ni mwenyeji wa njombe na huko Mkoani kajengewa nyumba tena kwa pesa zangu na miradi kafunguliwa kwa pesa zangu na hata viwanja vyangu vimeuzwa pesa kachukua yeye na wamefanya uwekezaji wa mashamba ya miti ya mbao njombe na kuna kuna baadhi ya viwanja vyangu vingine Dar aliuza pia vyenye thamani ya 16m .., hapa niliishiwa nguvu kabisa ila sikuwa na Cha kufanya..Akili yangu ikawa inawaza ni namna gani nitapata ada za watoto 3 walio shule tena private, mungu ni mwema nilifanikiwa kuwalipia na Mimi kwa mda wote sikuwahi kumchukia mzee nilijua ni makosa ambayo kila mtu anayafanya.

Mdogo wangu wa kidato Cha nne alimaliza shule na akafaulu kwa daraja la kwanza akapangiwa kilakala, ilibidi nirudi mijini kufanya maandalizi ya yeye kwenda Advance nikamkuta baba yupo nikatoa laki6 na kwa vile baba alikuwepo na yeye alisema atampeleka shule Mimi nikawaacha nikarudi kazini, Cha kushangaza baada ya miezi kadhaa napigiwa simu na mdogo wangu akinieleza anadaiwa Ada maana hajalipa hata shilling moja wakati baba alinithibitishia ashalipa, ilibidi nimpigie baba kupata ukweli akaniambia kulikuwa Kuna michango mingi, hivyo alinunua vifaa tu, na nguo,ada pesa ilipungua...sikutaka kubishana kwa sababu najua yeye ni mzazi lakini niliona kabisa baba kapeleka ile pesa kwa mama mdogo,...nilichofanya ni kumwambia mdogo wangu anipe namba ya mwalimu anaemuamini ili mimi nimtumie na nikafanya hivo na Ada ikalipwa pamoja na michango.

Ikabidi nianze kufikiria namna ya kuweka kitega uchumi pale nyumbani ili familia iweze kujimudu kwa matumizi madogo madogo, kwa vile pale nyumbani Kuna mafrem nikamfungulia mdogo wangu anaenifuata ( aliyegoma kusoma) restaurant, huyu japo alikataa kwenda shule ila alikuwa na akili ya biashara na utafutaji..aliiendesha vizuri sana ile restaurant na akawa anapata pesa sana, baba akaanza kumdai Kodi na kweli akawa anamlipa baada ya mda mzee akamfanyia fujo kubwa sana na akamfukuza akasema hataki kumuona hapo kwake akiendesha biashara anataka kupangisha frem zake kwa wengine hata nilipojaribu kumshauri hakunisikiliza ikawa ni fujo na vurugu kila siku akiwepo baba nyumba inakuwa ya Moto kwelikweli, hakuna wa kumshauri si ndugu zake, marafiki Wala majirani na Wala familia yake ilibidi mdogo wangu aondoke na mtaji ukafa wa zaidi ya 3m+ na frem hazina mtu mpaka leo.

Hapa nikawa na mzigo mkubwa sana watoto wanasoma private mmoja ndio yuko advance serikalini na mimi ndio kwanza mshahara wangu una mkopo na nyumbani wananitegemea mimi kwa matumizi ya kawaida ya kila siku na kila nikiwawekea miradi baba inaivuruga inakufa.

