Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Kulikoni,This Day ni magazeti yaliyoamua kufanya kazi zake kikweli tu,hakuna cha mtu au watu wenye nguvu nyuma yake wala nini.Tuliyaona magazeti ya Rai yalivyokuwa na baadae kununuliwa na wakina Rostam.Lbda wakina Rostam watayanunua na haya.

Na kama kuna mtu kama Mkono anaona kuwa wanampaka,naye basi kinachoonekana hapa ni kuwa anatumia sheria zilizopo,kama alivyofanya kudeal nao,sioni kuna tatizo gani.
Mkono ana uhakika kuwa zile habari ni za uongo, kwa hio challenge ni kwa This Day ku-prove kuwa they were correct.

Facts wanazo,tuna uhakika huo,kwa sababu kama hawana then wanakuwa wana agenda nyingine zaidi ya hio. Kwa hio tusubiri tuone,je wata apologise?
 
Mtanganyika,
mimi namkubali Mzee Mkono kwa juhudi zake za kusaidia elimu jimboni kwake. Kama kuna sehemu ana kula at least anakumbuka kusaidia jimbo lake.

Kila mwanasiasa/kiongozi Tanzania ni mlarushwa. Hakuna msafi. Tatizo ni kwamba wengi wapo hapo kula tuuu hawakumbuki kusaidia constituencies zao.
 
Mkono alihusishwa kwenye zile skendo za Bank M na ANBEN. Kwa hiyo hapa anataka kutumia uwezo wake wa sheria na pesa zake kumbana mbavu maskini Mengi kwa niaba ya viongozi wenzake wa CCM wanaokereka na uchunguzi wa magazeti haya mawili.

Hebu angalia tishio hili:

“If, however, you force him (Mkono) to go through along and draw out libel action in order to clear his name, his vindication will be an award to very substantial damages from court

Kuna gazeti lilitakiwa kumlipa Salim Ahmed Salim pesa nyingi sana. Je mambo yale yaliishia wapi?
 
Naamini hawa usalama wa taifa ni watu wwaliokwenda shule na wana uelewa mzuri kabisa.Wao kama watanzania wengine ambao wamekuwa wakitumiwa kama mafagio kusafisha uchafu wa viongozi,wasaidie katika kuwapatia informations watanzania wenye nia nzuri na nchi hii.

Hii vita si kati ya CCM na UPINZANI bali ni kati wala rushwa,wabadhilifu na majambazi wa mali ya watanzania katika ofisi za umma kwa upande mmoja na "integrity" kwa upande wa pili.

Tanzania iliyo bora yenye neema ni kwa manufaa yetu sote na watoto wetu.
 
Mlisikia mjadala leo mbungeni how much Mkono was/is paid to defend serkali ya TZ kwenye case ta CITI WATER.Utalia - $500 an Hr plus flight, accomodation ect.
 
Hivi Mkono ndio mtu wa kwanza kuyashtaki Thisday na Kulikoni?Mbona wakowengi tu na wenye majina makubwa.Kwa kumbukumbu ya haraka kuna Warioba,Prof Mahalu,Manji,and the list goes on and on.Wapo waliotabiri kuwa magazeti hayo yangeishia "kutoweka" kutokana na kesi hizo.

Nachofahamu ni kwamba magazeti haya mawili yalianzishwa MWAKA MZIMA kabla hayajaingia mtaani.Yaani mwaka mzima wa maandalizi huko timu ya waandishi ikipata stahili zake zote katika muda huo ambao Thisday na Kulikoni yalikuwa hayaja-hit newsstands.

Hawa watu wako makini zaidi ya wengi wanavyofikiri.Na wana uhakika sana na wanachoandika ndio maana wanapolipua mabomu ya watu hawasemi "fulani" bali wanataja na jina kamili kabisa.
 
Ukiwashtaki halafu wakagundua kwamba hawana ushahidi wanaacha kukuandama. Siku hizi Manji wameachana naye baada ya kuwadai mamilioni.
 
Kichunguu,

Wali settle out of court kwa dola 500,000. ni nation media

FD

Sawa, nashukuru kwa taarifa FD, lakini huu utamaduni wa kushitaki magazeti naona umepamba moto sana miaka ya hivi karibuni huku yakihusiha punitive damages za hela nyingi tu. Hebu tuone Mbunge Mkono ataishia wapi.

Nadhani ni afadhali waitane yaishie chini chini kuliko kuyablow mahakamani halafu ushahidi ukapatikana kuwa kweli jamaa alichota benki kuu. Watu wengi wana tabia ya ku-underate wenzao wakidhani kuwa hawajui lolote halafu wanakuja shtuka kuona kuwa jamaa alikuwa anakujua kila kitu.
 
Ilongo,

Wameacha kuandika mambo ya Manji? Mbona bado wanaandika? Hivi naye Manji ana maadili hata ya kuweza kumfikisha mtu mahakamani? Jamaa ni kama mchafu mno na akifika mahakamani uchafu wote huo utaanikwa kweli kweli.

Ningelikuwa mimi Thisday, case ya Manji ningeichangamkia kweli kweli maana hapo ndio mahali pa kufumua kila kitu cha jambazi huyo.
 
Hatimaye kinara wa mikopo leo atema cheche na kudai inawezekana kuwasomesha tena bure wanafunzi wa masomo ya sayansi tena bila ya kujali division . Ssaa je kwa nini wamechelewa kufanya hivi?

Hebu long usikike .Nimrodi kahoji kujengwa mashule bila ya vifaa na maabara. Je ni bora shule ama Elimu ama Elimu bora ? Karibu utete hapa .
 
ni kama tulivyo zungumza kwenye thread ya majibu ya waziri mkuu kwa mwanakijiji
 
Mwenzetu mmoja kasema hotuba ya bajeti ya Waziri Msolla imeshapitishwa na Bunge. Bado haijawekwa kwenye site ya wizara. Kama kuna aliyeweza kuisikia, naomba atufahamishe yafuatayo:

(1) Jumla ya fedha zilizoindinishwa kwa ajili ya wizara husika
(2) Kiasi gani kati ya hizo zitatumika kwa ajili ya maendeleo
(3) Kiasi gani ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi.
(4) Idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu 2007.

Hotuba ya bajeti ya Waziri Msolla ya 2006/07 inaonyesha mwaka 2006 tulikuwa na jumla ya wanafunzi wa vyuo vikuu 51,000. Tukikadiria kwenye wanafunzi wa vyuo vikuu 60,000 mwaka huu, basi maana yake ni kwamba kama kila mmoja akikopeshwa 4 mil./- basi zinafika jumla 240 bn./- (billion 240). Akikopeshwa kila mmoja milioni 2, basi zinafika bilioni 120 tu.

Augustine Moshi
 
Hapa duniani kuna vitu vinashangaza sana... Nimrod Mkoni ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu... talk about irony!
 
Back
Top Bottom