Oi wakuu siku zote mtu anapokuja mbele yenu kuomba msaada msikejeli na kudharau.
Kama una uwezo wa kusaidia basi fanya hivyo, kama huna uwezo basi hata maneno ya kufariji na sala inatosha. Lakini ukikejeli na kutukana na kudharau, kesho yako huijui ndugu.
Mungu huyu ni wetu wote, yaweza kuwa ni jaribu kwako, dhihaka hizo mnazofanya na kejeli kesho yaweza kuwa zamu yako na usipate msaada wowote hata wa maneno ya kufariji tu.
Tuchunge midomo yetu jamani na vidole gumba vyetu. Hata kama leo upo katika nafasi nzuri kimaisha huwezi kujua kesho yako, kuna wengi walikua matajiri leo hawana kitu, vipi kama walikua wanawadharau watu waliokua wanawazunguka? Wataishije?
Aheri kukaa kimya kuliko kukejeli. Hakuna anaeijua kesho yake.
"Tajiri mmoja alilima mazao na kisha kuvuna kwa wingi sana mpaka akakosa mahali pa kuhifadhi mazao yake, basi akajiambia kuwa atajenga ghala kubwa na kuhifadhi mazao yake humo kisaha yeye atakuwa mtu wa kula na kunywa tu maisha yake yote maana alikua na kila kitu, lakini Mungu akamwambia " mpumbavu wewe, naitaka roho yako usiku wa leo!"
Kumbe mambo unayopanga wewe sio final, Mungu nae anakuangalia, haifai kujiona fahari duniani kisa umefanikiwa kupata maisha mazuri wakati huwezi kusaidia wengine.
Hiyo story ya tajiri ipo kwenye bible ila sikumbuki ni injili ya nani! Hii ni kutokana na kuwa retired seminarian. Nakumbuka mafundisho yote ya neno la Mungu.