Baada ya mda nilianza kupata pesa nyingi tu hivyo nikawa stable kiuchumi swala la Ada kwa watoto shule halikuwa tatzo tena, pale nyumbani ile nyumba mzee aliyojenga zamani kwa kuunga unga nikaaanza kuikarabati kulikuwa na wapangaji wanapangisha elfu 25k kwa mwezi nikawalipa siku zilizobaki wakaondoka nikaanza kuifanyia matengenezo, ilinigharimu zaidi ya 32m mpaka ile nyumba inakuwa ya kisasa kabisa, Sasa Cha kushangaza baba anapangisha chumba Sasa kwa Tsh elfu60 mpaka 80k kwa mwezi kwa vyumba vinane na mafrem yake manne lakini hatoi hata pesa ya kununulia chumvi pale nyumbani wala kuwatumia wadogo zangu wanaosoma pesa za matumizi, inanilazimu niwatumie mimi yeye akishachukua kodi anaenda kuzipeleka kwa mke mdogo Mkoani na Mimi yule baba yangu siwezi kubishana nae inanibidi ninyamaze tu na pale nyumbani nilitenga chumba na sebule master nikakitengeneza vizuri Sana kuliko vyumba vyote kwa ajili ya kuwa nakaa ninapokuwa nyumbani na nikaweka kila kitu bado akawa ananiambia nikatoe vyombo apangishe.

Baba alipoona nimemaliza kukarabati ile nyumba akajua mama yangu anafaidi zaidi labda namtumia pesa nyingi akaanza kutoa maneno makali Sana, ambayo yalinishtua Sana maana baba sikuwahi kumuona Wala kumsikia hivi.., anafikia kuwaambia watu kwamba ni " Bora kijana wangu afe au agongwe na gari tukose wote na mama yake" maneno yaliniiumiza Sana ikizingatia nafanya kila niwezalo familia isimame na Iwe na amani pamoja na kwamba Mimi mwenyewe bado nilikuwa sijajenga nilibahatika kununua viwanja 6 baada ya kusimama tena na vyote vikiwa tupu ila familia nilitaka iishi sehemu salama akiwemo yeye, Maana pamoja na makosa yake ila sikuwahi kumsemesha Wala kumwambia Jambo baya naogopa kwa sababu Mimi bado ni mtoto kwake vyovyote itakavyokuwa, ila kwa Sasa amekuwa akisema waziwazi hatambui familia yetu anatambua nyumba ndogo hiyo ya Mkoani na Kuna maneno anaongea kwamba Kuna siku atamuua mama yangu na yeye ajiue ama auze nyumba ( hili nilimkatalia waziwazi)au aichukulie nyumba mkopo halafu asiulipe ije iuzwe na bank, nimejaribu kumuuliza Mara kadhaa kutokana na hizi kauli Kali kutoka kwake lakini anakuwa mkali anasema tunashirikiana na mama kutaka kumuua, namuuliza baba Mimi nawezaje kukuuwa wewe? Anasema Mimi nitazaa wengine nyie sio wanangu na anaongea waziwazi kwamba yeye anatambua familia ya huyo mama mdogo wa shinyanga, kwa Sasa wamefanikiwa kupata mtoto mdogo ana miezi 2 na pia huyo mwanamke alikuwa na watoto wakubwa tu mmoja yuko kidato Cha pili Sasa, mwingine la saba wamebadilishwa majina wanatumia jina la baba yangu Kama baba yao mzazi na baba anadai ile ndio familia yake.

Hapa katikati Kuna duka nilimfungulia mama Kuna siku mteja aliagiza soda mama akawa anamchukulia kwenye friza ghafla tu alipofungua akiwa hata hajaingiza mkono kwenye friji chupa mbili zilizokuwa kwenye friza chini zikapasuka bila kuguswa na zikamchana mama vibaya Sana usoni nilipigiwa simu nikiwa mbeya walimpeleka hospital na baada ya miezi miwli alipona, haikukaa mda ikatokea radi usiku tena bila mvua ikapiga upande wa dirisha wa chumba anacholala mama kwa bahati kabla ya dirisha kulikuwa na mnazi nje hivyo ikapiga mnazi, mnazi ukaanguka na kuungua nilivopigiwa simu ilibidi niombe ruhusa niende nyumbani kufika nikakuta watu wako nyumbani wanadiscuss lile tukio baba hakuwepo alikuwa shinyanga, alikuja baada ya wiki maana ilibidi nimsubiri tuzungumze kwa vile halikuwa Jambo la kawaida, kufika akakuta tupo na baadhi ya ndgu akasema " atajua mwenyewe, hayo Mimi hayanihusu" ilibidi kila mtu ashangae hata mimi nilishtuka kidogo nilikaa wiki moja halafu tukafanya maombi nikarudi kuendelea na kazi.. hata wiki haikuisha mama akaanza kuumwa na kwa vile Wazazi wangu Wana bima ilibidi niagize apelekwe hospitali wakaanza kumpeleka dispensary kila wakipima hawaoni ugonjwa na wanampa dawa za maumivu tu ambazo haikuwa zinamsaidia, wakampeleka hospitali kubwa nako kila wakipima hawaoni ugonjwa, ya mkoa nayo hivo hivo lakini akawa analalamika maumivu makali Sana na mwili Kama unawaka Moto, nikawaamuru wamsafirishe wampeleke muhimbili nako baada ya vipimo majibu yalikuwa hana ugonjwa, lakini kila siku alikuwa halali kwa kuugulia maumivu hali ilinifanya kutokuwa sawa kiakili, nikaomba ruhusa ili nikajiridhishe mwenyewe nilipofika nikampeleka tena hospitali nikapewa majibu yaleyale,.. tukageukia makanisani bado hakupata unafuu ndio hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya.., ikabidi nianze kutafta mawazo mbadala kwa wazee ( kipindi hiki mzee yuko shinyanga, yeye anapiga simu tu kuulizia) nilifika point kila mtu anaeniambia flani anaponya Mimi nampeleka mama kuona Kama anaweza kupata unafuu, Kuna kijana mmoja alikuja kumuangalia mama akaniambia huyu Kuna mtu pale tanga mjini nakuelekeza nenda atakusaidia, sikuwa na Cha kuuliza tena nilichohitaji mama arudi katika Hali ya kawaida tu akanipa namba ya huyo mtaalamu wa jadi siku hiyo hiyo nikaenda ubungo kupanda tashriff kwenda tanga nikiwa na mama tulifika salama yule mtaalam alimwangalia mama, huku Mimi hata nikiwa simuamini amini kwanza alikuwa bado msichana ni Kama 35+aged na mm najua nikisikia mganga Basi awe mzee, akaniagiza vitu vya kununua Mimi sikuwa mwenyeji tanga na nilivyoagizwa sikuvijua ilibidi nitoe pesa Kama 40elfu vikanunuliwe....akaanza kumfanyia dawa usiku huo baade nikamchukua mama nikampeleka hotelini kulala ( jina nadhani mtendele) karibu na nyinda, kesho yake mama akasema anasikia nafuu, ikawa ni Safari ya kwenda kwa mganga na kurudi hotelini mama alikuwa hatembei akilalamika miguu inawaka Moto lakini baada ya siku 2 akaanza kutembea mwenyewe na baada ya wiki moja mama akawa amepona kabisa, na yule mganga akahitaji elfu30 tu. Nikawa nimerudi na mama akiwa mzima mpaka Leo hajawahi kuumwa.

Baada ya kurudi na mama kutoka tanga na Mimi kazini nikapata barua ya uhamisho kwenda Arusha kikazi ambako ndio nyumbani,Sasa hapa kiuchumi sikuwa vizuri, mdogo wangu aliyekuwa advance ashamaliza anatakiwa kwenda chuo, na aliyekuwa Olevel alimaliza na matokeo hayakuwa mazuri nikampeleka chuo SAUT akasome diploma ya uandishi wa habari aliyochagua na mwingine ndio kwanza alikuwa kidato cha 3 hivyo pesa karibu yote ya uhamisho niliitumia kwa ajili ya mahitaji Yao ya shule na ada, karibu kila mwaka nilikuwa natumia zaidi ya 9m kwa ajili ya ada tu, ikanibidi niongee na mzee nirudi nyumbani kwa mda nikiwa najipanga maana pale nilitenga vyumba vyangu vikiwa na kila kitu na huku mimi nikiwa Sasa tayari nina watoto wawili mmoja akiwa na miaka7 Sasa na mdogo miaka 4, nilipofika pale nyumbani kimakazi nikakuta kuna kesi serikali za mitaa ikijiandaa kwenda polisi ambayo mimi binafsi sikuwa naijua Wala sikuwahi kuambiwa na mtu yeyote wa familia yangu, kesi yenyewe ni hii.

Mita chache kutoka pale nyumbani Kuna kanisa pamoja na kwamba linatoa huduma lakini bado lipo kwenye ujenzi, siku moja mchungaji alinunua vifaa vya ujenzi Kama mabati, nondo na vingine vinavyohusiana na ujenzi akaona kwa usalama aviweke pale nyumbani ikabidi aongee na baba na KWELI alimhakikishia usalama kabisa wa vifaa vyake ikabidi mchungaji aviweke pale., Baada ya siku kadhaa mzee alikodi gari akapakia vile vifaa vyote tayari kwa kwenda kuviuza,na alivizia watu wakiwa hawapo na hakuna aliyefahamu kwa wanafamilia zaidi ya wapangaji ndio walio muona na akawaambia anaenda kuezeka nyumba yake mpya anayojenga na wale wapangaji walijua yale mabati ni yake, baada ya siku kadhaa mchungaji akataka vifaa vyake ili aendelee na ujenzi mama alipoenda kufungua stoo hakukuta hata kifaa kimoja hapa ikawa mshikemshike MPAKA pale wapangaji waliposema, alipoulizwa baba akawa mkali na kutoa matusi kwa mchungaji na mama na kesho yake akaondoka kwenda Mkoani ikabidi mchungaji achukue hatua za kisheria, na mama akawa anasumbuliwa na kuitwa kuelezea serikali za mitaa ilivyokuwa wakati mzee hayupo, nilipofika nyumbani na kuikuta Hali ile ilibidi nimuite mchungaji nimuombe anipigie gharama ili nione namna ya kumlipa ili kuachana na ile kesi ambayo ni Kama ilikuwa inaidhalilisha familia pale mtaani, akaniletea risit za vifaa ambazo kwa ujumla wake ilikuwa Kama 3+mill, ambayo mama alithibitisha ni KWELI tulikubaliana nimlipe kidogokidogo kwa mda wa miezi 4 kitu ambacho alikubali na nikalimaliza Deni na amani ikarejea na kesi pia ikaisha

Baada ya siku kadhaa tangu nihamie pale nyumbani mzee kila siku akaanza Kuwa ananifukuza nitoke kwake apangishe chumba, tena kwa fujo Sana, na hata akiwa hayupo akirudi tu kutoka Mkoani anadai niondoke, wakati Mimi ndio nahudumia mahitaji muhimu yote ya nyumbani na kumbuka nilikuwa pale kwa mda nikikusanya nguvu nipange, na kipindi hicho yeye alishasema hanunui hata chumvi kwa familia ya pale nyumbani, Ananiambia nitoke japo hata nyumba Mimi ndio nimeirekebisha..na Mimi sishindwi kutoka uwezo ninao wa kupanga na kuishi vizuri kabisa na familia yangu tatzo nilihitaji kupunguza gharama kwa mda huo ili niwagharamie wadogo zangu waende shule kwanza then mimi nipange maana kama ningekurupuka ningewakwamisha.Imekuwa ni kelele mtindo mmoja mpaka Kuna mda nahisi baba kalogwa, kwa mambo ninayofanya ilitakiwa anisapoti, lakini kwa nini anifukuze wakati hata mwezi tu sikuwa nao pale nyumbani na kunichukia kiasi hiki wakati mimi ni mwanae, na sio mimi tu familia nzima hata ndugu zake wakati hakuwa hivi..? Na ikiwa pesa za wapangaji anachukua zote anapeleka Mkoani kwa nyumba ndogo na hakuna anaemuuliza na Mimi nilimwambia mama Wala asimuzuie.

Ndugu wanahisi mzee amepewa ndumba( limbwata) Kuna siku walikuwa wanagombana na ndugu yake mmoja na sisi watoto tukiwepo, yule ndugu yake akamwambia wewe hiyo sio akili yako ushapewa midawa tayari...mzee akajibu, hakuna wa kunipa dawa, Kama kuna mtu kanilisha limbwata ni mama flani ( anamtaja mama yangu)

Ungekuwa wewe ungefanyaje kwa Hali Kama hii, nishauri yawezekana nikajua Cha kufanya akili yangu imekuwa na msongo wa mawazo Sana japo nimepata mwanamke kiukweli ananisapoti Sana na namshukuru mungu kwa kunipa mke Kama huyu amekuwa faraja kwangu, kwa mama yangu, wadogo zangu na hata kwa ndugu zangu.. Baba pamoja na fujo zake zote za kutufukuza, matusi na kila Aina ya maudhi lakini bado haoneshi utofauti tena ndio amekuwa mstari wa mbele kunisisitizia niisaidie familia nilimfungulia biashara lakini asilimia kubwa anapigana kuwasaidia wifi zake wafikie mlaengo, ukifika nyumbani bila kuambiwa ni mke wangu utajua ni mdogo wangu.., maana mawifi zake wanavyoishi ni Kama dada zake, hata mama yangu wanachukuliana Kama mtu na mwanae wa kumzaa..

Ungekuwa wewe ndio Mimi kwenye familia ya baba Kama huyu, ungefanyaje
 
Aisee nimeshindwa kusoma, ila natumai kuna kitu tu kilichotokea kikasababisha mkafarakana, kwa kifupi unatakiwa kujifanya mjinga tu na kurudi chini na kumuomba msamaha kama mzazi, wanasema mzazi hakosei hata kama ndio mwenye makosa.

Rudi chini muendee mtake radhi na ukiri kuwa kweli uliyofanya yalikuwa ni makosa ila bado nafahamu kuwa wee ni mzazi wangu nahitaji kukuomba msamaha baada ya kugundua kuwa nilichokifanya ni makosa. Hata kama hataonyesha kukusamehe kwa muda ule lakini tayari kuna kitu deep inside his heart kitakuwa kimemuingia. Tafuta wazee wenye busara ikiwa ni marafiki zake au ndugu ikiwezekana uwaeleze wakusaidie kumueleza mzee wako kwa kuwa umemuomba msamaha lakini hajaupokea.

Mwsho ni kwamba, mzazi ni binadamu kuna leo kuna kesho, akitangulia mbele za haki kabla hujamuomba radhi mapema YOU WILL BE A LOSER usikubali kuwa hivyo aisee. Ila pia kumbuka NAZI HAISHINDANI NA JIWE.

Nakutakia kila la heri aisee.
 
Aisee nimeshindwa kusoma, ila natumai kuna kitu tu kilichotokea kikasababisha mkafarakana, kwa kifupi unatakiwa kujifanya mjinga tu na kurudi chini na kumuomba msamaha kama mzazi, wanasema mzazi hakosei hata kama ndio mwenye makosa.

Rudi chini muendee mtake radhi na ukiri kuwa kweli uliyofanya yalikuwa ni makosa ila bado nafahamu kuwa wee ni mzazi wangu nahitaji kukuomba msamaha baada ya kugundua kuwa nilichokifanya ni makosa. Hata kama hataonyesha kukusamehe kwa muda ule lakini tayari kuna kitu deep inside his heart kitakuwa kimemuingia. tafuta wazee wenye busara ikiwa ni marafiki zake au ndugu ikiwezekana uwaeleze wakusaidie kumueleza mzee wako kwa kuwa umemuomba msamaha lakini hajaupokea.

Mwsho ni kwamba, mzazi ni binadamu leo kuna kesho, akitangulia mbele za haki kabla hujamuomba radhi mapema YOU WILL BE A LOSER usikubali kuwa aisee. Ila pia kumbuka NAZI HAISHINDANI NA JIWE.

Nakutakia kila la heri aisee.
Mkuu hebu soma yote uelewe
 
Mkuu hebu soma yote uelewe

Daaaah tatizo situation niliyokuwa nayo hapa sipo kwenye utulivu wa kuweza kusoma yote at once ikaisha.

Ndio mana nilivyoona heading tu asema hapo ni lazma kutakuwa na kosa na kosa huwa linahitaji msamaha, ila nani wa kuomba msamaha, obviously ni wewe coz mzazi hawezi kufanya hivyo aisee.

Au hujakosa, mzazi ataweza kukuchukia/kukukasirikia tu bila ya sababu...? Au tayari umeshaomba msamaha akakataa kukusamehe...?
 
Sijasoma yote ila mkuu mzazi hakosei,jishushe uombe msamaha...sio kumridhisha yeye,bali na wewe pia utakua na Amani,sio siri mzee akitangulia kabla mahusiano yenu hayajarudi..utajichukia milele na unaweza kujiua..ukikumbuka mlikula nguvu zake..za shamba akilima ili mle,sidhani kama utajisamehe mkuu...muombe msamaha sababu huwezi kujua amebakiza mda gani kuishi….na usingependa afariki huku mna unresolved issues
 
Sijasoma yote ila mkuu mzazi hakosei,jishushe uombe msamaha...sio kumridhisha yeye,bali na wewe pia utakua na Amani,sio siri mzee akitangulia kabla mahusiano yenu hayajarudi..utajichukia milele na unaweza kujiua..ukikumbuka mlikula nguvu zake..za shamba akilima ili mle,sidhani kama utajisamehe mkuu...muombe msamaha sababu huwezi kujua amebakiza mda gani kuishi….na usingependa afariki huku mna unresolved issues
Ungemaliza kusoma ungefahamu nini zaidi nazungumzia
 
Daaaah tatizo situation niliyokuwa nayo hapa sipo kwenye utulivu wa kuweza kusoma yote at once ikaisha.

Ndio mana nilivyoona heading tu asema hapo ni lazma kutakuwa na kosa na kosa huwa linahitaji msamaha, ila nani wa kuomba msamaha, obviously ni wewe coz mzazi hawezi kufanya hivyo aisee.

Au hujakosa, mzazi ataweza kukuchukia/kukukasirikia tu bila ya sababu...? Au tayari umeshaomba msamaha akakataa kukusamehe...?
Ungesoma yote ungefahamu nini nazungumzia mkuu
 
Pole saana....maisha hubadilika.

Nikuambie tu pia wewe ni mpole saana.

Ingekuwa mimi pale mzee alipomfukuza dogo kwenye nyumba isingekubali...sikuambii upigane na Baba yako ila ulihitaji kuwa mkali...

Binadamu tunakosea kukosoana lazima awe Baba awe Mama...Nimefurahi kuona unaipenda familia....

Usingekubali familia itawanyike kwasababu ya mtu mmoja tu ambaye ni Baba.

Hili suala zito saana.....ndiyo nimemaliza kusoma.

Wanaume tunabadilika bwana tukikutana na vibinti vidogo...Baba ndiyo hivyo tena kumrudisha kazi hadi maisha yampige na sio leo.

Ningekuwa mimi.
Namwambia Mama adai chake/vyake kama ndoa ni ya kihalali....mwambieni mzee awape vyenu ampe na huyo mke mdogo vyake.sikubali mgawane naye alivyovikuta mmeshatafuta na baba yenu.

Baada ya hapo kata mawasiliano concentrate na familia ya mama yako na yako. La mama kuumwa ningemwachia Mungu muweza ndiye ajuaye.

U mvumilivu saana. .
 
Pole saana....maisha hubadilika.

Nikuambie tu pia wewe ni mpole saana.

Ingekuwa mimi pale mzee alipomfukuza dogo kwenye nyumba isingekubali...sikuambii upigane na Baba yako ila ulihitaji kuwa mkali...

Binadamu tunakosea kukosoana lazima awe Baba awe Mama...Nimefurahi kuona unaipenda familia...nipo hivyo pia...

Usingekubali familia itawanyike kwasababu ya mtu mmoja tu ambaye ni Baba.

Hili la kurudisha moyo ni suala la kisaikolojia...kutana na wanasaikolojia watakusaidia hatua za kufuata.
Ahsante sana mkuu, lakini nadhani siwezi kukoromeana Wala kubishana na mzee wangu sina ujasiri huo
 
Kwa mtazamo wangu.

Kaka tusijiingize kwenye kuzihudumia saana familia zetu labda iwe kwa kuzisaidia...kama unafanya nikusaidia au maisha nyumbani Baba hawezi.

Wazee wetu ukiwanyanganya majukumu mapema wanajiachia wanajisahau wanaona ni wajibu wako kumsomeshea watoto wake. Umezaa watoto wahudumie mwenyewe nitakusaidia ninapojiskia na sio wajibu wangu.
 
Hongera kwa kuwa Baba wa Familia zote mbili.
Sijui unataka ushauri gani tena?
Inaonekana umeweza kusimamia nafasi yako vizuri sana na usiache kuwatunza ndugu zako pamoja na Mama yako.

Baba yako ni muda tu, atakuja kuamka kwenye hiyo ndoto anayoiishi kwa sasa.....

Pole na Kila la Kheri.
 
Bro nakushaur kama mtu mzima niliyevuka 40
Kama unaweza kuanzisha makazi mapya anzisha kisha itoe familia yako kwenye mikono ya huyo mzee
Baada ya wewe kuondoka na kujiimarisha na mama yako na ndg sehemu mpya mzee atauza hizo nyumba hela atanpelekea mke mdogo
Baada ya hapo nakupa mwaka mmoja mzee atakuja anatembelea magoti kuomba msamaha maana kule atakuwa kafukuzwa
Ila mkiendelea kukaa hapo mnawwza kufanyiwa kubwa zaid ya kilichomkuta mama yako
Usigombane nae au kumjibisha we tafuta namna ya kujitegemea na kuanzisha maisha mapya na mamako ja wadogo zako
 
Pole saana....maisha hubadilika.

Nikuambie tu pia wewe ni mpole saana.

Ingekuwa mimi pale mzee alipomfukuza dogo kwenye nyumba isingekubali...sikuambii upigane na Baba yako ila ulihitaji kuwa mkali...

Binadamu tunakosea kukosoana lazima awe Baba awe Mama...Nimefurahi kuona unaipenda familia....

Usingekubali familia itawanyike kwasababu ya mtu mmoja tu ambaye ni Baba.

Hili suala zito saana.....ndiyo nimemaliza kusoma.

Wanaume tunabadilika bwana tukikutana na vibinti vidogo...Baba ndiyo hivyo tena kumrudisha kazi hadi maisha yampige na sio leo.

Ningekuwa mimi.
Namwambia Mama adai chake/vyake kama ndoa ni ya kihalali....mwambieni mzee awape vyenu ampe na huyo mke mdogo vyake.sikubali mgawane naye alivyovikuta mmeshatafuta na baba yenu.

Baada ya hapo kata mawasiliano concentrate na familia ya mama yako na yako. La mama kuumwa ningemwachia Mungu muweza ndiye ajuaye.

U mvumilivu saana. .

Wazo zur pia waombe talaka ya kisheria
 
Daaaah tatizo situation niliyokuwa nayo hapa sipo kwenye utulivu wa kuweza kusoma yote at once ikaisha.

Ndio mana nilivyoona heading tu asema hapo ni lazma kutakuwa na kosa na kosa huwa linahitaji msamaha, ila nani wa kuomba msamaha, obviously ni wewe coz mzazi hawezi kufanya hivyo aisee.

Au hujakosa, mzazi ataweza kukuchukia/kukukasirikia tu bila ya sababu...? Au tayari umeshaomba msamaha akakataa kukusamehe...?
Aombe msamaha kwa kosa lipi mkuu?
 
Back
Top Bottom